Wednesday

Nini jukumu letu kwenye ndoa?, hebu tuwekane sawa!

"Dinah pole na shughuli hizi za kutuelimisha, naomba nitoke nje ya mada kidogo. Inaonekana ndoa nyingi zina matatizo ya ajabu na sasa Dinah inabidi utoe mada mpya zinazowafanya wanandoa wajue majukumu yao, huenda mwanaume unakuwa hujui kwa nini umeoa tuelekezane hapa tujue majukumu yako na familia yako.

Mke ajue kwa nini ameolewa na amsaidie mume wake kwa kiasi gani maana inaonekana wanawake wakisaidia sana nayo ni tabu pia sasa tuishije katika ndoa zetu ili kupunguza haya matatizo?

Tuongeaje na wapenzi wetu ili tusigongane? pia imeonekana kuwa wanaume wa sasa wana tabia za kununa na hapo inakuwaje? zimekuwapo kasumba kuwa wanawake wakiwa na uwezo kiuchumi ni shida ktk familia lakini mjue kuwa wanawake wengi sasa wana kazi nzuri au sawa na wanaume je tusiwaoe?

Hebu tupeni na uzoefu nyie wanaume wenye wanawake wanaowasaidia sana hapo nyumbani muwe wawazi bila kuweka ile ya uanaume au kuona aibu. Mimi kwa kifupi nimeona wanawake wengi wakiwa msaada mkubwa kwa familia ikiwa baba ana upendo na anamjali mkewe na akiwa mwaminifu hapo matatizo hayapo.

Mie nayashangaa haya matatizo ya ndoa kila siku humu mpaka naona kama ni shida kuoa, nioe mwanamke wa aina gani du!"

Dinah anasema: Shukrani sana kwa kuwakilisha hili suala, hakika hali iliyopo hivi sasa inakatisha tamaa sana. Ndoa zimekuwa zikifungwa kwa kasi ya ajabu na zinavunjika haraka kuliko ilivyokuwa miaka ile ya bibi na babu zetu, mama na baba zetu. Watu wengi wamepoteza imani na baadhi hawaheshimu wala kuthamini ndoa.

Matatizo yanayosababisha ndoa nyingi kuvunjika yanatofautiana kwa kiasi kikubwa(nitaelezea jinsi ninavyoenda mbele), vilevile sababu zilizowafanya hao wanandoa kufunga ndoa pia zinatofautiana(nitaelezea jinsi ninayoendelea).

Sababu kuu ya kufunga ndoa ni mapenzi, japokuwa enzi za babu na bibi zetu hali ilikukuwa tofauti kutokana na mtindo wa maisha wakati ule na vilevile mfumo dume, wanawake na wanaume wengi walifunga ndoa bila mapenzi, yaani mapenzi hayakuwa sababu ya wao kutaka kushi pamoja bali Familia zao, umri, kuepuka aibu, kufaidika kiuchumi kutoka familia tajiri, ndoa n.k.

Ndoa hizo zilidumu kwa muda mrefu kwa sababu ya watoto, kuepuka aibu, kuachika ni kama kufukuzwa kazi kwavile enzi zile ndoa ilikuwa kama sehemu ya ajira, kwamba mwanamke kuolewa ni mwisho wa matatizo. Sasa ukiachwa ni wazi kuwa familia "watakufa njaa" na wewe hutoolewa tena kwani jamii ilikuwa inaamini kuoa mwanamke alieachwa ni mkosi.


Kutokana na maisha tunayoishi sasa wengi tunapata nafasi ya kupendana kwanza kabla ya kufunga ndoa, lakini baadhi hufunga ndoa kwa sababu zilizowafanya bibi na babu zetu kufunga ndoa which kwa maisha ya sasa ni sawa na kujipa kifungo/mateso ya maisha kwani ni ngumu sana kuishi na mtu usiempenda maisha yako yote.

Nitakuja kumalizia hili midaz........

Unene wa Mikono unanikosesha raha...nitaipunguzaje?

"Habari dada dinah pole na kazi ngumu uliyo nayo ya kuielimisha jamii. Nimekuwa mfuatiliaji mzuri sana wa mada zako ila sijawahi kuleta swali leo nimena na mimi nijitokeze kwa swali ili nipate msaada.

Nilikuwa sijajua tatizo langu nilipeleke wapi, nilisoma mada ya mazoezi na nikaona tu tangazo la jinsi ya kupunguza mikono minene kwa wanawake lakini sikuona maelezo ya kutosha ya nini hasa mtu anatakiwa kufanya.

Nilijitahidi sana lakini sikuona, naomba msaada wako wa maelekezo ya kufanya hayo mazoezi ya kupunguza unene wa mikono, kwani ni tatizo linanikosesha raha na ninashindwa hata kuvaa nguo za mikonoo mifupi au wazi kutokana na unene wa mikono yangu.

Mimi bado ni mdogo naomba msaada wako dada dinah, nategemea majibu yatakayo nipa furaha na nakuomba samahani kwa usumbufu."

Dinah anasema: Habari ni njema tu mdogo wangu, hujambo wewe? Asante kwa mail yako, sasa unaposema wewe bado mdogo unamaanisha ni chini ya miaka 21? Ni kweli kuna mazoezi ya kupunguza unene wa mikono kama unene wa mikono hiyo umesababishwa na unene wa sehemu nyingine ya mwili wako.

Mf kama sehemu nyingine ya mwili wako ni nyembamba lakini mikono pekee ndio minene basi utambue kuwa hili ndio umbile lako lakini kama sehemu ningine za mwili wako ni nene kama vile mapaja, kifua, kiuno, makalio n.k. ni wazi kuwa unene wa mikono utapungua ikiwa sehemu nyingine za mwili wako zitapungua yaani mwili wako ukipungua basi na mikono nayo itapumngua kwani ni sehemu ya mwili wako.

Inawezekana kabisa kuwa umeridhika na unene wa sehemu nyingine za mwili wako isipokuwa mikono....kumbuka huwezi kupewa/pata vyote hivyo kama unapenda maeneo mengine yabaki kama yalivyo itakubidi ukubali unene wa mikono yako na kuipenda kama ilivyo.

Kama asili yako (umbile lako) ni juu mkubwa ni wazi mikono yako itakuwa mikubwa tu, lakini bado unaweza kuifanya ipendeze nakuvutia na ukubwa wake sio unene tena kwani ukifanya mazoezi ya kupunguza unene/mafuta ukubwa wa mikono yako utakuwa umejengwa na misuli zaidi ya mafuta.....hivyo basi miko yako itakuwa firm na kujirudi kiasi nahivyo wewe unaona kuwa imepungua.

Ukiniambia umri wako then nitakuelekeza namna ya kufanya mazoezi ya kukaza misuli ya mikono yako ili kuepuka ukomavu, mana'ke ukifanya mazoezi haya wakati bado mwili wako unabadilika (chini ya miaka 21) ni wazi yatakufanya uonekane mkomavu.

Nasubiri jibu kutoka kwako...
Asante.

Monday

Mpenzi nampenda lakini vijimambo vyake mmh-Ushauri

"Mambo Dinah, mimi ni mpenzi mkubwa wa hii blog yako, kwa mara ya kwanza nimeamua kukuandikia ili na mie nipate ushauri. Mimi ni mwanamke wa miaka 27 nina mpenzi wangu ambae tumekua pamoja kwa muda miezi 10 sasa.

Bado tunazidi kujuana si unajua tena! huyu jamaa yuko tayari kuwa na mimi na baadae tumeamua kama penzi letu litakua mswano tutafunga ndoa na yuko tayari kwahilo ila tunataka kujuana zaidi. sasa kuna baadhi ya vijimambo mie sivifagilii kwa kweli kuhusu huyu jamaa na vitu vyenyewe ni kua anatabia ya kuchukulia vitu vidogo vidogo kuwa vikubwa that stresses me alot.

Tulikaa chini nikimwambia kuhusu hilo tatizo lakini anasema "mimi niko the same tangu mwanzo tulipokutaka ni wewe umebadilika" yaani mimi ndio mwenye matatizo kitu ambacho sikubaliani nacho lakini najaribu kustahimili .

Wakati mwingine nafikiria kuwa its too much hatujaona sasa akiamua kunioa mambo yatakuwa haya haya sasa sijui nifanyaje? nahisi labda nimbwage but naona ninampenda na yeye anasema amenifia na kweli ananionesha kama ananipenda ila pia nahisi bado nataka more and more naona kama haitoshi jinsi anavyonipenda.

So hapo ni mimi nina matatizo au inakuaje? please naombeni ushauri nimechanganyikiwa.
Mimi Waridi lisilo miba."

Dinah anasema: Mambo poua tu, vipi wewe Waridi? Mapenzi ni kitu cha ajabu sana sio tu kwavile hujui lini utamdondokea mtu kimapenzi pia hujui wapi wala nani hasa utapendana nae na je huyo utakaempenda atakuwa na kasoro/tabia gani? Kama tungekuwa tunajua ni wazi watu wengi tusingekuwa kwenye mahusiano achilia mbali ndoa.

Unapokutana na pea/wenza wanaopendana sana kwa kuwaangalia tu unajua hawa watu wanapendana kweli kweli lakini kama ungejua wanayokumbana nao huko ndani kutokana na tofauti zao (ndio tunaziita kasoro) unaweza ukashangaa. Mapenzi sio mteremko, kwamba umependa na yeye kakupenda basi utapenda kila kitu.....hapana, kuna vitu huwa tunajitolea mhanga na kuamua kuishi navyo....unadharau au unachukulia kawaida.


Hujasema kwa uwazi au hata kutoa mifano miwili ya vitu hivyo "vidogo vidogo" ambavyo yeye anachukulia kama vikubwa, je ni wewe kutumia muda wako mwingi na "marafiki" wa kiume? Kuchat/pigiwa simu mara kwa mara na wanaume/wanawake asiowajua, kwenda baa na mashoga sijui shosti bila yeye? masuala ya kingono? kutumia vibaya pesa anazokupa? wewe kumuomba senti mara kwa mara? Ulevi? kutokusafisha nyumba/chumba chako (Uchafu labda)?n.k.....hivi vyote nilivyotaja ni vikubwa kwa mwanaume yeyote anaekupenda?


Kitu kizuri ulichokifanya hapo ni kuwa wazi na kuwakilisha hoja yako kwake japokuwa yeye kakataa, kwasabau yeye ndio mwenye tatizo haoni kuwa ni tatizo isipokuwa wewe mtu wa pili. Lakini tatizo lake linaweza kuwa limesababishwa na tatizo lako yaani kw akifupi tofauti zenu kama watu sio wapenzi mwanamke na mwanaume.

Kwavile wewe unadharau vitu au mambo fulani kwa kudhani ni madogo kwake yeye ni vikubwa. Kumbuka ninyi ni wati wawili tofauti sio tu kijinsia, kimalezi, uwezo wa kufikiri, uelewa, mazingira mliyokulia n.k......sasa hapa unatakiwa kujifunza na kugundua ni vitu gani hasa ambavyo wewe kwako ni vya kudharau lakini kwake ni vikubwa? na kuvichukulia anavyovichukulia yeye au hata kuepuka kuvifanya.

Kutokana na maelezo yako ni kweli mnapendana na sababu uliyoitoa sio muhimu ya kukufanya wewe uachane na huyo Mpenzi, kama unafikiria kumuacha mtu kwa vile tu mnapishana kidogo kutokana na tofauti zenu kama individuals.....je ukimkuta kakunja mwanamke mwingine utafanya nini?

Kumbuka moja kati ya nguzo muhimu za kuimarisha mahusiano ya kimapenzi ni kuelewana, ukimuelewa mpenzi wako na kujitahidi kuepuka kufanya vitu vidogo kwako lakini kwake ni vikubwa, hakika mtaendesha maisha mazuri yenye amani.

Lazima kuna kitu au vitu ambavyo havipendi na vinamuudhi lakini kwa vile anakupenda anavifumbia macho, so why dont you do the same? Umuhimu wa uhusiano kabla ya ndoa (ni kinyume na maadili ya Imani zetu za Dini though) ni kuwa unapata nafasi ya kujifunza kuhusu mwenzio kila siku na hivyo kujipa nafasi ya kuyazungumzia na kuelewana ili kuandaa maisha yenu ya baade kama mke na mume.

Kila la kheri!

Sunday

Ushuhuda!!

"Habari Dinah,
Mimi ni yule mwanamke niliyetuma ujumbe kuhusu msg tata niliyotumiwa na mwanamke kuhusu mume wangu na namna mume wangu alivyomisbihave. Nashukuru Mungu kwani ile siku nilichanganyikiwa sana lakini zifuatazo ni step nilizopitia nataka na wanablog wengine wa D’HICIOUS wasome nao ikitokea wana shida kama mimi wafanyeje.



Pia nashukuru wachangiaji wengi kwa comments zao nyingi zikielekeza vizuri . Mtarejea maelezo yangu ile siku, mchana nilimtumia msg mume wangu nikamwambia majibu aliyonijibu asubuhi na mwenendo wake ni dhahiri kuwa anamwanamke mwingine na nikamwambia kuwa kama hatajirekebisha na kutulia na familia yake Mungu wa mbinguni atakwenda kumpa adhabu hapa hapa duniani.



Huwezi amini alituma msg ya kushuka na kuniomba kabla sijarudi home tukutane mahali tulivu tuongee. Akanambia kuwa yeye hana uhusiano na mwanamke mwingine isipokuwa anaomba msamaha kwa yale aliyosema akidai aliropoka kwa vile mie nilimfokea na kumwambia lazima kuna kitu anaficha.



Anasema hakupenda ile tabia na ndio ikamuipress aseme vile, tukarekebisha tofauti zetu na amezidisha mapenzi zaidi ya yale ya mwanzo. Anawahi kurudi kama kawaida, muda mwingi tunazungumzia mipango ya maendeleo yetu.



Namshukuru Mungu kwani nilikuwa nimeanza kufikiria kuondoka zangu maana maneno yale yalikuwa mazito.

Ushauri: Ndoa inahitaji uvumilivu, kuna mambo yanarekebishika, unaweza kuamua kudivorce kumbe ilitokea bahati mbaya. Tuvumilieni. Nawashukuru sana kwa mawazo yenu."

Monday

Uongozi wa Dini umenaharibu, je niendelee kumsubiri?

"Hi Dinah!
Naitwa a.k.a Doctor nikiwa hapa Dar. Nina mpenzi ambae anasoma Chuo kimoja hapa nchini, mwanzoni tulipendana sana hadi ikafikia tukapanga tuoane atakapomaliza masomo yake mwaka 2012.

Lakini alipoanza tu Chuo 2009, wiki mbili zikapita akakata mawasiliano ghafla! Nimeonana naye tena mwezi uliopita baada ya kurudi kutoka Chuo na akasema anataka uhusiano wetu uishe kwani anataka kusoma na amechaguliwa kuwa kiongozi kwenye kikundi cha Dini.

Hivyo anahitaji muda mwingi wa kufanya shughuli hizo. Kwa kweli simwelewi kabisa huyu binti, maana siku nyingine ukimpigia simu ili kupanga mihadi ya kuonana anakuja vizuri tu, siku nyingine ukimpigia simu ananikatia.

Yaani simwelewi au nimpige chini kabisa, nitafute mrembo mwingine maana nahitaji binti wa kuishi naye ifikapo 2011 au 2012. Naomba maoni ya wadau. Nipo katikati ya bahari na sijui wapi pa kuanzia!!!!!!"

Dinah anasema: Doctor asante kwa ushirikiano wako, kuzungumzia na kukubaliana kuwa siku moja mtafung andoa sio tiketi ya mtu kubaki na wewe, kama kweli uko serious unatakiwa kuchumbia kwa vitendo (jitambulishe kwao nakufuata taratibu zote) nadhani huyu Binti ameamua kuzingatia masomo yake kwanza bila kuchanganya mapenzi na wakati huohuo kaamua kubadili mtindo wa maisha yake na kumtumikia Mungu ktk hali halisi ni jambo jema sana hasa ukilichukulia kwa upande mwingine.

Mf: Badili kabao wewe uwe kaka wa huyo binti, kwambatufanye ni mdogo, hivi angekuwa na mpenzi ambae wewe kama kaka unaona kabisa kuwa "jamaa" ataharibu maisha ya kimasomo ya mdogo wako hata kama atamuoa (which sio guarantee as hajachumbia kwenu)......alafu kwa bahati nzuri mdogo wako huyo wa kike kachaguliwa kwenda Chuoni na ghafla akaamua kuachana na "jamaa" ili azingatie masomo yake Chuoni.....ungejisikiaje kama kaka?!!


Kama nia yako ni kufungandoa mwakani au mwaka unaofuata haimfanyi huyo Binti kutaka kuolewa muda huo pia, lakini kama mlipokuwa pamoja na mkajadili suala la ndoa muda huo na alipojiunga na Chuo/Uongozi wa Dini akaomba uhusiano wenu ufe ni wazi kuwa Imani yake ya Dini kama zilivyo nyingine zote hasikubaliani na mahusiano ya kingono kabla ya Ndoa.

Mimi nadhani ni vema kuheshimu uamuzi wake na kumpa muda ili azingatie masomo yake(huenda atabadili mawazo), usijenge hasira/chuki na ikiwezekana endeleza urafiki na mawasiliano ya mara kwa mara mpaka utakapokutana na mwanamke ambae atakuwa tayari kuolewa na wewe kipindi ulichojipangia bila kuwa na majukumu ya Kimasomo wala Dini.

Kila la kheri.

Wednesday

Nataka kuacha Mpenzi lakini naonea huruma watoto wangu-Ushauri

"Mambo vipi dada Dinah
Pole na kazi na hongera sana kwa kazi hii ya kutoa ushauri.
Mimi ni kijana mwenye umri wa miaka 32 kwa sasa ninaishi na mwanamke ambaye ninae kwa miaka nane sasa na tumebahatika kupata watoto wawili mmoja wa kiume na mmoja wa kike.

Mwanzo wa maisha ki ukweli tulikuwa tunaishi vizuri tu lakini kadri miaka inavyozidi kwenda mambo yamekuwa yanabadilika na tatizo kubwa naweza sema limekuwa sugu, nasema hivyo sababu ni tatizo la muda mrefu na nimejaribu kuliongelea lakini naona hakuna mabadiliko yoyote na hakuna sababu za msingi anazotoa .

Dada Dinah huyu mwanamke swala la kunipa unyumba kiukweli limekuwa ugomvi yaani hataki na hatoi sababu za msingi kama ambavyo nimeeleza hapo juu. Sasa nimechoka sana na nafikiria mambo mengi sana moja kubwa ni kuachana naye lakini nikifikiria watoto wangu nakosa raha.

Nafikiria katafuta mwanamke wa nje ambaye tutatimiziana hayo mambo hapa pia dada naogopa sana UKIMWI, siku chache zilizopita nilifikiria kupiga punyeto na nilivyofanya hivyo kwa kiasi fulani ilinipunguzia hamu lakini nitaendelea kufanya mapenzi na mkono wangu hadi lini?

Dada naomba ushauri nifanyeje?
Asante
J.M. KURASINI."
Dinah anasema: JM mpendwa asante sana kwa ushirikiano. Sasa kaka yangu umekaa na huyo dada miaka 8 na kakuzalia watoto wawili bado hujatangaza ndoa na inaonyesha huna mpango huo, yeye kama mwanamke hiyo hamu ya kungonoana na wewe kila utakapo ataitoa wapi?

Kama mwanamke hasa wa Kibongo hapo umemharibia maisha, kwanza kazaa watoto wawili (hakuna mwanaume atataka kuoa mwanamke mwenye mzigo), pili amekuwa nje ya "soko" kwa muda mrefu na hivyo itakuwa ngumu sana kwake kujiingiza kwenye masuala ya kimapenzi na mtu mpya.....miaka nane sio mchezo!

Kitu kikubwa ni kuwa umempotezea hali ya kujiamini na inaelekea wazi kabisa wewe huna hisia za kimapenzi nae (kwenye maelezo yako hakuna mahali umegusia kumpenda) tena bali uko nae hapo kwa ajili ya Ngono ambayo sasa huipati na inakufanya utake kutoka nje na watoto. Kinachokuzuia kutoka nje au kumsaliti ni UKIMWI, vinginevyo unekuwa na kimada.

Huyu dada kisheria ni ana haki zote kama Mkeo kwa vile mmeishi pamoja zaidi ya miaka 2, lakini hiyo haitoshi mpaka hatua zote kijamii zitakapofuata na kufunga ndoa kama wanavyofunga wengine.......kama alivyogusia mchangiaji, hicho ni kitu pekee huyu mdada anakitaka kutoka kwako.

Inaelekea alifanya yote ili kukufanya utangaze ndoa lakini hukufanya hivyo, akaamua kushika mimba mara mbili na kufanikiwa kuzaa wewe bado huna habari na ndoa, amendelea kuishi na wewe na sasa ni miaka nane (muda mrefu kuliko wanandoa wengi) lakini wewe ndio kwanza una-demand Ngono badala ya kutafuta tatizo ni nini hasa.

Huyo ni mwanamke, na ndoto ya mwanamke yeyote ni siku moja kufunga ndoa na mwanaume ampendae, huenda kwa wanaume hili ni suala la kijinga lakini kwa mwanamke ndoa ni kitu muhimu sana kwenye maisha yake.

Nini cha kufanya: Rudisha hisia za mapenzi kwenye uhusiano wako (kwani inaonyesha wewe umejisahau na yeye amekata tamaa kama sio kachoka), Muonyeshe huyu mama ni namna gani unampenda, onyesha kuwa bado unavutiwa nae japokuwa amezaa watoto wawili kwani mwanamke anapozaa mara mbili na zaidi mwili wake hubadilika.

Hivyo "Kisaikolojia" anaanza kuamini kuwa havutii tena na vilevile uke wake hauko vile ulivyokuwa awali na hivyo kujishtukia kuwa hatoweza kukuridhisha (anaweza kuwa na aibu pia), sasa kwa vile wewe hujui au hujali unadhani yeye anakunyima lakini ukweli ni kuwa humpi ushirikiano na wala huonyeshi kuwa bado unavutiwa na umbile lake.

Fanya yale yote ambayo ulikuwa ukimfanyia mwanzo wa maisha yenu kama wapenzi, unapohisi kutaka ngono usimuombe kama vile "haki yako" au "jukumu lake" bali itake ngono kwa kuonyesha mapenzi, kwa kumshika nakucheza na mwili wake, jitahidi kumfanya ajisikie kuwa anapendwa.....akielekea endelea lakini akigoma basi usimlazimishe na badala yake muulize kwa upole na upendo tatizo ni nini?

Usilalamike, bali tafuta ukweli kutoka kwake....."kitu gani nakosea mpenzi", " asali wa Moyo kwanini hutaki tufanye mapenzi?"....."naomba uniambie kama nimekosea nijirekebishe".....alafu mmwagie misifa (kulingana na kile unachokipenda na una uhakika anajua kuwa ni kweli).

Jinsi siku zinavyozidi kwenda ongeza kuonyesh amapenzi kisha tangaza ndoa(ndani ya mwezi mmoja), mchumbie mama watoto wako na mfunge ndoa. Nina kuhakikishia utaona mabadiliko na kila kitu kitakuwa sawa mara tu baada ya huyu dada kuwa na uhakika kuwa mnakwenda kufunga ndoa.

Hakikisha unafunga ndoa kiukweli,
Kila la kheri!!

Tuesday

Nahisi naibiwa, je niamini hisia zangu au?-Ushauri

"HABARI DADA DINAH,
POLE SANA KWA KAZI NZITO YA KUELIMISHA JAMII.
MIMI NI MWANAMKE MWENYE UMRI WA MIAKA 29 ,NINAMPENZI WANGU SASA YAPATA MIAKA MIWILI TANGU TUANZE MAHUSIANO, ILA NINAHISI KAMA VILE YUKO NA MSHICHANA MWINGINE.

HUWA HAPENDI NIENDE KWAKWE AKIDAI KWAMBA ANAHOFIA WADOGO ZAKE ANAOISHI NAO, MARA NYINGI HAPENDI TUWEPAMOJA MFANO WIKIENDI MUDA MWINGI ATASEMA YUKO NA RAFIKI ZAKE.

YAANI NAHISI KUNA JAMBO ANALOLIFICHA NA NAHISI ANAMWANAMKE MWINGINE ZAIDI YANGU, DADA NAOMBA USHAURI JE NIAMINI HISIA ZANGU AU NIFANYE NINI?
MAGDALENA
DAR ES SALAAM"

Dinah anasema: Magdalena mpendwa, dalili ya kwanza kabisa kuwa mtu anakupenda ni kutumia muda wake mwingi na wewe, kutambulishwa kwa ndungu, jamaa na marafiki zake ni dalili ya pili kuwa kafika kwako, kuwa wazi na huru kuwa na wewe au kukuonyesha kwa watu wake wa karibu ni dalili ya tatu, Mpenzi kutokuthamini mtu mwingine yeyote (rafiki zake) bali wewe na kama kuna shughuli/sherehe basi utakuwa wa kwanza kujulishwa na kushirikishwa kabla ya rafiki na jamaa wengine.

Haya yote hufanyika kwenye hatua za mwanzo kabisa za uhusiano wa mtu yeyote, miaka miwili ni mingi sana kwa mtu kuendelea kukufanya wewe "mpenzi wa siri" kwa wadogo zake.

Natambua suala la yeye kukutambulisha au kukupeleka nyumbani ili kuepuka vishawishi kwa wadogo zake hasa kama wako kwenye umri wa kushawishika (kubalehe), wanaweza wakadhani kuwa na girlfriend/boyfried na kumpeleka nyumbani ni kawaida kwa vile kaka anamleta wake hapa.

Lakini vilevile inawezekana anahofia wadogo zake kuuliza kuhusiana na mwanamke mwingine ambae labda wanamfahamu, ili kuondoa utata jamaa inabidi akatae wewe kufahamu nyumbani kwake n.k.

Mpenzi anapokuwa na tabia ambayo wewe unadhani kuwa sio kawaida au hajawahi kuwa nazo kabla hukupa maswali na hofu, vilevile kama unabahati pia unaweza kupata hisia fulani ambazo huwa zinawatokea watu wachache, zinajulikana kama "the sixth sense" inakuwa kama "maono fulani hivi", kama kuna kitu kinatokea behind your back you just know.

Lakini kabla hujakurupuka na kumshutumu mtu kuwa anafanya maovu, unatakiwa kufanya uchunguzi wa karibu ili kuwa na uhakika ili kufanya uamuzi wa maana.

Nini cha kufanya:Punguza ulalamishi kwamba usimuulize wala kulalamika kuhusu tabia yake ya kukukwepa na punguza mawasiliano na huyo Boyfriend wako. Ikiwa unajua mahali anapoishi basi fuatilia kwa karibu ili kujua nini kinaendelea pale nyumbani, je kuna mke(mwanamke mwingine n.k.).

Badilisha mtindo wako wa kimaisha kwa kuwa mwanamke mmoja anaevutia kuliko kawaida, hakikisha unajipenda na kujijali zaidi, vaa mavazi yanayokukaa vema kulingana na umbile lako (usilifiche) ili uvutie zaidi.

Ukiomba kuwa nae mwisho wa wiki na yeye kudai kuwa anakwenda kutumia muda wake na rafiki zake, kuwa calm na muulize kwa upendo ni wapi huko anakoenda? ukijua kona anazopenda kutembelea basi ibuka huko bila yeye kujua, ukifika hapo mahali endelea na starehe zako lakini hakikisha kuwa amekuona.

Baada ya kufanya haya utakundua ukweli na hivyo itakusaidia kufanya uamuzi wa busara ili uweze kuendelea na maisha yako hasa kama kweli ni cheater na pengine kukupa nafasi ya kuweza kukutana na mwanaume atakaejali hisia zako, atakae kuthamini, kukupenda kwa dhati, mwanaume atakae kuweka wewe juu/wa kwanza kabla ya rafiki zake.

Ikiwa umegundua kuwa ni mwanaume mwema lakini hajui namna ya kumpenda mwanamke then itakubidi umfundishe, umuelekeze namna ya kujali na kuthamini mpenzi, kuweka wazi hisia zako na kumwambia ni namna gani unapenda kutumia muda wako mwingi na wewe. Mueleze kuwa hupendezwi na siri na usingependa uhusiano wenu uwe siri, ungependa "Dunia" ijue kuwa ninyi ni wapenzi.....ukianzia na wadogo zake, ndugu, jamaa na marafiki.

Kila la kheri kwenye umauzi utakaoufanya kutokana na matokeo utakayo yapata.

Monday

Babu kicheche! lakini ananisomesha, nimpendae ni Kijana ambae.....

"Habari dada Dinah, natumaini wewe mzima, First and foremost thanks for the advice najua sijawahi kuuliza but seems like we all face the same problems.

Mimi ni mwanamke wa miaka 27 niko njia panda na sina mtu wakunisaidia zaidi yako. Niko kwenye relationship na watu wawili nasijui nifanyeje? Sitajali kama watu wakinishambulia kwasababu nahitaji msaada.

Nimekuwa kwenye relationship na baba mmoja mwenye umri wa miaka 60 kwa muda wa miaka 5, huyu baba amekuwa akinisaidia kwa kila kitu ukichukulia mie sifanyi kazi. Amenisomesha chuo cha bei ghali, ananijali na kunipenda kwa kweli lakini tatizo ni hili hapendi nifanye kazi japokuwa ndio namaliza degree yangu mwaka huu.

Hapendi niwe na marafiki na ikitokea nimetoka na marafiki nikirudi anakuwa hayuko happy, nikienda mahali ambako anakujua basi atanifuata kwa kisingizio cha kuja kunichukua. Hapendi ni-have fun like going to the disco or any activity.

Ajabu for the last few years ambayo tumekuwa pamoja amekuwa na wasichana wengi since anasafiri sana na kila mahali anakokwenda analala na wasichana but yote nimevumilia na sikuwahi kummuuliza kwasababu naogopa kukatishiwa huduma.

Miaka miwili iliyopita tulihama Tz na sasa tuko Australia still ananipenda na kunihudumia na bado akiwa anasafiri ana-sleep na wanawake wengine. Anapenda kuzungumzia mambo ambayo mimi sina mpango wa kuyafanya.

Kwa muda wa miaka minne amekuwa akiniomba tigo lakini nimekuwa nikikataa pia huwa anataka 3some na marafiki zangu na tukiwa tunasex anataja majina ya marafiki zangu na siku hizi tunaweza kukaa bila sex hata miezi miwili ila blow jobs nampa karibia every other day.

In a positive side yaani tunapatana, kuelewana na ananisaidia na mambo mengi sana ya kimaisha lakini tatizo hatujaoana na mie sijajijenga japokuwa nina vipesa bank bt sio vingi ki-hivyo, also nikiwa na idea za kufanya vitu au kutafuta kazi ana-ni turn down.

Ki-ukweli mie niko very bright na nikiamua na kupata mtu atakayenipush hapa na pale nitafika mbali, huwa najiuliza je akifa leo nitafanyaje kwa kuwa sina chochote na yeye hawezi kuniachia chochote kwasababu ana watoto na watoto wake hawajui hii relationship yetu, yaani hata ndugu zake pia hawajui isipokuwa ndugu yake mmoja tu ndio anajua.

Basi nikiwa huku nikakutana na mkaka yeye ana 38yrs, nilimsumbua 4 a year but akawa mvumilivu thereafter nikajikuta niko nae nikamdanganya kuwa that old man ni baba yangu, this guy ananipenda ajabu, amenitambulisha kwa rafiki zake wote na anatarajia kunipeleka nchini kwao kunitambulisha.

He’s so sweet yaani tuna-click big time na niko huru ku-speak my mind sex is great,ananijali,I’m in love & happy with him. Sijawahi kujisikia like this all my life, yaani naamini ananipenda for sure. Nikimwambia idea zangu anazikubali na ananipush nitafute maisha yangu, although sijamwambia relation iliyoko between me na this old man.

The problem is he’s married na hajanificha he has 5 kids all I know there’s a tension between yeye na mkewe for sometime now & he’s not happy with her.

Dada Dinah na walimwengu nifanyeje?what I have planed ni kuwa nikimaliza degree yangu at the end of ths year nitafute kazi nchi nyingine nihame niwaache wote nianze maisha upya as mimi? Kwa abilities nilizonazo naamini nitafika mbali sana.
Samahi kwa email ndefu,
Ahsante
Ni mimi PP"
Dinah anasema: PP asante sana kwa ushirikiano na maelezo yako. Babu anakutumia kama ambavyo wewe unamtumia (kwenye maelezo yako umesema anakupenda na mnaelewana, hujasema unampenda). Ikiwa mnapitisha miezi hata miwili bila ngono ni vema hasa ukizingatia kuwa anakuchanganya na wanawake wengine hun ajinsi ya kumkataza wala kulalamika kwa vile unajua wazi ukifanya hivyo atasitisha huduma hasa ile ya Kielimu.

Sio kwamba na-support kuwa na mwanaume bil amapenzi ili kupata unachokitaka (kumchuna) bali kutokana na maelezo yako inaonyesha kuwa life haiko sawa nyumbani na ndio maana unasomeshwa na huyo babu mzungu, wee sio wa kwanza.

Wapo kina dada wengi tu hapo Dar, huondoka na vijibabu vya kizungu na hata kufunga navyo ndoa kwa sababu za ikuchumi lakini hakuna mapenzi, so ugumu wa maisha na tamaa ya kuendesha maisha ya juu inafanya Mabinti wadoo wengi kufanya unachokifanya, ikiwa sasa una miaka 27 na umekuwa na huyo babu kwa miaka 5 ni wazi umekuwa nae ukiwa na miaka 22.

Kutokana na maelezo yako inaonyesha unajua nini ulikuwa unakifanya na kukitaka......Elimu na maendeleo yako kimaisha, sasa ukifanikisha hili ni vema kufanya kama ulivyosema kuhama nchi na kuanza upya.

Nini cha kufanya: Wakati unaendelea na haratati za kumalizia Digrii yako hakikisha unaachana na huyo mume wa mtu na jitahidi kutumia kinga kila mara huyo kibabu anapotaka ngono na wewe ili kujilinda.....kama unaweza usimpe kabisa mwili wako kwa kutafuta sababu atakazoziamini.

Kwa vile ni babu na mzungu haina maana kuwa hapati Ngoma, Australia wanapima Ngoma wageni lakini watu wao hawawapimi Ngoma wanapotoka na kuingia hivyo wanapokwenda Afrika au nchi nyingine na kungonoka ovyo uwezekano wa kuukwaa UKIMWI ni kuwa kuliko unavyofikiria. Kuwa mwangalifu, usipoteze maisha yako ktk umri mdgo ulionao.

Baadhi ya mabinti wanaoondoka nyumbani na vibabu vya Kikoloni (kizungu) huishia kufanya sex slaves (watumwa wa ngono), wengine hulazimishwa kuwa makahaba, wengine huteseswa na baadhi huishia kuuwawa.

Baadhi ya Wazungu bado ni wabaguzi, na wanapopata nafasi ya kumiliki binti wa Kiafrika huishia kufawafanyia maovu na mabaya mengi (kuwangonosha na wanyama, kuwafanya watumwa, kuwauza kwa Wazungu wenzao ambao hawajawahi kutomba wanawake weusi ambao wengi wanaamini kuwa ni watamu,kuwafanya mande n.k), kuweni waangalifu mnapojichanganya na hawa jamaa wanaokuja kutembea Bongo kwa ajili ya Ngono (Sex tourists).

Ni matumaini yangu Post hii ya PP itakuwa imesaidia mabinti wengine wanaibabaikia Wazungu wanakuja kutembelea Tanzania wakidhani ni mwisho wa matatizo, baadhi bado wanaunyama miyoni mwao dhidi ya Muafrika.

Kila la kheri kwenye masomo yako na katika kuhama makazi.

Pages