Monday

Mpenzi nampenda lakini vijimambo vyake mmh-Ushauri

"Mambo Dinah, mimi ni mpenzi mkubwa wa hii blog yako, kwa mara ya kwanza nimeamua kukuandikia ili na mie nipate ushauri. Mimi ni mwanamke wa miaka 27 nina mpenzi wangu ambae tumekua pamoja kwa muda miezi 10 sasa.

Bado tunazidi kujuana si unajua tena! huyu jamaa yuko tayari kuwa na mimi na baadae tumeamua kama penzi letu litakua mswano tutafunga ndoa na yuko tayari kwahilo ila tunataka kujuana zaidi. sasa kuna baadhi ya vijimambo mie sivifagilii kwa kweli kuhusu huyu jamaa na vitu vyenyewe ni kua anatabia ya kuchukulia vitu vidogo vidogo kuwa vikubwa that stresses me alot.

Tulikaa chini nikimwambia kuhusu hilo tatizo lakini anasema "mimi niko the same tangu mwanzo tulipokutaka ni wewe umebadilika" yaani mimi ndio mwenye matatizo kitu ambacho sikubaliani nacho lakini najaribu kustahimili .

Wakati mwingine nafikiria kuwa its too much hatujaona sasa akiamua kunioa mambo yatakuwa haya haya sasa sijui nifanyaje? nahisi labda nimbwage but naona ninampenda na yeye anasema amenifia na kweli ananionesha kama ananipenda ila pia nahisi bado nataka more and more naona kama haitoshi jinsi anavyonipenda.

So hapo ni mimi nina matatizo au inakuaje? please naombeni ushauri nimechanganyikiwa.
Mimi Waridi lisilo miba."

Dinah anasema: Mambo poua tu, vipi wewe Waridi? Mapenzi ni kitu cha ajabu sana sio tu kwavile hujui lini utamdondokea mtu kimapenzi pia hujui wapi wala nani hasa utapendana nae na je huyo utakaempenda atakuwa na kasoro/tabia gani? Kama tungekuwa tunajua ni wazi watu wengi tusingekuwa kwenye mahusiano achilia mbali ndoa.

Unapokutana na pea/wenza wanaopendana sana kwa kuwaangalia tu unajua hawa watu wanapendana kweli kweli lakini kama ungejua wanayokumbana nao huko ndani kutokana na tofauti zao (ndio tunaziita kasoro) unaweza ukashangaa. Mapenzi sio mteremko, kwamba umependa na yeye kakupenda basi utapenda kila kitu.....hapana, kuna vitu huwa tunajitolea mhanga na kuamua kuishi navyo....unadharau au unachukulia kawaida.


Hujasema kwa uwazi au hata kutoa mifano miwili ya vitu hivyo "vidogo vidogo" ambavyo yeye anachukulia kama vikubwa, je ni wewe kutumia muda wako mwingi na "marafiki" wa kiume? Kuchat/pigiwa simu mara kwa mara na wanaume/wanawake asiowajua, kwenda baa na mashoga sijui shosti bila yeye? masuala ya kingono? kutumia vibaya pesa anazokupa? wewe kumuomba senti mara kwa mara? Ulevi? kutokusafisha nyumba/chumba chako (Uchafu labda)?n.k.....hivi vyote nilivyotaja ni vikubwa kwa mwanaume yeyote anaekupenda?


Kitu kizuri ulichokifanya hapo ni kuwa wazi na kuwakilisha hoja yako kwake japokuwa yeye kakataa, kwasabau yeye ndio mwenye tatizo haoni kuwa ni tatizo isipokuwa wewe mtu wa pili. Lakini tatizo lake linaweza kuwa limesababishwa na tatizo lako yaani kw akifupi tofauti zenu kama watu sio wapenzi mwanamke na mwanaume.

Kwavile wewe unadharau vitu au mambo fulani kwa kudhani ni madogo kwake yeye ni vikubwa. Kumbuka ninyi ni wati wawili tofauti sio tu kijinsia, kimalezi, uwezo wa kufikiri, uelewa, mazingira mliyokulia n.k......sasa hapa unatakiwa kujifunza na kugundua ni vitu gani hasa ambavyo wewe kwako ni vya kudharau lakini kwake ni vikubwa? na kuvichukulia anavyovichukulia yeye au hata kuepuka kuvifanya.

Kutokana na maelezo yako ni kweli mnapendana na sababu uliyoitoa sio muhimu ya kukufanya wewe uachane na huyo Mpenzi, kama unafikiria kumuacha mtu kwa vile tu mnapishana kidogo kutokana na tofauti zenu kama individuals.....je ukimkuta kakunja mwanamke mwingine utafanya nini?

Kumbuka moja kati ya nguzo muhimu za kuimarisha mahusiano ya kimapenzi ni kuelewana, ukimuelewa mpenzi wako na kujitahidi kuepuka kufanya vitu vidogo kwako lakini kwake ni vikubwa, hakika mtaendesha maisha mazuri yenye amani.

Lazima kuna kitu au vitu ambavyo havipendi na vinamuudhi lakini kwa vile anakupenda anavifumbia macho, so why dont you do the same? Umuhimu wa uhusiano kabla ya ndoa (ni kinyume na maadili ya Imani zetu za Dini though) ni kuwa unapata nafasi ya kujifunza kuhusu mwenzio kila siku na hivyo kujipa nafasi ya kuyazungumzia na kuelewana ili kuandaa maisha yenu ya baade kama mke na mume.

Kila la kheri!

No comments:

Pages