"Hi Dinah!
Naitwa a.k.a Doctor nikiwa hapa Dar. Nina mpenzi ambae anasoma Chuo kimoja hapa nchini, mwanzoni tulipendana sana hadi ikafikia tukapanga tuoane atakapomaliza masomo yake mwaka 2012.
Lakini alipoanza tu Chuo 2009, wiki mbili zikapita akakata mawasiliano ghafla! Nimeonana naye tena mwezi uliopita baada ya kurudi kutoka Chuo na akasema anataka uhusiano wetu uishe kwani anataka kusoma na amechaguliwa kuwa kiongozi kwenye kikundi cha Dini.
Hivyo anahitaji muda mwingi wa kufanya shughuli hizo. Kwa kweli simwelewi kabisa huyu binti, maana siku nyingine ukimpigia simu ili kupanga mihadi ya kuonana anakuja vizuri tu, siku nyingine ukimpigia simu ananikatia.
Yaani simwelewi au nimpige chini kabisa, nitafute mrembo mwingine maana nahitaji binti wa kuishi naye ifikapo 2011 au 2012. Naomba maoni ya wadau. Nipo katikati ya bahari na sijui wapi pa kuanzia!!!!!!"
Dinah anasema: Doctor asante kwa ushirikiano wako, kuzungumzia na kukubaliana kuwa siku moja mtafung andoa sio tiketi ya mtu kubaki na wewe, kama kweli uko serious unatakiwa kuchumbia kwa vitendo (jitambulishe kwao nakufuata taratibu zote) nadhani huyu Binti ameamua kuzingatia masomo yake kwanza bila kuchanganya mapenzi na wakati huohuo kaamua kubadili mtindo wa maisha yake na kumtumikia Mungu ktk hali halisi ni jambo jema sana hasa ukilichukulia kwa upande mwingine.
Mf: Badili kabao wewe uwe kaka wa huyo binti, kwambatufanye ni mdogo, hivi angekuwa na mpenzi ambae wewe kama kaka unaona kabisa kuwa "jamaa" ataharibu maisha ya kimasomo ya mdogo wako hata kama atamuoa (which sio guarantee as hajachumbia kwenu)......alafu kwa bahati nzuri mdogo wako huyo wa kike kachaguliwa kwenda Chuoni na ghafla akaamua kuachana na "jamaa" ili azingatie masomo yake Chuoni.....ungejisikiaje kama kaka?!!
Kama nia yako ni kufungandoa mwakani au mwaka unaofuata haimfanyi huyo Binti kutaka kuolewa muda huo pia, lakini kama mlipokuwa pamoja na mkajadili suala la ndoa muda huo na alipojiunga na Chuo/Uongozi wa Dini akaomba uhusiano wenu ufe ni wazi kuwa Imani yake ya Dini kama zilivyo nyingine zote hasikubaliani na mahusiano ya kingono kabla ya Ndoa.
Mimi nadhani ni vema kuheshimu uamuzi wake na kumpa muda ili azingatie masomo yake(huenda atabadili mawazo), usijenge hasira/chuki na ikiwezekana endeleza urafiki na mawasiliano ya mara kwa mara mpaka utakapokutana na mwanamke ambae atakuwa tayari kuolewa na wewe kipindi ulichojipangia bila kuwa na majukumu ya Kimasomo wala Dini.
Kila la kheri.
No comments:
Post a Comment