"Habari dada dinah,
Pole na hongera kwa kazi yako nzuri kwani tunajifunza mengi.
Dada dinah, mimi ni msichana mwenye umri wa miaka 28 na nina BoyFriend wangu ambaye niko nae takribani miaka 6 japo hatujaoana kwani yeye bado anasoma. Kwa ufupi tulisoma wote ila kutokana na sababu mbali mbali nimemtagulia na sasa nafanya kazi.
Mahusiano yetu yamekuwa ya vuta nikuvute kutokana na sababu mbali mbali za hapa na pale japo tatizo kubwa ni WIVU na UBABE alionao BoyFriend wangu, mara nyingi amekuwa mgumu sana yeye kuomba hata samahani pale anaponikosea badala yake hugeuza kosa kuwa la kwangu.
Ili kuepuka ugomvi na mambo yaishe naishia kuomba mimi samahani. Niseme ukweli tunapendana na ktk upelelezi wangu sijawahi kusikia hana mtu nje zaidi yangu japo siwezi jua mambo ya wanaume.
Mara kwa mara amekuwa akidiriki kusema maneno ya fedhea na hata kunitukana. Pia mkipanga appointment muda fulani tukutane yeye anachelewa sana na anaweza akafika baada ya masaa hata 3. Kwakweli huwa nashindwa kuzificha hasira zangu na kujikuta nachukia (kununa). Nimuulizapo hunigeuzia kitabu lakini hawezi kusema samahani, Mimi hiki kitu kinanikera sana.
Siku moja alikuja chumbani akitaka mambo fulani, kama kawaida ya wapenzi kutaniana basi alitaka kufunga pazia nikamkataza na baadae aliporudi kitandnani nikamwambia kafunge. Kwa hasira alinyanyuka na kutaka kuondoka.
Nilipoona hivyo nikamvuta nikamwamia "hutaniwi"! Cha ajabu alinisukuma na kuniburuza nikiwa NAKED huku akielekea kufungua mlango wa nje na kisha akaondoka zake. Kwa kweli iliniuma sana n akuaibika kama pale nje kungekuwa na mtu.
Baada ya muda nilimtumia msg kuwa ktk mahusiano yetu amenionyesha picha halisi yeye ni mtu namna gani. Wadau hakujibu na tulichuniana takribani wiki 2 mpaka pale mimi nilipomwambia aje home. Tukiirudia topic ile lakini kama kawaida yake hakuomba samahani na kuniuzia kesi mimi.
Siku nyingine tulikubaliana tukutane Town ili nichukuwe pesa fulani kwani yeye alinisisitiza kuwa anashughuli nyingi hivyo niwahi. Ni kweli nilijihimu mida ya saa moja nikawa nimefika. Nilipompigia simu alidai bado amelala. Honestly niliumia na kwa hasira niliondoka nikarudi home. Wadau huyu mpenzi hakusema lolote wala samahani mpaka leo, baadae alinipigia simu mida ya saa 6 akiuliza niko wapi. Nilimjibu niko home.
Kutokana na tabia hii, nipatapo nafasi ambapo tukio kama lake linaweza kufanyika basi na mimi humlipiza ili aone uchungu wake. Huwezi amini huja juu na kulalamika kuwa ni kwanini nafanya vile, hapo ndipo ninapopata nafasi ya kumuliza je ni vibaya? Na je wewe uliponifanyia hivi uliona ni sawa?
Dada dinah, yeye huishia kusema niache kulipiza kisasi, Hata mimi humwabia kama hutaki kutendewa basi jirekebisha. Niliamua kuliweka hili suala mezani na tukalijadili kwa kina kama wapenzi lakini alihishia kusema atabadilika japo mpaka leo sioni mafanikio.
Nimechoshwa na hii tabia, yaani nimekuwa mtu wa kulia na kuumwa vidonda vya tumbo sababu ya hasira. Imefikia hatua anatoa maneno yake ya kejeli eti mimi na yeye nani mwanaume?anadai tutashindana mpaka lini?
Kununa nuna ndio haswaa, kwani hasione nina marafiki wakiume hata akiwa mfanyakzi mwenzangu. Kafanya juu chini niachane na nabest zangu wanaume ila nimegoma. Imefikia hata hatua tukienda kwenye fuction yoyote kama harusi basi mambo huko hayaendi tutanuniana mpaka tunarudi nyumbani, kisa watu wamenihug.
Dada dinah na wadau wote nisaidieni kwani nimechoka, mara nyingine nawaza kuachana nae ila naogopa magonjwa na kutengeneza CV za wanaume. Nifanye nini jamani? Naamini hakuna kitu kizuri kama kubembelezana na kuombana msamaaha pale mwenzi wako anapokukosea. Pia nimechoka kuona natendewa mimi na nishiwa mimi kupiga magoti kuomba samahani.
Nishaurini wadau kwani hayo ni machache tu."
Dinah anasema: Asante sana mpendwa kwa kuniandikia na kwa ushirikiano, kutokana na maelezo yako nadhani huyo jamaa hakulelewa kwenye mazingira ya nidhamu kwamba hajui kusema asante wala samahani.
Watu waliokulia kwenye mazigira hayo ni vigumu sana kwako kujua umuhimu wa shukrani na kuomba radhi, vilevile jinsi wanavyokuwa na kuwa na wapenzi huwa ni wagumu sana kusema "nakuepnda", "nimekukumbuka" "ninafuraha sana kuwa nawe" na wengine kuwa wabinafsi linapokuja suala la ngono.
Miaka sita kama wapenzi bila ndoa ni mingi mno yaani mmezoeana kupita kiasi na hivyo kulichukulia uhusiano wenu kama kitu mlichokizoea na mnashindwa kujitoa pamoja na kuwa wakati mwingine mnahisi kabisa kuwa " sasa basi, huyu mtu hanifai" lakini mnashindwa kufanya uamuzi na kusonga mbele kila mmoja wenu na maisha yake. Hilo moja.
Pili, mpenzi wako bado ana-elements za Mfumo Dume, yeye kuwa shule na wewe kufanya kazi (kuwa na kipato) n wazi anatishika nakuhisi kuwa haeshimiwi kama mwanaume na ndio maana amekuwa na maneno ya kashfa na hata kukuuliza wewe na yeye mwanaume ni nani? hii inaonyesha ni kiasi gani anahofia kupoteza "Uanaume wake".
Nini cha kufanya: Tangu umechoshwa na tabia ya huyo Mpenzi wako ningependa uondoe hofu ya kutengeneza CV ya wanaume kwani ukijipa muda wa kutosha wa kupumzika kutoka kwenye uhusiano wa muda mrefu na huyu Kijana wa sasa ni wazi utakutana na kijana mwingine na mkapendana nakuishi vizuri tu kama wapenzi na hatimae mkafunga ndoa.
Uoga mwingine ulionao ni "ugeni" wa kuwa single tena baada ya kuwa kwenye uhusiano kwa muda mrefu, hujui namnagani ya kujichanganya na hata nini cha kujibu ikiwa mtu atakutokea n.k., lakini ukijipa muda wa kutosha hakika utakuwa ok na utafurahia maisha yako wewe kama wewe.
Bado binti mdogo, unajitegemea kiuchumi na unajua nini mapenzi (umeonyesha wazi kwa kuishi na mtu mmoja kwa muda wa miaka sita na kuvumilia yasiyovumilika).....you can do better than that baby Girl.
Kila la kheri.
No comments:
Post a Comment