"Habari dada dinah pole na kazi ngumu uliyo nayo ya kuielimisha jamii. Nimekuwa mfuatiliaji mzuri sana wa mada zako ila sijawahi kuleta swali leo nimena na mimi nijitokeze kwa swali ili nipate msaada.
Nilikuwa sijajua tatizo langu nilipeleke wapi, nilisoma mada ya mazoezi na nikaona tu tangazo la jinsi ya kupunguza mikono minene kwa wanawake lakini sikuona maelezo ya kutosha ya nini hasa mtu anatakiwa kufanya.
Nilijitahidi sana lakini sikuona, naomba msaada wako wa maelekezo ya kufanya hayo mazoezi ya kupunguza unene wa mikono, kwani ni tatizo linanikosesha raha na ninashindwa hata kuvaa nguo za mikonoo mifupi au wazi kutokana na unene wa mikono yangu.
Mimi bado ni mdogo naomba msaada wako dada dinah, nategemea majibu yatakayo nipa furaha na nakuomba samahani kwa usumbufu."
Dinah anasema: Habari ni njema tu mdogo wangu, hujambo wewe? Asante kwa mail yako, sasa unaposema wewe bado mdogo unamaanisha ni chini ya miaka 21? Ni kweli kuna mazoezi ya kupunguza unene wa mikono kama unene wa mikono hiyo umesababishwa na unene wa sehemu nyingine ya mwili wako.
Mf kama sehemu nyingine ya mwili wako ni nyembamba lakini mikono pekee ndio minene basi utambue kuwa hili ndio umbile lako lakini kama sehemu ningine za mwili wako ni nene kama vile mapaja, kifua, kiuno, makalio n.k. ni wazi kuwa unene wa mikono utapungua ikiwa sehemu nyingine za mwili wako zitapungua yaani mwili wako ukipungua basi na mikono nayo itapumngua kwani ni sehemu ya mwili wako.
Inawezekana kabisa kuwa umeridhika na unene wa sehemu nyingine za mwili wako isipokuwa mikono....kumbuka huwezi kupewa/pata vyote hivyo kama unapenda maeneo mengine yabaki kama yalivyo itakubidi ukubali unene wa mikono yako na kuipenda kama ilivyo.
Kama asili yako (umbile lako) ni juu mkubwa ni wazi mikono yako itakuwa mikubwa tu, lakini bado unaweza kuifanya ipendeze nakuvutia na ukubwa wake sio unene tena kwani ukifanya mazoezi ya kupunguza unene/mafuta ukubwa wa mikono yako utakuwa umejengwa na misuli zaidi ya mafuta.....hivyo basi miko yako itakuwa firm na kujirudi kiasi nahivyo wewe unaona kuwa imepungua.
Ukiniambia umri wako then nitakuelekeza namna ya kufanya mazoezi ya kukaza misuli ya mikono yako ili kuepuka ukomavu, mana'ke ukifanya mazoezi haya wakati bado mwili wako unabadilika (chini ya miaka 21) ni wazi yatakufanya uonekane mkomavu.
Nasubiri jibu kutoka kwako...
Asante.
No comments:
Post a Comment