Monday

Nashindwa kumtongoza!

Habari yako dinah.

Mimi ni Msomaji mzuri wa Makala zako kwenye blog yako muda mrefu.







Kuna mwanamke nimetokea kumpenda sana ila naomba nijulishe kwa uchache nifanyaje ili niweze kumpata mwanamke ninayempenda baada ya kuchukua namba yake ya simu.







Ili asinione mimi ni muhuni na nisingependa nimpoteze huyu dada. Mimi naamini kutongoza kuna utalaamu wake  na ndio hapo panaponishinda mimi....ahsante.



****************





Dinah anasema: Habari ni njema kabisa, shukurani kwa Ushirikiano. Mail yako imenifanya nicheke kwanza, maana mie sijui mbinu za kutongoza mwanamke kwani mimi ni mwanamke.







Hata hivyo, kuwa na namba yake ya Simu ni mwanzo mzuri, itumie hiyo namba kumsalimia/julia hali asubuhi na jioni (kabla ya muda wa kulala).







Kitendo cha yeye kuamka/kulala na kusoma ujumbe wako au kusikia sauti yako kitaanza kumfanya ajihisi kuwa unamjali.







Inabidi ufanye uchunguzi ili ujue mida yake ili uwe wa kwanza kumjulia hali anapoamka na wa mwisho kusikiwa kabla hajalala.







Hii itasaidia wewe kubaki kichwani mwake akijiuliza maswali, kama yupo interested na wewe hatokukatisha tamaa, ila kama hana interes ni wazi utakuwa msumbufu hehehehe usikate tamaa though.







Akianza kuonyesha interest ongeza mawasiliano ya kumjulia hali na maongezi yawe marefu zaidi kiasi.







Maongezi yasihusu Ngono lakini yanaweza kuhusu upendo, maisha, kazi, familia, watu, celebs hobbies n.k (inategemea na yeye/wewe).







Muhimu ni kuhoji anapendelea nini ili ujue namna ya kuanzisha maongezi, then omba makutano siku ya kawaida na muda wa kawaida sio Mwisho wa Wiki na isiwe Usiku.







Tengeneza Msingi wa urafiki na kuaminiwa kabla hujaanza kumwambia unampenda n.k.







Ukifanikiwa, omba kutoka nae (a date) weekend kwa ajili ya Chakula au kinywaji, Sinema, Muziki...







Mpaka hapo atakuwa kajua kuwa unamtaka/penda na wewe utajua....!



Ikitokea vinginevyo basi kumbuka Penzi halilazimishwi.





Tuone wanaume wenzio watakusaidia zaidi.....



Kila la kheri.

Mapendo tele kwako...

No comments:

Pages