Tuesday

Sina raha na Mume wangu!

Dada dinah hongera sana kwa kazi unayofanya. Nina miaka
22, nimezaliwa ndani ya familia ya watoto 11. Nilipokuwa na miaka
14 nilizaa na kaka fulani aliye ni lazimisha kufanya mapenzi na kuharibu usichana wangu.

Wazazi wangu wali nikubali nyumbani baada ya hapo niliendelea na Masomo na niliendelea kuwa na wapenzi mpaka nika mpata ninayeishi nae leo yaani Mume wangu.

Tulifunga ndoa yeye ananizidi
miaka 22. Kwanza nilikataa kuolewa, ila Wazazi wakanisihi sana eti
nitawaaibisha.


Jamani tatizo langu ni kwamba kila kukicha naona mapya. Nikaja gunduwa kuwa mume wangu ana watoto zaidi ya 10 wote amewazaa kwa wanawake tofauti.


Mimi nilijuwa ana watoto wawili lakini siku ya Ndoa yetu alisema ya kwamba ana wa Tano, kitu kilichofanya hata tusile tunda ya ndoa usiku wa Ndoa.


Mpaka sasa mimi na mume wangu hatujapata mtoto na yeye ameifanya Ndoa yetu kuwa Kero kwani ana mwanamke mwingine nje, hamtaki mwanangu, Chumbani haniridhishi.

Hapa nilipo sijielewi kwani na sijui nifanyeje? Naomba ushauri.

**********


Dinah anasema: Ahsante na shukurani kwa Ushirikiano.

Pole sana kwa uzoefu mbaya ulioupata ukiwa bado ni mtoto, ningemshika huyo kijana ningemtesa mpaka atamani kufa mwenyeweee(I hate wabakaji that's all).

Naelewa kwanini Wazazi wako walikusihi uolewe na libaba jitu zima hivyo lakini sikubaliani nao. Pamoja na kusema hivyo Wazazi wako wanastahili Heko ya kuendelea kukulea na kukusomesha baada ya Ujauzito!

Ni vema (jambo la kumshukuru Mungu) kwamba hujazaa na mumeo ambae inaonyesha anamzigo mzito wa Ex na watoto wao. Hakuna mwanamke mwenye akili timamu anataka lundo la watoto na mama zao kwenye Maisha yake hata kama wanaishi mbali. Angalau mtoto mmoja utadharau....KUMI?!!! Akuuu. Anyway!


Sijui mlifunga Ndoa katika Mingini gani na kutokana na Uandishi/Ongeaji wako (nimehariri) inaonyesha unatoka pande za Burundi/Rwanda hivi nami sina uhakika na Sheria za Ndoa na Familia za huko.


Lakini natambua Nchi nyingi za Afrika zinatambua Haki za Mwanamke na sheria nyingi za kusaidia Wanawake zilibadilishwa miaka ya 90s mwanzoni na kati.

Ushauri wangu ni wewe kutoka kwenye hiyo Ndoa ambayo ni wazi ulikubali ili kuridhisha wazazi, sasa umekutana na Kero nyingine ambazo zinaongeza uzito wa wewe kutotaka kuendelea kuishi Ndoani humo.


Hatua muhimu ni:- Moja; rudi kwenu na kuelezea tatizo na kutoonyesha nia ya kutaka kurudi kwa Mumeo kwani tayari anamwanamke mwingine na kero nyingine uzijuazo.


Pili; Tafuta Wanasharia Wanawake au wanaosaidia wanawake kwenye masuala ya Familia na Watoto au Ndoa(inategemea huko mnaitaje)......wao watakupa ushauri wa kisheria ili kumtaliki Mumeo via Mahakama.

Kila la kheri.

Mapendo tele kwako...

No comments:

Pages