Wednesday

"Atatembea sana lakini at the end atarudi kwangu" Ukweli..

Mpenzi wako iwe ni mwanaume au mwanamke siku zote anakupa wakati mgumu lakini wewe unamvumilia, inafikia wakati anatoka nje ya ndoa/uhusiano wenu na kujakukuomba msamaha wewe unasamehe kwa vile tu labda unampenda, unawatoto nae na usingependa watoto kumpoteza baba/mama yao au kwenda kulelewa na mtu mwingine ikiwa utamtaliki/acha mpenzio.

Umewahi kujiliza kwanini siku zote akikosa (wakati mwingine anakuacha kabisa) lakini baada ya muda anarudi kwako mbio akikulilia na kuomba misamaha yote kwa kuhapia Miungu yote ajuayo na kukupa ahadi lukuki ili uendelee kuwa nae?

Mpenzi/mwenza mume/mke kama kweli anakupenda au nisema anakupenda kwa dhati na kukuthamini hawezi kwenda kulala nje na watu wengine na pengine kukuacha kabisa kisha ya kimshinda anarudi kwako na wewe kama juha unadhani huko ndio kupedwa, kwamba hapati "penzi" kama lako huko nje ndio mana kila wakati anarudi.

Endelea hapa

Ukweli ni kuwa mpenzi huyo anafanya hivyo kwa vile anajua wewe unampenda kwa dhati na huwezi kumuacha au kumkataa hata akuumize vipi, anahisi kuwa-secured (sio penzi) mikononi/ubavuni mwako...kumbuka usemi usemao "mpenzi akijua unampenda sana anakusumbua" hasa akiwa hana mapenzi na wewe bali yuko na wewe kwa sababu zake binafsi japokuwa alitumia au anatumia neno "nakupenda" n.k.


Sote tunatambua kuwa kuna wakati tunahitaji "mapumziko" kutoka kwenye mahusiano yetu ya kimapenzi /wenza wetu kutokana na uzito wa matatizo kikazi au kimaisha, kuna wakati mtu unahisi kwamba unataka kuwa mwenyewe bila kelele za watoto au maswali kutoka kwa mpenzi au hata "kupetiwa-petiwa" (hasa kwa wanaume pale mambo yao kiuchumi hayaendi vema).

Hili likitokea(ni tofauti ) haina maana kuwa hupendwi bali mwenzio yuko ktk wakati mgumu akifikiria jinsi ya kuilinda familia yake ikiwa ni pamoja na wewe mpenzi/mkewe na mara zote mwanaume huyo ambae anakupenda kwa dhati hatolala na mwanamke mwingine yeyote mpaka kipindi cha "mpito" kipite then atarudi kwako na kuomba radhi kwa kujiweka mbali na wewe na hata kwenda kwa kaka/rafiki yake kupumzisha akili na kupata maoni ya "kiuanaume" ambayo wewe mama huwezi kumpatia.

Hivyo wewe kama mwanamke ni vema ukaondoa hiyo kasumba au imani kuwa mumeo/mpenzi wako atatembea kote lakini lazima tarudi kwako, kwa yeye kufanya hivyo sio penzi juu yako bali penzi lako kwake ndio linamrudisha kwa vile anatambua wazi kuwa hakuna mtu atampenda kama unavyompenda wewe.

Kumbuka nia na madhumuni ya kusihi hapa Duniani kumtukuza Mungu na kufurahia maisha, hivyo ni vema kuwa kwenye uhusiano ambao nyote mnapendana na kuthaminiana, ukiona/hisi hupendwi ni vema kujitoa badala ya kuwa "unhuppy na lonely in love".

Tafadhali usisite kuongezea maelezo/uzoefu wako ili sote tujifunze....karibu.

Tuesday

M'naume M'namke, nani anamuhitaji mwenzie?


Wengi wetu tunazaliwa kisha kukua na kukuta baba na mama pamoja, bibi na babu pamoja, shangazi na mjomba pamoja, baba mdogo/mkubwa na mama mdogo/mkubwa pamoja na kudhani hivyo ndivyo sote tunavyotakiwa kuwa mara tunapokuwa watu wazima n.k.

Tunapoanza au jiingiza kwenye mahusiano ya kimapenzi na baadae maisha ya ndoa (milele pamoja) tunakuja kuhisi kuwa hawezi kuishi bila wenza wetu sio kwa vile wanatulisha na kutuvisha bali tunawapenda napengine ni kwavile umri umeenda na unahofia kuwa "nani atanitaka na mikunjo hii".

Sasa wewe kama wewe unafikiri ni nani zaidi anamhitaji mwenzie zaidi?

Endelea hapa.....

Mwanaume ni mwindaji na uwindaji huo sio wa kupata kitoweo tu (pesa) bali kukupata wewe mwanamke pia, inasemekana kuwa wanaume wengi wanaamua kuwa “single” au wagumu ku-commite karne hii kwa vile wanawake hawawindiki tena.

Kwamba wanawake wamekuwa rahisi kupatikana (kukubali kirahisi) na hivyo wanaume hawahisi kama unawafaa kama wapenzi wao wa kudumu kwa vile hawakukuwinda bali ulijitega mwenyewe (kutokana na U-feminist a.k.a Ubeijing wa wanawake wengi wakidhani ni Usawa).

Hali hiyo inasababisha wanawake wengi kukata tamaa na wanaume ambao hawa-commite kwenye mahusiano ya kudumu na hivyo kuamua kuwa ile “jamii mpya ya Bi au Lesbo”, Hey sitaki kukupoteza hapa let me go to the Point.

Mwanaume anamuhitaji mwanamke zaidi kama msaidizi wake kuliko mwanamke anavyomhitaji mwanaume na sema hivyo sio kwa kuegemea swala la ngono bali kwenye maswala mengine mengi ya kimaisha.


Inasemekana kwamba wanawake ambao hawajaolewa (spinsters) wanaishi zaidi ukilinganisha na wale walio ndani ya ndoa na Wanaume waliondani ya ndoa huishi maisha marefu zaidi kuliko wale walio nje ya ndoa(bachelors), umewahi kujiuliza kwanini wataalamu wanadai hivo?

***************************************************
My only man @ Belsize area this is for you. Asante for visiting here daily even though You don’t understand much Kiswahili. I love you to death baby!xx

Thursday

Ni usawa au Kiburi?

"After thousands of years of male dominance, we now stand at the beginning of the feminine era, when women will rise to their appropriate prominence, and the entire world will recognize the harmony between man and woman". The Rebbe.

Unakumbuka ule Mkutano wa wanawake kule Beijing au unatambua kwanini wanawake wanaitwa "wabeijing"?

Swala la usawa baina yetu wanawake na wanaume lilizua au linaendela kuzua utata kutokanana baadhi ya wanawake ku-abuse maana halisi au nia na madhumuni ya Usawa huo......na matokeo yake wanawake wamekuwa kama wanaume, wamejawa na viburi mbele za wapenzi/waume wao n.k. hii ni kutokanana kutoelewa kwanini hasa wamama wale walikusanyanakule "Beijingi" kudai Usawa.

Ukweli ni kwamba hakuna mwanaume anataka kuwa au kuoa "mwanaume mwenzie" kwa maana kwamba unatakiwa kubaki mwanamke no matter how much you earn, no matter how educated you are, no matter how tall you are.....having said that sina maana kuwa ndio uwe kila kitu "sawa/ndio bwana/mume wangu" type.


Usawa tunaotakiwa kuutolea mcho ni ule wa kujitahidi ktk elimu, ufanyaji wa kazi kwa bidii (kupata cheo kutokanana uwezo wako sio kwa jinsia yako), kuchangia maendeleo ya familia zetu namaisha yetu kwa ujumla, kuongoza aukushika nyazifa mbali-mbali ambazo awali zilidhaniwa kuwa ni za kiume tu n.k.


Sio kuwa mlevi kwa vile wanaume wanalewa, kuwa na wapenzi wengi wengi kwa vile baadhi ya wanaume wanafanya hivyo, kutongoza kama wanavyotongoza wanaume kwa vile tu "tuko sawa", kula kiasi kikubwa cha chakula kwa vile tu wanaume wanakula kuliko sisi (hushangai kwanini wanaume wanakula sana lakini hawana pot bellies eti?) na mambo mengine mengi ambayo wanaume wanayafanya kwa sababu zao binafsi kwa vile ni wanaume au kulinda ego zao.

Ukikutana na mwanaume ambae anapenda au vutiwa na "kiburi chako" ukidhani ndio usawa ujue huyo ni Player.

Ndio "fact" ya leo......unamchango? swali je?

Mwisho mzuri wa wiki.

Wednesday

Nini kiswahili kwa "affectionate"


Kwa wanawake wengi wa Kibongo hawajui au hawajali umuhimu wa kuwa “affectionate” as long as anapatiwa pesa za chakula na manunuzi mengine binafsi kila siku, sina hakika kuwa hawatilii maanani hii kitu kwa vile wanaume wetu wa kibongo wengi sio “affectionate” kwa sababu zao binafsi au kudhani kuwa ni sio kitu muhimu sana au “sio utamaduni wetu”(hata denda sio utamaduni wetu lakini mbona tunakulana tu eti?)


Katika hali halisi ni muhimu sana japo mpenzi wako hajui jinsi ya kuomba au akijaribu kukupa “affection” anakatishwa tamaa au kushushuliwa (told off) kuwa anadeka mno au “hukui tu” au hajiheshimu n.k. labda kwa vile wamekuwa pamoja muda mrefu au tayari kawa mama.


Nimeshuhudia baadhi ya wanaume wakilalama kuwa wapenzi wao hawaonyeshi shukurani kwa yale mwengi ambayo wanawafanyia wake/wapenzi wao lakini wanashindwa kuelewa kuwa mtu hawezi kushukuru kwa vitu au mambo unayomfanyia wakati hayaitaji au kwake sio muhimu sana kama yale ambayo anayahitaji ambayo wewe mwanaume huyafanyi.


Au ni kweli unayafanya lakini jinsi unavyo yawakilisha hayo uyafanyayo kama “affection” kwa mpenzi wako ni tofauti na vile mpenzi wako anataka au angependa na kwa bahati mbaya hasemi au hakuambii vile anataka na matokeo yake nyote wawili mnakuwa hamna raha au amani mioyoni mwenu japo kuwa mnapendana kwa dhati.


Ni wazi kuwa kila mmoja wetu anamahitaji yake ktk swala zima la uhusiano wa kimapenzi ambayo ni tofauti kabisa “no matter how compatible you might be”, hivyo ni jambo la muhimu sana kuyaweka wazi mahitaji yako(sio chakula, maladhi na matibabu bali mambo ya kushikana, busu, outings, ukaribu, mazungumzo, ngono, kuwa pale kwa ajili yake n.k.) kwa mwenza wako ili aweze kuyatimiza.


Kumbuka kuwa hakuna mtu anazaliwa anajua kila kitu bali sote tunajifunza kila siku, na nafasi nzuri ya kujifunza ni kumzoea (bila kumshushia heshima) mpenzi wako kama rafiki,mpenzi na mwenza….ondoa au acha kabisa heshima ya uongo (Uoga) na badala yake be youself ili akupende 4 who u are sio who u pretend 2 be.


Huwezi kuamini kuwa baba mtu mzima hawi-affectionate kwa mkewe aliyeoa miaka ya 80s lakini anakuwa “very affectionate” kwa binti mke mdogo anaetoka nae a.k.a kimada……I don’t real get it?


Jamani mapenzi hayana ukubwa wala udogo, mapenzi hayazeeki, mapenzi huendelea kuwepo bila kujali mmekuwa pamoja kwa muda mrefu kiasi gani…..mapenzi ni hisia zilizo ndani yako na hazina uhusiano na kuzaliwa kwa watoto au kuzeeka hivyo sote hatuna budi kuyaonyesha kwa uwazi kwa wenza wetu


Muonyeshe mwenzio jinsi unavyompenda kwa vitendo sio kwa kungonoana kwani huko sio kupenda kwa vitendo bali ni hitaji lingine linalojitegemea ambalo nalo ni muhimu pia kwenye uhusiano (sio zamu yake leo).

*Sasa hebu leo mwambie mpenzi wako ni nini hasa hupendi akufanyie na nini hasa unapenda afanye kuonyesha “affection” kwako.


Natambua kutokana na utamaduni wetu kuna mambo mengine huwa tunashindwa kuyafanya kwa kuhofia jamii itatudhaniaje…..who cares….hawakulishi…..hawakuvishi na kila mtu anaishi kimtindo wake na kufurahia maisha kivyake hivyo wewe ukihisi unataka kuonyesha penzi kivitendo mkiwa marikiti au kituo cha daladala just do it! sio mpaka mfike uchochoroni!


Kuwa "affecionate" ni muhimu sana pia ikiwa wewe na mpenzi wako hamlingani kiuwezo ktk kubilingishana.......kuna watu kungonoka sio muhimu sana kwao kutokana na sababu zao mbali-mbali lakini hiyo haina maana hawahitaji kupendwa au kupetiwa-petiwa.

Siku njema.

Pages