Monday

Wanataka nioe "Mtoto" ili asinizeekee!

Mimi ni mfuatiliaji mzuri wa blog yako,nikupongeze kwa kazi yako nzuri
unayoifanya.

Umri wangu ni miaka 24, nipo kwenye uhusiano na binti mwenye umri wa miaka 23. Tumekuwa pamoja tangia nikiwa kidato cha Tatu na mwenzangu cha pili, hivi sasa niko Chuoni mwaka wa pili.

Kiuweli tunaelewana vizuri na
tumepanga na kuahidiana mambo mengi sana ikiwemo kufunga Ndoa hapo baadae.

Tatizo linalonisumbua ni umri! Yaani umri wake na wangu tofauti ni
mwaka mmoja je, hii mbeleni haitasumbua? kwa sababu wanaonishauri wengi
wanasema atanizeekea!

Ama pengine itapelekea nianze kuchepuka nje ya Ndoa angalau nitafute ninaye mzidi miaka 5 au mpaka 10.

Kiukweli inanichanganya coz nakumbuka alishawahi kukataa uchumba kwa
ajili yangu, naogopa sana kumuumiza.

Na je, kama tatizo ni umri sasa
ni tofauti ipi inafaa ya umri. Naomba ushauri katika hili ili nifanye maamuzi sahihi. Asante.


**********


Dinah anasema:Hi Dogo, Shukurani kwa ushirikiano.


Mpenzi wako akipunguza miaka na akakuambia anamiaka 10 au 16 itakufanya ujisikie vema na kuwa na uhakika hutoCheat baada ya ndoa kwenda kutafuta mwenye umri mdogo zaidi eti?

Hao marafiki zako au washauri need to go out a bit more, wanamawazo ya Kizee yaliyopitwa na Wakati au niwaite maPedo (wanapenda watoto wadogo kingono which ni Kosa Kisheria).

Umri ni namba ambayo "Mzungu" katulazimisha tuamini kuwa siku unayozaliwa ndio siku ya kwanza kuanza kuhesabu umri wako. Unauhakika gani kuwa miaka 24 uliyonayo ni kweli 24? Pengine ni 12 au 48!!...kwa mfano.


Kinachomzeesha mtu ni mawazo yake, mwili na jinsi anavyojiweka/beba sio siku aliyozaliwa kwani inaweza kubadilishwa wakati wowote.

Wewe na yeye wote mtazeeka ila kumbuka siku hizi wanawake wanajipenda sana, wanajua kujitunza nje na ndani, wanaijua miili yao hivyo utajikuta wewe umezeeka kuliko yeye....hii ni 2014 babaa, sio 1994!


Kinachopelekea watu wawili kukubaliana na kufunga ndoa Mara zote ni mapenzi sio Umri, kama mnapendana, mnaheshimiana kweli na mmepanga na kukubaliana kufunga ndoa, stick to it, achana na hao "washauri" wako ambao inaonyesha ama wanakuonea Wivu au hawampendi Mpenzi wako.

Kutoka nje ya Ndoa kunategemeana na tabia yako binafsi na heshima uliyonayo kwa Wanawake (mama yako incl) na Mkeo, sio umri wa mtu.


Nikijibu swalo lako la mwisho; hakuna umri sahihi au unaofaa kufunga Ndoa ailimradi tu mhusika na wewe mwenyewe mpo juu ya Miaka 17(Chini au hapo ni abuse dhidi ya mtoto na ni kosa Kisheria).

Kila la kheri.

Mapendo tele kwako...

Sunday

Kusonga mbele baada ya kutoswa...

Habari dada dinah, mimi ni msichana wa miaka 24. Mwaka 2009 nilianzisha mahusiano na kaka mmoja alikuwa anasoma Chuo Mkoa ninaoishi.

Tuliendelea mpaka akamaliza Chuo, akiwa katika harakati za kutafuta Kazi mie nikawa nimeshika Ujauzito. Nilimueleza akakubali akasafiri.


Baada ya muda nikagundua alipata Kazi na alipangiwa huko Mkoani alikoenda na anaishi na mwanamke.


Kabla sijagundua hayo yeye alinambia yupo kwa Wazazi na anasimamia Miradi ya kwao, nilipomuuliza akakana lakini baada ya kumpa ushahidi akakubali na kusema ndio anaishi na mwanamke na ndio Mkewe mtarajiwa. Mimi na yeye basi ila tulee tu mtoto kwani mapenzi hakuna tena!


Niliumia sana nilifikiria alivonidanganya kwamba yupo kwao na anasimia miradi na anaendelea tafuta kazi na akipata nitaenda ili tukaishi wote.

Mpaka sasa maelewano hakuna ni ugomvi tu maana mie nimekuwa namlalamikia sana na yeye hapendi.

Naomba nishauri nifanyaje ili nimpotezee maana nampenda sana, yaani nimepungua mno Uzito kwa mawazo.


Tangu mtoto kazaliwa hajawahi kumuona, hivi sasa anamwaka mmoja, anatoa matunzo ya mtoto anatoa kiasi na kasema lazima atakuja kumchukua Mtoto ili nisimsumbue.


Nifanyaje pia ili asimchukue mtoto maana sitaki alelewe na mama mwingine, mie uwezo wa kumhudumia ninao nataka nikae na mwanangu.

Nisaidie kwa ushauri.

************

Dinah anasema: Habari ni njema tu Mrembo, ahsante kwa ushirikiano.


Kuachwa/Kuacha/Kuachana na mtu unaempenda kote kunauma sawa....sababu za Kuachwa/Kuacha/Kuachana hutofautiana lakini bado maumivu yake hufanana. Ili kusonga mbele siku zote unapaswa kukumbuka na kukubali kuwa Penzi halilazimishwi!

Najua unavyojisikia (najaribu kujiweka kwenye situation yako). Unadhani alikupenda kama ulivyompenda, kwa vile ulikuwa mdogo (at 19), huenda alikuwa ndio wa kwanza kwako na hiyo ikakupa Matumaini kuwa yeye ndiye atakaye kuwa mume wako....baada ya ujauzito ukadhani hakuna kitakachomfanya akuache kwa sababu mtakuwa na mtoto pamoja!

Unaumia, pengine unajutia muda wako, unajutia kwanini hukua Makini na kumjua mapema, Unajuta kwanini hukutumia Kinga na mengineyo....Unahisi kutaka au unataka kujua sababu hasa iliyomfanya akuterekeze na kuendelea na Maisha yake bila wewe na mtoto wenu ili uweze kusonga Mbele!

Kwavile hakuambii na hatokuambia basi mie nitakuambia....alikuwa anakutumia kwa Ngono akiwa Masomoni lakini hakuwa akikupenda wala hakuwa na mpango wa kuishi na wewe kama Mkewe.

Alitegemea wewe ujikinge kwa namna yeyote ili kuzuia Mimba na akikushawishi au kataa kutumia Condom na wewe kupata Mimba basi Kosa ni lako na sio lake.

Vijana wengi tu huwatumia mabinti wa watu kwa ajili ya kumaliza mahitaji yao ya Mwili, tatizo la wasichana hasa wale wadogo ni kuamini kuwa kwa vile "kanikuta Bikira basi atanioa".....unajisahau au unashawishika kirahisi kutojikinga dhidi ya Mimba ukiamini ukiishika basi ndio Tiketi ya Ndoa.


Bikira sio guarantee ya Kuolewa au mwanaume kuwa Muaminifu kwako, pia Mimba/Mtoto sio sababu ya kufunga ndoa au Uhusiano kudumu na kamwe usiitumie Mtoto ili kumkomoa/sumbua Mwanaume aliekuacha na Mimba.

Mwanaume aliekuacha baada ya Mimba hajali kwani hakai na Mtoto(Mimba) kwa miezi tisa, hana connection/bond na mtoto kama wewe Mama yake....Mwanaume habadiliki Kimwili, Kihomono wala Kiakili!

***Ufanye nini ili umpotezee:


Sio rahisi na itachukua muda lakini inawezekana. Nitakupa "therapy" yangu binafsi (sio rasmi) ya kufuata hatua za kuomboleza kama vile umefiwa na mpendwa wako ila tofauti ni kuwa hutomuombea au kumkumbuka Ex wako....ambayo naamini inaweza kukusaidia pia.

Hatua ya kwanza: Omboleza...ruhusu Akili na Moyo kwa mara ya MWISHO kukumbuka yote mazuri mliyofanya, ahadi mlizopeana, maeneo mliotembelea na kila jema ulilomfanyia na yeye kukufanyia.

Hiyo inakufanya ulie sana na kujiuliza kwanini? Umekosa nini wewe....lia huku unajiangalia kwenye kioo, lia wee na kujisemea mpaka upate hisia za kujiona Mjinga.


Hatua ya Pili: Unapohisi au kujiona Mjinga ni kwamba unakubali kuwa hata ukilia hawezi kurudi kwako, sasa kwanini Ukufuru wakati una afya njema, Mshukuru Mungu kwa hilo (au kwenye Msiba unakubali kuwa Kaenda na hawezi kurudi, jina la Bwana litukuzwe).

Hatua ya Tatu: Kabla hali ya kujiona "mjinga" haijakutoka kusanya(bila kusoama au kuangalia) kila kinachomhusu (sio mtoto) bali Picha, zawadi alizokupa (kama ni Vito vya Thamani, viuze), Kadi, Nguo n.k kisha piga Moto (teketeza) huku unamlaani kwa lana zote uzijuazo.


Hatua ya Nne:Kama ilivyo kwenye Msiba, baada ya Mazishi huwa unapata "unafuu" na hali ya kutokukumbuka alieenda exactly....unamkumbuka lakini hupati taswira yake halisi (Mungu wa ajabu bana)....basi utahisi unafuu huo ila tofauti ni kuwa hujamzika bali "umemteketeza kwa moto".

Hatua ya Tano: Ifunze akili yako kupoteza kumbukumbu nzuri kuhusu Ex, kwamba zikianza kuja tu unaziziba kwa ku-focus kwenye Kasoro zake....Mf: Mdomo ulikuwa unanuka, alikuwa hajui kubusu....Miguu yake sijui ilikuaje, kwanza alikuwa serial muongo n.k.


Trust me kila mwanadamu anakasoro zake sema Penzi hufunika....ila mkiachana lazima utaziona Kasoro za kutosha tu!


Hatua ya Sita: Kama hapo unapoishi sasa ndipo alipokuachia (mlikuwa mmepanga) basi angalia uwezekano wa kuhama ili uanze maisha Upya.


***Ufanye nini ili Ex asimchukue Mtoto:


Hawezi kumchukua, anakutishia tu ili uache kumtumia mtoto unapomsumbua na malalamiko yako ya Uhusiano mliokuwa nao, hasira za kudanganywa n.k.


Sasa pima umuhimu kati ya hisia zako za zamani juu ya Ex ambae keshasema wazi kuwa hakutaki au Maisha na uhai wa Mwanao kisha chagua moja.



Kama Maisha ya Mtoto ni muhimu zaidi kuliko hisia zako kwa Ex, basi kuanzia leo poteza mawasiliano yake na mengine yote yanayomuhusu yeye (sipokuwa mtoto ambae asilimia kubwa ya DNA yake ni yako na sio ya Baba yake anyway) na ndio iwe mwisho wa kuwasiliana nae.

Kisheria (Tz) hawezi kumchukua akaishi nae kwani umri wake ni chini ya Miaka Saba, akija kumchukua "kwalazima" au kwa nguvu atakuwa kafanya Kosa la kuiba Mtoto na unaweza kumfungulia mashitaka.

Na hata kama Mtoto akifikisha Miaka Saba sio lazima aende kwa Baba yake hasa kama wewe huna matatizo (ugonjwa) na unauwezo wa kumtunza mwenyewe.


Kubali kosa ulilolifanya na kusababisha Mimba na sasa ni Mtoto.....hakikisha hurudii tena kosa hilo.

Ni muhimu kutumia Kinga kwa kila tendo ili kuepuka Mimba na Mgonjwa ya Zinaa kwa faida yako na Mwanao pale utakapokuwa tayari kuanza Mahusiano ya Kimapenzi tena.


Jipe muda wa kutosha kupona na kukuza mwanao kabla hujaanza tena kutoka na Mwanaume mwingine.

Mtoto akikua na akitaka basi atamtafuta baba yake. Usimjaze mtoto maneno mabaya kuhusu baba yake. Akifikia umri wa kuelewa na kuanza kuhoji "kwanini baba hakai nasisi?", "Kwanini fulani ana baba mimi sina?" mueleze ukweli.


Uamuzi ni wake kumchukia Baba yake kwa kitendo chake(naturally kwa kuanzia atamchukia) au kumpenda na kumheshimu kwa kuwa sehemu yake.....Usilazimishe au kuhamishia Chuki yako juu ya Ex kwa mtoto.

Kila la kheri.

Mapendo tele kwako...

Thursday

Utajuaje kuwa Unanyanyaswa na Mpenzi?

Kuna tofauti kati ya Tabia mbaya na Unyanyasaji.


Wake kwa Waume hunyanyaswa na Wenza wako lakini naamini Wanawake tunanyanyaswa zaidi.....pamoja na kusema hivyo, haijalishi kama wewe ni Mwanaume au Mwanamke....Unyanywasaji/Unyanyaswaji(aiii chagua lililo sahihi) ni Kosa Kijamii na Kisheria, hakuna visingizio.

Wengi huvumilia Vitendo viovu na vya Kikatili (Kinyanyasaji) kutoka kwa wapenzi kwa kutumia visingizio kama "nampenda sana"...."Ni moja ya matatizo madogo tu ya Ndoa, vumilia"...."Nikitoka hapa nitaenda wapi?"...."Nimeisha zaa nae, sitaki watoto waishi bila Baba/Mama" n.m (na mengineyo).

Nisikupotezee muda, nitakuorodheshea vitendo vichache kadri ninavyokumbuka as I go(write) ambavyo ni vya Kinyanyasaji lakini wewe hujui au unachukulia tu kuwa "ni sehemu ya maisha ya ndoa/Mapenzi" hivyo ni lazima Uvumilie.....Hapana! Ndoa sio Mateso....ndoa ni Furaha na inapaswa kuendelea kuwa yenye furaha.

*Mpenzi kutwa/kucha (anatumia muda mwingi na watu wengine) yupo nje na marafiki ambao huwajui....au online kwenye Social media ana chat, haonyeshi kukujali na ukijaribu kuongea nae anakujibu kwa mkato.

Au Akiwa nyumbani yeye na Simu yake au Tablet huku akionyesha kufurahi na kucheka na watu wake.....wewe ukimsemesha au kujaribu kuwasiliana anakujibu kwa hasira na haonyeshi furaha; Unakunyanyasa Kihisia.

*Badala ya "kulianzisha" kimahaba kwa kukushika au kukuita kwa Huba na Mapenzi, yeye anasema "nataka/nipe haki yangu ya ndoa".

Unaponyesha kukataa ama unampa sababu kwanini hutaki Tendo (unaumwa, umechoka) lakini yeye hajali anapanda na kuendelea.

Anajua hutaki tendo Kinyume na Maumbile, lakini anategea ukiwa umejisahau au umelewa "Kilele" yeye anajiingilia "Tigoni" bila ridhaa yako(anakubaka); Unanyanyaswa Kijinsia na Kimwili.

*Kila mnapozungumza, yeye hujibu kwa kufoka....kosa dogo tu lazima ufokewe, ususiwe kama ni chakula au nyumba.


Anapenda kukufananisha na Ex au watu wengine kwenye familia yake au jamii mf: "Wanawake wengine wanafanya hivi, sio kama wewe unafanya hivyo". Au hakuna mwanamke alewahi kunifanyia hivi, wote walikuwa hivi na vile, sio kama wewe.

Anakusimanga, anakutukana na kukuita majina mabaya Mf; Malaya, Mvivu, Mchafu, Unaroho mbaya, Unanuka, hujui kulea, kwenu Masikini, Goli kipa, hujasoma(huna Elimu) n.k; Unanyanyaswa Emotionally.

*Anakupiga au kukushika kwa nguvu, anakusukuma na kukupiga masingi; Unanyanyaswa Kimwili na ki-emotional.

*Anakupangia namna ya kutumia pesa zako au pesa anazokupatia kwa ajili ya matumizi na mara zote anataka aone orodha ya vitu ulivyofanya kwa kutumia Pesa husika....akiona umenunua kitu cha kike kama Vipodozi, Nguo n.k anakuwa Mbogo....anaweza kuvitupa au kuviharibu; Unakunyanyaswa Kiuchumi na Ki-emotional.

*Anakupiga stop usiwe karibu na Ndugu zako, anakataza usiende kwenu ila analazimisha uende kwao; Unakunyanyasa Ki-emotional.

*Mnaweka pesa(Mishahara yenu) pamoja, lakini yeye ndio mwenye Mamlaka na Akaunti husika....siku zote hujui Balance na huambiwi pesa zimetumikaje na kwanini? Huoni wala hujui pesa zinapokwenda, lakini kila mwisho wa mwezi Akaunti haina Hela wakati wote mnapiga mzigo(fanya kazi) na pesa zinalipwa Direct kwenye Akaunti; Unanyanyaswa Kiuchumi, Kihisia na Ki-emational.

*Watoto wakifeli au wakifanya makosa makubwa mf: Kupata Mimba au kumpa Mimba Binti.....Baba anakasirika na kukususia akisema "wanao hao" badala ya kukaa chini na kujadili namna ya kumsaidia mwanenu kama Wazazi; Unanyanyaswa Kijinsia.

*Bila makubaliano unaletewa Mtoto/Watoto wa Nje au waliozaliwa kabla hujaolewa/Oa na kulazimishwa kuwapenda au kuwalea kwasababu Mume/Mkeo ni Baba/Mama yao; Unanyanyaswa Kihisia, Ki-emotional na Kiuchumi (ikiwa kama unatumia pesa zako au mlizotunza pamoja bila Mchango wa Mama zao).


*Anatereza Nje ya Ndoa/Uhusiano; Unanyanyaswa Kihisia na Ki-emotional.

Baadhi ya watu wamelelewa katika Mazingira ya Kinyanyasaji (Baba anamnyanyasa Mama au Mama anamnyanyasa Baba) hivyo wanakuwa wakiwa "wameaminishwa" kwa kuona kuwa hivyo ndivyo watu wanapaswa kuishi, bila kujua kuwa ni Kosa Kisheria kumnyanyasa mwenzio.

Kwa leo naishia hapa, lakini kama una hofu na vitendo vya Mwenza wako kwako, tafadhali usisite kuongezea kwenye Comments.


Natumaini maelezo haya yatakupa mwanga mpya kwenye maisha yako ya Kimapenzi na Mhusiano na hivyo ku-fight back au kutoka kwenye Uhusiano/Ndoa rather than kuwa "ndio bwana".

Tunakubali kuishi na tunaowapenda ili kwa pamoja tufurahie maisha, lakini kama hakuna furaha kwanini uendelee kuwemo kwenye Maisha na an abuser?


Shukurani.

Mapendo tele kwako...

Tuesday

Penzi pasipo Penzi

Pole na kazi na Mungu akusaidie kwa kuendelea kutusaidia, nina miaka 24 na ni Mwanafunzi wa Chuo. Nimeanza  kujihusisha na masuala ya relation  nikiwa na miaka 22,nimekuwa na mahusiano na watu wawil tu!

Wa kwanza nilipokuwa nimemaliza Form 6 lakini sikumpenda na nilimwambia akanisubiri kama mwaka mzima nimpe jibu langu.

Wapili nikiwa nae mwaka wa kwanza naye sikumpenda na nilijitahidi lakini wapi na pia hakuwa mwaminifu katika mazingira fulani.


Sasa nimehisi kwa mara ya kwanza kumpenda mtu kutoka moyoni kabisa yaani hata nikilala nataja jina lake. Nimefanya kila juhudi kufikisha hisia zangu kwake lakini wapi!


Imefikia mahali nikawa kama nachanganyikiwa, lakini yeye hana hata mpango na mimi.


Nikamtumia rafiki yangu ambae anafahamiana na huyo Kijana ninaempenda kwa bahati nzuri nikapata namba yake. Ikapita miezi kadhaa nikijipanga nitaanzaje kuwasiliana nae.

Mwanzoni mwa mwaka nikamtafuta na tukawa tunawasiliana. Muda mwingine anaonyesha hisia za kunipenda lakini asilimia kubwa ndio hivyo anani-humiliate.

Hivi karibuni aliniita niende kwake! nilikuwa MP nikafika tukasalimiana tu nikageuza kurudi Chuoni. Baada ya hapo ndio kabisaa akakaa kimya hata hakuniuliza kama nimefika salama wala nini? kwa kuwa nampenda hata sikuona tatizo.

Nimekaa kama siku tatu hivi, nikamtext nikimwambia "ukimya wako unaniua" akanijibu "achana na mimi endelea na maisha yako", niliumwa wiki nzima nikiwaza hayo maneno napiga makelele napata maluweluwe.


Nikamwambia hali yangu lakini hata hakujibu. Baada ya kupona nimempigia simu lakini hapokei nikapiga kwa mtu mwingine anajibu "achana na mimi". Yaani naona kama nakufa.

Nikajitolea kwenda mpaka huko aliko lakini mtu wapi! Dada kinachoniuma mwanaume hana hata huruma.

Mpaka nimeshauriwa na Mwanasaikolojia sasa nimepona niko ok, ila nimefika mahali sitaki mpenzi wala mapenzi kutokana na kunyanyaswa kihisia.

Nikijiangalia mimi so mbaya wengi sana wananipenda wako tayari kunioa ila ninaempenda hana mpango na mimi nifanyaje?

Siko sahihi nimempenda sana na nampenda nifanyaje dada angu? Nimekulia malezi ya Kidini, sina uzoefu wa kumconvince hata.


***********

Dinah anasema: Ahsante na shukurani kwa ushirikiano, Mungu atusaidie sote.

Oh baby girl! Umri wako bado unatafuta kujitambua na kutambua hisia zako kama mwanamke. Ni umri unaochanganya sana wakati mwingine(kwa baadhi ya watu), lakini ni mpito tu.

Wanawake hatukuwa "programed" kukabiliana na "rejection" kama wanaume, ndio maana Mwanamke hawindi bali anawindwa....Mwanamke unapoamua kuwinda hakikisha hakuna kukataliwa kwa maana kwamba unauhakika na hisia za mwanaume husika kwako....sio kubahatisha kama wanaume wanavyofanya wakati mwingine.


Kuna namna/mbinu ya mwanamke "kumuwinda" mwanaume ili kujua kama ni single, kama ndio je "atakukubali" Kiswahili wanaita "kujitongozesha".


Kwamba unatumia mwili, Macho, maongezi(hutongozi bali unapiga interesting stories) n.k ili kufikisha ujumbe. Ukianza kuona dalili za jamaa kuingia "mtegoni" ndio unamtokea.....hii yote ni kujiepushia Maumivu ya kukataliwa.


Najua ni ngumu sana tena sana lakini inawezekana....itabidi umuache aende kwani kesha kuambia "achana na mimi, endelea na maisha yako" hayo ni strong words & serious, usikute tayari ana Mke au Mchumba.

Nadhani ni Kijana mwema kwani hakutumia nafasi uliyompa na kufanya ngono na wewe kisha kukuambia "achana na mimi, endelea na maisha yako"....ungejichukia, ungejiona Mchafu kuliko!!

Hakuna namna ya kumshawishi ili akukubali....lazima kuna sababu ya Msingi na muhimu kwake kwanini hataki kuwa na wewe, kama nilivyosema inawezekana na commitment kwa mtu wake.


Jitahidi kumuondoa akilini au ku-switch off kuwa hayupo, yaani ha-exist hapa Duniani ili uweze kuwa na amani na kuendelea na maisha yako na utapenda na kupendwa na mtu mwingine.

Itakuwa rahisi kwako kwasababu hujawahi kuwa na uhusiano nae lakini itachukua Muda. Muhimu ni kuifunza akili yako yako kuweza kudharau, kusahau na kukubali kuwa Penzi halilazimishwi.


Jipe muda wa kutosha ili uweze kuipa akili yako nafasi ya "kujifunza" niliyoyataja hapo juu. Inaweza kukuchukua Miezi Sita mpaka Mwaka hivi then utakuwa sawa, utakuwa tayari kupenda na kupenda.

Hope maelezo haya yatakupa mwanga na uelewa kiasi ili uweze ku-focus kwenye Masomo na mambo mengine Muhimu maishani zaidi ya mapenzi(kwa sasa).

Furahia maisha yako kama Mwanamke, heko kwa Ujasiri wako na Uwazi wako.


Kila la kheri.

Mapendo tele kwako...

Monday

Umekuja kunipenda au Kunitawala?

Dada dinah shikamoo
Mimi ni mfuatiliaji mzuri wa blog yako, nakupongeza kwa kazi nzuri na umekua msaada kwa wengi, Ubarikiwe.

Mimi ni binti/mama mwenye umri wa miaka 24 mhitimu wa chuo kikuu shahada ya kwanza na nina mtoto mzuri wa kiume mwenye mwaka 1 na nusu.

Dada nimeishi na baba wa mtoto wangu (hatuna ndoa ya Kidini wala ya Kanisani) kuanzia nikiwa Mjamzito mpaka sasa lakini ndani ya hicho kipindi sijawahi kuwa na furaha ya kweli kwa sababu nimegundua ni mwanaume Mgomvi, Mkatili (ameshanipiga na kuniumiza vibaya mara mbili na kutishia kuniua zaida ya mara 1) ana dharau (ananijibu ovyo hata mbele ya kadamnasi), hajali hisia zangu kila usiku anataka haki yake ya kufanya mapenzi hata kama anajua naumwa/nimechoka).

Ananipa conditions kwamba nitafute kazi Mkoa tunaoishi tu nikipata kazi nje ya Mkoa nichague mahusiano au kazi na isitoshe ndani ya Mkoa ananipangia sehemu za kuomba kazi.


Dada, ananikagua simu yangu kila akirudi kazini, ikiingia sms anataka kujua nani kaituma na nimemjibu vipi hata kama ni wazazi wangu au ndugu (nimekata mawasiliano na classmate wangu na hata marafiki zangu wa kike na wakiume lakini wapi kunikagua hakuishi). Kununa/kuzira kula nyumbani ni kawaida kwake!!

Dada nimechoka! mapenzi yangu kwake yanafifia na kufa kila kukicha. Ushauri please.

NB; Anamjali mtoto kwa kila kitu, lakini mimi nikiomba kitu (naomba sababu sina kazi kwa sasa) naishia kuahidiwa tu bila utekelezaji.


Shukrani kwa ushauri na naahidi nitaufanyia kazi.

************

Dinah anasema: Marhabaa Mrembo, shukurani kwa Ushirikiano wako.

Kwanza pole sana!! Katika umri mdogo unakabiliana na unyanywasaji wa Kijinsia, Kimwili, Kihisia, Kisaikolojia na Kiuchumi.

Kama ilivyo kwa wanawake wengi, pengine hata hujui kama Unanyanyaswa, wewe unadhani tu kuwa Jamaa anatabia mbaya.


Lakini kuja hapa na kuliweka wazi ni mwanzo mzuri na Hongera sana kwa ujasiri wako.

Kisheria (kama hawajabadilisha) ukikaa na mwanaume nyumba Moja kama Mume na kuzaa nae kwa jumla ya Miaka miwili au zaidi mnatambulika Kiserikali kama Mke na mume kwamba kukitokea mfarakano na Uhusiano kufa basi watoto/mtoto na Mama yao hupata Haki sawa kama mke na Watoto waliokuwa kwenye Ndoa.

Isingekuwa kukupiga na kukutishia kukutoa Uhai, ningekushauri uchukue mapumziko kutoka hapo ulipo na uende kwenu au kwa Ndugu yako wa karibu(tumbo Moja) unaemuamini ukapumzike.

Mapumziko hayo yangemfanya atafute sababu za kwanini umeondoka nyumbani na hapo ndio ungehusisha Wazazi wake na Wazazi wako na kuweka wazi sababu zako zote kama ulivyonieleza mimi, wao wangemonya na kumsihi abadilishe tabia.

Kwavile anakupiga, anakutishia uhai na anakuwekea vikwazo kwenye kutafuta Kazi ni wazi kabisa nitakushauri UKIMBIE, yaani achana nae (Naamini katika Wivu wa kuonyesha mapenzi lakini sio kutawalana) huyu Mwenza wako ANAKUTAWALA, huo sio Wivu, pia ni abuser....lazima ana issues kichwani.

Nenda kwenu bila kumuaga, alafu ukifika ndio umwambie via wazazi wako. Kama unahofu na fujo au ukatili wake kwa familia yako basi usimwambie ulipo.

Kapumzike na wakati upo huko anza kutafuta kazi....pia jaribu kutafuta Wanasheria Wanawake ambao huwa wanasaidia akina mama(wanawake) Kisheria wenye issue kama yako ya kunyanyaswa wenza wao.

Ukiwakosa hao basi nenda moja kwa moja Ustawi wa jamii ili wakushauri kuhusu nini cha kufanya Kisheria ili kulinda "mafao" ya mtoto wenu (ili aweze kuhudumiwa na Baba yake).


Waelezee unyanywasaji wote kama ulivyoweka kwenya mail yako, na wao watakusaidia.


Elimu inahitajika kwa wanawake ili tutambue tofauti ya Wivu wenye kivuli cha Unyanyaswaji (kupo kwa aina nyingi nitaweka topic nikipata wasaa) na Wivu wa Mapenzi.


Kila la kheri.

Mapendo tele kwako...

Sunday

Napendwa na wawili

Pole na kazi, samahani naomba ushauri wako. Kuna Wanaume wawili wananipenda sana na wote wanania moja ya kutaka kunioa, sasa sijui mkweli ni yupi?











Mmoja wapo nilishakuanae kwenye uhusiano miaka ya nyuma na tuliishi vizuri sana ila mimi ndie niliemsaliti. Sasa amerudi tena na kudai bado ananipenda.











Moyoni bado nampenda ila naogopa asije nifanyia revenge baadae na pia naogopa kuhusu ndugu zake wakijua kuwa mimi ndie niliye muumiza ndugu yao itakuaje?









Japo yeye amenihakikishia kuwa hakuna baya litakalotokea. Please dada nisaidie kwa ushauri wako.





*******



Dinah anasema: Ahsante kwa ushirikiano.







Kabla hujaanza kujipa mastress kuhusu Ndoa na Ex uliemtenda....unapaswa kurudi nyuma na kukumbuka kilichokufanya umsaliti mwenzio, je unadhani hakipo tena? Unadhani kabadilika? Je wewe umebadilika na unauhakika ukiwa kwenye Ndoa hutoshawishika tena na kumsaliti mwenzio pale atakapokuwa Mumeo?











Kutokana na maelezo yako inaonyesha unamtaka uliemtenda (Ex) kwasababu ume-claim wazi kwamba Moyoni unampenda na maelezo yote yameegemea kwake kuliko huyo mwingine.











Lakini pia maelezo hayo yanakubana, kwani yanaashiria kuwa hujabadilika kwa maana kuwa unao wote kwenye Uhusiano ila hujui ni yupi wa kubaki nae.











Kama hiyo ndio case basi ni vema kuachana na huyo ambae inaonyesha hujamfia kiviiile (Haiwezekani kupenda watu wawili kwa wakati mmoja huku una Moyo Mmoja tu) ubaki na huyo uliewahi kuwa nae (Ex) alafu uangalie mambo yanavyokwenda kabla ya kukimbilia Ndoa.











Huna haja ya kuhofia ndugu zake so long umejirekebisha na unauhakika hutorudia kumsaliti mwenzako tena. Sidhani kama atakurudishia Kisasi ila hofu yako kutokana na ulichomfanyia inaweza kukusumbua na kukufanya uhisi anakusaliti ili akurudishie maumivu uliyompa.









Ijue thamani ya Mwili wako, tambua tofauti ya kupendwa na kutamaniwa kisha fanya uamuzi wa busara.





Kila la kheri.

Mapendo tele kwako...

Wednesday

Nitamjuaje mwenye lengo nami?

Hello dinah samahani mimi ni binti wa miaka 24 natamani sana kuolewa ila sijui nitamjuaje mwanaume aliye mkweli na mwenye lengo na mimi.

Na pia ni kweli mwanaume mtu mzima ndio anajua kujali kwenye Mapenzi kuliko kijana?


**********

Dinah anasema: Hi! Bila ya samahani.


Kumjua mtu kabla hujawa nae karibu (bila uhusiano) sio jambo rahisi kwani hata nafasi ya kumuuliza haitokuwepo.


Hata ukiwa kwenye uhusiano haikupi "guarantee" kuwa huyo mtu ni mkweli na anataka siku moja mfunge Ndoa. Lakini inakurahisishia kumsoma mhusika na kujua kama anapoteza muda tu(anapita) au anataka Uhusiano wa kudumu na hatimae Ndoa.


Pia inakuwa rahisi kumuuliza kuhusu uhusiano wenu unaenda wapi? Mf; miaka 3 imepita hakuna dalili ya kuposwa, unaeza uliza "Mpenzi unadhani tutaishi kienyeji mpaka lini?" Akijibu kwa hasira au akizunga au akisema "tuangalie itakavyokuwa" ujue huyo hana mpango na Ndoa kwa wakati huo.....ni mfano tu.

Sio kweli kuwa wanaume watu wazima ndio wanajali kwenye Mapenzi kuliko Vijana. Kujali nadhani inategemea na mtu na sio umri.

Asilimia kubwa ya Wanaume watu wazima 40+ wenye wake zao ndio wanaongoza kwa kuwa na Vimada.....wanaacha wake na watoto wao wanakula kwa kujinyima, kusoma kwa shida huku wao wakisomesha na kulisha Familia za Vimada wao....sasa kujali hapo kupo wapi eti?

Sielewi unamaana gani unaposema "mtu mwenye nia na Malengo na wewe" kwani wewe ni "object"?!!....Ndoa ni muungano wa watu wawili wanaopendana/waliokubaliana kuishi pamoja kwenye "commitment" ya kutotanga-tanga na watu wengine mpaka mwisho wa Maisha yao.

Utamjuaje; inategemea na mhusika ila maongezi yake kwako tangu mwanzo wa uhusiano yatakuwa yanalenga Maisha ya baadae kama ninyi na sio yeye(kwamba inakuwa wewe na yeye).

Hatokuwa mtu wa kuzungumzia mambo ya starehe (outings sana) na utaona dalili za yeye kutaka familia....atakusogeza kwa watu wake muhimu (Mama, Baba, Kaka)....dada ni muhimu ila sio kivile.

Kutamani kuolewa kwa baadhi ya wanawake ni kitu cha kawaida au niseme ni moja ya Malengo waliojiwekea Maishani na wangependa yatimie......Kama ilivyo kwenye Kifo, hujui ni lini lakini unauhakika kuwa ipo siku utaondoka....sasa Ndoa nayo wakati mwingine ichukulie hivyo....wacha haraka.

Jaribu kutafuta kitu kingine ambacho ni muhimu kwako ili uweze ku-focus on wakati unaendelea kusubiri kukutana na mtu atakae kupenda na wewe kumpenda na mengineyo.


Umri wako kuna wengi watajitokeza, vijana na wazee, wenye wake na watoto, wanene na wembamba.....muhimu ni kutulia na kufuata Moyo wako na usisahau Akili....kwa maana epuka mwanaume wenye familia na epuka kuwa Mke wa pili hata kama Dini inaruhusu na Moyo unataka kwenda huko.


Kuwa na mume wako peke yako ambae hajawahi kuoa(hana uzoefu na ndoa au kuishi na mwanamke nyumba Moja) kuna raha yake atii.


Kila la kheri.

Mapendo tele kwako...

Tuesday

MAJINA YA WANAFUNZI WALIO CHAGULIWA KUJIUNGA NA SHULE za SIRIKALI KIDATO CHA TANO 2014/15

Majina ya Wasichana wote waliochaguliwa
A to Z  haya hapa
http://www.pmoralg.go.tz/menu-data/adverts/form-five-selection-2014/WASICHANA-SHULE-ZOTE.pdf


Majina ya wavulana wote waliochaguliwa kujiunga na kidato cha tano shule
Kwanzia A to L haya hapa
http://www.pmoralg.go.tz/menu-data/adverts/form-five-selection-2014/WAVULANA-MAJINA-YA-SHULE-A-mpaka-L.pdf

Majina ya wavulana wote waliochaguliwa kujiunga na kidato cha tano shule Kwanzia M mpaka Z haya hapa
http://www.pmoralg.go.tz/menu-data/adverts/form-five-selection-2014/WAVULANA-MAJINA-YA-SHULE-M-mpaka-Z.pdf


Sina raha na Mume wangu!

Dada dinah hongera sana kwa kazi unayofanya. Nina miaka
22, nimezaliwa ndani ya familia ya watoto 11. Nilipokuwa na miaka
14 nilizaa na kaka fulani aliye ni lazimisha kufanya mapenzi na kuharibu usichana wangu.

Wazazi wangu wali nikubali nyumbani baada ya hapo niliendelea na Masomo na niliendelea kuwa na wapenzi mpaka nika mpata ninayeishi nae leo yaani Mume wangu.

Tulifunga ndoa yeye ananizidi
miaka 22. Kwanza nilikataa kuolewa, ila Wazazi wakanisihi sana eti
nitawaaibisha.


Jamani tatizo langu ni kwamba kila kukicha naona mapya. Nikaja gunduwa kuwa mume wangu ana watoto zaidi ya 10 wote amewazaa kwa wanawake tofauti.


Mimi nilijuwa ana watoto wawili lakini siku ya Ndoa yetu alisema ya kwamba ana wa Tano, kitu kilichofanya hata tusile tunda ya ndoa usiku wa Ndoa.


Mpaka sasa mimi na mume wangu hatujapata mtoto na yeye ameifanya Ndoa yetu kuwa Kero kwani ana mwanamke mwingine nje, hamtaki mwanangu, Chumbani haniridhishi.

Hapa nilipo sijielewi kwani na sijui nifanyeje? Naomba ushauri.

**********


Dinah anasema: Ahsante na shukurani kwa Ushirikiano.

Pole sana kwa uzoefu mbaya ulioupata ukiwa bado ni mtoto, ningemshika huyo kijana ningemtesa mpaka atamani kufa mwenyeweee(I hate wabakaji that's all).

Naelewa kwanini Wazazi wako walikusihi uolewe na libaba jitu zima hivyo lakini sikubaliani nao. Pamoja na kusema hivyo Wazazi wako wanastahili Heko ya kuendelea kukulea na kukusomesha baada ya Ujauzito!

Ni vema (jambo la kumshukuru Mungu) kwamba hujazaa na mumeo ambae inaonyesha anamzigo mzito wa Ex na watoto wao. Hakuna mwanamke mwenye akili timamu anataka lundo la watoto na mama zao kwenye Maisha yake hata kama wanaishi mbali. Angalau mtoto mmoja utadharau....KUMI?!!! Akuuu. Anyway!


Sijui mlifunga Ndoa katika Mingini gani na kutokana na Uandishi/Ongeaji wako (nimehariri) inaonyesha unatoka pande za Burundi/Rwanda hivi nami sina uhakika na Sheria za Ndoa na Familia za huko.


Lakini natambua Nchi nyingi za Afrika zinatambua Haki za Mwanamke na sheria nyingi za kusaidia Wanawake zilibadilishwa miaka ya 90s mwanzoni na kati.

Ushauri wangu ni wewe kutoka kwenye hiyo Ndoa ambayo ni wazi ulikubali ili kuridhisha wazazi, sasa umekutana na Kero nyingine ambazo zinaongeza uzito wa wewe kutotaka kuendelea kuishi Ndoani humo.


Hatua muhimu ni:- Moja; rudi kwenu na kuelezea tatizo na kutoonyesha nia ya kutaka kurudi kwa Mumeo kwani tayari anamwanamke mwingine na kero nyingine uzijuazo.


Pili; Tafuta Wanasharia Wanawake au wanaosaidia wanawake kwenye masuala ya Familia na Watoto au Ndoa(inategemea huko mnaitaje)......wao watakupa ushauri wa kisheria ili kumtaliki Mumeo via Mahakama.

Kila la kheri.

Mapendo tele kwako...

Monday

Ex mwenye Mke...

Habari dada dinah, pole na majukumu. Napenda vile unavyotushauri, mimi ni mdada nina miaka 28 nimemaliza Chuo japo sijabahatika kupata kazi.


Kinachonichanganya miaka saba iliyopita nillikua na mpenzi lakini tukapotezana nimekuja kukutana nae 2O11. Akanambia amekwishaoa, japo tunapenda sana na kuna wakati mpaka analia sana kutokana na ile kupotezana.


Yeye anadai yuko tayari afanye utaratibu wote, hivi sasa huduma zote ananipa na akigundua nina mahusiano na mtu mwingine analia sana mpaka anadai nitamuua au atajiua kama baba yake mzazi alivyojiua.


Kijana nampenda sana ukizingatia ndio mpenzi wangu wa utotoni, hapa nilipo nina Operation nilifanyiwa mwaka 2O12 na naweza kusema yeye ndio chanzo cha Operation dada.

Nishauri nifanyeje kwani sijawahi kuwa na mwanaume akaniridhisha kama huyo kwenye maisha yangu hasa upande wa penzi.


Napata wanaume lakini sifurahi kuwa nao najilazimisha lakini nashindwa dada.


**************

Dinah ansema: Ahsante na shukurani kwa ushirkiano.

Kwanza kabisa achana na excuses za kipuuzi kama "mpenzi wangu wa kwanza", "mpenzi wangu wa utotoni" ....tena futa hilo akilini na liondoe Moyoni mwako kwani utakuwa Mtumwa wa Excuses hizo.


Pili, huyo kijana sasa ni Mume wa mtu mwenye familia aliyoijenga kwa Miaka Saba, yeye kuwa mpenzi wako wa kwanza au wa utotoni sio sababu tosha ya kumuiba Mume wa mwenzio. Yeye kuwa wa kwanza/utotoni haikupi haki kama "Mke wake wa Kwanza".....HUKUPASWA kuingilia ndoa ya watu.

Tatu, Mwanaume kukutimizia mahitaji yako yote sio sababu ya wewe kumkubali au kuendelea kuwa nae. Bibie hii ni 2014....Kama mwanaume anaweza kutafuta na kupata Senti za kutimiza mahitaji so can you! Jitume mwanamke ujitegemee Kiuchumi na mwambie apeleke visenti vyake kwa Familia yake na awekeze kwenye Elimu ya watoto wake.


Nne, Kabla ya Daktari kukuambia kuwa unahitaji Upasuaji lazima alikuambia tatizo ni nini? Naamini kilichopelekea wewe kufanyiwa Upasuaji ni tatizo lako la kiafya sema lilitokea baada ya Mpenzi wako huyo "kupotea" na wewe ukaamini yeye ndio alikuwa sababu....ungekuwa Depressed/mwehu ningekubaliana na wewe.

Tano, Huyo Kijana angekuwa anakupenda hakika angetafuta namna yoyote ile ya kuendeleza Mawasiliano na wewe hata kama ni mara moja kwa mwezi, lakini yeye akuu! hakujali na akaamua kusonga mbele na Maisha yake bila wewe, tena akafunga na Ndoa kabisa.


Baada ya Miaka saba ndio aja kwako analia na kukutishia atajiua. Legacy pekee aliyonao kutoka kwa Baba yake ni kujiua kama alivyojiua Baba yake.

Yeye kulia-lia, kum-cheat mkewe na familia yake, Wivu wa kijinga na vitisho vya kujiua ni wazi mwanaume huyo atakuwa na issues akilini mwake.

Ikiwa alitoweka na akaenda kuoa miaka Saba iliyopita...kitugani kitamfanya ashindwe kurudia tendo hilo tena pale akiwa "high" (nimekwambia ana issues akilini)....kumbuka anataka kumuacha Mkewe kwa ajili yako....technically alikuacha wewe kwenda kuoa....nini kitamzuia kurudia?....Jiulize.

Kwanini utake kuishi kwa hofu na Mashaka na mwanaume ambae inaonyesha ni "Mgonjwa" na tayari anamzigo wa Familia?!!


Ushauri wangu kwako ni wewe kukimbia, kama kujiua mwache ajiue salama kwani hilo ni tatizo lake na familia yake wewe halikuhusu, isitoshe kama uliweza kuishi bila yeye kwa Miaka Saba akijiua si ndio itakuwa kheri ili uwe huru zaidi, yaani bila harufu ya Ex mwenye familia kukufuata-fuata....eti!

Kuna wanaume wengi tu wanajua kuridhisha wanawake, ukiwa muwazi na unajua utakacho na kumuelekeza Mwanaume hakika utaridhishwa.

Kila la kheri.

Mapendo tele kwako...

Unampenda kimapenzi hautaki kumpoteza, ila humuelewi amebadilika.

"Je upo kwenye uhusiano wa mapenzi na mtu maalumu ambaye hutaki kumpoteza?, Je unapata hisia mbaya na unahisi kunakitu hakiko sawa maana kila ukitaka kumbusu mpenzi wako au kukaa nae muongee hana hisia tena kama alizokuanazo awali, kila kitu anakuwa na kisingizio na mizungusho mpaka unapata hisia labda kuna mt

Sifa wanawake wanazopenda, wanazoangalia na kuzitafuta kwa mwanauwe...

"Kila mwanamke kuna tabia ambazo yeye binafsi  hupendezwa nazo, iko kama ilivyo kwa wanaume wakati napo mwona msichana ila wanawake wao kidogo huwa vigezo vyao vingi huwa kama vina fanana japo

Mfanye Mpenzi Wako Unayempenda Achanganyikiwe Juu Yako Na Kukupenda Zaidi.

"Kwenye mahusiano ya kimapenzi ni vizuri uzito wa mahusiano uwe pande zote mbili, mapenzi huwa matamu zaidi iwapo umpendae naye anakupenda kwa kiwango umpendacho wewe, na si vinginevyo maana tofauti na hapo mapenzi huwa kama kero au mzigo na hisia hukupelekea kujiumiza moyo na kujiharibu kisaikolojia

Unaujua mvuto wa kimapenzi na siri zake, unajua ni nini kinachomfanya mwanamke avutike kwako na alama za iwapo kama atakukubali ukimtongoza?

Mwanamke ameumbwa kutoka kwenye ubavu wa mwanaume na siku zote mvuto wa mwanamke au hamasa juu ya mwanaume uwa ipo kwa kipindi chote ila kinachotofautisha hali ya upendo ya mwanamke kuvutika na wewe au la, ni kiasi cha mvuto[hamasa] alicho

Nini cha kuandika kwenye ujumbe wako wa kwanza wa meseji kwa msichana uliekutana nae kwa mara ya kwanza?

☆☆☆★ Umemwangalia machoni na kumsoma lugha ya kimatendo na ishara ya mwili, ukamsogelea kwa mbwembwe huku ukijiamini na kumsalimia ukiwa unamchombeza kwa maneno mazuri ya hapa na pale na kuyafanya maongezi kukolea na kuzidi kuwa matamu, mwisho mkabadilishana namba za simu, baada ya hapo na muda kupita unajikuta ukiwaza uandikeje ujumbe mfupi wa meseji utakaomtumia huyu mrembo mliokutana kwa mara ya kwanza anaekugusa moyo ili umfanye aongezea mvuto zaidi kwako, umuandikie meseji gani kumchanganya zaidi kihisia, na ni nini cha kuandika kwenye meseji yako ya kwanza kwa huyu kimwana?.☆☆☆★



Hakuna hisia nzuri kama ya kupata namba ya msichana uliyevutika naye, hii hisia inakuwa mahara pake na inasisimua zaidi iwapo msichana mwenyewe ndie aliyekupatia hio namba yake na ujumbe wako mfupi wa kwanza ndio utakaokupatia ufumbuzi kama ataendelea kuwa anakujibu meseji zako au vipi, na iwapo kama mvuto wake utaongezeka kwako au la, na kujibiwa kwa sms zako inategemea zaidi na jinsi na mazingira ya wewe ulivyoipata hio namba, iwapo hukuonyesha hisia wakati unaomba hio namba, na uliiomba hio namba kama rafiki, atakuchukulia kama rafiki daima na kubadilisha hio hali ya kundi alilokuweka kama rafiki ni ngumu mno hata kama unaujuzi wa hali ya juu kumrubuni kwa ujumbe fupi itakuwia vigumu kidogo kufanya hivyo, kwahiyo wakati wa mazungumzo hakikisha unaweka wazi japo bila kumweka wazi moja kwa moja, tumia maneno kumuelekeza uendako ila usiwe wazi ya kuwa unamtaka.

Iwapo namba hiyo umeipata kwa rafiki zake au watu wake wa karibu tegemea mambo kwenda kombo, ni mara chache sana na mara nyingi haiwezekani kuweza kumuhamasisha msichana kihisia wakati hujawahi kuongea naye na kwanza kile kitendo pekee cha wewe kutafuta namba yake kwa njia ya panya kunakufanya uonekane wa ajabu kwake kama mtu usiyejiamini mwenye wasiwasi na kutokuwa na msimamo wa kijisimamia mwenyewe hivyo unakuwa umejipotezea nafasi kwake na anakuwa hakupi uzito wowote ule ndani ya moyo wake.

Wanaume wengi huwa na hofu na kushindwa kutambua ni muda gani hasa ndo unaopaswa kuwa mwafaka kutuma ujumbe mfupi wa maneno kwa msichana waliovutika naye, maana huona iwapo wakiwahi kuutuma wataonekana kama malimbukeni na iwapo wakichelewa kuutuma itaonyesha kama hawakuvutiwa na huyo msichana hapo mwanzo na hivyo kumfanya msichana apate uwamuzi mbadala wa kuwatoa kichwani maana kwa muda waliochelewa kunaufanya mvuto wa msichana kupungua.

Ni vizuri zaidi na inaongeza mguso na mvuto wa msichana iwapo ukimtumia meseji mda kidogo mara baada ya kuonana kwenu, kupitisha muda kidogo kutasaidia kumpa nafasi ya kukuwaza na kumpa matamanio ya kujiuliza ni saa ngapi utapiga simu, kitendo hichi kitamfanya hausishe hisia zake na kumfanya aongeze mguso zaidi wa kihisia juu yako, hakikisha muda unaompa akufikilie usiwe mrefu sana na usizidi zaidi ya siku moja na nusu au atapata hisia mbaya na kuhisi labda hukuvutika na yeye kipindi mlipokua mnaongea pamoja na utamfanya apoteze ule mguso mliokua nao kwenye maongezi hapo kabla.

Wakati unamtumia ujumbe mfupi wa maneno, mkumbushe vitu vilivyokua vinamfurahisha wakati mlipokua mnazungumza kwa mara ya kwanza, hii itamkumbusha furaha aliyokua nayo pindi mlipokuwa pamoja, hakuna njia nzuri ya kumfanya akujibu meseji zako kama sio kumkumbusha nyie wawili mkikaa pamoja huwa kuna kitu kizuri kinaendelea baina yenu.

Je, nini cha kuandika na mambo ya kuzingatia wakati wa kuiandika meseji yako ya kwanza.

#1, Anza kwa kujitambulisha kwanza.
Salamu ni kitu muhimu na ni vizuri wakati wa kujitambulisha unaweza kumpa jina la utani ambalo linaendana na mada au kitu alichokua anapendelea, anafanya au alichokuwa amevaa siku siku ya kwanza mlipokutana, kama mlikutana kwenye sherehe na alikua anatumia soda pekee unaweza kutuma meseje inayoendana na hicho kitendo.

> Mambo mtoto mdogo, bado unaendelea na soda zako mpaka jioni hii, siku yako inaendaje?,

Hapa neno mtoto mdogo linakuwa kama jina lake la utani na kumfanya akukumbuke kwa urahisi zaidi, kuongeza jina la utani linakuwa linaleta hali flani ya ucheshi kwenye sentensi na kumfanya atabasamu wakati anaisoma hio meseji.

Hata ukitumia jina lake, tafuta namna utakavyoliita wewe ambavyo watu wengine hawamuiti hivyo,

Kama anaitwa Christine - Muite Tina
Francisca - Sisca,
Upendo - Love,
Angel - Malaika.

#2, Usitume meseji ya kumkweza, jaribu kuwa tofauti na wanaume wengine.
Kila mwanaume huanza kwa kumkweza msichana, mara nyingi huandika "Jana nilifurahi sana kuonana na wewe, namshukuru mungu kwa kunikutanisha na wewe, kwa ukweli ulipendeza sana sijawahi kuona katika maisha yangu toka nizaliwe", maneno kama haya yanakupotezea nafasi ya kuwa naye na yanafanya kukushusha hadhi yako, yanampunguzia msichana mvuto kwako na kukuona wewe ni wa kawaida tu na wala si chochote wala lolote kama wanaume wengine aliowakataa, kujishusha hadhi kunapoteza mvuto wa maneno unayoyaongea, kuna poteza ile heshima aliokuwa amekupa awali, kwa sababu unakua umejitoa kwenye hali yako uliokuwa umepewa ya umaalumu flani na kujiweka kuwa mtu wa kawaida, umaalumu ndo unakufanya umpate msichana na sio utu wa kawaida, tunza hadhi yako na utamvutia kama sumaku.

#3, Msifie.
Sifa zinawafanya wanawake wajione wa pekee, wanawake wote wanapenda kusifiwa na sifa inamfanya ajisikie yeye ni mzuri na anavutia ambacho ni kitu kizuri sana msichana anachoweza kujisikia na hukifurahia kwa hali ya juu ila msifie pale panapo haitajika kusifiwa sio kila muda, akizoea sifa unazompa atakuona huna jipya na mvuto aliokua nao kwako hapo mwanzo ndo utaufanya upungue kwa hali ya juu, usitoe toe sifa kijinga, pangilia sifa zako na utaona matokeo mazuri.

#4, Usitume meseji ndefu za kuchosha na kukatisha tamaa kusoma.
Ukituma meseji jaribu iwe fupi na inayoeleweka.

#5, Kuwa mbunifu na usitabilike.
Kuwa tofauti na jaribu kuwa na kitu kipya kila wakati na utafanya mvuto wake kwa kwako kuripuka kama mlima wa volikano, ubunifu unafanya maongezi kuwa matamu zaidi, kama akikuuliza siku yako imeendaje,

Jibu > "Siku yangu ilikua tata, watu huwa hawaishi kunishangaza".

Hii itampa hamu zaidi ya kutaka kujua na kufanya maongezi yazidi kupendeza zaidi.

#6, Usitume meseji nyingi kwa mkupuo.
Ukituma meseji moja subiri majibu, unapoteza mvuto unapotuma meseji mfululizo na kuonekana unashida naye sana na kupunguza ile hali yake ya mvuto kwako, kuwa mwanaume kiongozi na tuma meseji moja, subiri jibu ndo utume nyingine.

#7, Tumia alama za maneno.
Zinaleta mvuto zaidi na uelewa wa kihisia kwa kile unachoandika, andika neno zima na usitumie vifupisho vya maneno.

#8, Fanya utani.
Utani unaleta ukaribu na unafanya mzoeane kwa haraka zaidi, ila fanya utani ukiona utani unanafasi, usianze kwa kumtania kwanza jua yupo katika hali gani, kama ni hali ya kiucheshi unaweza weka utani kidogo kukoleza mambo vizuri maana wanawake wanapenda sana utani.

#9, Mkaribishe mahali ulipo ila usimwalike.
Kama upo unafanya kitu unaweza mwambia kile unachofanya na inakuwa vizuri zaidi usimwalike, hii itamuongezea hali ya mshangao kwako, na atashindwa kukuelewa we ni mtu wa aina gani na itamfanya awe mdadisi zaidi ambao utasababisha mvuto wake kuongezeka zaidi juu yako na kupata hamu zaidi ya kukujua.

> Nipo ziwani naangalia jua linavyozama, hali ya hewa imependeza kweli na anga limekua la manjano, natamani ungekuwepo!, baadae nitakutumia ujumbe nikifika nyumbani.

Mtamanishe mazingira uliyopo ila usimwambie njoo na kuonyesha hitaji la wewe kumtaka awepo mahali hapo, hii inamuongezea husuda ya kutaka kuwa sehemu ya maisha yako.

#10, Wahi kuaga.
Ukiona maongezi yamenoga sana wahi kuaga na hakikisha anaeanza kumuaga mwenzie ni wewe, hii itafanya awe na hamasa zaidi na wewe na utamzidishia hamu zaidi ya kutaka kuwa anaongea na wewe na wakati wa kuaga mpe ahadi ya kuchati nae wakati mwingine baadae.

Jua namna na nini cha kuongea wakati wa utongozaji, ili kumtongoza mwanamke kwa mafanikio zaidi.

★"Ulishawahi kujikuta unatamani kumtongoza msichana mzuri sehemu flani japo upate namba yake ya si
mu ila unajikuta huna jinsi yeyote au wazo juu ya nini cha kufanya au kuongea, unatamani kumfata nguvu miguuni zinakua zimekuishia unashindwa hata kupiga hatua moja kumsogelea, lile wazo pekee la kutaka kumsogelea linakufanya moyo uwende mbio, mikono iloane na jasho jembamba kukutoka huku akili yako ikishindwa kufikiria vizuri nini cha kuweza kuongea iwapo ukimsogelea?."★


Leo tunaangalia mwendelezo wa mada ya jinsi ya kuto

Njia rahisi za kuwavutia wanawake kihisia na kufanya wakupende, Je unazijua?

"Saa nyingine ni vitu vidogo vidogo tu ndo vinavyotengeneza mshiko mkubwa kihisia, sifa moja ya akili au ishara ndogo tu inaweza kumshika kihisia mwanamke, vile vile ukitoa sifa mbaya ndo mwisho

Misamaha Lukuki lakini wapi!

Hi dada,
Mimi ni binti wa miaka 25 na mfuatiliaji wa blog yako japo si sana. Nahitaji msaada.

Nilikuwa na mpenzi wangu miezi kadhaa imepita sasa, hatuwasiliani coz tuligombana. Nilijaribu kumuuliza tatizo la yeye kunichunia (maana yeye ndio aliacha kunitafuta ghafla) anasema hamna shida.

Nikajitahidi mtoto wa kike nikamwomba misamaha lukuki kwa kosa ambalo halijulikani,lakini wapi!. Nikashirikisha baadhi ya ndugu zake na marafiki....hamna kitu.


Mwisho nikaona ya nini nifeli Chuo mie nikakaa kimya. Lakini Moyoni bado nampenda sana, taratibu upendo ukaanza kupotea.


Juzi kati akanitafuta akiniambia kwamba "unajua kazi nyingi" nikaona huyu asinizingue, basi nikawa namsikiliza anavyonipa kesi ya kunitenga mara huyo akapotea.

Sasa tatizo ni kwamba kila ninapopata hisia za mapenzi nakimbilia kwenye Mtandao nasoma au naangalia picha za mapenzi basi nakuwa sawa kiasi, na hii tabia naona inakua na mimi sipendi mchezo huo. Ukizingatia kwa sasa Ex wangu wa ananisumbua sana na nahisi
nahitaji mapenzi .


Sasa ndio sijui nifanye nini. Naomba unisaidie.

*********


Dinah anasema: Hello there, shukurani kwa ushirikiano.


Hako kaeksi kako nako hakakuwa tayari na Uhusiano. Kutokana na maelezo yako nadhani "Ex" wako hakuwa anachukulia muungano wenu kama Uhusiano wa kimapenzi bali "company" kwamba mnatoka na pengine kufanya ngono....nothing serious yaani hakuenda mbali huko kwenye Uhusiano ambako wewe ndio ulikuwepo.

Unajua ni vigumu kwa mwanaume kueleweka kwa binti wa miaka 20nakitu akisema wazi "nataka niwe na wewe kwa ajili ya kutoka kila ninapokuhitaji, sitaki uhusiano".

Ila ni rahisi kumtongoza mwanamke kumapata kisha kuingia mtini kila anapohisi hakuhitaji.....siku akikuhitaji anakutafuta tena na kuomba msamaha au kukupa hadithi.


Kama unahitaji uhusiano serious basi achana nae na songa mbele na Maisha yako mpaka utakapopenda tena.


Kuhusu kukimbilia kwenye Mitandao kila unapojisikia Nyege sio kitu kibaya ailimradi unajua "limit" yako.....kuna wanawake wengi hufurahia Porn pia sema huona haya kusema.


Ila nadhani itakua vema kama utakuwa unajipa Mkono kuliko kutegemea Picha za X. Sio mbaya kujisaidia mara mbili-tatu kwa mwezi, inasaidia kukuweka vema Kingono na pia kuujua mwili wako zaidi kama mwanamke.


Kila la kheri.

Mapendo tele kwako...

Ex aomba turudiane...

Shikamoo dada dinah.
Mimi ni msichana wa miaka 20na naishi Dar. Ninatatizo, hapo mwaka 2010 nilijihusisha na mahusiano na kijana mmoja ambae hakua na kazi alikuwa anaishi na rafiki yake.

Ila mara nyingi alipokuwa akiumwa nilimhudumia kwa matibabu, chakula na hata pesa ya matumizi wakati mwingine nilikuwa nampatia sababu mimi nilikuwa nafanya kazi.

Baada ya Mwaka mmoja nikaanza kuwa namfanyia surprises mara nyingine naenda anapoishi bila kumwambia nikawa nafuma sms za mapenzi nakuta amemtumia msichana. Akawa ananiomba msamaha namsamehe.


Baada ya muda tena nakuta sms za mapenzi mwishowe nikachoka nikaamua kuachana nae. Japokuwa niliachana nae ila bado alikuwa ananifuatilia na kuniomba msamaha.

Hivi karibuni alinifuata tena na kuniomba msamaha na kuomba turudiane sababu anakumbuka wema wangu nilomfanyia wakati hana kitu.
Sasa hivi yeye ni General manager wa kampuni fulani Dodoma.

Anasema anajisikia vibaya kutumia na msichana mwingine wakati nipo niliyemvumilia wakati wa shida. Sasa sielewi dada nifanyeje kiukweli  bado nampenda ila naogopa kuumizwa tena na mapenzi.

*************


Dinah anasema: Marhabaa Mrembo, shukurani kwa Ushirikiano.


Nina chuki ya kipekee na Exes (wajinga-wajinga) ila huyu wako tumpe robo Moyo (nafasi) kama rafiki kwanza ili tuone kama yaliyomo yamo kabla ya kutoa Moyo wote.

Maana ukikurupuka ukatoa Moyo wote alafu ukaja kugundua kuwa jamaa anamtoto au mpenzi mwingine utaumia mpaka upoteze hamu ya kuwa na Mwanaume mwingine maishani mwako.

Sasa kabla ya yote ni vema mkae chini na kuzungumza kuhusu mnachokwenda kukifanya.....weka hisia zako wazi kuwa mlipokuwa pamoja hakuwa muaminifu na tabia hiyo ilikuumiza sana na unahitaji kuthibitishiwa kuwa ni muaminifu ili umuamini.

Hoji (huku unachunguza taratibu) ili kupata ukweli kama yupo "single" au anataka kulipa Wema wako (kutumia na wewe) wakati ana Mpenzi mwingine. Ukigundua yupo ni m-clean (hana mpenzi wala baby mama) basi ongeza robo iwe Nusu Moyo.


Mkiendelea vizuri na akawa muaminifu basi mkabidhi Moyo wote ila ubaki na akili zako.


Mambo yasipoenda vizuri basi songa na maisha yako na utapenda tena.

Inaonyesha ni binti unaejielewa, unajitegemea kiuchumi, Mvumilivu na mwenye utu na huruma (kutokana na maelezo yako).

Kila la kheri.

Mapendo tele kwako...

Sunday

Ukaribu na Mpenzi...

Halo! vipi mzima dada?

Mimi ni mdada ambae nahangaika sana mwenziko, sina hata raha. Kuna mkaka ambaye mwanzo alinipenda sana, ki ukweli nami nilimpenda kwani ni Mstarabu sana na kila nimuombacho hunipa.

Ila sasa hanitafuti mara kwa mara yaani labda baada ya wiki kama mbili hivi ndio huwa ananitafuta. Nikimpigia na kumwambia anadai kazi nyingi na huko yupo kijijini.


Sometimes akija weekend ananiambia to meet but ni wa kwanza kubreak hiyo promise yaani ni Mr promiseless!!


Pamoja na kuwa ananipa chochote nitakacho bado nahitaji ukaribu wake kwangu sasa sijui hata nifanyajee please help
me.


Najua nakusumbua ila I know unajua more na unaweza nisaidia vizuri tu.

**********

Dinah anasema: Hello! Namshukuru Mungu mie ni Mzima. Ahsante kwa ushirikiano.


Kwanini uhangaike Mrembo wakati unajua kabisa mwenzio anahangaikia Maisha ambayo wewe pia unafaidika(anakupa kila umuombacho).


Natambua kuwa ukaribu na mpenzi umpendae ni muhimu na it feels GOOOOOOD lakini kuna kitu kinaitwa Compromises.....wakati mwingine kwenye maisha ya kimapenzi inabidi tujaribu kuwaelewa wenzetu na kukubali ku-compromise so long as Mpenzi alie busy hafanyi Ushenzi nje ya Uhusiano husika.....sio kulalamika na kufikiria na kujali hisia zetu pekee.

Kutokana na maelezo yako inaonyesha wazi kuwa Mpenzi wako anabanwa sana na shughuli zake na pengine anapokuwa mbali na Mji(kijijini) labda network inasumbua na anashindwa kuwasiliana nawe(umewahi kufikiria hili?).


Pia ni vema utambue kuwa kuna Umri fulani ambapo baadhi ya Wanaume hu-focus zaidi kwenye kuweka Maisha sawa alafu mapenzi ndio hufuata. Huenda Mpenzi wako ni mmoja wao.

Nadhani anadhani kuwa ni rahisi kwako kumuelewa akivunja promise kuliko Boss au Mama/Baba yake na hii inatokana na "priorities" zake.

Inawezekana kwenye priorities zake za maisha wewe unachukua nafasi ya 2 au tatu, kwamba kazi yake kwanza, familia yake pili na wewe tatu....au Kazi kwanza(Pesa), wewe pili kisha familia yake. Hii haina maana kuwa hakupendi bali umuhimu wako na kazi kwenye maisha yake vinatofauti(kwa sasa).

Pamoja na kusema hivyo ni vema mkipata nafasi mzungumze kuhusu hili, Mawasiliano yenu yatasaidia kila mmoja wenu kutambua umuhimu wake kwa mwenzie.


Wakati huohuo mkubaliane namna ya kuwasiliana, kwa kumwambia Mf; "sio vema kukaa kimya kwa Wiki mbili, tujaribu kuwasiliana mara kwa mara ili kuondoa hofu kwani siku moja ni ndefu sana kwa uhai wa mtu umpendae".


Uhusiano ukikomaa(kama bado) au mkiwa tayari kwenda "level" nyingine basi ukaribu utakuwepo bila kuuomba...namaanisha Ndoa au Kuishi pamoja kama "Trial" kabla ya Ndoa.


Badala ya kukosa raha kutokana na umbali (anapokuwa kazini) jaribu kufanya mambo mengine ambayo yatakufanya ufurahie maisha yako kama Mwanamke. Ikiwa huna Kazi/Shughuli basi tumia muda mwingi na familia yako, ndugu, jamaa na marafiki....hii itasaidia kukimbiza masaa na siku.

Kamwe usifananishe maisha yako ya kimapenzi na yale ya watu wengine au uyaonayo kwenye TV au usomayo kwenye Magazeti.

Kila uhusiano wa kimapenzi ni tofauti kwasababu wahusika wake ni watu tofauti hivyo hakuna uhusiano ambao ni sawa na mwingine na pia hakuna uhusiano ambao ni perfect kama uonavyo kwenye TV progs.

Usiizoeshe akili yako kukosa raha kwani itapelekea Depression na hivyo kuwa mtu wa huzuni(kukosa raha) tu kila kukicha.


Ni bahati kuwa na Mwanaume anaekupenda, Mstaarabu, Mchapa kazi na anaekujali(kukupa chochote utakacho)......Most men wana moja au mawili kati ya hayo.


Kila la kheri.

Mapendo tele kwako...

Friday

Mke wangu na Jamaa, siwaelewi....

Dinah pole na majukumu pia usituchoke mimi ninamatatizo na Mke wangu ambayo yamepelekea kuwa Mlaji wa Milungi maana silali.

Inshu na Mke wangu ilianzia pale alipokuwa hanipi ushirikiano Kitandani na kila nilipo mwambia anasema kachoka. Nikahisi kunajamaa anamazoea nae yamepita kiasi, nikaanza kufuatilia mara nikakuta Vidonge vya kuzuia mimba.

Nilipomuuliza akaniambia havitumii vilikuepo kwa muda, mie sikuridhika na maelezo yake. Basi nikamwambia twende kweo lakini akataa, ikabidi niondoke pale kwenye ile nyumba nikarudi kwetu.

Mara akaja na yule jamaa niliekua namhisi na Mke wangu eti kaja kuchukua kifaa chake so jamaa kaja kumsaidia, wakachuka hao wameondoka sasa dada dinah hii inshu imeniathiri sana kwani nimetokea kumchikia sana mke wangu.


Hivi muda wowote namuacha coz kila nikimfikiria jamaa na Mke wangu nakosa hamu yakufanya Mapenzi, hata awe mwanake mwingine sitamani.


Mimi na Mke wangu tumezaa mtoto mmoja wa kike naomba ushauri wako please!


*************

Dinah anasema:Ahsante na shukurani kwa ushirikiano. Walaa sichoki, nikichoka nitafunga Blog.


Inshu yako imechichanganya....pale uliposema ukamwambia mkeo arudi kwao, akakataa kisha wewe ukatudi kwenu.....kwani mlikuwa mnaishi wapi? Hotelini au Mkeo anaishi na huyo Jamaa?....hata hivyo nitakujibu kama ifuatavyo.


Kutumia Vidonge vya kuzuia Mimba sio kosa kama Mkeo hataki kuzaa tena, haina maana kuwa anatoka na mtu mwingine.....inawezekana kweli ni vya zamani, kwani baadhi ya wanawake hubadilisha Vidonge pale wanapohisi kuwa haviwafai....Vidonge sio kielelezo cha kucheat.

Kutokukupa ushirikiano kitandani inategemea na shughuli zake za kutwa nzima, pia sio sababu kuwa anaridhishwa huko nje. Kuna wanaotoka nje na bado wanatoa ushirikiano wa kutosha na kuonyesha mapenzi tele kwa waume zao.

Nadhani kwenye uhusiano wenu kuna ukosefu wa Nguzo muhimu iitwayo MAWASILIANO. Unahitaji kuongea na Mkeo, sio kumuambia. Kaeni chini na mzungumzie issue ya Uaminifu na unavyojisikia kuhusu huyo Jamaa, uhusiano wenu, mapenzi yenu na Mtoto wenu.

Siamini kuwa humpendi Mkeo, ila unahasira ambazo zinapelekea kuhisi kuwa "humpendi" lakini ukweli ni kuwa humuamini tena kwa vile unahisi kuwa anatoka na Mwanaume mwingine. Hali hiyo inapelekea kupoteza hamu ya kuwa nae karibu kimapenzi....

Issue yako haina ushahidi wa kutosha kuwa Mkeo anatoka na huyo jamaa ila inaonyesha unampa nafasi(unamsukuma) ili atoke na huyo jamaa.

Zungumzeni....vyovyote itakavyokuwa rudi tena na ujibu maswali yangu hapo juu.


Uliuliza via Comment ndio maana sikuweza kurudisha mail ili ufafanue kuhusi maswali yangu pale juu.


Tafadhali tumia Email kuuliza na sio comments.

Kila la kheri.

Mapendo tele kwako...

Wednesday

Hata sijielewi...

Shikamoo dada dinah, pole kwa kazi na hongera kwa kutuelimisha. Mimi ni
mwanamke mwenye umri wa miaka 26 naomba unipe ushauri kwani mpaka sasa sijielewi.


Mwaka 2005 nikiwa Kidato cha pili
nilijiusisha na mapenzi nikapata Mimba 2006 mwishoni, mwenye mimba
nikamueleza akaikataa. Yeye alikuwa mwanafunzi wa Chuo lakini Mama
wa uyo kijana alinihudumia kipindi nimejifungua mtoto ila kwa bahati mbaya akafariki.

Kwavile nilikuwa nampenda yule Kijana nikamsamehe tukawa pamoja lakini hakuwa mwaminifu na tabia yake ilinishinda nikaachana nae 2010 mwezi wa Tisa.


Nikiwa Chuoni mwaka 2011 nilianzisha uhusiano wa kimapenzi na Kijana mwingine ambae aliniahidi atanioa akanitambulisha kwa ndugu zake na Mwaka 2012 mwezi wa
Sita nikapata mimba.


Akaniambia nitoe Mimba kwani hayuko tayari kulea lakini mimi nikagoma kutoa na kumwambia sitoshindwa kulea mwanangu kwasababu nilikuwa
nafanya kazi. Huyo kijana hafanyi kazi na tulikuwa tunaishi Mikoa tofauti.

Nilikuwa namfata huko aliko, natumia hela zangu kwa mahitaji yake yote na akiwa na shida nilimtumia hela, lakini akanikataa nikalea Mimba lakini nyumban wanahitaji wamjue baba wa mtoto.

Nikakutana na Baba ambae ni Mume wa mtu, huyu baba kanihudumia katika kipindi kigumu nilichopitia naogopa
kumwacha sababu alinitendea mema sana.

Wakati huo huo kuna Kijana mwingine ambae nimejuana nae kwa Miaka Kumi na Mbili. Kwa sasa hana kazi ila anasimamia Miradi ya kwao, nikitumiwa hela na yule Baba(Mume wa mtu) natumia nae lakini hajui inatoka wapi.

Sasa yule Kijana amenambia niendelee na yule Baba kwa kuwa alikukuta nae kwani hawezi kunikataza. Akasema kwa sasa hana hela hawezi kunihudumia ila atapata. Kijana wa watu akalia nami nikalia kwasababu iliniuma.

Nampenda huyo kijana kwani katika hiki kipindi kifupi kanionyesha mapenzi ambayo sijawahi kuyapata. Ananijali, ananiheshimun ananipenda na kunithamini.


Japo nampenda lakini simwamini
sana sababu wadada na wanawake wanamsumbua kwa sms na kumpigia
simu.


Huyu kaka nilikuwa nampenda toka nilipokuwa Primary Miaka 12 iliyopita sasa sijui nifanyeje. Tumeanzisha
mahusiano toka mwezi wa pili mwaka huu ndiye ninae mpenda.

Naomba ushauri dada yangu, pole na
hongera kwa kutuelimisha.

***********


Dinah anasema:Marhabaa! Ahsante na shukurani kwa Ushirikiano.

Ingependeza zaidi kama ungekuwa unafikiria Watoto wako kabla hujafanya maamuzi yako na hao wanaume. Wanao bado ni wadogo na wanahitaji full attention yako...kumbuka Baba zao wamewakataa.

Sio vema kuanza kuwaongezea wanaume holela holela maishani mwao ambao sio baba zao...Kumbuka mtoto anatunza kumbukumbu ambazo humuathiri Kisaikolojia ukubwani kuanzia umri wa miaka Mitatu.

Ni vema ukaachana na huyo Mume wa mtu ambae inaonyesha humpendi ila upo nae kama "malipo" kutokana na wema wake wakati wa matatizo. Mume wa mtu ataongeza "mzigo" wa aibu kwa watoto wako hasa kama jamaa anawatoto.....Hawana baba alafu Mama kazaa na Mume wa mtu(kwa mfano ikitokea unashika Mimba tena).

Ni vigumu kumuamini Mpenzi wako Mpya kutokana na ukaribu wake na wanawake....lakini huna nguvu ya kumuambia aache mazoea hayo wakati wewe ulimkubali ukiwa na Mtu mwingine(mume wa Mtu).

Uwezekano ni Mkubwa akawa anatoka na mwanamke mwingine ili muwe sawa...kwamba yeye anakuiba kutoka kwa Mume wa mtu na wewe unamuiba kutoka kwa mtu mwingine.

Pamoja na kumpenda ni vema ukafanya "jaribio" ili ujue kama mpo kwenye Jahazi moja au anakutumia ili kukidhi mahitaji yake Kiuchumi.

Acha mazoea ya kumpa pesa(kutumia nae) huyo kijana kwani atazoea vibaya....yeye ni Mwanaume anapaswa kutafuta namna ya kuingiza Kipato ili mkichanganya msaidiane. Mpe ushauri ili aombe kulipwa kwenye hiyo Miradi anayosimamia...hata kama ni ya Kifamilia ni vema akapewa "kifutia jasho".

Baada ya "jaribi" na ukagundua jamaa anakupenda pia basi endelezeni uhusiano wenu na muone utakavyokwenda.

Pesa zako zitumie kwa watoto (wekeza kwa watoto), kumbuka yeye hana watoto na wewe unawatoto Wawili ambao hawapati Msaada kutoka kwa Baba zao. Hakikisha watoto wanapata Elimu nzuri, wanakula vizuri, afya njema na wanapata mahitaji mengine Muhimu.

Natambua unamaisha yako kama mwanamke na ungependa kuwa na mpenzi, lakini kwa vile sasa wewe ni Mama badilisha mpangilio wa Maisha yako (priorities)....Watoto kwanza, Kazi pili, kisha Wewe alafu wengine wafuate.

Vyovyote utakavyoamua hakikisha watoto hawawazoei wanaume unaotoka nao, kwasababu wakiwaozoea kisha baadae mkaachana....itaongeza athari kwa watoto Kisaikolojia hapo baadae (wakikua).


Kila la kheri.

Mapendo tele kwako...

Monday

Ex anigombanisha na Mama

Habari yako dada dinah, hongera kwa kazi nzuri yakuelimisha jamii. Mungu akuzidishie upeo wako. Mimi ni mwanamke wa miaka 25 na pia ni Mwanafunzi wa Mwaka wa mwisho Chuoni.


Naishi Marekani na familia yangu (mama na wadogo zangu). Kukata maelezo ni hivi; nilijuana na Ex wangu kupitia Mitandao ya Kijamii. Yeye anaishi Dar na kufanya kazi kwenye Kituo kimoja cha Radio.


Ni Mkaka alienizidi miaka 7, tulizoeana kwa muda na hatimaye tukawa wapenzi. Najua unaweza usinilewe kwa nini nilianzisha mahusiano kwenye Social Networks while am miles away.

Basi tulipendana kama ujuavyo mapenzi akanieleza maisha yake ambayo kwa alivyoyaeleza kama ya kawaida na mimi nikamweleza ya kwangu vile vile.

Nikiwa bado sijaonana nae nilifanya mpango wa yeye kuonana na Mama yangu mkubwa ambae amenilea tokea mdogo. Kweli alienda kuonana na Mama yangu mkubwa ikawa rahisi kwa mimi kuzidi kuweka imani na huyu kijana.

Mwaka ukapita nikasema nitajibana hivyo hivyo ilimradi nirudi nyumbani nikamwone. Kweli tulionana mwaka jana mwezi wa Pili nia na madhumuni ilikuwa tujuane zaidi lakini nikagundua matatizo yake kwa kipindi kifupi nilicho ishi nae ambayo ni Miezi Minne. ‎


Niligundua kuwa ni Mvivu sio maisha tu mpaka na mambo ya chumbani. Sikuwa free na yeye maana hakutaka nijiachie alisema hapendi kusikia miguno kwa kuwa anahofu majirani watasikia. nikamsikiliza kwakuwa nilikuwa nimezimika kwake.

Kero ya pili ikaja hataki niongee usiku yaani nisiwe free anaasema napiga kelele. Nikajipa moyo nivumilie kwa sababu nilivichukulia vitu vidogo.


Kero ya ya tatu ilikuja ni kwamba familia yake inamtegemea yeye kwa kila kitu hali inayofikia mpaka Mkate wa ahsubuhi apeleke na sio kwamba kwenye familia yake hakuna Vijana wapo kama wa 5 wakubwa na wadogo kwake lakini hawataki kazi hivyo yeye ndio aliebeba Msalaba.


Kabla sijaondoka akaniambia kuwa ameridhika na mimi nakutamani siku moja niwe Mkewe. Nilifurahi hivyo tukawekana kwenye mikakati ya maisha nini tufanye na nini tuepukane nayo.
Muda ‎wangu ukafika nikaondoka zangu na kurudi huku.


Nilipofika familia yangu ikamwambia akajitambulishe rasmi kwetu hivyo akatoa Posa lakini kabla hajafanya hivyo nilimsihii asifanye mambo kwa papara au kwakuwa familia yangu imesema ndio afanye akajibu anafanya hivyo kwakuwa anamalengo na mimi.


Basi baada ya miezi michache baada ya posa nikamwambia kwa kuwa saivi anawaza mimi kuwa Mkewe ajipange atafute Biashara afanye maana kazi yake inalipa Mshahara mdogo kulipia Kodi ya Nyumba yake plus familia yake.


Akanijibu sawa lakini hakuna kilichofanywa nilijitahidi kila wazo kumshauri afanye haikuwezekana. Ni mtu aliezoea kuingia Kazini jioni muda wa masaa matatu kamaliza kipindi anarudi Vijiweni/Bar kwa washkaji zake.

Ile hali iliniumiza maana ni mtu anaejulikana mjini lakini hataki kusaidiwa na watu zaidi ya kujionesha ana kitu ilahali anakufa na tai yake shingoni.


Nikaona nisimng'aninize sana nikamshauri afanye basi chochote anachokipenda ili mradi kimwingizie Kipato. Ikawa hola! Hakufanya. Muda ukaenda kuna hela nilipata ya Mkopo nikanunua mzigo Nguo, Viatu na Accessories za kike tufanye biashara hapo Dar ili tusogeze maisha lakini pia ili mshinda aliuza robo tu na vyengine kubaki navyo huku akiwa na sababu nyumbani biashara ngumu.

Kuanzia hapo ndio nilipoanza kumtoa Moyoni maana niliona najitahidi kupanga nae mipango ya maisha lakini mwenzangu ananiangusha hivyo nikawa mchungu maana nimetoa hela ya Mkopo yote kwenye biashara while yeye hata Sumni yake sioni mtu anaejita mchumba kwangu.


Nikaanza kumpotezea hali iliofikia mpaka tukawa tunagombana kila siku. Yeye akawambia familia yangu waongee na mimi ambapo mama yangu aliniambia nimvumilie nisiwe haraka na maisha.


Nikawasikiliza familia yangu lakini still yale mapenzi na hisia zilizokuwepo before zikatoeka sikuwa namuona kama bwana wangu tena. Nikamvumilia hivyo hivyo kwakuwa sikuwa na mtu wa kunisupport upande wangu zaidi ya wadogo zangu tu. 

Baada ya miezi mitatu‎ nikiwa na fanya shopping na familia yangu nikakutana na mkaka ambae ni Mwafrica ila si Raia wa Tanzania. Tukabadilishana namba na kuanza mawasiliano.


Nikaanza kutoka nae maeneo mbali mbali yote kupunguza stress kichwani mwangu na wala sikuwa na wazo la kuja kufall kwa huyu jamaa mpya ambae amekuwa karibu na mimi pamoja na familia yangu.

Ex wangu akaanza kero maneno maneno yakawa mengi baada ya kuona na mpuuza maana sikuwa tena na ile kumshauri kama ilivyokuwa ada yangu nilimwacha afanye ajisikiavyo yeye.


Akaanza kuambia familia yangu na other relatives kwamba nimebadilika simjali kama zamani kitu ambacho kilinipiss off maana kila mtu ikawa mimi ndio mbaya.

Nikamwomba ex wangu kistaarabu tuachane maana sioni kinachoniweka na kero zimeashakua too much. Yeye akasema nisahau icho kitu hawezi kuniacha labda kama nataka kusikia kajiua.


Mara akawa ananiambia jamii itamcheka akiachana na mimi. Ilimradi nikawa simwelewi na threatens kibao‎.
Mbaya zaidi izo threatens zake kawaeleza mpaka familia yangu hali iliyofikia kwetu hasa mama yangu mzazi kunilazimisha nijari‎bu kukaa na huyo jamaa hata kama mapenzi yamepungua kwake.


Ukweli nigombana na mama yangu kwenye hili suala na hii hali imechangia mimi kukaa na huyu kijana mwengine muda mwingi maana nyumbani kwetu kuna waka moto.

Kwa sasa najiona nimeshaanza kumpenda huyu mwengine. Ila ndio hivyo Ex wangu vitisho vingi, sijui hata nimweleze vipi anielewe.

Hata Mama yangu nimweleze vipi akae upande wangu kama mwanae. Maana sasa hivi mama yangu amemchukia Kijana wa watu as if yeye ndio alieanzisha ugomvi mimi na ex wangu wakati ugomvi uko tokea zamani.


Nitashukuru mawazo yako maana sina wakumuelezea hisia zangu akanielewa.

Ahsante.


***********


Dinah anasema: Wee niamkie....Habari ni njema tu Mrembo, shukurani kwa ushirikiano.


Huyo nae wa wapi?!!....wacha ajiue bana, Msiba ukiisha life goes on without him....kwani mlikuja wote Duniani? Kila mtu kaja kivyake na ataondoka kivyake. ( I hate Exes with passion....that's all)!!


Nadhani kuchekewa kwako kumaliza/ua Uhusiano ndio tatizo kuu. Ulipoanza tu kuhisi kuwa "hakufai" maishani basi ungeomba kwenu warudishe Posa ya jamaa na kuua Uchumba there and then.

Usijali wala kufuatilia anasema nini kwa nani, yaani kaa mbali na kila kitu kinachomhusu. Alafu muweke chini Mama yako....Mama haitaji kukuelewa, anahitaji kukubali uamuzi wako with or without her support.


Kwanza wao (Familia yako) ndio walikuwa na kiherehere kutaka huyo Ex ajitambulishe na kutoa Posa, sio wewe. Sasa wasianze kukulazimisha uvumilie sijui nini na nini....hii ni 2014 sio 1974....hatulazimishani wala kuolewa ili kulinda "heshima" ya familia....tunaolewa ili kufurahia Maisha na tuwapendao, kama hakuna mapenzi na furaha Ndoa ya nini?.


Au kama vipi mtokee Mdingi na umuombe kurudisha Posa....kama unaweza ilipe mwenyewe via Baba, Baba huwa waelevu sana kwa sisi watoto wa Kike hasa kwenye issue za Maisha na Mapenzi/Ndoa kuliko Mama.

Piga marufuku Mama yako, Familia na ndugu zako kujihusisha na huyo Mtangazaji na wakiamua kuendeleza "Mahusiano" ni wazi kuwa wanakana undugu wao kwako na ku-claim undugu na Mtangazaji....weka wazi kuwa hutaki kusikia lolote kutoka kwa huyo Ex.

Hayo yote hayawahusu, Mapenzi ni ya wawili....ukihitaji ushauri wao utawaambia lakini kwasasa waachane na huyo Ex kwani huna mpango wa kurudi huko. Wasikufuatilie na huyo kijana wa sasa unless wewe mwenyewe utake kuwahusisha.

Mama akiendelea kukuletea habari za Ex, mlie bati....yaani piga Kimya aka mnunie. Unamsalimia na unaendelea kumheshimu lakini hupigi nae stori(kama mnaishi pamoja).

Lakini kama upo kwako, na Mama kwake basi huna haja ya kumsalimia hata kwa Text....Mchunie mpaka agundue kuwa anachokifanya ni kosa na halikupendezi.....akikupigia mpe majibu mafupi na makavu ili kufikisha ujumbe kuwa hunafuraha na tabia yake ya "kushikilia Bango" issues zako binafsi...(works all the time).


Kama unahisi mapenzi na huyo Kijana mpya, hakuna haja ya kujibana....jiachie uone kama yaliyomo yamo ila usikimbilie mambo ya Posa na makorokocho Mengine kama vile Kuzaa mpaka uwe na uhakika na unachokwenda kukifanya na huyo Mwafrika (Asijekukutumia kwa ajili ya Makaratasi....Mjini hapa...)!


Hakuna haja ya kuwa stressed na maisha yaliyopita.....akijiua ni kutokana na matatizo yake mwenyewe na ataiumiza zaidi familia inayomtegemea na si wewe wala familia yako so akili kichwani mwake.


....fanya kama vile hujawahi kukutana nae....furahia maisha yako na kila la kheri katika kumalizia Masomo yako.


Kila la kheri

Mapendo tele kwako...

Sunday

Kutoka Mpenzi to Rafiki....

Nilikua na boyfriend wangu tulilkaa vizuri tu kama miezi mitano hivi lakini hakuwahi hata kunibusu wala kuongelea mambo ya Ngono.


Ni mtu wa Dini hivi, sa siku moja tukiwa out nikasema nimjaribu nikamwambia naomba nikukiss na nikihug, alishtuka akasema ni mapema, basi akanirudisha nyumbani.


Cha ajabu kuanzia siku hiyo akanichunia hapokei simu wala kujibu sms. Ikabd niwe mpole, baada ya miezi kama Nane hivi akaanza kunitumia sms za kunisalimia na mimi nikawa narespond bila kuonysha knyongo.

Baada ya Wiki mbili tangu mawasiliano yaanze upya akaanzisha topic ya utaniutani tu wakati tunachat maana ni kama rafiki sasa. Akasema kuwa anatamani kuwa na mtoto, na mie nikamjibu hata mimi natamani mtoto unaonaje ukinipa mmoja?


Duu si akauchuna tena hadi leo ni wiki mbili sasa kauchna. Kiukwel Dinah nampenda huyu jamaa na natamani anitangazie Ndoa ila sasa sielewi nitafanyaje maana ana misimamo yake ambayo inanipa vikwazo mie kumsogeza karibu kimapenzi.

***********


Dinah anasema: Hello there! uelezeaji wako mzuri (unavutia kusoma) hasa pale "duu si akauchuna tena".....usijali kichaa mie!


Nadhani kuna kutokuelewana kati yako wewe na huyo Kijana, kwamba yeye anataka urafiki ili mfahamiane kwanza kabla ya kujikita kwenye "Mapenzi ya Mwili" na wewe unataka kwenda moja kwa moja kwenye Mapenzi.

Katika hali halisi miezi Mitano ni muda mfupi (kama mnakutana mara mbili kwa wiki).....hasa ukizingatia ni MwanaDini.

Kitendo cha wewe "Mwanamke" kulianzisha kimemtisha....yeye ndio mwanaume na pengine alidhani kuwa umechukua nafasi yake.


Kumbuka sio wanaume wote ambao wanakubaliana na "usasa" wa wanawake....kwamba hata mwanamke anaweza "kulianzisha"(well mie na usasa wangu walaa nisingethubutu....hehehehe 1st time ni nafasi na mwanaume atiii).

Nadhani kujiamini kwako na kuomba Busu na Kubato kulimtisha na kuhisi "huyu mwanamke vipi" ikabidi ajipe muda.


Tangu unajua ni mpenda Dini, alipokuja na utani wake wa kutamani mtoto, ungemwambia...."Hata mimi natamani mtoto, lakini nasubiri mpaka nitakapofunga ndoa"....ingemrudishia imani. Jibu lako lilimtisha....ni kama vile unataka kuzaa kabla ya Ndoa wakati Imani yake hairuhusu....sijui umenielewa.


Pamoja na kuwa unampenda lakini usipokuwa Makini utakuwa unapoteza muda wako kusubiri Jamaa ambae huna uhakika kama atakuwa na wewe kimapenzi au la, na hata ukiwa nae utaweza kuishi maisha ya Kumpendeza huyo anaemuamini kama ni Mungu au Kanisa n.k?.

Kwasababu hakuna uhusiano ni vema ukamuambia wazi unavyojisikia....na ku-demand kujua msimamo wake kwako...je tuendelee na urafiki tu au mtegemee mapenzi out of urafiki?


Akijibu urafiki basi mchukulie kama rafiki na umuache kama alivyo na ufunge Mlango wa mapenzi kwake. Kisha ufungue mlango wa pili kwa ajili ya mtu mwingine utakaependana nae.


Tangu hamjaonana mkiwa watupu then mnaweza kabisa kuwa mafariki hata kama ukipata Kijana mwingine.


Kila la kheri.

Mapendo tele kwako...

Pages