Thursday

Nini cha kuzingatia siku ya kwanza?

"Habari za asubuhi dada Dinah, pole na kazi. Nilikuwa naomba mnisaidie mawazo yenu. Mimi ni mwanamke ambae nasoma Chuo kwa sasa na nina maswali yafuatayo:-




1-Sijawahi kufanya tendo hata sikumoja na nina hamu kweli ila tatizo naogopa, naomba masaada.




2- Je! nitakapoamua kufanya ni mambo gani ya kuzingatia kwenye ile siku ya kwanza maana sijui kitu.




3-mambo ya kitandani sijui kabisa, naomba mnipe mastaili ya ukweli mpaka mwenyewe achanganyikiwe.




4-la mwisho da Dinah kama unaweza kunisaidia picha za watu wanafanya majambozi hapo utakuwa umenisaidia.




Kazi njema"

Tuesday

Nikisema sina hela ananuna, busu, kumbatio ni tatizo, nimbadilishe vipi?

"Hi da Dinah

Pole na hongera kwa kutoa elimu kwa vijana wa kitanzania. Mimi ni kijana wa miaka 23 na ni muajiliwa wa kampuni moja hapa Tanzania, tatizo langu ni kutopata mpenzi anayejali na kuthamini hisia zangu .



Natamani kuwa na mpenzi anayeendana na mitazayamo yangu ya kimaisha, kwa sasa ninae mpenzi lakini ni mtu anayependa pesa zaidi, siku ukimwambia huna basi atanuna na wakati mwingine anasema kuwa anahisi humpendi.



Na mbaya zaidi huwa hapendi kutoka na mimi ila marafiki zake its okay na hata hugs and kisses huwa kwake ni tatizo.Niini nifanye niweze kumbadilisha au niachane nae na kupata yule anayeendana na hisia nizitakazo? kwamba tupendane na tuendane kwenye masuala ya kimaisha?



Kwasababu wakati mwingine nahisi kuwa labda nina mkosi na sitokuja pata chaguo la moyo wangu nitakae mpenda na yeye anipende na sio kupenda pesa zangu."



Asaliti ndoa yetu usiku asubuhi anaenda kuhubiri neno la Mungu-Nimfanye nini?

"Mimi ni mwanamke ambae niko kwenye ndoa miaka minne sasa. Ila ninatatizo naomba mnipe maoni na ushauri. Mume wangu ambae nilimpenda kupitiliza nimegundua amekuwa akitoka nje ya ndoa yetu pale nilipoanza kumufatilia sana ingawa alikuwa mjanja sana.



Kinachoniuma saaana huyo mwanamke aliekuwa akitoknae nilianza kumuhisia kipindi hatujafungandoa, kila siku nilikuwa nikiona msg zake akimtukana mtu fulani ila nikijaribu kumuuliza mume wangu anasema kuwa ni mambo tu ya kazini. Lakini kila nilipokuwa nikiona msg nahisi kusutwa!



Hivi sasa tuna watoto wawili na nilikuwa muamini zaidi mume wangu nakila ninapo shitukia ishu kuwa labda anatoka kusaliti ndoa yetu na kumhoji kama ni kweli, mume wangu anakasirika na kuniomba nipige magoti nisali na kuomba Msamaha.



Nilikuwa nikifanya hivyo na hata yeye kuomba pamoja nami huku maombezi yake yakiwa Mungu atupe tuweze kuaminiana. Hajawahi kupunguza mapenzi kwangu wala kuonyesha ila siku moja nimekamata msg nyingine nikajifanya mimi ni mume wangu na hapo ndipo nilipogundua mwanamke huyo anavyo enjoy na mume wangu.



Kinachoniumiza sana alikuwa akitumia rafiki yake huku mara nyingi nyingi kujifanya kuwa ni mgonjwa anahitaji kwenda hospitoli anadai asindikizwe na mume wangu kumbe ilikuwa njia yakumtoa tu. Akitoka asubuhi kusaliti ndoa yetu anahubiri Kanisani kama kawaida na huku akisukuma Injili.



Yaani nikifikiria hapo nahisi kumchukia, hata mida mingine sijisikii kumpikia kutokana na ahadi nyingi tele tele na huku akionya watu wengi kuhusu ndoa. Naombeni jamani mniambie nifanye nini kumsamehe sijamsamehe ila aliishaomba msamaha nakunieleza kuwa kila nililoligundua ni ukweli! ninaumia sana.



Nilimwambia asubiri nitampa jibu. Sasa mawazoni mwangu najiandaa na nikipata kazi nitamuacha kwani nikifanya uamzi mapema naweza kuumia sijuwi niko sahihi au nakosea?



Hii yote ni kwasababu hakuna njia nyingine ya kumuamini hasa pale anaponiambia yote "tumkabizi Mungu" nahisi hata hilo jina asiwe analitaja. Nikiwa mbali na yeye ninajihisi kufurahi nikimuona nahisi kujinyonga sasa jamani mnasemaje hapo naombeni ushauri wenu. Asante"



Monday

Naogopa mkewe asije kujua uhusiano wetu, nifanyaje?

"Thanxs dada dinah kwa ushauri unaotupa wanawake wenzio. Ila dada naomba ushauri wako pamoja na wachangiaji wengine. Mimi nina mahusiano na mume wa mtu na nampenda sana naye ananipenda sana na pia ndio mwanaume wa kwanza kwangu.

Ila dada naogopa mke wake asije kujua, huwa namwambiai huyu mwanume lakini yeye ananipa moyo kuwa hilo halitotokea. Huyu mwanaume ananitunza vizuri tu na pia kaninunulia nyumba na full furniture. Nyumba hii iko mbali na anapoishi na familia yake.

Tatizo wakati ninapomuhitaji huwa simpati kwani unakuta muda mwingine yupo bisy na kazi au familia yake. Dada nifanye nini wakati nampenda sana?"

Dinah anasema:Natambua kuwa hii Post itawakera wengi, Mimi binafsi sikubaliani na tabia hii kwani kitendo cha kutoka na mume wa mtu ni Kosa kubwa. Lakini tukumbuke matusi na maeno makali hayatosaidia huyu dada kufanya uamuzi wa maana. Tafadhali mshauri kwa busara bila kum-attack huyu Binti.
Asante!

Pages