Monday

Njia rahisi za kuwavutia wanawake kihisia na kufanya wakupende, Je unazijua?

"Saa nyingine ni vitu vidogo vidogo tu ndo vinavyotengeneza mshiko mkubwa kihisia, sifa moja ya akili au ishara ndogo tu inaweza kumshika kihisia mwanamke, vile vile ukitoa sifa mbaya ndo mwisho wako!."

Mwanamke hutumia muda mdogo sana kuamua kama una uzito wowote wa kumfanya yeye atoke na wewe kutokana na vitu vidogo vidogo unavyofanya na vile ambavyo huvifanyi ndo vinamsaidia kufikia kwenye maamuzi yake.
WaulizeWanaume imejaribu kukusanya njia rahisi za kumshika kihisia mwanamke ambazo sio ngumu wala za kupoteza mda na zitatoa tofauti kubwa kati ya kuangaliwa vibaya na kupewa namba ya simu...

♡♡Msifie kwa kitu kizuri...
Ukimwambia mwanamke anaharufu nzuri inayosambaza furaha, kutamfanya ajisikie vizuri, harufu ya furaha ni harufu ambayo kila mtu anatamani kuwa nayo kila saa, hii itakufanya upate wasaa wa kumuuliza vitu gani kwenye maisha yake vinavyomfanya awe na furaha?, ambapo swali hili litamfanya avutiwe zaidi na maongezi yako na kujisikia vizuri zaidi, ukimsifia kwa kitu kizuri unakua mwanzo mzuri utakaokupa fursa na nafasi nzuri zaidi ya kuendelea nae kimaongezi.

♡♡Muombe ushauri...
Wanawake wanapenda sana kutoa ushauri na wanavutika zaidi kwenye njia hii maana utamfanye apate hisia umeona kitu kizuri kwake mpaka ukampatia hio heshima ya kumuomba ushauri, kuwa mwangalifu hapa maana hautakiwi kuonekana kama haujui kabisa juu ya kitu unachomuomba ushauri na hakikisha usifanye asijisikie vizuri.
Ukiwa unaomba ushauri onyesha na wewe ulikua unafikiriaje juu ya hicho kitu au jambo ulilokua unaombea ushauri, na maswali yawe ya urahisi ambayo atatoa majibu kwa urahisi zaidi na hatimaye kuanzisha mazungumzo mengine.

♡♡Msifie kwa jinsi anavyoonekana...
Unatakiwa wakati ukitoa sifa, sifa ionekane ni ya ukarimu na sio vinginevyo, kwa hio inabidi utoe sifa ambayo ni ya asilia, kwa mfano usitoe sifa kama "Unamacho mazuri sana!", jaribu kusema "umependeza kwenye hio nguo uliyoivaa!". Ni njia nzuri ya kumwambia kuwa ni mrembo kuliko njia ya kwanza ambayo inaonyesha wazi sehemu mazungumzo yako yanakoelekea.

♡♡Mfungulie mlango...
Kumfungulia mrango mwanamke ni kitendo cha kiungwana sana, jionyeshe uungwana wako.

♡♡Muulize maswali...
Ukiwa unataka kumjua msichana ni lazima ufanye unachoweza ili kumfanya ajisikie vizuri, hii inamaanisha kuelekeza maongezi kwenye mambo ambayo ukiiyaongelea atajisikia vizuri na kwenye mazingira aliyoyazoea, unaweza kuelekeza maongezi yamuhusu yeye mwenyewe, wanawake wanapenda sana kujiongelea kuhusu wao wenyewe.
Ukimuuliza maswali juu ya maisha yake ya zamani na vitu anavyovipendelea utamfanya aongee kwa kujiamini zaidi, huku ukionyesha hamasa zako zipo sio tu kwa ajiri ya muonekano wake.

♡♡Puuzia simu yako...
Hakuna kitu kibaya kinachoonyesha mtu ulienae hana umuhimu kama kupokea simu au kusoma meseji katikati ya maongezi, ukiwa unaongea na msichana fanya akuone kama kuna mtu anakupigia na uikate simu mbele yake na kizima kabisa, akikuuliza kwanini umefanya kitendo hicho, mwambie mazungumzo yake yamekuvutia na unataka umsikilize yeye kwanza mengine hayana umuhimu, utamfanya ajisikie na thamani kubwa sana kwako.

♡♡♡Ongea na marafiki zake na jihusishe kwenye mazungumzo yao...
Ukiwa unafikiria kumtongoza msichana, lazima utakua unatathimini utu wake, muonekano wake na mengineyo kama uwezo wake wa kuelewa mambo na kufurahi, ndivyo hivyo hivyo mwanamke nae anatathimini, na hututathimini ni kiasi gani ambacho tunaendana na jamii yake.
Wanawake huvutiwa na mwanaume mcheshi, anayependeka kwa urahisi na ni mtu wa kijamii, kwa hio jiingize kwenye maongezi na rafiki zake na ukiweza kuwavutia rafiki zake, utakua umemvutia na yeye pia, hakikisha kipindi chote cha maongezi, uwe umeweka wazi kwamba yeye ndio vutio lako kubwa.

♡♡Kuwa katika hali ya usafi na uvaaji mzuri na wakupendeza...
Wanawake wanapenda wanaume watanashati, wanapenda kuwaona wakiwa wanapendeza na kunukia vizuri mda wote na nywele zilizo katika hali nzuri.
Hembu fikiria wewe unawatathimini wao kwa muonekano, kwa nini na wao wasifanye hivyo vivyo?.

♡♡Mwangalie machoni...
Ni majaribu makubwa kutomwangalia mwanamke mzuri toka juu mpaka chini, anavyokua mzuri zaidi ndivyo ilivyo ngumu kuweka akili yako kwenye maongezi, hakikisha unamwangalia machoni, akikukamata unaangalia maziwa yake wakati anakupa stori kuhusu mama yake ujue atakuona kuwa wewe ni wa ajabu sana.

No comments:

Pages