"Dinah pole na shughuli hizi za kutuelimisha, naomba nitoke nje ya mada kidogo. Inaonekana ndoa nyingi zina matatizo ya ajabu na sasa Dinah inabidi utoe mada mpya zinazowafanya wanandoa wajue majukumu yao, huenda mwanaume unakuwa hujui kwa nini umeoa tuelekezane hapa tujue majukumu yako na familia yako.
Mke ajue kwa nini ameolewa na amsaidie mume wake kwa kiasi gani maana inaonekana wanawake wakisaidia sana nayo ni tabu pia sasa tuishije katika ndoa zetu ili kupunguza haya matatizo?
Tuongeaje na wapenzi wetu ili tusigongane? pia imeonekana kuwa wanaume wa sasa wana tabia za kununa na hapo inakuwaje? zimekuwapo kasumba kuwa wanawake wakiwa na uwezo kiuchumi ni shida ktk familia lakini mjue kuwa wanawake wengi sasa wana kazi nzuri au sawa na wanaume je tusiwaoe?
Hebu tupeni na uzoefu nyie wanaume wenye wanawake wanaowasaidia sana hapo nyumbani muwe wawazi bila kuweka ile ya uanaume au kuona aibu. Mimi kwa kifupi nimeona wanawake wengi wakiwa msaada mkubwa kwa familia ikiwa baba ana upendo na anamjali mkewe na akiwa mwaminifu hapo matatizo hayapo.
Mie nayashangaa haya matatizo ya ndoa kila siku humu mpaka naona kama ni shida kuoa, nioe mwanamke wa aina gani du!"
Dinah anasema: Shukrani sana kwa kuwakilisha hili suala, hakika hali iliyopo hivi sasa inakatisha tamaa sana. Ndoa zimekuwa zikifungwa kwa kasi ya ajabu na zinavunjika haraka kuliko ilivyokuwa miaka ile ya bibi na babu zetu, mama na baba zetu. Watu wengi wamepoteza imani na baadhi hawaheshimu wala kuthamini ndoa.
Matatizo yanayosababisha ndoa nyingi kuvunjika yanatofautiana kwa kiasi kikubwa(nitaelezea jinsi ninavyoenda mbele), vilevile sababu zilizowafanya hao wanandoa kufunga ndoa pia zinatofautiana(nitaelezea jinsi ninayoendelea).
Sababu kuu ya kufunga ndoa ni mapenzi, japokuwa enzi za babu na bibi zetu hali ilikukuwa tofauti kutokana na mtindo wa maisha wakati ule na vilevile mfumo dume, wanawake na wanaume wengi walifunga ndoa bila mapenzi, yaani mapenzi hayakuwa sababu ya wao kutaka kushi pamoja bali Familia zao, umri, kuepuka aibu, kufaidika kiuchumi kutoka familia tajiri, ndoa n.k.
Ndoa hizo zilidumu kwa muda mrefu kwa sababu ya watoto, kuepuka aibu, kuachika ni kama kufukuzwa kazi kwavile enzi zile ndoa ilikuwa kama sehemu ya ajira, kwamba mwanamke kuolewa ni mwisho wa matatizo. Sasa ukiachwa ni wazi kuwa familia "watakufa njaa" na wewe hutoolewa tena kwani jamii ilikuwa inaamini kuoa mwanamke alieachwa ni mkosi.
Kutokana na maisha tunayoishi sasa wengi tunapata nafasi ya kupendana kwanza kabla ya kufunga ndoa, lakini baadhi hufunga ndoa kwa sababu zilizowafanya bibi na babu zetu kufunga ndoa which kwa maisha ya sasa ni sawa na kujipa kifungo/mateso ya maisha kwani ni ngumu sana kuishi na mtu usiempenda maisha yako yote.
Nitakuja kumalizia hili midaz........
No comments:
Post a Comment