Wednesday

Nataka kuacha Mpenzi lakini naonea huruma watoto wangu-Ushauri

"Mambo vipi dada Dinah
Pole na kazi na hongera sana kwa kazi hii ya kutoa ushauri.
Mimi ni kijana mwenye umri wa miaka 32 kwa sasa ninaishi na mwanamke ambaye ninae kwa miaka nane sasa na tumebahatika kupata watoto wawili mmoja wa kiume na mmoja wa kike.

Mwanzo wa maisha ki ukweli tulikuwa tunaishi vizuri tu lakini kadri miaka inavyozidi kwenda mambo yamekuwa yanabadilika na tatizo kubwa naweza sema limekuwa sugu, nasema hivyo sababu ni tatizo la muda mrefu na nimejaribu kuliongelea lakini naona hakuna mabadiliko yoyote na hakuna sababu za msingi anazotoa .

Dada Dinah huyu mwanamke swala la kunipa unyumba kiukweli limekuwa ugomvi yaani hataki na hatoi sababu za msingi kama ambavyo nimeeleza hapo juu. Sasa nimechoka sana na nafikiria mambo mengi sana moja kubwa ni kuachana naye lakini nikifikiria watoto wangu nakosa raha.

Nafikiria katafuta mwanamke wa nje ambaye tutatimiziana hayo mambo hapa pia dada naogopa sana UKIMWI, siku chache zilizopita nilifikiria kupiga punyeto na nilivyofanya hivyo kwa kiasi fulani ilinipunguzia hamu lakini nitaendelea kufanya mapenzi na mkono wangu hadi lini?

Dada naomba ushauri nifanyeje?
Asante
J.M. KURASINI."
Dinah anasema: JM mpendwa asante sana kwa ushirikiano. Sasa kaka yangu umekaa na huyo dada miaka 8 na kakuzalia watoto wawili bado hujatangaza ndoa na inaonyesha huna mpango huo, yeye kama mwanamke hiyo hamu ya kungonoana na wewe kila utakapo ataitoa wapi?

Kama mwanamke hasa wa Kibongo hapo umemharibia maisha, kwanza kazaa watoto wawili (hakuna mwanaume atataka kuoa mwanamke mwenye mzigo), pili amekuwa nje ya "soko" kwa muda mrefu na hivyo itakuwa ngumu sana kwake kujiingiza kwenye masuala ya kimapenzi na mtu mpya.....miaka nane sio mchezo!

Kitu kikubwa ni kuwa umempotezea hali ya kujiamini na inaelekea wazi kabisa wewe huna hisia za kimapenzi nae (kwenye maelezo yako hakuna mahali umegusia kumpenda) tena bali uko nae hapo kwa ajili ya Ngono ambayo sasa huipati na inakufanya utake kutoka nje na watoto. Kinachokuzuia kutoka nje au kumsaliti ni UKIMWI, vinginevyo unekuwa na kimada.

Huyu dada kisheria ni ana haki zote kama Mkeo kwa vile mmeishi pamoja zaidi ya miaka 2, lakini hiyo haitoshi mpaka hatua zote kijamii zitakapofuata na kufunga ndoa kama wanavyofunga wengine.......kama alivyogusia mchangiaji, hicho ni kitu pekee huyu mdada anakitaka kutoka kwako.

Inaelekea alifanya yote ili kukufanya utangaze ndoa lakini hukufanya hivyo, akaamua kushika mimba mara mbili na kufanikiwa kuzaa wewe bado huna habari na ndoa, amendelea kuishi na wewe na sasa ni miaka nane (muda mrefu kuliko wanandoa wengi) lakini wewe ndio kwanza una-demand Ngono badala ya kutafuta tatizo ni nini hasa.

Huyo ni mwanamke, na ndoto ya mwanamke yeyote ni siku moja kufunga ndoa na mwanaume ampendae, huenda kwa wanaume hili ni suala la kijinga lakini kwa mwanamke ndoa ni kitu muhimu sana kwenye maisha yake.

Nini cha kufanya: Rudisha hisia za mapenzi kwenye uhusiano wako (kwani inaonyesha wewe umejisahau na yeye amekata tamaa kama sio kachoka), Muonyeshe huyu mama ni namna gani unampenda, onyesha kuwa bado unavutiwa nae japokuwa amezaa watoto wawili kwani mwanamke anapozaa mara mbili na zaidi mwili wake hubadilika.

Hivyo "Kisaikolojia" anaanza kuamini kuwa havutii tena na vilevile uke wake hauko vile ulivyokuwa awali na hivyo kujishtukia kuwa hatoweza kukuridhisha (anaweza kuwa na aibu pia), sasa kwa vile wewe hujui au hujali unadhani yeye anakunyima lakini ukweli ni kuwa humpi ushirikiano na wala huonyeshi kuwa bado unavutiwa na umbile lake.

Fanya yale yote ambayo ulikuwa ukimfanyia mwanzo wa maisha yenu kama wapenzi, unapohisi kutaka ngono usimuombe kama vile "haki yako" au "jukumu lake" bali itake ngono kwa kuonyesha mapenzi, kwa kumshika nakucheza na mwili wake, jitahidi kumfanya ajisikie kuwa anapendwa.....akielekea endelea lakini akigoma basi usimlazimishe na badala yake muulize kwa upole na upendo tatizo ni nini?

Usilalamike, bali tafuta ukweli kutoka kwake....."kitu gani nakosea mpenzi", " asali wa Moyo kwanini hutaki tufanye mapenzi?"....."naomba uniambie kama nimekosea nijirekebishe".....alafu mmwagie misifa (kulingana na kile unachokipenda na una uhakika anajua kuwa ni kweli).

Jinsi siku zinavyozidi kwenda ongeza kuonyesh amapenzi kisha tangaza ndoa(ndani ya mwezi mmoja), mchumbie mama watoto wako na mfunge ndoa. Nina kuhakikishia utaona mabadiliko na kila kitu kitakuwa sawa mara tu baada ya huyu dada kuwa na uhakika kuwa mnakwenda kufunga ndoa.

Hakikisha unafunga ndoa kiukweli,
Kila la kheri!!

No comments:

Pages