Tuesday
Naomba Ufumbuzi wa Haraka nisimpoteze Mpenzi!
Sunday
Romance kuisha
Nimevumilia tofauti zake kwa Ex, ila hili lanishinda...
Jamani nimeshawishika kukuchagua wewe kama msaada kwangu, umri wangu ni miaka 29ti mwenye jitihada sana katka maisha. Kinachonikatisha tamaa ni mpenzi wangu ambae simuelewi kama ana ugonjwa au la, maana ni miezi tisa sasa hanifikishi kila tukianza kufanya mapenzi.
Hali hii aliyonayo mpenzi wangu hakuwepo awali, imejitokeza mwaka huu na sasa ni mwezi wa tisa anawahi kukojoa sekunde chache tu tangu tuanze tendo. Imefikia hatua ya kujichua mwenyewe na hata kufikiria kutoka nje ya uhusiano wetu ili niridhike kingono...so horrible!
Licha ya tatizo hilo nimekuwa nikivumilia tofauti alizonazo compared to my ex relations, ukweli ni kuwa he is not smart as my either he is romantic, nimejaribu kum-pimp atleast aweze kunivutia lakini habadiliki, yaani ni kama anapuuzia vile.
Tatizo ni uoga wa kumuacha kwani ataniona kama namkimbia kwa mapungufu aliyonayo kimwili na kikazi. Nisaidieni mwenzenu kwani nahisi nina mwanaume jina. Asanteni"
Nifuate ndoa nchi nyingine, niache ajira?-Ushauri
Nina mchumba wangu ambae tunataka kufunga ndoa, lakini nitakapofunga ndoa nitalazimika kuhama kutoka Nchi moja kwenda nyingine na kuacha ajira yangu.
Kinachonichanganya hasa ni suala la kuacha kazi, yaani mawazo juu ya hilo hunipa maumivu ya tumbo na huonga huniingia.
Naomba ushauri kutoka kwa yeyote aliyepitia hii hali katika maisha yake, asanteni"
Nahisi Bf hajali, je nifanye nini?
Monday
Mjamzito, Kazini Moto nyumbani hakuna mapenzi, Nifanyeje?
Hongera kwa kazi kubwa unayoifanya ya kutuelimisha, ubarikiwe sana. Mimi nina umri wa miaka 28, ni mama wa mtoto mmoja na kwa sasa ni mjamzito.
Dada Dinah ninapitia kwenye kipindi kigumu kwani baba mtoto hanijali kabisa yaani hajishughulishi kunisaidia kitu chochote na anapachukia nyumbani. Hana mapenzi na mimi na nimeacha kazi baada ya manyanyaso kazini.
Maisha yangu yamekuwa na huzuni kubwa, najiona nina bahati mbaya nasijui nifanyeje? Mume wangu hana muda wa kuongea na mimi, nashindwa hata kula chakula vizuri. Naombeani msaada wa mawazo na namna ya kumfanya mume wangu anijali na kunionyesha mapenzi kipindi hiki cha ujauzito."
Dinah anasema: Pole sana, kwakweli ni kipindi kigumu kwani sasa najua mtu unavyojisikia unapokuwa mjamzito. Ni ngumu kuamini mume anaweza kumfanyia mkewe vitendo hivyo.
Nashindwa kujizuia kuuliza maswali hili:-
Kabla hujashika Ujauzito huu wa pili mliwahi kujadili suala la kuzaa mtoto wa pili au mimba imetokea tu bila kupanga?
Mimi nakushauri uzungumze na Mama mkwe wako kuhusu tabia/vitendo vya mume wako na yeye anaweza kuzungumza na mwanae (lazima atamsikiliza mama yake) na wakati huohuo zungumza na mama yako mzazi wa ndugu yeyote wa karibu kutoka upande wako na wote kwa pamoja wanaweza kuitisha mkutano/kikao.
Ikiwa mumeo ataendelea na tabia yake baada ya kikao cha familia zote mbili, usilazimishe sana na badala yake wewe tafuta namna ya kurudi nyumbani kwenu/kwa wakwe (inategemea na taratibu za huko uliko olewa) kwajili ya mapumziko mpaka utakapojifungua.
Ujitahidi kula vizuri na kujitahidi kuondoa mawazo ili usiharibu afya yako na ya mtoto tumboni. Baada ya kujifungua utakuwa na nguvu ya kukabliana na mumeo uso kwa uso na kujaribu kurekebisha tofauti zenu.
Sasa hivi jitahidi ku-focus kwenye afya yako na afya ya mtoto alafu hayo mengine yafuate baadae. Mungu akutie nguvu, akupe amani na ujasili ili uweze kujifungua salama.
Kila la kheri!
Thursday
Nini cha kuzingatia siku ya kwanza?
Tuesday
Nikisema sina hela ananuna, busu, kumbatio ni tatizo, nimbadilishe vipi?
Pole na hongera kwa kutoa elimu kwa vijana wa kitanzania. Mimi ni kijana wa miaka 23 na ni muajiliwa wa kampuni moja hapa Tanzania, tatizo langu ni kutopata mpenzi anayejali na kuthamini hisia zangu .
Natamani kuwa na mpenzi anayeendana na mitazayamo yangu ya kimaisha, kwa sasa ninae mpenzi lakini ni mtu anayependa pesa zaidi, siku ukimwambia huna basi atanuna na wakati mwingine anasema kuwa anahisi humpendi.
Na mbaya zaidi huwa hapendi kutoka na mimi ila marafiki zake its okay na hata hugs and kisses huwa kwake ni tatizo.Niini nifanye niweze kumbadilisha au niachane nae na kupata yule anayeendana na hisia nizitakazo? kwamba tupendane na tuendane kwenye masuala ya kimaisha?
Kwasababu wakati mwingine nahisi kuwa labda nina mkosi na sitokuja pata chaguo la moyo wangu nitakae mpenda na yeye anipende na sio kupenda pesa zangu."
Asaliti ndoa yetu usiku asubuhi anaenda kuhubiri neno la Mungu-Nimfanye nini?
Kinachoniuma saaana huyo mwanamke aliekuwa akitoknae nilianza kumuhisia kipindi hatujafungandoa, kila siku nilikuwa nikiona msg zake akimtukana mtu fulani ila nikijaribu kumuuliza mume wangu anasema kuwa ni mambo tu ya kazini. Lakini kila nilipokuwa nikiona msg nahisi kusutwa!
Hivi sasa tuna watoto wawili na nilikuwa muamini zaidi mume wangu nakila ninapo shitukia ishu kuwa labda anatoka kusaliti ndoa yetu na kumhoji kama ni kweli, mume wangu anakasirika na kuniomba nipige magoti nisali na kuomba Msamaha.
Nilikuwa nikifanya hivyo na hata yeye kuomba pamoja nami huku maombezi yake yakiwa Mungu atupe tuweze kuaminiana. Hajawahi kupunguza mapenzi kwangu wala kuonyesha ila siku moja nimekamata msg nyingine nikajifanya mimi ni mume wangu na hapo ndipo nilipogundua mwanamke huyo anavyo enjoy na mume wangu.
Kinachoniumiza sana alikuwa akitumia rafiki yake huku mara nyingi nyingi kujifanya kuwa ni mgonjwa anahitaji kwenda hospitoli anadai asindikizwe na mume wangu kumbe ilikuwa njia yakumtoa tu. Akitoka asubuhi kusaliti ndoa yetu anahubiri Kanisani kama kawaida na huku akisukuma Injili.
Yaani nikifikiria hapo nahisi kumchukia, hata mida mingine sijisikii kumpikia kutokana na ahadi nyingi tele tele na huku akionya watu wengi kuhusu ndoa. Naombeni jamani mniambie nifanye nini kumsamehe sijamsamehe ila aliishaomba msamaha nakunieleza kuwa kila nililoligundua ni ukweli! ninaumia sana.
Nilimwambia asubiri nitampa jibu. Sasa mawazoni mwangu najiandaa na nikipata kazi nitamuacha kwani nikifanya uamzi mapema naweza kuumia sijuwi niko sahihi au nakosea?
Hii yote ni kwasababu hakuna njia nyingine ya kumuamini hasa pale anaponiambia yote "tumkabizi Mungu" nahisi hata hilo jina asiwe analitaja. Nikiwa mbali na yeye ninajihisi kufurahi nikimuona nahisi kujinyonga sasa jamani mnasemaje hapo naombeni ushauri wenu. Asante"
Monday
Naogopa mkewe asije kujua uhusiano wetu, nifanyaje?
Ila dada naogopa mke wake asije kujua, huwa namwambiai huyu mwanume lakini yeye ananipa moyo kuwa hilo halitotokea. Huyu mwanaume ananitunza vizuri tu na pia kaninunulia nyumba na full furniture. Nyumba hii iko mbali na anapoishi na familia yake.
Tatizo wakati ninapomuhitaji huwa simpati kwani unakuta muda mwingine yupo bisy na kazi au familia yake. Dada nifanye nini wakati nampenda sana?"
Dinah anasema:Natambua kuwa hii Post itawakera wengi, Mimi binafsi sikubaliani na tabia hii kwani kitendo cha kutoka na mume wa mtu ni Kosa kubwa. Lakini tukumbuke matusi na maeno makali hayatosaidia huyu dada kufanya uamuzi wa maana. Tafadhali mshauri kwa busara bila kum-attack huyu Binti.
Asante!
Sunday
Kitu kidogo tu anitishia kuachana, nimuache kweli au?-Ushauri
I hope upo pouwa sana and well, thanks for everything you have been taught us and may God Bless u always...
My name is (dinah kahifadhi jina) am Tanzanian but currently am in Malaysia studying, I am having a problem with my GirlLover and I completely dont understand her! My girllover lives in Tanzania and am here (in Malaysia). Every end of the year I go to Tanzania to see her, I have no other reasons for me to go there apart from seeing her.
Anapenda sana kunitishia kuniacha yaani kitu kidogo tu atanuna na kunitumia msg'z kama "maisha mema na usinipige simu wala kuni text" tena kwa kosa dogo sana ambalo liko juu ya uwezo wangu, kosa lenyewe ni kutopokea sms zake kwavile network ilikuwa inamatatizo.
Pia nikifanya kosa bahati mbaya basi atanuna wiki moja au mbili, yaani nisimsemeshe. Lakini yeye akifanya kosa kama nililofanya mimi na akiomba msamaha ni hapo hapo umsamehe na usimpomsamehe hapo on the spot ataanza kunitishia kuwa "basi kama huwezi kusamehe on the spot tuachane" na kosa hilo hilo nilikifanya mimi naweza kuomba msamaha kwa wiki mbili mfululizo lakini hanisamehei and it's annoying.
Nampenda sana na nimeshamtambulisha home na yeye ameshanitambulisha kwao na familia zetu ni friends lakini hii tabia yake inaniboa sana, pia hivi vitisho vyake vya "tuachane" vinanifanya nisisome kwa raha yaani performance inashuka.
Nampenda sana na I can't afford to loose her... sasa nifanye nini ili aache kunitishia hivo vitisho au njia ni kuachana nae na nikiongea nae sometimes anakubali kuendelea na mimi but kitu kidogo anarejea hiyo tabia.
Naomba ushauri jamaa, ni kuachana nae au njia ni ipi hasa?"
Niliolewa nikiwa nampenda wa zamani, nimuepuke vipi?
Kwa kweli napata tabu hebu nisaidie kwa hili; Mpenzi niliekuwa nae zamani nilimpenda sana lakini kwa bahati mbaya tukakosana. Sasa nimeolewa as you know ndoa hupangwa na Mungu lakini bado nampenda na huku nina mume what should I do kuepukana nae huyo wa zamani"?
Wednesday
Mpenzi hanijali, hanithamini tena,nifanyeje?
Kikubwa kinachonikera kwake ni kwamba hanijali tena, hanithamini wala haoni na mimi ni sehemu ya maisha yake,nasema hivyo kwa sababu kila ninapohitaji msaada wowote toka kwake hanisaidii kabisa.
Ukija katika suala la kugonoka jamani mimi mwenzenu naweza kaa hata mwezi mzima hajanigusa wala nini na tunalala kitanda kimoja kila siku na hata tuki sex yeye anafanya mradi yafike basi na si kutombana ili kila mmoja wetu aridhike nakumfurahia mwenzie.
Kingine, anachelewa kurudi nyumbani yeye ni mfabiashara k/koo na duka anafunga saa kumi na moja kamili ila mpaka afike nyumbani ni saa 3-4 au hata saa 5 usiku nimeshaongea naye lakini wala hanielewi kabisa.
Jamani naomba ushauri wako dada na wachangiaji wengine kwani nahisi kutokumpenda tena, mwenzenu nifanyeje ili tuwe na mapenzi kama walivyo wengine? Poleni kwa msg ndefu".
Tuesday
Miaka 10 kwenye uhusiano na mtoto moja bila ndoa, je nimuache?
Pole kwa majukumu na hongera kwa kuelimisha jamii. Mimi ni mdada nina miaka 32 toka Arusha. Nina uhusiano na mwanaume kwa muda wa miaka 10 na nimezaa naye mtoto mmoja.
Kabla ya kuwa na mimi huyu mwanaume alishawahi kuwa na wanawake tofauti na amezaa watoto wawili kila mmoja na mama yake.Katika uhusiano wetu tumefanikiwa kununua nyumba moja yeye alichangia hela nyingi kuliko mimi ila mimi niliifanyia ukarabati mkubwa, hati nilisaini mimi na alinikabidhi.
Nyumba hiyo ninaishi mimi na mtoto wangu, yeye anaishi nyumba nyingine na watoto wake hao wawili na huwa nafika hapo ila hajawahi kunikaribisha ndani wala kunitambulisha kwa watoto wake.
Alishawahi kunitambulisha kwa baadhi ya ndugu na rafiki zake na kwa staff wenzie ofisini. Huyu mwanaume amekuwa msaada sana kwangu na familia yangu, kwetu wanamfahamu kama baba wa mtoto wangu.
Mimi nataka kuachana na huyu mwanaume kwa sababu naona ananipotezea muda pamoja na kwamba ananisaidia. Ila kuna ndugu zangu wananishauri nisimuache. Mimi binafsi naona hayupo serious kwani angekuwa serious na mimi au kuwa na mpango na mimi sidhani kama angekaa nyumba tofauti na mimi.
Pili, muda wa miaka kumi ni mrefu sana kama angekuwa na mpango na mimi nadhani angenioa. Nimejaribu kuongea naye mara nyingi takribani miaka 6 sasa kuhusu suala la ndoa lakini kila siku jibu lake kuwa ana mipango anaikamilisha kwanza lakini haniweki wazi ni mipango gani hiyo.
Tatu, Pamoja na kwamba huwa anakuja kwangu na tunafanya mapenzi lakini si kivile na mara nyingi huwa nakuwa mpweke, kwa kifupi huwa anakuja anavyotaka yeye so nakuwa sipo uhuru na mapenzi.
Nne hakuna relation yeyote kati ya mtoto wangu na watoto wake yaani kwa kifupi mambo yake mengi haniweki wazi hizo ndio sababu ambazo zinanifanya niamue kuachana naye pamoja na kwamba ananihudumia kwa kila kitu.
Binafsi bado nampenda sana, tena kwa dhati ila kwa kweli nimechemsha kwa hilo. Nilishawahi kumwambia kuwa nimechoka na ninataka tuachane, aliumwa presha mpaka akalazwa. Toka nimekuwa na uhusiano naye sijawahi kuwa na mwanaume mwingine nje ya uhusiano wetu na nilishawakataa wengi kwa ajili yake lakini kwa sasa nimechoka.
Hofu yangu ni kuwa baada ya kuachana itabidi tuuze hiyo nyumba na nitahangaika na makazi mimi na mwanangu. Pia nahofia usalama wake maana bado atabaki kuwa baba wa mtoto wangu.
Ninaomba wana-blog wenzangu mnishauri katika hili ili niweze kuchukua maamuzi sahihi. Samahanini sana kwa maelezo yangu marefu, Madada wa Arusha".
Monday
Wazazi na jamaa wanasema nitafute msomi kama mimi, does it matter?
Mimi na boyfriend wangu huyu tunapendana sana, na pia namsaidia mambo mengi sana ya kifedha na hata yakimaisha (nikimaanisha ushauri), kwani kwa bahati mbaya hakufanikiwa kwenda shule kutokana na matatizo ya kifamilia, elimu yake ni ya kidato cha nne.
Hiyo yote ni kutokana na Wazazi wake kutojishughulisha nae tokea zamani, hawakujali suala la elimu, kutokana na hili alipitia maisha magumu saana kiasi cha kumfanya aanze kufanya dili mbalimbali ili apate hela za kuendesha maisha, na pia aliweza hata kupanga chumba akawa anaishi mwenyewe na kununua assets mbalimbali za nyumba.
Kwa ujumla ni mtu ambae anajipenda na anapenda maisha mazuri tatizo ni uwezo tu na kazi ya maana ambayo itakidhi mahitaji yake yote. Pamoja na hili anasaidia hata ndugu zake pia. Hivi karibuni mambo hayamuendei vizuri kabisa japo hajakata tamaa.
Anajitahidi hivyo hivyo, kwa sababu hii mara nyingi ananiomba mimi nimsaidie kifedha kwa sababu nampenda inabidi nimsaidie nimpe hela za matumizi na muda mwingine hata za kulipia nyumba. Na fanya hivyo kwasababu nampenda, na yeye ananipenda, yupo tayari hata kesho kuishi na mimi.
Swali langu lina kuja hivi, mimi nimesoma nategemea kupata master degree yangu miezi kadhaa ijayo, kwa ujumla namshukuru Mwenyezi Mungu ninamahitaji yangu yote, ila tatizo huyu boyfriend wangu, hajasoma ila ni mtu ambaye anajitahidi hivyo hivyo sio mvivu anapenda maisha mazuri, ila watu wanasema hatutadumu kwa muda mrefu kutokana na tofauti zetu, je mnasemaje kwa hili?
Swali la pili ni hili, tumejuana kabla hata sijaanza chuo, kwa kipindi chote hicho tulikuwa pamoja mpaka sasa nategemea kumaliza masters tupo pamoja, na pia ndio boyfriend wangu wa kwanza sijawahi kuwa na mwingine, je mnanishauri vipi hapa?
Kwani baadhi ya watu wananiambia nitafute mtu aliesoma kama mimi kwani tutaelewana zaidi kimaisha. Kuhusu suala la wazazi, wazazi wake wananipenda saana, ila tatizo lina kuja upande wa wazazi wangu wanataka nitafute msomi mwenzangu, ila kwa mimi siko tayari kwani nampenda huyu nilionae.
Kwasasa haijalishi kwani nipo tayari kumsaidia kwa lolote ili tu awe na maisha mazuri. Je hii ni sahihi? Naombeni ushauri wenu, je kuna future hapa kweli au tunaforce mambo tu kwa muda kwani yatakuja nizidia huko baadae kama asipo pata kazi au biashara ya maana.
Naombeni ushauri wenu na mtazamo wenu.
Dada K".
Dinah anasema:Asante mdogo wangu, natumaini kuwa umefanyia au unaendelea kufanyiakazi maelezo mazuri kutoka kwa wachangiaji, yasome yote kisha uyachanganue alafu uchanganye ndio ufanye uamuzi.
Amemdis mdada aliekuwa nae kwa miaka 4, je atafanya the same kwangu?
Naomba unishauri kitu, mimi nina boyfriend wangu ambaye ametoka kwenye mahusiano na msichana waliedumu naye miaka 4.Hofu yangu je atanidis na mimi kama alivyomuacha huyo mwingine baada ya muda mrefu?
Sasa hivi simuelewi-elewi kwani anapenda sana kushika simu yangu na kusoma sms zangu tena wakati mwingine sms inaingia hata mimi sijaisoma tayari yeye anasoma.
Juzi nilienda kulala kwake lakini hakuonyesha kunijali, je ni dalili kuwa atakuwa na mwingine? je niachane nae? au niendelee nae lakini nisiwe naenda kwake?
Nilijaribu kumuuliza kama anamalengo yeyote na mimi,akasema ndioa anamalengo mazuri. Hiyo juzi nilipokwenda kwake nilimfulia nguo na kwa bahati mbaya zikaibiwa.
Nimemtumia sms lakini hajanibu hadi this time, je na mimi nikae kimya au nimtafute? Nitashukuru nikipata ushauri wako dada na nitaufanyia kazi ushauri wako.Please usiniweke kibarazani.
Kazi njema, be blessed"
Dinah anasema:Asante sana kwa mail yako, namshukuru Mungu ananipa nguvu kila siku.
Wengi wetu tunapoingia kwenye mahusiano mapya ni wazi tumeacha au tumeachwa. Kuachwa kwa mtu hakukuhusu wewe,japokuwa ni muhumu kujua nini kilitokea au kusababisha mpaka wakaachana ili ikusaidie wewe kuepuka au kujua namna ya kukabiliana na same tatizo kama litajitokeza.
Kwa kawaida humchukua mtu yeyote muda mrefu kuwa tayari kupenda tena na kujenga uhusiano mpya baada yakutoka kwenye uhusiano wa zamani.
Sina hakika mpenzi wako amekuwa na wewe baada ya muda gani tangu aachane na huyo mpenzi wake wa awali, lakini kutokana na ulichokisema hapa(vitendo vyake) inaonyesha jamaa bado hajapona maumivu ya mapenzi aliyopata kabla yako.
Kutokana na maelezo yako ni wazi kuwa unaharaka ya kufunga ndoa na wakati huohuo unaogopa kuachwa ukiamini kuwa "kama aliacha yule, hatamimi ataniacha". Sio lazima iwe hivyo.
Unapoingia kwenye uhusiano unatakiwa kuzingatia nini utawekeza kwenye uhusiano ili uhusiano na mpenzi wako kuwa Imara na uliotawaliwa na mapenzi. Huitaji kuishi kwenye hofu ya kuachwa au kufikiria maisha yake kabla yako!
Kosa dogo ulilofanya ni kuanza kwenda nyumbani kwake na kumfanyia shughuli kama vile wewe ni mchumba/mkewe, mwanaume hafuliwi wala kupikiwa mara kwa mara ikiwa uhusiano bado ni mchanga, unaweza kumsaidia vijishughuli kwa mapenzi lakini isiwe kila weekend, utakuwa unamugopesha na atakudhania kuwa unataka kufanya nyumbani kwake ni kwako.....hii can scare him off.
Vilevile hukupaswa kumuuliza malengo yake kwako na badala yake ungetumia mbinu nyingine ili kujua msimamo wake juu ya uhusiano wenu kama wapenzi, kumbuka uhusiano unajengwa na watu wawili.
Hawezi kuwa na malengo kwako kwani wewe sio mwanae bali ni mpenzi wake, lakini anaweza kuwa na malengo fulani juu ya uhusiano wenu na wewe unapaswa kuwa na malengo fulani kwenye uhusiano huo ila nina uhakika yeye hajawahi kukuuliza unamalengo gani kwake....has he?
Huyu mwanaume inaonyesha kuwa aliachwa(wanaume wengi hawapendi kusema waliacha kwa vile ni aibu kwao)kutokana na kitendo chake cha ku-withdraw na kuangalia-angalia simu yako ni dalili tosha kuwa jamaa alitendwa au niseme alikuwa cheated na hivyo inakuwa ngumu kukuamini na ndio maana anafuatilia sana SMS na simu ili asije umizwa tena.
Kitendo cha yeye kutokukujali ulipokuwa kwake inawezekana alikuwa amechoka au anamawazo(kama ulikuwa unataka ngono), na mwanaume anapokuwa ktk hali hiyo huwa ngumu sana kungonoka lakini kwa kumsaidia (kuzungumza nae na kumpa matumaini, kumpoza, kumliwaza n.k.)anaweza kuwa sawa na tendo likafanyika.
Nini cha Kufanya: Mtumie ujumbe au mpigie simu na kumuomba msamaha kwa kusababisha nguo zake kuibiwa. Najua kosa sio lako lakini omba radhi kwa hilo, kwani anaweza kuwa na hasira kuwa usingezifua zisingeibiwa hasa kama uliamua kufua bila yeye kutaka ufanye hivyo....hilo moja.
Pili, mdogo wangu punguza safari za kwenda kwake na badala yake mpigie zungumza nae kwa simu na kupanga mihadi ya kukutana mahali au kwenda kutembea sehemu na ikitokea anakualika kwenda kwake baada ya matembezi au chakula then nenda kwake lakini usilale unless anaomba ufanye hivyo.
Unapokuwa huko kwa Jamaa usijipe shughuli kama vile wewe ni mchumba/mkewe tayari. Unaweza kuandaa labda Chai asubuhi na kutandika kitanda kwa vile mmekitumia, pia unaweza kusafisha vifaa ulivyotumia lakini sio unafanya usafi nyumba nzima na kumfulia juu.
Muonyeshe mapenzi ya dhati ulionayo bila kuhoji malengo yake, hakikisha unampatia ile hali ya kukuamini kuongeza mawasiliano Mf:kwa kumueleza mipango yako ya siku na kuomba yeye akueleze mipangilio yake ya wiki au siku na hivyo kujua lini mtakutana tena kama wapenzi n.k
Mfanyie mambo yakingono na ya kimapenzi (nje ya kitanda) na kitabia ambayo unauhakika hakuna mtu amewahi kumfanyia.....njia rahisi yakujua ni kuwa wazi kwake na kumhoji kimahaba na yeye atakuambia anapenda Binti mwenye tabia gani, nini hawaji kufanya lakini angependa kujaribu/kukifanya kingono n.k.
Acha kuwa na haraka za kuolewa, furahia uhusiano wako kama ulivyo na hakikisha unafanya mambo ya kimapenzi ili atangaze ndoa yeye mwenyewe bila kusukumwa na maswali yako kuhusu malengo yake.
Kumbuka ndoa nzuri ni ile inayotokana na uamuzi wa watu wawili wanaopendana kwa dhati na wenye lengo la kuishi pamoja maisha yao yote yaliyobaki.
Kila la kheri.
Sunday
Ndoa ni Mwaka huu! Mwenzangu anatereza na mdada nimjuae!
Naitwa M*(Dinah amehifadhi jina) na ninaishi Sinza,
Kwa upande wangu sina swali ila ninapenda kupata ushauri kutoka kwako.
Nina umri wa Miaka 30 na nipo katika uhusiano kwa takribani miaka miwili na ninatarajia kufunga ndoa mwezi huu wa tano.
Tatizo linakuja kwa huyu mwenzangu anajihusisha kimahusinao na dada mmoja ambae namfahamu na kila nikimuuliza anakataa lakini Ofisini kwa huyu mwenzangu wanafahamu uhusiano wao, yeye na huyo mdada mwingine.
Sasa nashindwa nifanye nini na nikangalia ndoa ipo karibu,
naomba ushauri wako/wenu.
Hivi sasa amebadirika sana kitabia."
Nimeshika Mimba, Je nitamwambiaje mama?
mimi ni msichana wa miaka 25, bado nipo chini ya himaya ya bi mkubwa, nimepata mimba na siku zote nasema sitatoa mimba. Sema bi mkubwa wangu nitamueleza vipi? Naombeni msaada jamani tafadhali dada dinah na wachangiaji wengine kwani nipo njia panda.
Boyfriend yeye yu tayari kuwa baba japo wote bado twamalizia masomo si fikirii sana juu ya yeye kwa sasa, yeye si ngumu kujadiliana naye isipokuwa mama yangu, sijui nianzie wapi kumwambia??? msaada tafadhali tafadhali...".
Monday
Mume wangu anatereza nje na "dada" zake na kuzaa ovyo, nifanye nini?
Wednesday
Baada ya kutendwa ndoani, nachukia wanaume wote....nifanyeje?
Monday
Haya nimerudi full time, Shukrani za dhati kwa ushirikiano na uvumilivu!
Thursday
Nianzie wapi Kisheria kumtaliki mume wangu?-Ushauri
Monday
Uhusiano una Mwaka, Ex wa Mpenzi amejifungua mtoto wake mwaka huu! Nifanyaje?
wa mwaka na miezi mitatu hivi. Nampenda sana mchumba wangu na yeye naamini ananipenda.
hiyo mimba kapata wakati ndio tunaanza uhusiano wetu.
hajaniambia nitamuacha, amesema yeye ananipenda mimi na anataka niwe mke wake. Hapa nilipo nimechanganyikiwa mbaya zaidi badonampenda sana huyu kaka na sijui nifanyaje!
Saturday
Nifanye nini ili mimi na mpenzi tukojoe pamoja?-Ushauri
Sunday
Nifanye nini ili nami nipate raha na Utamu wa Kungonoka?
Mimi ni mwanamke wa miaka 29 na nimeanza kujihusisha na masuala ya kimapenzi na ngono na mwanaume wa kwanza nikiwa na miaka 26, tulikuwa tunakutana mara mbili kwa mwezi na hivyo hatukuwa na muda wa kungonoana vizuri. Mwanaume huyu alikuwa anajipendelea yeye kwani hakuwa na communication na mimi alikuwa anataka anavyotaka yeye.
Sasa hivi nimepata mwanaume mwingine na muda wa kuwa nae na kufanya mapenzi ni mwingi zaidi kuliko awali ila tatizo langu kubwa ni kuwa sijawahi hata siku moja kusikia raha ya kufanya tendo kama ninavyosikiwa kutoka kwa wenzangu au kwako Dinah hasa pale mahali ulipoandika kuwa "mnaweza kukojoa pamoja".
Kukojoa kwangu ni mpaka anichezee K kwa muda mrefu wakati mwingine huwa namuonea huruma kwani nahisi kama vile namchisha na hivyo naishia kumwambia "tayari nimefika" kumbe bado. Nashukuru Mkaka huyu najali na huwa hapendi kuacha mpaka ahakikishe nimekojoa ilandio hivyo tena.
Naomba ushauri kutoka kwenu kwenye haya mawili: (1)-Nifanye nini ili na mimi angalau nifurahie ngono kama wenzangu?
(2)-Niifanye nini ili niweze kumaliza na mwenzangu kwa wakati mmoja?
Asanteni.
Natafuta njia ya kushika na kubemba mimba-Nifanyeje?
Vilevile nimejaribu kutumia dawa za Kienyeji lakini sijafanikiwa kushika mimba mpaka leo, je kuna njia nyingine yeyote inayoweza kunisaidia kushika mimba tena bila kunywa dawa za Clomid? Naomba mnisaidie....
Nimefurahi sana kupata email yako.
Asante."
Mume Mzinzi lakini hataki kunipa Talaka, nifanyaje?
Wakati huo mie nikawa niko field Airport tukawa tunaishi pamoja kam amume na mke, visa vikaanzia hapo. Mwanaume akawa anapigiwa siku na wanawaka mara akanza kuwa anarudi nyumbani asubuhi. Ikafikia hatua ya kunifukuza pale na kuanza kubadilisha wanawake dada dinah.
Vitu vilivyoko pale nyumbani vingi tulishirikiana kama wapenzi kwakweli niliumia sana kwasababu nilikuwa nampenda. Basi tulitengana nikarudi kwetu na nikapata ajira baadaya Field. Baada ya miezi kama sita hivi akaja kunibembeleza huku akiniahidi hatarudia tene na amekuja kwa ajili ya kunioa.
Nilikubali dada, tukafunga ndoa na tukabahatika kupata mtoto wa kike, ndungu zangu wakanisaidia kunishughulikia tukapata nyumba ya NHC naye pia alitoa pesa zake ila hati zote ziliandikwa jina langu.
Kama ilivyokuwa kabla ya ndoa akaanza visa tena, sasa akawa ananitukana matusi makubwa mbele ya h/girl mpaka majirani wanasikia mara aniambie "wewe mwanamke gani mie sinimekusaidia tu kukuoa", mara anipige, anarudi Alfajiri akiwa amelewa.
Nimejaribu kumwambia nataka Talaka yangu hataki kunipa, sasa nilichoamua mwezi wa tatu sasa sitaki kabisa kushare nae love. Kinachonikera kwasasa ni kwanini hataki kunipa Talaka yangu aendelee kufanya mambo yake!
Naombeni mnishauri, nitaipataje Talaka yangu kutoka kwa huyu mume ili na mimi niwe huru?
Asanteni.
Saturday
Je kuna namna ya kuamua jinsia ya mtoto?-Msaada
Naomba ushauri kutoka kwa mtu yeyote mwenye utaalam wa kujua jinsi ya kuamua kupata mtoto wa kiume au wa kike. Cha muhimu ni kujua wakati gani nikikutana na mke wangu atakuwa na mimba ya mtoto wa kiume au wa kike?
Asanteni.
Friday
Nipo na Mpenzi alie-cheat on her X with Me, je anaweza kuni-cheat na mimi?
Mimi ni kijana mwenye miaka 33, nina mpenzi niliyekutana naye mwaka mmoja uliyopita na tumeanza kuishi pamoja tangia mwezi wa kumi mwaka 2010. Nina maswali mawili. Mpenzi wangu alishawahi ku-cheat na mpenzi wake wa zamani ambao waliokuwa pamoja miaka 7.
Kwa maelezo yake miaka miwili ya mwisho mpenzi wake wa zamani alikuwa anamdangaya mambo mengi na akapoteza trust kwake, mapenzi yakapungua na kwa kipindi hicho cha miaka miwili wakawa wanaishi nchi tofauti ila walikuwa wanakutana mara moja kwa mwaka kwa mwezi mmoja.
Swali la kwanza;Anadai alim-cheat jamaa yake na mimi na ndio ukawa mwisho wa mahusiano yao. Hivi mwanamke kama huyu anaweza kuaminika kwa mahusiano ya kudumu na mimi?
Mimi binafsi niko commited kuwa naye bila ya kuwa na mwanamke mwingine ila nahisi kama alivyofanya kwa wa zamani yanaweza kunitokea na mimi. vipi maoni yako na wachangiaji wengine kuhusu hili?
Swali la pili: Ninamridhisha mpenzi wangu huyu kwa ratio ya 6:10 yaani kwa kufanya mapenzi mara 10 mara 6 anakuja. Swali ili mwanamke kuridhika na mwanamme kabisa anapenda afike mara zote kumi? yaani kila mkifanya mapenzi lazima aridhike(akojoe)? ninakuwa sina furaha hizo siku ambazo hafiki.
Je mwanamke akiji-stimulate Clitoris akiwa on top huku uki-pump na akafika, itatafsiriwa kama amekuja kwa Vaginal orgasm au Clitoris Orgasm? mimi binafsi napendelea aje kwa Vaginal Orgasm zaidi.
Pia,Je mwanamke anaweza kufurahia ngono ukiishi naye zaidi ya miaka 3 sawa na jinsi mlivyokuwa ndani ya mwaka mmoja? je hamu ya mapenzi itapungua? haitasababisha kutamani new adventure?
Asante dada Dinah".
Sunday
Nilitalikiwa Kisa Usomi, sasa nimepata mpya lakini....Ushauri!
Mimi ni msomaji na mfuatiliaji wa blong yako, shortly I like it and I you as well. Nina 30years nafanya kzi kama Mhasibu Ofisini kwa mkuu wa nchi hii! Dinah tatizo langu ni kutaka ushauri kuhusiana na mwanaume nilie nae, lakini kabla naomba nikupe hadithi ilivyokuwa.
Nilipokuwa na 25yrs niliolewa na mwanaume wa Kiislam kama mimi na nikaenda Chuo soon after ndoa! Baada ya kuanza chuo ikawa ni tatizo kwa wifi zangu na Baba mkwe that kwanini nisome kabla ya kuzaa alafu pia mume wangu ni Form 4? Kwa nini nimpite kielimu?
Tatizo likandelea na likawa kubwa, Baba mkwe alimwambia mwanae achague moja a Divorce au la yeye sio baba yake. Nilipokuwa mwaka wa pili mume wangu akanishauri niache chuo nami nikakubali lakini after 2 months mama yangu akaja juu kwanini niache chuo kisa shinikizo la baba mkwe?
Nikaenda kwa mshauri wa wanachuo Chuoni for ushauri, yeye ndio akanishangaa na kuiomba nirudi Chuoni ! In a dilema nikarudi chuo na within a week wifi yangu akaniletea Talaka Chuoni ! Nusu nijiue kwa kuchanganyikiwa ila kwa sababu ni Muislam tena safi sikufanya hivyo!
Niliumia kwasaabu yeye ndio alikuwa mwanaume wangu wa kwanza na sikuhitaji mtu mwingine tena maishani mwangu! Maisha yakapita na nikamaliza Chuo salama na kuanza kazi. Siku moja nikakutana na Ex baba mkwe akiwa na shida fulani, kwenye maongezi akaniambia "mwenzio anakuhitaji tena na bado hajaoa".
Mimi nikamsaidia shida yake bila kumjibu lolote, nilimsaidia kama binadamu lakini roho iliniuma sana kwa kusikia habari kuhusu Ex hubby wangu. Kwa bahati mbaya Baba mkwe alifariki Dunia mwaka 2009 na my Ex hubby akaja kutaka turudiane lakini mimi nikakataa.
Akaanzakunifanyia fujo wherever he sees me! One night nilikutana nae wakati narudi kutoka Kitchen party alinitolea Bastola , thanks God alikamatwa na kuswekwa rumande for a long time !Niliapa siitaji tena mwanaume, ila watu na wazazi hawakukubaliana na mimi , then nikaamua kuwa na mtu ingawa nilikuwa naogopa sana!
Sasa tatizo ni kitandani, yaani kuwa zaidi ya mara kumi nilizojaribu kuwa nae kitandani akitaka kugusa tu basii "kashacheka", akijitahidi na kusimamisha tena bado anaceka kabla hajagusa. Kaenda kwa daktari, kajaribu mazoezi , kasoma article zako nk ! imeshindikana !
NIFANYEJE? Je niachane nae na kusubiri mwingine au nivumilie?
jemmy, DSM "
Nampenda Mdada alienizidi miaka 9, je naweza kuoa?-Ushauri
Sijamtamani kingono but I feel that I am in love with her. Hajawahi kuolewa na wala hana mtoto. Bado sijamweleza nia yangu ya kutaka tuhame kutoka kwenye urafiki tulionao kwenda kwenye uhusiano wa kimapenzi. Kwasasa mimi ni mwanafunzi wa mwaka wa tatu chuo kikuu hapa Tz, mwenzangu yeye ni mwalimu.
Tumekuwa pamoja kama marafiki kwa mwaka mmoja sasa. Urafiki wetu ni zaidi ya urafiki kwani tushafanya romantic talk/romance kwa njia ya simu. Naogopa kumweleza nia yangu kwani nahofia kuumiza hisia zangu ikiwa atanikatalia.
Moyo wangu unapata faraja na mateso juu yake. USHAURI ninaoomba kwako dada Dinah na wanablog wengine ni, Je kuna athari zozote yinazoweza kujitokeza kutokana age gap iliopo ikiwa tutaoana?
Na je nimweleze nia yangu au nifute wazo hilo? Wanawake mnalichukuliaje swala la kuolewa na mume mdogo kuliko mke kwa gap kubwa? NAOMBENI MAWAZO YENU NA HEKIMA ZENU. Facts are sacred, opinion are welcome and ideas are respected.
I love u All,
NB. Kilichonivutia kwake ni akili yake iliyokomaa, upendo alionao juu yangu na uelewa mkubwa alionao. Sura huwa si kigezo cha muhimu sana kwangu".