Monday

Ex mwenye Mke...

Habari dada dinah, pole na majukumu. Napenda vile unavyotushauri, mimi ni mdada nina miaka 28 nimemaliza Chuo japo sijabahatika kupata kazi.


Kinachonichanganya miaka saba iliyopita nillikua na mpenzi lakini tukapotezana nimekuja kukutana nae 2O11. Akanambia amekwishaoa, japo tunapenda sana na kuna wakati mpaka analia sana kutokana na ile kupotezana.


Yeye anadai yuko tayari afanye utaratibu wote, hivi sasa huduma zote ananipa na akigundua nina mahusiano na mtu mwingine analia sana mpaka anadai nitamuua au atajiua kama baba yake mzazi alivyojiua.


Kijana nampenda sana ukizingatia ndio mpenzi wangu wa utotoni, hapa nilipo nina Operation nilifanyiwa mwaka 2O12 na naweza kusema yeye ndio chanzo cha Operation dada.

Nishauri nifanyeje kwani sijawahi kuwa na mwanaume akaniridhisha kama huyo kwenye maisha yangu hasa upande wa penzi.


Napata wanaume lakini sifurahi kuwa nao najilazimisha lakini nashindwa dada.


**************

Dinah ansema: Ahsante na shukurani kwa ushirkiano.

Kwanza kabisa achana na excuses za kipuuzi kama "mpenzi wangu wa kwanza", "mpenzi wangu wa utotoni" ....tena futa hilo akilini na liondoe Moyoni mwako kwani utakuwa Mtumwa wa Excuses hizo.


Pili, huyo kijana sasa ni Mume wa mtu mwenye familia aliyoijenga kwa Miaka Saba, yeye kuwa mpenzi wako wa kwanza au wa utotoni sio sababu tosha ya kumuiba Mume wa mwenzio. Yeye kuwa wa kwanza/utotoni haikupi haki kama "Mke wake wa Kwanza".....HUKUPASWA kuingilia ndoa ya watu.

Tatu, Mwanaume kukutimizia mahitaji yako yote sio sababu ya wewe kumkubali au kuendelea kuwa nae. Bibie hii ni 2014....Kama mwanaume anaweza kutafuta na kupata Senti za kutimiza mahitaji so can you! Jitume mwanamke ujitegemee Kiuchumi na mwambie apeleke visenti vyake kwa Familia yake na awekeze kwenye Elimu ya watoto wake.


Nne, Kabla ya Daktari kukuambia kuwa unahitaji Upasuaji lazima alikuambia tatizo ni nini? Naamini kilichopelekea wewe kufanyiwa Upasuaji ni tatizo lako la kiafya sema lilitokea baada ya Mpenzi wako huyo "kupotea" na wewe ukaamini yeye ndio alikuwa sababu....ungekuwa Depressed/mwehu ningekubaliana na wewe.

Tano, Huyo Kijana angekuwa anakupenda hakika angetafuta namna yoyote ile ya kuendeleza Mawasiliano na wewe hata kama ni mara moja kwa mwezi, lakini yeye akuu! hakujali na akaamua kusonga mbele na Maisha yake bila wewe, tena akafunga na Ndoa kabisa.


Baada ya Miaka saba ndio aja kwako analia na kukutishia atajiua. Legacy pekee aliyonao kutoka kwa Baba yake ni kujiua kama alivyojiua Baba yake.

Yeye kulia-lia, kum-cheat mkewe na familia yake, Wivu wa kijinga na vitisho vya kujiua ni wazi mwanaume huyo atakuwa na issues akilini mwake.

Ikiwa alitoweka na akaenda kuoa miaka Saba iliyopita...kitugani kitamfanya ashindwe kurudia tendo hilo tena pale akiwa "high" (nimekwambia ana issues akilini)....kumbuka anataka kumuacha Mkewe kwa ajili yako....technically alikuacha wewe kwenda kuoa....nini kitamzuia kurudia?....Jiulize.

Kwanini utake kuishi kwa hofu na Mashaka na mwanaume ambae inaonyesha ni "Mgonjwa" na tayari anamzigo wa Familia?!!


Ushauri wangu kwako ni wewe kukimbia, kama kujiua mwache ajiue salama kwani hilo ni tatizo lake na familia yake wewe halikuhusu, isitoshe kama uliweza kuishi bila yeye kwa Miaka Saba akijiua si ndio itakuwa kheri ili uwe huru zaidi, yaani bila harufu ya Ex mwenye familia kukufuata-fuata....eti!

Kuna wanaume wengi tu wanajua kuridhisha wanawake, ukiwa muwazi na unajua utakacho na kumuelekeza Mwanaume hakika utaridhishwa.

Kila la kheri.

Mapendo tele kwako...

No comments:

Pages