"HABARI DADA DINAH,
POLE SANA KWA KAZI NZITO YA KUELIMISHA JAMII.
MIMI NI MWANAMKE MWENYE UMRI WA MIAKA 29 ,NINAMPENZI WANGU SASA YAPATA MIAKA MIWILI TANGU TUANZE MAHUSIANO, ILA NINAHISI KAMA VILE YUKO NA MSHICHANA MWINGINE.
HUWA HAPENDI NIENDE KWAKWE AKIDAI KWAMBA ANAHOFIA WADOGO ZAKE ANAOISHI NAO, MARA NYINGI HAPENDI TUWEPAMOJA MFANO WIKIENDI MUDA MWINGI ATASEMA YUKO NA RAFIKI ZAKE.
YAANI NAHISI KUNA JAMBO ANALOLIFICHA NA NAHISI ANAMWANAMKE MWINGINE ZAIDI YANGU, DADA NAOMBA USHAURI JE NIAMINI HISIA ZANGU AU NIFANYE NINI?
MAGDALENA
DAR ES SALAAM"
Dinah anasema: Magdalena mpendwa, dalili ya kwanza kabisa kuwa mtu anakupenda ni kutumia muda wake mwingi na wewe, kutambulishwa kwa ndungu, jamaa na marafiki zake ni dalili ya pili kuwa kafika kwako, kuwa wazi na huru kuwa na wewe au kukuonyesha kwa watu wake wa karibu ni dalili ya tatu, Mpenzi kutokuthamini mtu mwingine yeyote (rafiki zake) bali wewe na kama kuna shughuli/sherehe basi utakuwa wa kwanza kujulishwa na kushirikishwa kabla ya rafiki na jamaa wengine.
Haya yote hufanyika kwenye hatua za mwanzo kabisa za uhusiano wa mtu yeyote, miaka miwili ni mingi sana kwa mtu kuendelea kukufanya wewe "mpenzi wa siri" kwa wadogo zake.
Natambua suala la yeye kukutambulisha au kukupeleka nyumbani ili kuepuka vishawishi kwa wadogo zake hasa kama wako kwenye umri wa kushawishika (kubalehe), wanaweza wakadhani kuwa na girlfriend/boyfried na kumpeleka nyumbani ni kawaida kwa vile kaka anamleta wake hapa.
Lakini vilevile inawezekana anahofia wadogo zake kuuliza kuhusiana na mwanamke mwingine ambae labda wanamfahamu, ili kuondoa utata jamaa inabidi akatae wewe kufahamu nyumbani kwake n.k.
Mpenzi anapokuwa na tabia ambayo wewe unadhani kuwa sio kawaida au hajawahi kuwa nazo kabla hukupa maswali na hofu, vilevile kama unabahati pia unaweza kupata hisia fulani ambazo huwa zinawatokea watu wachache, zinajulikana kama "the sixth sense" inakuwa kama "maono fulani hivi", kama kuna kitu kinatokea behind your back you just know.
Lakini kabla hujakurupuka na kumshutumu mtu kuwa anafanya maovu, unatakiwa kufanya uchunguzi wa karibu ili kuwa na uhakika ili kufanya uamuzi wa maana.
Nini cha kufanya:Punguza ulalamishi kwamba usimuulize wala kulalamika kuhusu tabia yake ya kukukwepa na punguza mawasiliano na huyo Boyfriend wako. Ikiwa unajua mahali anapoishi basi fuatilia kwa karibu ili kujua nini kinaendelea pale nyumbani, je kuna mke(mwanamke mwingine n.k.).
Badilisha mtindo wako wa kimaisha kwa kuwa mwanamke mmoja anaevutia kuliko kawaida, hakikisha unajipenda na kujijali zaidi, vaa mavazi yanayokukaa vema kulingana na umbile lako (usilifiche) ili uvutie zaidi.
Ukiomba kuwa nae mwisho wa wiki na yeye kudai kuwa anakwenda kutumia muda wake na rafiki zake, kuwa calm na muulize kwa upendo ni wapi huko anakoenda? ukijua kona anazopenda kutembelea basi ibuka huko bila yeye kujua, ukifika hapo mahali endelea na starehe zako lakini hakikisha kuwa amekuona.
Baada ya kufanya haya utakundua ukweli na hivyo itakusaidia kufanya uamuzi wa busara ili uweze kuendelea na maisha yako hasa kama kweli ni cheater na pengine kukupa nafasi ya kuweza kukutana na mwanaume atakaejali hisia zako, atakae kuthamini, kukupenda kwa dhati, mwanaume atakae kuweka wewe juu/wa kwanza kabla ya rafiki zake.
Ikiwa umegundua kuwa ni mwanaume mwema lakini hajui namna ya kumpenda mwanamke then itakubidi umfundishe, umuelekeze namna ya kujali na kuthamini mpenzi, kuweka wazi hisia zako na kumwambia ni namna gani unapenda kutumia muda wako mwingi na wewe. Mueleze kuwa hupendezwi na siri na usingependa uhusiano wenu uwe siri, ungependa "Dunia" ijue kuwa ninyi ni wapenzi.....ukianzia na wadogo zake, ndugu, jamaa na marafiki.
Kila la kheri kwenye umauzi utakaoufanya kutokana na matokeo utakayo yapata.
No comments:
Post a Comment