Tuesday

Maeneo ya Kumshika Mwanaume...

Habari dada Dinah
Mimi ni binti mwenye umri wa miaka 28 na ni bikira tatizo  nimepata mchumba tumepima ukimwi na tuko kwenye process za ndoa.


Tatizo mimi ni mwembamba yeye ni mnene na mboo yake ni kubwa na ndefu akitaka kuanza kuniingilia kwa ajili ya kufanya mapenzi naumia mno anaishia kuingiza kichwa tu.

Hebu nisaidie nifanyeje na nakaribia kuingia kwenye ndoa. Pili nataka kujua sehemu zipi nimshike ili apate raha.

******************************


Dinah anasema: Kwanini unasema "tatizo nimepata mchumba"? Inamaana haukotayari kuolewa nae? Kwanini udhanie kuwa na mchumba ni tatizo?

Wembamba wako hauna uhusiano wowote na unene wake kwenye suala la kufanya mapenzi.


Kwa kawaida kuingiliwa kwa mara ya kwanza (tolewa Bikira) kunauma na sio wanawake wote wanaotolewa Bikira siku ya kwanza kwani hushindwa kuvumilia maumivu na hujawa na Uogoa hivyo misuli ya uke inashindwa kujiachia(relax).


Ndio maana zamani wakati Mabinti wanaolewa na Bikira walikuwa wanakaa ndani siku Saba, Usiku wa ndoa Bikira inatolea na siku saba baada ya hapo mwanamke "anazoeleshwa" uume(kuingiliwa ukeni) na yeye kuonyesha mambo mengine ya kimapenzi aliyofundwa kwao.


Ikiwa Mchumba wako amefanikiwa kuingiza kichwa ni wazi kuwa wewe sio Bikira tena, isipokuwa Uke wako haujazoea kuingiliwa na kitu kinene na kigumu + hofu ya kuumia.


Vilevile kichwa cha uume huwa kikubwa kiasi kuliko sehemu ya nyuma ya Uume, ikiwa kichwa kinaingia ni vema kama utavumilia ili aendelee kuingia taratibu na kwa hatua, sio anaingia moja kwa moja na kwanguvu na shauku zake zote....utaumia na kumchukia!!


Weka uaminifu kwa Mchumba wako na muombe aingie taratibu-taratibu, usiwe na haraka ya kuzoea leo au kesho! Unaweza kusubiri mpaka mtakapofunga ndoa na kwenye Fungate ndio mkazoeshane.


Wanaume wanatofautiana hivyo siwezi kusema umshike wapi ili afurahie kwani mie simjui(sijawahi kuwa nae hehehehehe)....anyway! Kuna maeneo ambayo ni General na mengine jaribu kubahatisha au kutafuta jinsi mnavyozidi kuzoeana.

--Kubusu shingo katika mtindo wa kuuma kwa mbaaali


--Busu au papasa juu ya Kinena(sehemu inayoota mavuzi) au niseme kiunoni kwa mbele hivi kama unaelekea chini ila usifike kwenye uume.


--Lamba katika mtindo wa kunyonya Chuchu, hakikisha unazinyonya kwa kupokezana, usibaki kwenye chuchu moja kwa muda mrefu kwani utampoteza "msisimko".


--Masikio, unaweza kuwa ni sehemu ya chini, kwa nyuma au kwa ndani kama sio sikio lote. Tumia midomo yako kulamba, busu, hemea na nong'oneza maneno matamu kumfanya Mchumba wako asikie raha na kuelewa hisia zako kwake.


--Busu katika mtindo wa kulamba sehemu ya ndani ya mapaja yake, pia busu sehemu ya nyuma ya kiuno(juu kidogo ya makalio yake).


--Shika Kende zake na kuzichezea(taratibu usimuumize) na tumia midomo yako kutumbukiza pumbu na kuzitoa kama vile unapuliza ki-slow-mo.

Anza na hivi, vingine tutaendelea kuelekezana jinsi unavyoendelea na maisha yako ya ndoa.


Maana ukionyesha mengi jamaa anaweza kukushangaa....Lol!


Hongera sana kwa kuchumbiwa na kila la kheri kwenye maandalizi ya Ndoa yenu. Mungu awaongoze na kuwalinda.
------------------

Sunday

Ndani ya Wiki mbili kesha "move on" na jamaa kwenye WhatsApp!

Habari yako dada Dinah,

Mimi ni kijana Mtanzania, nina jambo ambalo ningependa ushauri wako. Jambo lenyewe ni kwamba nina mpenzi wangu ambaye tuligombana na tukakaa kama wiki mbili hivi hatuelewani...ndani ya hizo wiki mbili akafanya ngono na mwanaume mwingine.


Sasa baadae, baada ya hizo wiki mbili tulikuja kuelewana tukasameheana yale yaliyotugombanisha. Hapo bado sikuwa najua kama alifanya ngono na mtu huyo mwingine.


Sasa baada ya hapo tukarudiana na kuendelea na uhusiano kama mwanzo, Mpenzi alikuwa anatumia simu ya Blackberry ambayo baadae alinipa mimi niitumie kwasababu yeye tayari alishapata simu nyingine ambayo sio Blackberry lakini anaipenda zaidi. Nikaichukua ile simu nikaweka line yangu ya vodacom.

Cha kushangaza, baada ya siku kama mbili tatu hivi napokea Message kutoka kwa mtu ambaye walikuwa wakiwasiliana kupitia WhatsApp, hiyo message ilikuwa ya kimapenzi...then muda mfupi nikapokea picha mbili ambazo huyo jamaa alizituma.

Hizo picha zilionyesha walipiga wakiwa wote, moja wamelaliana yeye mpenzi akiwa amejifunga khanga moja tu, na nyingine wanakipeana busu yeye akiwa amemkalia huyo jamaa...


Nikaamua kumuuliza taratibu kwanza kabla hata ya kumuonyesha hizo picha, nikamuuliza kama anazijua namba za huyo jamaa nilimuonyesha maana kwenye whatsApp namba ya alietuma inaonekana, akasema anamjua.


Nikamuuliza wakoje naye, akasema ni rafiki tu japokuwa jamaa anamfuatilia mara nyingi kwani amekuwa akimtaka...akakataa kabisa kusema ukweli.


Baadae nikawa mkali na kumwambia tuachane kabisaa aendelee na huyo jamaa yake! Akawa mkali, hapo bado sijamuonyesha zile picha, akawa analia machozi kabisa kila siku ananibembeleza nimsamehe kwakuwa hakuwahi kuniambia kuwa huyo jamaa huwa wanatongozana japo bado hajamkubali.


Ndio siku moja nikamwambia upo tayari kusema ukweli ili nikusamehe?..akasema ndio! basi nikamwambia tukutane sehemu tuongee....ukweli ni kwamba hakuna alichokisema kipya zaidi ya kusisitizia kuwa huyo jamaa yeye ndiyo anaemfuatili (kumtongoza) lakini yeye hamtaki na wala hawajawahi kukaa au kukutana faragha popote.

Nikamuuliza je? nikikuonyesha ushahidi kwamba yule ni bwana yako, nimfanye nini?...akanijibu niachane naye nisimsikilize tena na akasema yeye atakuwa Malaya na hafai...


Mmh nikaguna kidogo, nikamuuliza tena kama kuna jambo ambalo amefanya nae halafu hajaniambia basi aseme lakini wapi...akang'ang'ania msimamo wake.


Ndipo nikamuonyesha hizo picha mbili. Alitahamaki, akaanza kulia na kuoba msamaha tena kwa kunipigia magoti, ila moyo wangu ulishakufa ganzi nilipomuona anajiamini baada ya kupinga maswali yote niliomuuliza wakati ni uongo ambao hata yeye alikuwa akiujua kuwa ni uongo.


Kwasababu baada ya kumuonyesha zile picha tu alianza kulia na kuomba samahani nisifanye yale aliyojiapiza, wakati nilitegemea angezikana zile picha au angalau abishe bishe kidogo lakini alizikubali pale pale na kuanza kulia na kuomba samahani akinisihi nisifanye yale aliyojiapiza...


Hapo mimi nilinyanyuka na kuondoka zangu nikimwambia tusijuane tena...aendelee na huyo jamaa yake...


Hivi ninavyoongea mpaka sasa bado hatuna mawasiliano mazuri, mimi ndio sitaki kuwa naye tena japo roho inaniuma lakini nikimuangalia nasikia hasira sana.


Nimejaribu kumuuliza maswali kadha wa kadha kwamba kwanini na ilikuwaje ndani ya muda mfupi vile alifikia umbali wote huo wa kufanya ngono na mtu mwingine?


Akanijibu eti frustration tu..ndio zimemchanganya akajikuta kafanya hivyo...Mh akilini kweli mimi hainiiingii...Frustration?...Sasa swali langu mimi kwako na hata wadau wengine wanisaidie mawazo.

Je! sio kwamba huyo mtu alikuwa naye muda mrefu tu?...au ni kweli inawezekana ndani ya hizo wiki mbili ndio wamekubaliana na kutiana kweli?...

Na je! ni vyema mimi kumkubali na kumsamehe turudiane kama mwanzo?....je! Inawezekana ndio tabia yake?, kwasababu nijuavyo mimi, mwanamke yeyote anaweza akatongozwa karibu kila siku na watu tofauti, lakini kukubali ndani ya muda mfupi hivyo kumvulia mtu chupi na kufanya naye mapenzi sio rahisi tena ukiwa katika kipindi kibaya umegombana na mpenzi wako ambaye leo au kesho unaomba akusamehe ili mrudiane?


Pamoja na maswali hayo ukweli ni kwamba nimemchukia sana yule dada.

Sasa dada Dinah na Wadau wengine naombeni ushauri...nini cha kufanya hapo?

Natanguliza shukrani zangu, Ahsanteni"

------------------

Thursday

Yeye 40s with 2 Kids, Mimi 27 anataka ndoa! Je nikubali?

Habari Dada Dinah!
Naomba ushauri wako lakini naomba usinitaje jina langu.


Awali nilikuwa na uhusiano na kijana mmoja ulidumu kama miaka saba hivi. Hatukuweza kuwa pamoja kwa sababu mwenzangu alikuwa anasoma hivyo tulivumiliana kwa shida na raha.

Kwa kweli kaka huyo nilimpenda kupita maelezo lakini alikuwa na tabia zake nyingi ambazo nilizivumilia nikitegemea kuwa ipo siku atakuja kubadilika na hata hivyo niliziona kama ni ndogo kwani penzi la dhati lilitawala juu yake.


Mimi nilianza kazi huku mwenzangu akiwa bado anasoma, hivyo nilikuwa nikimsaidia kwa vitu vidogo vidogo na hata kumnunulia zawadi hasa kila siku yake ya kuzaliwa. Hivyo vyote sikuvihesabu kwani nilikuwa natoa kwa mtu nimpendae.


Kuna kipindi alianzisha biashara mbalimbali na kuna wakati alihitaji msaada wa pesa na mimi bila kinyongo nilitoa kwa moyo. Lakini zile biashara zilikuja kuisha kimya kimya na nikimuuliza anasema eti hajapata kitu chochote.


Yaani kwa kipindi chote hicho sikuona wala kupewa zawadi ya mafuta ya kupaka kama moja ya kifaida alichokuwa anapata katika biashara hizo.


Akaanza kuwa rafu kweli kwani alikuwa anafuga mindevu na nywele ndefu na kila nikimshauri ananiambia hii ndio life style yake na mimi siwezi kumuambia kitu na bangi alikuwa anavuta.


Hayo mambo yote niliyavumilia japo yalikuwa yaniuma sana hasa ukizingatia unamshauri mtu kitu na yeye anakipinga. Yaani ni mambo mengi alinifanyia kiasi kwamba nikasema enough is enough japo yeye hakutaka tuachane kwa kigezo kuwa amebadilika lakini sivyo.

Mapenzi yetu tulianza mwaka 2002 hadi mwaka 2009 nilipotosheka na vituko vyake. Niliamua kujikalia peke yangu bila mahusiano ya kimapenzi na mtu yoyote hadi leo.


Japo kwa kipindi chote hiki cha ukimya wangu huwa ananitumia meseji za kuomba msamaha kwa mambo yote aliyonitendea na kusema amebadilika na ikitokea nimemwambie mimi sitaki mahusiano tena na wewe basi atatuma meseji za kashfa na matusi kibao then anakuja kusema nimsamehe tena eti ni hasira ndizo zinamsababisha afanye hivyo.


Kwa kifupi Dada Dinah mimi kwake ni basi tena japo bado ananitumia meseji za kuniomba msamaha.

Sasa Dada kuna hili ambalo limenifanya niombe ushauri kwako, ni kwamba kuna Baba mmoja tulianza kufahamiana katika kazi niifanyayo japo nilianza kuona dalili za kunitaka kimapenzi lakini hakuwahi kuniambia hata siku moja.


Basi akawa anakuja kama kawaida kufanya kazi zake kunipigia simu kunisalimu. Ikatokea kipindi fulani akawa haonekani nina maana mkoa nilipo mimi yeye amekuja kusoma masters lakini makazi yake ni mkoa mwingine kabisa.

Siku moja akaniomba akutane na mimi na majibu yangu nikamwambia mimi sipendelei kutoka na mume wa mtu yaani kukaa nae sehemu. Akanijibu mimi nina watoto lakini sina mke nikamwambia mtu mzima kama wewe utawezaje kukaa bila mke? Akanijibu naomba utafute muda nikwambie maana ni story ndefu.

Basi tukaa akaniambia yeye ana watoto wawili wakike (darasa la saba) na wakiume (chekechea) na mkewe amefariki kama miezi minne iliyopita. Nikamwambie wanaume mara nyingi mnaweza kumuua mtu akiwa bado mzima.


Basi siku nyingine akaniletea mikanda ya video ya mazishi na nikagundua kweli amefiwa na mke.

Dhumuni lake kubwa anataka kunioa na sasa imepita kama mwaka mmoja tangu mkewe afariki. Nikamwambia swala la kupima amesema hamna shida twende tena mara tatu.


Yeye ni mwajiriwa wa Serikalini na tena ni Afisa Kitengo fulani huko mkoa anaofanyia kazi.

Dada Dinah, Mwanzoni nilikuwa najisemea mwenyewe kuwa mimi siwezi kuwa na mwanaume anayenizidi miaka saba na kuendelea maana nilikuwa nawaona ni rahisi sana kudanganya binti kwa upeo wangu.


Sasa huyu baba kiumri yeye amesema ana miaka 40 na kitu na mimi nina miaka 27 Je, hii ni sahihi kwa yeye kunioa mimi? na je kwa mtazamo wako huyu baba ana msimamo wa dhati kwangu?
*******************************


Dinah anasema: Habari ni njema tu, asante. Pole kwa kusumbuliwa na Ex, kuna Ex wengine wasumbufu sana. Hongera kwa kuwa na Msimamo ulionao mpaka sasa.


Kutokana na maelezo yako imeonyesha umakini na kutaka kujua "mzigo" alionao huyo Baba (Mjane). Inaonyesha anahitaji "mother figure" kwa ajili ya watoto wake na ndio maana amekuwa wazi tangu mwanzo.


Kitendo cha kuwa wazi na kukuonyesha mkanda wa mazishi ambao atakuwa kakuonyesha watoto wake na kuna maelezo yanayo-support maelezo yake kuwa ndio alikuwa Mfiwa, sioni tatizo hapo.


Umegusia kupima na yeye amekubali kufanya hivyo mkiwa wote nayo pia inatia moyo lakini hakikisha mnapima kweli Usiridhike na kukubali kwake haraka.


Pia ni vema wewe ukachagua pa kwenda kupima bila yeye kujua (kuna watu huonga Madaktari kutoa vyeti "fake").


Tofauti ya Umri sioni kuwa ni tatizo, kutokana na maelezo yako inaonyesha kabisa umekomaa na unajitegemea kiuchumi na kiakili (katika kufanya maamuzi).


Hayo hapo juu yakiwa sorted (ukiwa comfortable) kitakacho fuata ni kuendeleza uhusiano na kujuana zaidi, wewe uwajue wanae na wanae wakujue wewe na wakuzoee/kukubali.


Usiharakishe wala kulazimisha wakupende, kumbuka wamepoteza Mama yao mzazi hivyo wanaweza wakafurahi kuwa na "mama" au kukasirika kuwa umechukua nafasi ya mama yao....yote ni sawa tu, kuwa mvumilivu na muelevu.

Tuone nyongeza ya wachangiaji wengine.

Nakutakia kila la kheri!

------------------

Safari ya Ughaibuni imebadili Mume wangu!

Habari za kazi dada Dinah, mimi nina matatizo na ndoa yangu niliyofunga mwaka 2009 mwezi 4 Kanisa la Romani Katoliki.


Mwaka 2010 nikapata post ya kwenda nje ya nchi kwa mkataba wa miaka 2 , baada ya kuondoka nilikuwa napata likizo ya siku 21 au wiki moja. Chakusikitisha tangu mwaka jana mume wangu alianza kubadilika.


Nikirudi likizo mara ananiambia nenda kwenu ukawatembelee. Naweza kukaa wiki nzima lakini anafanya sex na mimi mara 1 tu mpaka naondoka.


Mwaka jana mwezi wa kumi na mbili nilipata taarifa kuwa amezaa na mwanamke wa pale mtaani kwetu na mtoto anamiezi 3.


Mwezi wa kwanza tarehe 12 alikwenda kumtabulisha kwao kijijini pamoja na mtoto na pia hapo hapo ana mwanamke mwingine anamimba anakaribia kujifungua na hao wanawake wote huwa anawaleta pale kwenye nyumba kwetu wanalala kitandani kwangu!


Mimi nategemea kumaliza huu mkataba mwezi wa sita mwaka huu, nimejaribu kuongea na mume wangu na amenitamkia kuwa hanitaki tena.


Nimeongea na wazazi wake mpaka sasa sijapata jibu lolote, roho inaniuma sana kwani nilipokuja huku tulikubaliana vizuri.

Sasa hivi nikienda likizo anafunga chumba hataki nionane naye, nikipiga simu ananikatia,nikituma sms hajibu, naomba ushauri wako dada maji yamenifika shingoni dada.

****************************

Dinah anasema: Pole sana kwa matatizo unayokabiliana nayo. Sina hakika ni kitugani hasa kilipelekea ninyi wawili kufunga ndoa...kwani si ndoa zote zinafungwa chini ya misingi ya mapenzi...wapo wanafunga kwa ajili ya kuanzisha familia? Kurahisisha maisha(pesa), Umri, Mkumbo, kuondoa mkosi n.k


Kutokana na maelezo yako inaonyesha kuwa hamkuwa na muda wa kuzungumza au kuwasiliana kama pea na pengine hamkuweka au hamkuwa na nia/mipango inayofanana ya kimaisha hapo baadae.


Inaonyesha mumeo alitaka sana kuanza familia na wewe ulitaka career vyote ni vizuri na ni muhimu ila vimekutana wakati mbaya na labda kwavile hamkujadili haya mwanzoni kabisa mwa uhusiano wenu kabla ya ndoa.


Hongera kwa jitihada zako za kutaka kurudisha ndoa yako, hakika inauma lakini suala zito kama hili huwezi kulizungumza wakati wewe mwenyewe uko mbali.


Ni vema kuzungumza na mumeo na wakati huohuo kujaribu kuwasiliana na aliewafungisha ndoa Kanisani au wale waliowapa Semina kabla hamjafunga ndoa.


Natambua Ndoa za Kikatoliki zina hatua zake, basi ni vema ukijaribu kuzifuata mara utakaporejea nyumbani.


Umejaribu kuzungumza na wazazi wake ambao kwao kidogo inaweza kuwa ngumu kufanya chochote kwani hujui mtoto wao(mumeo) amekuzungumziaje kabla ya kutambulisha mwanamke mwingine na mtoto.

Muombe Mungu akutie nguvu kipindi hiki uko mbali kikazi lakini pia shukuru kuwa mumeo anakukwepa kwenye kufanya mapenzi...:uwezi jua anakuepusha mangapi.


Maneno yangu sio sheria, lakini nashindwa kujizuia kusema haya:-

Mwanaume aliekosa uaminifu kwa mkewe na kungonoka na wanawake ovyo na hata kuwapa ujauzito hafai kuwa Mume.


Unaweza kushawishika kupigania penzi lako na hata kushika mimba ili umpe mumeo mtoto so that ndoa iokolewe lakini baadae ikakuongezea matatizo zaidi.


Hatua mliyofikia sidhani kama kuna umuhimu wa "kupigania penzi" ni vema kuanza maisha yako upya.


Kisheria unaweza kumtaliki mumeo lakini Kikristo huwezi kufanya hivyo. Sasa kwasababu imani yako ya Dini inakataza Talaka haina maana uendelee kuishi mpweke ndani ya ndoa.

Tusikilize wengine watasemaje...
Pole na kila la kheri!!

------------------

Wednesday

Natoka na X wa Mchizi wangu, je nimwambie!

" Hello Dinah,

Tatizo ni kwamba nina girlfriend ambae alikuwa ni wa mchizi wangu wakaachana, baada ya muda mdada akawa ananizimia mimi sana sana alivyoshoboka mie nikatoka nae kingono.

Sasa naona dizaini mdada ananipenda na anataka uhusiano ila mchizi wangu hajui kama mimi nipo nae huyo dem, hapa nifanye nini?

Dinah anasema: Heyaa! Well sio kwamba umemuimba huyo Dem hivyo mimi sioni kama wewe una makosa, makosa ni ya huyo Dem ambae inaonyesha hakuheshimu urafiki kati yako wewe na ex wake ambae ni mchizi wako.

Pamoja na kusema hivyo haina maana kuwa Mchizi wako atakuwa cool akijua kuwa unatoka na Ex wake.

Kitu muhimu cha kuzingatia kabla rafiki yako hajajua ni hisia na mpango wako juu ya binti huyo. Je nawe unampenda? Je ukotayari kuanzisha uhusiano na kutetea penzi lenu?

Ikiwa jibu ni ndio kwa maswali hayo basi taratibu anza kutoka na binti huyo bila kutangaza kuwa ni mpenzi wako kwa kusema wala kuonyesha....Mchizi anaweza kukuuliza au akamuuliza ex wake kama ninyi ni pea.

Hilo likitokea tafuteni njia nzuri ya maelewano na kesi itakuwa imekwisha na hivyo mtakuwa huru na uhusiano wenu.

Ikiwa majibu ni hapana basi achana na huyo Binti na uendeleze urafiki na Mchizi wako.

Wachangiaji wengine wataongezea.

Kila la kheri!
------------------

Sunday

Wivu

Mambo vipi!

Hebu leo tulizungumzie hili suala la Wivu, natambua watu wengi wanaamini kuwa Wivu ni chanzo cha kufarakana na kutokuelewana. Baadhi huamua kuficha hisia hizo za wivu kwa vile wanaogopa kuachwa na wenza wao.

Vijana wa sasa ndio wanaongoza kwa kupinga hisia hizi za wivu, lakini tukirudi nyuma enzi zile za Hayati Bibi yangu kumfanya mtu akuonyeshe wivu ilikuwa ni sehemu ya mapenzi na ikiwa mpenzi wako hakuonyeshi wivu ni dalili kuwa humvutii tena (namna ya kumfanya mume awe na wivu ni somo kwenye kufundwa).

Pia wapo wanaopenda kuweka "Wivu" kama ubora wa hali ya chini sana kwenye uhusiano wa kimapenzi na hata ndoa. Ukifuatilia kwa ukaribu utagundua kuwa sehemu kubwa ya watu wanaopinga hisia za Wivu kwenye uhusiano ni ama wanawapenzi zaidi ya mmoja au hawajui Wivu ni nini? kama sio wanachanganya wivu na kuwa "obsessed"(kwa kiswahili ni?).


Inashangaza unapomkuta mtu anataka mpenzi wake awe mlevi wa penzi lake (addicted) lakini hataki mpenzi huyo awe na wivu juu yake....hapo huwa najiuliza ikiwa unamkolezea mwenza wako mapenzi motomoto kiasi kwamba unakuwa "tiba" yake na bila tiba hiyo hajiwezi tena, kwanini asiumie kihisia ikiwa haupo karibu yake au umechelewa kurudii nyumbani?


Wivu ni hisia kama ilivyo penzi, hupangi au kuchagua bali inatokea tu. Wivu mara zote uhusisha mtu wa watatu, inaweza kuwa jirani, rafiki, mfanyakazi, mpenzi wa zamani n.k.

Wivu hauna tafsiri wala sababu kama ilivyo kwenye hisia za kimapenzi, anaekupenda siku zote huwa hana sababu ya kukupenda bali hutokea tu anakupenda, japokuwa kukupenda huko kunaweza kuongezeka siku hadi siku kutokana na matendo mema au mapenzi unayompa n.k basi hata wivu ni hivyo hivyo na huongezeka kutokana na matendo mema na mapenzi unayotoa.

Wivu unaweza kuwa maumivu ya hisia (mtu unakonda tu...lol), hasira, Uoga, hofu, na huzuni. Vilevile wivu unaweza kujionyesha kwa mhusika kuwa mfuatiliaji, muuliza maswali, uhakiki wa muda/mahali au kutaka kujua maisha ya mpenzi wako ya kimapenzi kabla yako.

Wivu unahimarisha uhusiano na kukufanya uhisi/ujue kuwa mwenza wako anakujali, inakufanya wewe mpenzi kuona namna gani unamrusha roho japokuwa mmekuwa pamoja kwa miaka mingi.

Wivu mzuri nii ule unaokwenda sambamba na na mapenzi na kujaribu kumsukuma mtu wa 3 ambae labda humuamini mbele ya mpenzi wako kutokana na mazoea yao.

*Kuna ila hali ya kutomuamini mpenzi kwa vile tayari amewahi kukutenda, au umewahi kumfuma na mtu mwingine "wakidukuana", hali hiyo sio Wivu kama wengi ambavyo huita bali ni kutomuamini mwenza wako.

Pia kuna ila hali ya "umilikishi" kwamba kwa vile tu ni mpenzi wako basi hutaki awe karibu na mtu yeyote....yaani ni marufuku hata kwenda kwao, shughuli zote za kutoka unazifanya wewe kwa vile unahofia watu wengine watamuona na kumtamani....wengi huita wivu, lakini kiukweli sio wivu ni kuwa "obsessed".

Kila la kheri.

*Samahani L inagoma-goma kwani mwanangu kaing'oa hivyo nahitaji kubonyeza kwa nguvu na mie nasahau kutokana na mwendo wa haraka wa kuchapa.....

Wednesday

Siri ya Mafanikio kwenye uhusiano wako.

Sio pesa....Lol!!

Hakuna mtu asiependa kuwa na uhusiano wa kimapenzi mzuri na wenye afya, mimi binafsi napenda sana kuona watu wanapendana, huwa napata maumivu na wakati mwingine hasira ninaposikia au kupata kesi ya uhusiano au ndoa kuvunjika.


Wakati wa kufundwa mara zote niliambiwa kuwa ukizubaa mapenzi kati yako na mumeo hayatokuwa kama mtakavyoanza hivyo basi unahitaji kuwa mstari wa mbele kuhakikisha hakuna kuzoeana bali kujuana.


Sasa kwa vile Mfundaji mwenyewe alikuwa ni Hayati Bibi yangu aliezaliwa na kukua enzi za Mfumo Dume aliwakilisha somo kwangu kwa kusema “hakikisha unakuwa mstari wa mbele” lakini kutokana na maisha yalivyo sasa mimi nitasema kwako HAKIKISHENI (wake kwa waume) kuwa hamzoeani na badala yake mnajuana kiundani zaidi.


Uhusiano huwa mtamu kweli kweli unapoanza, hakuna hata mmoja kati yenu anaekumbushwa na mwenzie kufanya mambo/jambo, unajikuta tu unafanya mambo mazuri-mazuri kwa mpenzi wako, uhusiano unaendelea mnafikia mahali mnakubaliana kuishi pamoja part time(mf: mwisho wa wiki tu) au full time kwavile inakuwa ngumu sana kupitisha siku nzima bila kumuona Asali wa Moyo na baadae
ndoa.


Baada ya kuishi pamoja au kufunga ndoa mmoja wenu au wote mnaanza kupunguza speed na hatimae inafikia mahali wote kwa pamoja mnajikuta mnadharau kufanya mambo mliokuwa mkifanyiana awali kwa sababu ya mapenzi......hatua hii ni mbaya sana na ndio huwa chanzo cha ugomvi au kutafuta mtu atakaekufanyia mambo bila kumkumbusha, hatua hii inaitwa KUZOEANA.


Baada ya kuzoeana na ku-miss hamasa, chachu ya mapenzi kutoka kwa mwenza wako, unaanza kulinganisha uhusiano wako na uhusiano wa watu wengine na kuanza kuona wivu na hata ku-wish kuwa mkeo au mumeo angekuwa kama yule au
tungekuwa kama wale n.k.


Sasa nini siri ya mafanikio kwenye uhusiano?


1-Usijisahau na hakikisha unarudisha uliyokuwa ukimfanyia mwenza wako miaka 4 iliyopita, kabla hamjafunga ndoa, yafanye tena sasa. Inawezekana
maisha yenu yamebadilika na sasa mmekuwa familia kwamba kuna watoto,
bado watoto hawakuzuii wewe mume/mke/mpenzi kuwa wapenzi. Ndio ni
baba na mama lakini pia ni Wapenzi.


2-Jipende ili uvutie, usipojipenda wewe mwenyewe na kuvutia itakuwa ngumu kwa
mwenzio kuvutiwa nawe. Kwavile tu mmefunga ndoa au mnaishi pamoja
haina maana ndio mwisho wa kuvutia.
3-Penda/pendezwa,
kukubaliana au kubali mchango wa mawazo yake kwenye jambo mnalotaka
kufanya, mshirikishe mwenza wako kabla ya kufanya uamuzi wowote,
peaneni matumaini na ushirikiano inapobidi....sio kila wakati wewe
ndio msemaji mkuu na muamuzi wa mwisho na yeye ni wa kupokea tu, hata
akichangia mawazo yake huyafanyii kazi(unadharau).


4-Muda, kazi na watoto huchukua muda mwingi na hivyo kutopata muda wa
kuzungumza na kuonyeshana mapenzi, hivyo kutenga muda wenu kama
wapenzi ni muhimu. Ninaposema muda wenu kama wapenzi sina maana ya
kufanya ngono kwani ngono inaweza kufanyika watoto wakiwa wamelala,
nazungumzia ule muda wa ninyi wawili kama ilivyokuwa mf: miaka 4
iliyopita kabala hamjafunga ndoa.


5-Mawasiliano kwa maana ya kuzungumza ni njia pekee ya kumwambia mwenza wako vile unavyojisikia, unataka nini, kwanini umefanya jambo fulani, usaidiwe
vipi, kwanini uko hivyo ulivyo n.k. Hii ni njia pekee ya kuwekana sawa na kuepuka maumivu ya kihisia ambayo yanaweza kukupa upweke ndani ya uhusiano/ndoa.

6-Kubali mabadiliko,
jinsi miaka inavyozidi kusonga ndivyo ambavyo tunabadilika/tunakua,
maisha yetu yanabadilika....japokuwa wakati mwingine mabadiliko hayo
hayaji kama tulivyotarajia bado hatuna budi kuyakubali na kwa pamoja
ku-adopt badala ya kulalamika na kufananisha.

*Mabadiliko yanaweza kuwa upungufu wa hamu ya kungonoka, kupendana zaidi, kuwa wazazi, kuishi maisha ya chini au ya juu kuiko ilivyokuwa hapo awai,
kuugua, ulemavu n.k


7-Kuzozana/gombana kwa maneno, kubishana sio ukorofi inategemea mnabishanaje na kuhusu nini? Katika hali halisi kubishana kwenye uhusiano kunahashiria afya ya uhusiano wenu....ikiwa kuna watu wanaishi pamoja kama wapenzi na hawajawahi kubishana basi ni either wanadanganya au mmoja wao anamuogopa mwenzie.


Pamoja na kuwa ninyi ni wapenzi bado mnatofautiana kijinsia, kimawazo,
kikazi, kipato, matumzi binafsi ya pesa, kimalezi na hata kasoro zenu
hazifanani....hivyo kubishana ni lazima ikiwa kunatofauti hizo na
nyingine ambazo unazijua.


Kubishana kunaweza kuwasaidia mmoja wenu kujirekebisha kwani itawawezesha
kutambua kosa lako ni lipi hasa kama mwenza wako sio mtu wa kukosoa
papo kwa hapo (kosa linapotokea), pia itakuwa nafasi nzuri ya kutambua au kugundua nini hasa mwenzako anafikiria kuhusu kosa/tendo ulilofanya au tabia yako na nini anataka kifanyike ili kuepuka mabishano ya mara kwa mara.


8-Shukuru, omba radhi ni maneno mafupi na pengine unaweza kudhani kuwa hayana umuhimu wowote, licha ya kwamba yanaashiria kuwa umelelewa katika maadili mema pia yanauzito na maana kubwa sana kwenye maisha yetu kuliko unavyofikiria.


Unapohisi kuwa umemuudhi mwenza wako, sio mpaka akununie kwa wiki moja au
akufokee ndio uombe radhi, akionyesha tu kuwa hajafurahia tendo lako
au maneno yako basi omba radhi.


Shukuru kwa kila jambo unalofanyiwa na mpenzi wako....unakumbuka wakati
mnaanza uhusiano akiku-check during the day unasema “asante mpenzi
kwa kunijulia hali”, sasa kwanini ushindwe kusema asante kwa chakula mpenzi?!!

Kila la kheri!

Pages