Thursday

Kunatatizo nikioa Shemeji yangu!

Mambo vip dada Dinah. Pole sana na shughuli za kila siku. Mimi ni
Mwanaume mwenye miaka 25 nipo mwanza.



Nimemaliza Chuo Kikuu cha Dodoma
(UDOM) mwaka jana (2013). Kwa sasa naishi na Kaka yangu, Shemeji (mke
wa kaka) pamoja na mdogo wake Shemeji, wa kike.




Kwa sasa tumetokea kupendana sana sana na Shemeji (mdogo wake Mke wa Kaka). Mapenzi yetu ni siri sana kwa sababu Kaka hajui wala Mke wake hajui chochote.



Tumeshapanga mambo mengi ambayo tutafanya hapo baadae. Naomba ushauri, hivi kuna tatizo nikimuoa shemej yangu?!
*************************



Dinah anasema: Ahsante na Shukurani kwa Ushirikiano. Well huyo Binti sio Shemeji yako bali ni Shemeji ya Kaka yako. Huyo Binti ni mdogo wa shemeji yako au niseme ni Shemeji ya Kaka yako. Huna uhusiano wowote hapo.



Kinachofanya Ndugu wa pande mbili tofauti zilizofunga ndoa kutopendana ni Heshima au Uoga (inategemea na Kabila na Mazingira).


Enzi za Bibi yangu, Mwanaume akiwa anajiweza kiuchumi na kuchumbia familia nyingine, Baba Mkwe alikuwa anatoa Binti yake mwingine kama zawadi/Nyongeza.


Hivyo Mwanaume anaoa Dada na Mdogo wake....hehehehe, My point is:- Hakuna tatizo lolote Kiimani na Kitamaduni kuoa Mdogo wa Shemeji yako.

Kila la kheri.
Mapendo tele kwako...

Monday

Dalili za Utasa kwa Mwanaume!


Habari za kazi Doctor. Nimekua nikifwatilia mada zenu nami nina maswali yafuatayo naomba unisaidie. Swali langu la 1 ni je? kuna dalili zozote za mwanaume ambaye ni Tasa? Mfano kwa kuangalia rangi ya shahawa ama kujua shahawa zilizokomaa zinakua na rangi gani?



Dinah anasema: Ayee! Mie sio Dakitari ila nina Elimu ya Awali ya Kiasili na kauzoefu tu kiasi , siku ni njema kabisa nashukuru kwa ushirikiano Ndugu yangu.


Hapana! Sidhani kuwa kuna dalili yeyote inayoashiria kuwa Mtu ni Tasa iwe ni mwanaume au mwanamke. Ukomavu wa Shahawa ni pale unapobalehe.....ukibalehe hata kama una miaka 7 bado utaweza "kusababisha" mimba na hatimae Mtoto ikiwa utafanya ngono bila kinga.



Isipokuwa kama una matatizo ya kiafya yanayoweza kusababisha tatizo la uzazi basi kutakuwa na dalili zinazohusiana na tatizo hilo la kiafya (Ugonjwa). Pamoja na kusema hivyo kuna dalili zinazoweza kusadiki Ugumba kutokana na Shahawa zako, kwamba hazina ubora/afya kutokana na rangi, harufu na uwingi/uchache, uzito/wepesi.



Japokuwa utahitaji vipimo Kitibabu ili kuhakiki Ugumba na kupata Ushauri yakinifu wa Kitaalam. Tambua kunatofauti ya Utasa (tatizo la kudumu) na Ugumba (tatizo la muda).



2. Ninaye mpenzi wangu, siku moja nilifanya nae mapenzi ambapo siku hiyo anadai Yai lilikua tayari then wakati nafanya nika-withdraw nje.Ila kwa bahati mbaya niliacha Shahawa kidogo sana ndani na nyingi nilimwaga nje, lakini hakupata Ujauzito je? Kuna uashiria wowote kua naweza kua Tasa?



Dinah anasema: Kujua kuwa Yai lipo tayari sio "business" rahisi ndio maana kuna Bidhaa maalumu za kukusaidia kujua kama upo tayari au la! Huenda alichanganya kukaribia siku zake na Yai kupevuka (kuwa tayari).



Pia kuna dalili za kimwili kama vile Ute mwepesi kuongezeka, joto kupanda na Nyege kuongeza....ila sio wakati wote mwanamke huwa sahihi kwenye hili. Unahitaji muda na kujua mahesabu ya Mzunguuko wa Hedhi kwa undani na ukaribu zaidi.



Kama alikuwa tayari kushika Mimba na hakushika basi Manii zilikuwa chache au zilisafiri taratibu na kufika wakati Yai limekwisha telemka. Pia ni vema utambue kuwa kwa mwanaume Kukojoa (kumwaga Shahawa) na kufika Kileleni ni vitu viwili tofauti.



Wakati mwingine mwanaume anaweza kukojoa bila Mbegu (Sperms)....Vilevile Kitaalam (huku niliko sijui kwa Bongo) mtu anahesabika Mgumba ikiwa kajaribu "kusababisha" au "kushika" Mimba kwa Miaka miwili.



Na hii ni kwa kufanya Mapenzi mara nyingi kila wiki bila Kinga kwa miaka hiyo 2.Baada ya hapo unafanyiwa Uchunguzi Kitibabu alafu mnajaribu tena, kama ni Mgumba utafanikiwa baada ya matibabu/kufuata ushauri.


Vinginevyo unafanyiwa uchunguzi zaidi ili kuhakikisha kuwa wewe ni kweli Tasa na kwanini.



3. Hivi karibuni nimekua nikikaa hata wiki moja bila kufanya mapenzi, nikienda kuoga wakati nakojoa mwanzoni huanza kutoka kalundo mfano kitu kama shahawa ila hakuna maumivu. Je? Naweza kuwa na tatizo lolote? Au ni hali ya kawaida?



Dinah anasema: Mwanaume mwenzio angekupa Jibu vizuri zaidi.....Inawezekana "Mfuko wa kuhifadhi Shahawa" umejaa, hebu jaribu kuzipunguza alafu uone inakuaje ndani ya siku chache.


Nikijibu swali lako, sidhani kama unatatizo lolote, ila unahofu ya Utasa hali inayopelekea kuwa na wasiwasi kila unapoona tofauti huko sehemu- sehemu.



4. Nimekukua nikijichua kwa muda wa miaka 10 sasa, mfano muda mwingine nikiwa mbali na mpenzi wangu huwa napiga punyeto je? Kuna madhara yoyote labda naweza nisipate mtoto hapo baadae?


Hayo ndiyo maswali yangu ambayo yamekua yakiniumiza kichwa na kunikosesha amani.Nitashkuru kwa majibu na kazi njema.

*************************************************


Dinah anasema: Kujipa Mkono kuna madhara Kisaikolojia ikiwa huwezi kujizuia au niseme ukiwa addicted. Nijuavyo mie kujichua mara 1-3 kwa wiki ni Afya na Salama kama huna Mpenzi au Mpenzi yupo mbali.


Punyeto haiwezi kukusababishia tatizo la kupata mtoto hapo baadae.

Kila la kheri.

Mapendo tele kwako...

Saturday

Samahani....

Kurekebishana!

Habari ya Sasa!


Unapofundwa, unaelekezwa namna ya "kumrekebisha" mumeo, pamoja na kuwa wewe ni mkewe pia wewe ni "Mama" yake kwani akiendelea kuwa na mwenendo mbaya ambao labda Mama yake hakufanikiwa kumrekebisha akiwa mikononi mwake basi wewe kama mke unachukua jukumu hilo.


Hali kadhalika Mumeo achukua nafasi ya baba yako, ikiwa Baba hakukunyoosha ulipokuwa mikononi mwake basi jukumu hilo achukua mumeo (sina hakika kama wanaume huambiwa hili, lakini wanawake tunapokuwa mafunzoni huambiwa hivyo).



Ikiwa mumeo au mkeo anatabia mbaya, aibu ni yenu wawili na watoto wenu na sio ya Wazazi wenu.....Kila mmoja wetu hupenda/Ombea kupata Mke/Mume/Mpenzi mwema na bora wa kuishi nae, japo sio mara zote unabahatika kumdondokea mpenzi bora atakaekufaa maishani, mpenzi mwenye "values" kama zako, alielelewa vyema na mwenye heshima na adabu(iwe mwanaume au mwanamke, inategemea na jinsia yako).



Kabla hujamdondokea mtu, unaanza na kutamani unachokiona Mf: umbile au muonekano wake, sauti pia inawezekana harufu kama sio mwendo (miondoko yake) na mara chache sifa njema anazotupiwa na majirani au watu wanaomfahamu.



Ukibahatika kumshawishi na yeye kukubali kuwa nawe na kuanza uhusiano, hapo ndio unapokwenda kumjua zaidi na yeye kukujua zaidi. Uhusiano huo utakufanya ufanye uamuzi wa kudharau "habits" mbaya na kuendelea kuwa nae au kuukatisha kwa vile kuna "vijitabia" vyake havikufurahishi na huoni kama unaweza kuvivumilia ikiwa utaamua kuishi nae Daima Milele (only if Milele exists hihihihi)!



Kwa kawaida huwa tunajinadi na "kujiaminisha" kuwa hatuwezi kubadilika kwa ajili ya mtu mwingine, lakini tunasahau kuwa unapokuwa kwenye uhusiano (sio dating stuff, nazungumzia UHUSIANO kuanzia Miezi 6 kwenda mbele) nia na madhumuni ni kuwa na furaha, kupeana imani na matumaini, kusaidiana na kushirikiana katika kila jambo (kimaisha na kimwili) ili kufurahia Maisha yenu pamoja.



Sasa ikiwa kubadilika kwako ni sehemu ya kumfurahisha mwenza wako na kuongeza imani kwenye nyumba yenu, kwanini usibadilike?Huwezi ukaishi maisha yaleyale uliyoishi na watu wengine na pengine yakawashinda na ndio maana ukawa "single" na hatimae kukutana na huyo uliyenae....perhaps!



Mimi binafsi naamini kuwa watu tunatofautiana, sio kijinsia tu bali kiakili, kielimu, kiuelevu, kimalezi, kimazingira n.k.Hivyo basi unapoamua kuishi na mtu mwingine usitegemee yeye kukubali "habits" zako na yeye asitegemee wewe kukubali vijitabia vyake... Hapo ndipo suala la kurekebishana huingia.



Ni rahisi sana kwa mtu ku-pretend kwa muda fulani alafu akisha kuzoea au akiwa comfortable anajiachia...Kurekebishana huko ni kuanzia kwenye vitu vya kawaida mf:

-Matumizi ya pesa, Mmoja wenu anaweza kuwa anafuatilia kila Senti imetumikaje na kwanini (which inaudhi) hasa kama wewe ume-relax kimatumizi....lakini ukiangalia kwa undani utagundua kuwa ni vema kubadili tabia yako ya ku-relax na kutumia pesa vema.


-Ulaji wa chakula, kula huku mdomo upo wazi au unaongea na chakula mdomoni, kubeua/Cheua kwa sauti, kuchokonoa meno wakati watu wengine wanakula.-Namna anavyokuandaa na kufanya mapenzi hupendezwi, hupendi weka wazi ili ajue wapi pa KUREKEBISHA....tulishaambizana hili Mwaka 2007!



-Uvaaji, Vazi au mavazi humfanya Mwanamke ajisikie "safi"/mwenye furaha, anavutia au bado Kijana...usipokuwa muangalifu hapa unaweza kuitwa (bully)!


-Unywaji wa pombe, Pombe sio nzuri kwa afya yako kimwili (kigono) na kiakili, ni vema ku gadually punguza intake yako kwa wiki, na kama ni mwanamke na hutaki kuwa na kitambi, basi wacha kabisa.


-Ulalaji wake, wavuta shuka/Duvert Mpo!!! -Marafiki, "umekuja kabla ya marafiki zangu hivyo siwezi kuwaacha kwa ajili yako"...."Kama marafiki zangu huwapendi basi hatuwezi kuwa pamoja"...."Marafiki zangu kwanza, mengine (including mpenzi/Mke/Mume) baadae"...."Mpenzi huja na kuondoka lakini marafiki are for life" NIENDELEEE?!!!


Hizo ni sentensi ambazo tumezoea kuzisikia, mtu anafanya maamuzi ya maisha yake na familia yake(mke/mume) based on what a rafiki kashauri.


**Kumbuka kuna tofauti kati ya Watu unaofahamiana nao na Marafiki, huwezi kuwa na Marafiki 3 na wote wakakupenda the same. Kati yao lazima kuna adui.


Heri ya Mwaka Mpya!

Mapendo tele kwako...

Kurekebishana!

Habari ya Sasa!
Unapofundwa, unaelekezwa namna ya "kumrekebisha" mumeo, pamoja na kuwa wewe ni mkewe pia wewe ni "Mama" yake kwani akiendelea kuwa na mwenendo mbaya ambao labda Mama yake hakufanikiwa kumrekebisha akiwa mikononi mwake basi wewe kama mke unachukua jukumu hilo. Hali kadhalika Mumeo achukua nafasi ya baba yako, ikiwa Baba hakukunyoosha ulipokuwa mikononi mwake basi jukumu hilo achukua mumeo (sina hakika kama wanaume huambiwa hili, lakini wanawake tunapokuwa mafunzoni huambiwa hivyo). Ikiwa mumeo au mkeo anatabia mbaya, aibu ni yenu wawili na watoto wenu na sio ya Wazazi wenu..... Kila mmoja wetu hupenda/Ombea kupata Mke/Mume/Mpenzi mwema na bora wa kuishi nae, japo sio mara zote unabahatika kumdondokea mpenzi bora atakaekufaa maishani, mpenzi mwenye "values" kama zako, alielelewa vyema na mwenye heshima na adabu(iwe mwanaume au mwanamke, inategemea na jinsia yako). Kabla hujamdondokea mtu, unaanza na kutamani unachokiona Mf: umbile au muonekano wake, sauti pia inawezekana harufu kama sio mwendo (miondoko yake) na mara chache sifa njema anazotupiwa na majirani au watu wanaomfahamu. Ukibahatika kumshawishi na yeye kukubali kuwa nawe na kuanza uhusiano, hapo ndio unapokwenda kumjua zaidi na yeye kukujua zaidi. Uhusiano huo utakufanya ufanye uamuzi wa kudharau "habits" mbaya na kuendelea kuwa nae au kuukatisha kwa vile kuna "vijitabia" vyake havikufurahishi na huoni kama unaweza kuvivumilia ikiwa utaamua kuishi nae Daima Milele (only if Milele exists hihihihi)! Kwa kawaida huwa tunajinadi na "kujiaminisha" kuwa hatuwezi kubadilika kwa ajili ya mtu mwingine, lakini tunasahau kuwa unapokuwa kwenye uhusiano (sio dating stuff, nazungumzia UHUSIANO kuanzia Miezi 6 kwenda mbele) nia na madhumuni ni kuwa na furaha, kupeana imani na matumaini, kusaidiana na kushirikiana katika kila jambo (kimaisha na kimwili) ili kufurahia Maisha yenu pamoja. Sasa ikiwa kubadilika kwako ni sehemu ya kumfurahisha mwenza wako na kuongeza imani kwenye nyumba yenu, kwanini usibadilike? Huwezi ukaishi maisha yaleyale uliyoishi na watu wengine na pengine yakawashinda na ndio maana ukawa "single" na hatimae kukutana na huyo uliyenae....perhaps! Mimi binafsi naamini kuwa watu tunatofautiana, sio kijinsia tu bali kiakili, kielimu, kiuelevu, kimalezi, kimazingira n.k. Hivyo basi unapoamua kuishi na mtu mwingine usitegemee yeye kukubali "habits" zako na yeye asitegemee wewe kukubali vijitabia vyake... Hapo ndipo suala la kurekebishana huingia. Ni rahisi sana kwa mtu ku-pretend kwa muda fulani alafu akisha kuzoea au akiwa comfortable anajiachia... Kurekebishana huko ni kuanzia kwenye vitu vya kawaida mf: -Matumizi ya pesa, Mmoja wenu anaweza kuwa anafuatilia kila Senti imetumikaje na kwanini (which inaudhi) hasa kama wewe ume-relax kimatumizi....lakini ukiangalia kwa undani utagundua kuwa ni vema kubadili tabia yako ya ku-relax na kutumia pesa vema. -Ulaji wa chakula, kula huku mdomo upo wazi au unaongea na chakula mdomoni, kubeua/Cheua kwa sauti, kuchokonoa meno wakati watu wengine wanakula. -Namna anavyokuandaa na kufanya mapenzi hupendezwi, hupendi weka wazi ili ajue wapi pa KUREKEBISHA....tulishaambizana hili Mwaka 2007! -Uvaaji, Vazi au mavazi humfanya Mwanamke ajisikie "safi"/mwenye furaha, anavutia au bado Kijana...usipokuwa muangalifu hapa unaweza kuitwa (bully) -Unywaji wa pombe. Pombe sio nzuri kwa afya yako kimwili (kigono) na kiakili, ni vema ku gadually punguza intake yako kwa wiki, na kama ni mwanamke na hutaki kuwa na kitambi, basi wacha kabisa. -Ulalaji wake, wavuta shuka/Duvert Mpo!!! -Marafiki, "umekuja kabla ya marafiki zangu hivyo siwezi kuwaacha kwa ajili yako"...."Kama marafiki zangu huwapendi basi hatuwezi kuwa pamoja"...."Marafiki zangu kwanza, mengine (including mpenzi/Mke/Mume) baadae"...."Mpenzi huja na kuondoka lakini marafiki are for life" NIENDELEEE?!!! Hizo ni sentensi ambazo tumezoea kuzisikia, mtu anafanya maamuzi ya maisha yake na familia yake(mke/mume) based on what a rafiki kashauri. **Kumbuka kuna tofauti kati ya Watu unaofahamiana nao na Marafiki, huwezi kuwa na Marafiki 3 na wote wakakupenda the same. Kati yao lazima kuna adui. Heri ya Mwaka Mpya!

Mapendo tele kwako...






















Pages