Wednesday

Nenda taratibu lakini changamka!



Mara nyingi mwanawake huwa anapenda au kutaka kuwa kwenye uhusiano wa kimapenzi na kila kitu kiende sawia kabisa bila matatizo, hii ni kutokana na sababu nyingi tofauti kama vile kuwa mpweke kwa muda mrefu, kuwa na "foleni"ndefu ya mahusiano mafupi na sasa anahisi kuwa wakatiumefika wa kukaa na kutulia na mtu mmoja, uoga wa kuachwa/kuumizwa, kuhisi ameachwa(left out) kwa vile rafiki zake wanawapenzi, kuhisi umri umekwenda n.k.


Haijalishi unauzoefu mbaya au mzuri ktk mahusiano yakimapenzi…unachotakiwa kufanya ni kutuliza akili na kucheza taratibu. Ukichukulia mambo taratibu itakusaidia sana kujua hisia zako juu ya mwenzio na pia kumjua/fahamu huyo mpenzi kabla mambo hayajawa “makini” hali itakayokusaidia kutoumia sana ikiwa atagundua kuwa humfai au wewe kutambua kuwa hayuko vile ulivyotegemea n.k.


Vilevile kwenda kwako taratibu kutamfanya huyo “mpenzi mpya” kuwa “comfortable” na wewe, kwa vile hautokuwa mtu wa kulazimisha mambo yatokee vile unavyotaka……..wanaume wengi hawapendi kuwa “pushed” kwa vile uhisi hawapendwi bali unapenda kufanikisha jambo fulani kama ktk maisha yako na sio kwenye maisha yenu “as a couple”.


Kumbuka kuwa wanaume hutumia uongo mwingi ili “washinde” na wakupate, hivyo kuwa mwangalifu najifunze “kuchuja” maneno/mistari yao wanapokushawishi/tongoza uwe nao, mara nyingi hutoa ahadi nyingi ambazo hu-“sound” kama wanaji-“commite” kwako kabla hata hujawajua vema.


Wewe kama mwanamke unatakiwa kuwa makini, msikivu, mwelevu na mwepesi kuhoji ikiwa utahisi unayoambiwa ni “too much….too soon”, sio macho chini na kila kitu….Ok, haya, sawa, ai wewe……ndio…..wasema kweli mjuba…hihihihi..n.k.……changamka!


Kumbuka kitakacho kufanya umdondokee mtu kimapenzi kabla hata ya kungonoana sio muonekano wake tu (au pesa kwa wengine wazembe-wazembe) bali kumjua kiundani baada ya kuzungumza nae……unapomhoji mwenzio ni rahisi kujua uta-offer nini kwenye uhisiano ili uwe bora na yeye atachangia vipi ili mtoke “pea” nzuri na ya muda mrefu.


Maelezo yake kutokana na maswali yako yatakuwezesha wewe utafakari na kufanya uamuzi wa busara hali kadhalika maswali yako yatamfanya yeye afikiri zaidi ikiwa ni myeyushaji/muongo lakini “anakutaka” basi anaweza kubadili yote aliyosema/ahidi jana kwani kagundua kuwa wewe sio wa kudanganyika…..na akiendelea hamtofika mabli….hii yote nitakuwa imetokana na kuchangamka kwako kwenye kuhoji pale ulipohisi jamaa natoa ahadi kamavile ninyi ni “couple” tayari kumbe ndio kwanza mna-date.


Kumbuka mtu anapoku-“date” haina maana kuwa mko kwenye uhusiano na mara nyingi hushauriwi kufanya ngono ktk kipindi hicho……”date” inaweza kuchukua siku tatu mpaka miezi 4 kabla hujajitolea mwili wako.

Unaswali?

Sunday

Unatarajia nini unapoelekea kwenye uhusiano?





Kuna swala la wanawake kudhani kuwa "ndio imetoka hiyo" yaani ndio milele, mara tu anapoanzisha uhusiano na mwanaume……..

na kwa bahati mbaya wengi huishia “disappointment” na kuwaita wanaume wa kibongo hawana mapenzi ya kweli…….sio hawana mapenzi ya kweli bali wewe ndio ulikuwa na haraka au nyote wawili mlikuwa na haraka na hamjui nini maana halisi ya neno “mapenzi”.


Siku hizi vijana tunaharaka sana ya kufanya mambo ambayo hufanywa kwenye commitment relationships sasa sijui ni maendeleo au ni wanaume kutokuwa wazi pale wanapotaka kuwa na uhusiano fulani na mwanamke?


Napenda utambue kuwa kukutana na mwanaume/mwanamke na kuwa nae na kupena miili yenu haina maana huyo ni uhusiano tayari, uhusiano hujengeka baada ya kutoka na huyo mtu kwa muda fulani minimum miezi kama 3 hivi au zaidi……

Hata kama alikujia na gia ya “nataka uwe mpenzi wangu”…..huwezi ukawa mpenzi ktk siku chache……unahitaji muda kuwa na uhakika na hisia zako.


Unajua zamani watu walipokuwa wakikutana, walikuwa hawakimbilii kungonoana, walikuwa wanaheshimiana na kama ni kukutana basi inakuwa mahali peupe kuepusha vishawishi vya kungoana na hali hiyo iliwawezesha kuvuta muda na kuwa na uhakika na hisia zao kuwa kweli wanapendana.


Na ndio maana wakati huo walikuwa wakiamini (jua) kuwa mwanaume akikupenda kweli basi atavumilia na atakuja kuwaona wazazi na kufunga ndoa na wewe……ndio kungonoka kunafuata.


Tofauti na sasa ambapo tuna swala la ku-date ambapo penzi la huibuka....…kisha tunahamia kwenye Trial (move in together and all) na kuangalia mambo yanavyokwenda….je mnapatana? mnaendana ki-life style, kingono mko sawa n.k.


Alafu ndio penzi la dhati hujengeka vema zaidi kwa vile utakuwa unamjua mwenzio kwa undani na hivyo kufanya uamuzi wa busara kama unaweza kumvumilia na kushi nae maisha yako yote au la.


Natambua kuwa kuna watu wengi (hasa wanawake) wanaendeleza imani kuwa kama mwanaume anakupenda kweli basi atakwenda kujitambulisha kwa wazazi wako na atafunga ndoa na wewe……..


Kutokana na nyakati hizi za mwisho I MEAN SAYANSI YA TEKINOLOJIA a.ka maisha ya kisasa ni wazi kuwa hawajui tofauti ya kupendwa na uamuzi wa kuishi na wewe maisha yake yote na matokeo yake ni disappointment.

Zingatia haya.....
Napenda kukwambia kuwa unapoanza uhusiano na mwanaume chukulia mambo taratibu na usikimbilie kufanya ngono kwani kufanya hivyo automatically kutakufanya udhani kuwa tayari uko kwenye uhusiano,


*Angalia mambo ambayo uta-offer ikiwa utakuwa kwenye uhusiano na sio kutegemea afanye hivi au vile

*Weka 50-50 na sio asilimia mia moja kuwa uhusiano utakuwa kama unavyotaka kwani

*Usitegemee mambo makubwa yafanyike ndani ya uhusiano wako na badala yake acha yatokee yenyewe bila kulazimisha.

*Kuwa wazi na kuyazungumzia yale ambayo ungependa yafanyike ktk maisha yenu ya baadae lakini sio kwa kulazimisha au kununa ikiwa mwenzio anaonyesha kutovutiwa na mazungumzo hayo na badala yake wewe furahia kila siku kama inavyokujia……


* Kumbuka mapenzi ya kweli huchukua muda kujengeka na yakijengeka huwa hayabomoki……hata kama mtaamua kuachana baadae mahaba yataisha lakini penzi siku zote hubaki moyoni.

Nitaendelea……

Tuesday

Mwanamke ni "Victim" 2 & 3!


2-Tumuone mwanamke huyu ktk kuzuia mimba.

Mwanamke siku zote ndie anaeachiwa swala la kuzuia mimba, sote tunafahamu wazi kabisa kuwa matumizi ya madawa haya ya nabadili afya ya mwanamke, yanabadili utaratibu mzima wa kupata damu ya mwezi (hedhi) kwamba kuna baadhi ya wanawake huenda mara mbili hadi tatu kwa mwezi.


Wengine hawaedi kabisa (jiulize damu hiyo inakwenda wapi wakati ni lazima itoke ikiwa yai halijarutubishwa) hali hiyo husababisha mkanganyiko wa chembechembe asilia na hivyo kusababisha SARATANI ndani ya mwili au kutopata mtoto/watoto tena….kila ukipata mimba inachoropoka (inatoka sio kwa kudhamilia) n.k.


Linapokuja swala la kumalizia ndani mwanaume hujitoa kabisa na kusukuma jukumu lakuzuia mimba kwa mwanamke. Natambua kuwa hakuna madawa ya muda mfupi yakuzuia mimba kwa wanaume lakini kuna bidhaa ambayo ikitumiwa vilivyo mimba itazuilika, sasa kwanini bidhaa hii (Condom) isitumike kwa nyote wawili badala ya “kusakizia” mwanamke jukumu hilo as if yeye ndio mhusiaka mkuu wa kupata ujauzito?


Ile tabia au niseme kasumba ya “situmii condom kwa vile inapunguza ukaribu wangu na mke/mpenzi wangu” haina ukweli wowote, kuwa karibu na mpenzi/mkeo wako sio lazima umalizie ndani au ugusanishe ngozi yako ya uume na ngozi yake ya uke kwa ndani!



Kitendo cha wewe kufanya nae mambo mazuri na kwa ufundi yatakayowafikisha kwenye hatua hiyo tayari ni ukaribu, jinsi unavyo zungumza nae, jinsi uanvyomshika, unavyomheshimu, mthamini, unavyo onyesha mapenzi,msikiliza n.k. wakati mnafanya tendo hilo takatifu ndio mambo yatakayo kufanya uwe karibu nae a.k.a “Intimately” na sio kupiga bao ndani.


Mwanaume jaribu kuwa mbunifu na mtundu ktk anga nyingine ili kuwa “Intimate” na mkeo/mpenzi wako zaidi ya nyama 2 nyama ili kuepuka mimba na wakati huo huo kumsaidia huyu mama kulinda afya yake ili asiendelee kuwa “victim” ktk uhusiano wenu.



3-Tumuangalie mwanamke huyu ktk Ufungaji wa kizazi.

Baada yakujipatia watoto Fulani ambao mnadhani kuwa wanawatosha au ndio manaweza kuwamudu na hivyo kufanya uamuzi wa kufunga kizai 4 good ili muweze kufanya mapenzi bila kuhofia mimba/mtoto tena, kama kawaida Mwanamke husukumwa akafunge kizazi.


Mwanamke huyu sina uhakika kama ni kasumba, ujinga, kutokujua, kuwa tegemezi au? Habishi “in good way” wala haulizi/hoji kwanini yeye ndiye anaepaswa kufanya hivyo na sio mumewe/mpenzi wake au wote....waende mguu kwa mguu kwenda kufunga kizazi?.


Mara nyingi (nimeshuhudia kwa masikio yangu) mwanaume anakuja na sababu kama “watoto wakifa kwa ajili au magonjwa na nikataka kuzaa tena nitafanyaje?”…..Ukifa (mke) na nikaoa/kutana na mwanamke mwingine na akataka kuzaa na mimi nitamwambiaje?”…..ikitokea tumeachana (peana talaka) na nikaoa tena nakutaka kuzaa na huyo mwanamke nitafanyaje?”……

Sasa huoni kuwa sababu zako za “kibinafsi” zinamhusu pia mwanake huyo? Hayo yote yakitokea kwake yeye atafanyaje?

Nitashukuru kama nitapata maoni, mawazo, maelezo tofauti kuhusu hili au ukiweza ushauri zaidi kutokana na uzoefu wako……sote tunajifunza na nivema tukiweka mambo wazi ili tujifunze kwa kina zaidi.

Asante sana kwa ushirikiano.

Monday

Mwanamke ni "Victim" bila kujijua!




Leo na-promote Uanamke….

Wiki iliyopita nilikuwa kwenye sherehe za kamuagano (Sendoff) na Kesho yake nikaenda kwenye sherehe za ndoa..….kama mjuavyo penye wengi ndio mahali pa kupata mengi sio?

Nilikuwa nimekaa na wamama Fulani wenye uzoefu mzuri tu ktk maswala ya ndoa, wakitoa ushauri, nasaha, maonyo n.k kwa binti aliyekuwa akienda kuanza maisha mapya ya ndoa ili akawe mke mzuri.

Kama kawaida yangu mimi ni mtu wa kudadisi na kuhoji mambo mengi ila ngono ndio hunivutia zaidi, hivyo nilitaka kujua ngono ikoje kwa wanawake hasa kwenye maisha ya ndoa au niseme ndani ya ndoa.

Wachache walikuwa sio wazi sana kama kawaida ya wabongo wengi hasa watu wazima (nadhani waliona mimi katoto Fulani hivi kumbe ni kamwili tu haka)……nilivyoona wanadengua nikahamia kwa kwa wanawake vijana lakini walio kwenye ndoa na kuuliza tena “wao kama wanawake ngono ikoje ktk maisha ya ndoa?”.


Kila mtu akatoka na majibu yake kutokana na uzoefu wake lakini nilivutiwa na maelezo ya wale ambao waliolewa wakiwa bikira, wale wanaotumia madawa ya kuzuia mimba na wale wanaosukumwa/lazimishwa kufunga kizazi baada ya kupata watoto fulani…….

Nikapata jawabu kuwa wanawake wengi ni “victim” ndani ya ndoa/uhusiano wa kimapenzi bila wenyewe kujijua…..nasema hivyo kwa sababu zifuatazo:-

Akizaliwa ni binti wa mzee Fulani……..Akiolewa anakuwa mke wa Fulani…….Akizaa anakuwa mama Fulani…….alafu akijaaliwa nakuwa bibi fulani anamalizia na swala zima la kukabiliana na kukoma hedhi…..Kila hatua ya maisha yake mwanamke anakabiliana na majukumu lukuki……mwanamke huyu hajawa na nafasi ya kuwa yeye na kufurahia maisha kama yeye bali siku zote za maisha yake amekuwa akiishi kwa ajili ya watu wengine.


*Hebu tumuangalie mwanamke huyu anapofunga ndoa/ingia kwenye uhusiano…..

1)-Mimba usiku wa harusi (usiku wa kutolewa bikira).
-Mwanamke kafunga ndoa akiwa bikira na kwa bahati mbaya au nzuri wanashika mimba usiku huo au wakati wa fungate…….binti huyu hajui lolote kuhusu ngono wala utamu wake….usiku huo anafanywa kwa mara ya kwanza na mume wake anajisikia safi kuwa mkewe hakuguswa na mtu mwingine bali yeye….


Hisia za kumiliki zina mjia na bila kujali maumivu ya binti yule, haki yake ya kupata utamu au kufurahia tendo la ndoa….mume anajimalizia ndani kwa vile tu ni mke wake.

Baada ya miezi 9 mwanamke anajifungua anaanza kukuru kakara za malezi na kukabiliana na mabadiliko kutoka msichana kuwa mama…..mabadiliko haya huwa ni magumu sana as u can imagine.

Kwa vile mwanamke huyu hajui lolote kuhusu ngono na hakuwahi kufundishwa au ambiwa lolote hukusu maswala yamwili yeye anachukulia au kuamini kuwa kilichofanyika au kinachofanyika ni kawaida……binti anahisi kuwa labda anakasoro kwani akikumbuka huko nyuma aliwahi kusoma, sikia, kuambiwa kuwa ukifanya mapenzi unasikia utamu au raha…..au anaona mumewe anavyofurahia….lakini masikini yeye haijui na wala hajawahi pupate utamu huo.

Mwanamke anashindwa ku-share na watu wengine kwa vile anadhani hiyo issue ni nyeti sana na ni kinyume na maadili ya kitanzania au mila na destru za kwao…..hivyo maisha yanaendelea na watoto wanaongezeka hali inayoongeza mabadiliko ktk mwili wake na sasa kila unapofanya mapenzi yeye ni kilio tu kutokana na maumivu (kwa vile hapati hamu ya kungonoana wala utamu wake) hali hiyo inamfanya mwanamke huyu amkwepe mumewe kwa kutafuta sababu nyingine……..


Mwanamke anaenda kulalamika kwa Daktari wake wa Magonjwa ya kike na anafanyiwa vipimo inagundulika kuwa mwanamke huyu anaelekea kwenye kukoma hedhi au kikomo cha hedhi (Menopause) kwa mwanamke huyu wa kibongo aliye ndani ya bongo kupata hamu au utamu wa kungonoana ndio inakuwa basi tena……na she is only 40yrs old.


*Ofcoz huwezi kutegemea binti wa watu bikira awe akitumia madawa ya kuzuia mimba au akujie na Condom ili azuie mimba…….wewe kama mwanaume chukua jukumu la kujizuia ili usimtie mimba binti wa watu ambe hajui chochote kuhusu unachokifanya……


Hili halitokei kwa Bikira tu bali kuna wale wanawake ambo walibakwa hivyo kisha wakaja funga ndoa, wapo walijiingiza kwenye maswala ya ngono wote wakiwa bikira hivyo hawakujifunza kitu, vilevile wapo waliokuwa kwenye uhusiano na wanaume ambao hawajali hisia za mwanamke bali tama zao za mwili….nakadhalika!



***********************************************
Waendesha "Kitchen party"......tumieni wasaa huo kuwa wazi zaidi na kuwaeleza/andaa hao watarajiwa watarajie nini ktk maisha yao ya ndoa, jinsi ya kukabiliana baada ya kujifungua......sio mnashupalia jinsi ya kumfurahisha, heshimu, pika mahanjumati, kuwa sexy (pendeza na kuvutia @all times) na kum-keep mume......there are more than hayo in any relationship.....kumbukeni kuwa mwanamke anabadilika jinsi miaka inavyokwenda.....huyo binti anahitaji kulijua hilo kwa undani zaidi.


Wapenzi wanaume.......jaribuni kuvuta muda na mshirikishe mwanamke umpendae kwenye swala zima la kuzaa…..pangeni na muelewane mzae baada ya muda gani…..ondoa “umilikikaji” kumbuka huyo ni mkeo lakini pia ni mpenzi wako……mpe nafasi ya kuujua mwili wake kabla haujabadilika.


Kaka zangu hebu chukua jukumu la kuzuia mimba badala ya kumuachia mwanamke, kumbuka kuwa yeye mayai yake hayatoki lakini mbegu zako zinatoka na kumuingia kwenda kujenga kiumbe hivyo wewe ndio mwenye ku-control hilo na sio yeye.

Ni vema kujadiliana au kujua kama mkeo/mpenzi wako yuko tayari kukabiliana na mabadiliko yanayohusisha uzazi, kumbuka kuwa kuoa au kuwa na mpenzi sio tiketi ya kum-mimba mwenzio (cum inside).


Wanawake.......ambao mnaamini kuwa kupata mimba au kuzaa na Fulani basi ndio utapendwa zaidi au kutoachwa…… nakushauri uache huo Ujinga na Ushamba…..


Only Kubali kushika mimba ikiwa unadhani kuwa ndio kitu unachokitaka, hakikisha unajua faida, hasara, matatizo ya mimba mpaka kujifungua na baada ya kujifungua, kuwa na uhakika kuwa utakuwa tayari kukabiliana na yote hayo.


Epuka kukimbilia kuzaa/achia mimba kwa vile jamii inakukandamiza/sukuma, mtaani kwenu kila binti anamtoto, unahofia jamii kukudhania kuwa wewe ni tasa, ili wakwe wakupende zaidi, ili mwanaume/mume asikuache au aendeleze huduma kiuchumi n.k.....


Sikutishi….bali nakwambia ukweli kuwa kushika mimba maana yake ni mabadiliko…….je unauhakika uko tayari?


Tuende na wakati sio ktk mikao na mitindo ya kufanya ngono tu bali kila kitu kinachoendana na ngono na matokeo yake......tujaribu kuwa Taifa lenye vijana wajanja ei!.....sio tunapelekwa pelekwa na kasumba za kizembe.


Endelea kuwepo ili nimalizie vipingele 2 vilivyobaki….

Pages