Friday

Ndoa na Kaka wa kambo (step Brother) ni sahihi?

"Mimi ni msichana wa miaka 23, nina kaka yangu baba mmoja na mama tofauti. Yeye ananipenda na mimi nampenda na tumekwisha wahi kufanya mapenzi mara kadhaa. Yeye ameahidi kuwa atanioa. Sisi ni Waislamu, je ni sawa tunachokifanya kama sio sawa tufanyeje?"

Dinah anasema:Inasemekana na kuaminika kuwa Kibaiolojia na Kiuumbaji ( Mungu alivyotuumba ) mtu na ndugu yake hawawezi kutamaniana, ndugu kwa maana ya kuwa mmechangia damu ya mzazi mmoja. Lakini ndugu wengine kama Binamu, wapwa n.k. wanaweza kutamaniana na hata kupendana kwa vile hawachangii damu moja bali wazazi wao ndio wanaochangia damu.

Pia inasemekana watoto waliochangia sehemu moja ya damu (kama wewe na kaka yako wakambo) wakitamaniana ina maana kuwa uwezekano mmoja wenu sio toto halisi (Kibaolojia) wa baba. Yaani huenda wewe baba yako ni mwingine na sio huyo unaeamini kuwa ndio baba yako au kama wewe ni mtoto wa huyo Baba basi kuna uwezekano kuwa huyo kaka yako sio mtoto wa kweli wa Mzee wenu (mama zenu ndio wanajua ukweli halisi ktk hili au mfanye vipimo vya DNA kujua ukweli).

Kwenye jamii yeyote ile Duniani bila kujali Imani zao za kidini mtu na kaka yake waliochangia damu hawaruhusiwi kuwa wapenzi achilia mbali kufunga ndoa na kuzaa, kwa baadhi ya nchi za Ulaya ndugu kupendana ni kosa la jinai.

Kama hisia za mapenzi ni kali sana miongoni mwenu (which sio kawaida kwa ndugu) basi ni wazi kuwa ninyi sio ndugu na hivyo mnapaswa kuanza mikakati ya kutafuta ukweli kuhusu baba yenu na njia pekee ni either kuongea na mama zenu ili kuwapa ukweli halisi au kufanya DNA test.

Namna ya kupata ukweli:
Msikurupukie mama zenu na ku-demand bali mnahitaji kuwa na mipango nakujua namna za kupata ukweli bila wao kujua kama mmekwisha wahi kungonoana, mana'ke wakijua tayari mnamahusiano mtarushiwa shutuma na mtashindwa kujitete na wao kina mama watakuwa saved kutokana na "kutokujua baba yako au baba wa kaka yako".

Wewe na yeye kwa nyakati tofauti na kila mtu kivyake zungumzeni wazazi wenu wa kike......mwambie "mama mimi nahisi kama vile huyu sio baba yangu! Sina mapenzi wala hisia za baba na mtoto, unadhani kuna uwezekano kuwa huyu sio baba yangu?"......atakupa jibu, hakikisha majibu yake sio ya kusita na wala haonyeshi mshituko pia ukali lakini kama atashituka, kuwa mkali na kusita ujue kuna walakini.

Mwambie kwa kusisitiza kuwa " nataka kujua ukweli kwanini napata hisia hizi, hivyo nitaenda kufanya vipimo vya DNA ili nijue kama kweli huyu ni baba yangu"......mpe muda!

Sisemi kuwa huo ndio ukweli kuwa huyo Mzee sio baba yenu halisi bali kuna uwezekano mkubwa sana kuwa ninyi wawili sio ndugu! Nadhani mmoja wenu huyo sio baba yake mzazi bali ni baba mlezi (alisingiziwa au mama alikuwa hana uhakika na aliyem-mimba).

Kumbuka kuna asilimia kubwa ya akina baba ndani na nje ya ndoa nchini Tanzania wanalea au walilea watoto ambao sio wao. Ili kujua ukweli, ni mama pekee anatakiwa kutoka msafi au kufanya vipimo vya DNA.

Vinginevyo Ni mwiko kuwa na uhusiano wa kimapenzi na mtu yeyote ambae mmechangia damu. Toka kwenye uhusiano huo mara moja na usirudie tena.

Kila la kheri!

Sunday

Mikono mikubwa kuliko mwili....nitapendeza gauni la Harusi?







"Pole kwa kwa ngumu dada Dinah.
Mimi ni mwanamke mwenye umri wa miaka 24 tatizo nililonalo ni kwamba, mikono yangu ni minene kuliko mwili.

Nina umbo zuri, sura nzuri lakini mikono imezidi. Nahofia siku ya harusi yangu sintapendeza, kwa kawaida huwa sivai nguo za mikono mifupi au midogo. Nimekaribia kufunga ndoa na wasi wais wangu ni mikono, je kuna namna yeyote ya kuipunguza au hata kama kuna dawa yoyote unayoijua ya kupaka naomba unisaidie au kama kuna mazoezi yoyote ya kupunguza mikono. Mpenzi wangu huwa ananiambia huna mikono minene basi mimi sipendi, wakati najua ni minene"



Dinah anasema: Hey mtarajiwa, hongera sana na kila la kheri ktk maandalizi ya kufunga ndoa. Hakika suala la kutafuta na kupata gauni litakalokupendeza kutokana na umbile lako sio kazi rahisi, hata hivyo shukrani kwa wabunifu wa mitindo yanguo za kufungia ndoa kwani wanabuni kutokana na maumbile ya watu.



Ukubwa wa mikono itakuwa ni sehemu ya umbile lako na hivyo sio rahisi kuifanya iwe midogo au miembamba, pamoja nakusema hivyo kuna aina ya mazoezi ya kuifanya mikono yako kuwa "firm" na hivyo kuonekana minene lakini haijajitokeza kwa nyuma au kwa chini (kama mbawa), tafadhali kama utakuwa tayari mimi kukuelekeza namna ya kuzoezika basi usisite kuniandikia.



Vinginevyo mimi nakushauri uchague Gauni ambalo litaficha mikono yako (angalia picha hapo juu), usifuate trend kwamba kila mtu anavaa gauni bila mikono basi na wewe utake hivyo (mara nyingi huwa too common) na badala yake nenda kwa a classic one lakini inayoendana na umbile lako.


Kila la kheri na furahia siku yako ya ndoa.

Tuesday

Sitaki kumpotezea muda na nimekuwa honest,lakini hanielewi-Ushauri

s"Dada Dinah, ni mara yangu ya kwanza kukuandikia lakini nimekuwa nafuatilia sasa blog yako hii na kwa kweli ni kitu ambacho tunakihitaji sana kwani inasaidia sana kufumbua matatizo mbalimbali ya kimapenzi.

Sasa mimi nina mpenzi wangu ambaye tumekuwa mbali kwa muda wa miaka mitano hivi, kutokana na mimi kuwa nje ya nchi. Katika kipindi chote hiki tumekuwa katika mawasiliano ya mara kwa mara ambayo kwa kweli yamesaidia kuweka live penzi letu.

Sasa kwa jinsi mambo yalivyo ukiwa nje ya nchi ni kwamba mambo yanaweza kuwa unpredictable sana, kwani kutokana na mambo yanavyokwenda sioni kama nitaweza kurudi nyumbani hivi karibuni, kwa kuzingatia hilo na pia kwa kuzingatia kwamba umri unakimbia sana mimi nina miaka 31 na mpenzi wangu ana miaka 30 nikaona kuwa itabidi kuchukua maamuzi mazito.

Kwahivyo nikamwambia mpenzi kuwa mimi naona kuwa ni vizuri kama kila mmoja wetu akaamua kumove on ikitokea kuwa atapata wa kumfaa ili isije ikafika kesho na kesho kutwa tukaza kupeana lawama kutokana na ukweli kuwa labda nikarudi nyumbani tukakuta kuwa hatuwezi kuishi pamoja sababu labda wote wawili tumebadilika sana kwani tumekuwa mbali mbali kwa muda wote huu kufikiria kuwa tungeishi pamoja.


Nilipomueleza hivyo mwenzangu aliumia sana na ikawa akinitupia lawama mimi kuwa eti labda nimepata mwingine na ndio maana naamua kumtosa, lakini kwa ukweli ni kuwa mimi nilikuwa naangalia picha nzima kwamba tusiwe tunapotezeana wakati kwani umri wetu ndio unakimbia.

Kwa jinsi mwenzangu alivyo react ni kwamba hakubaliani na hilo na kwakweli ameumia sana kitu kilichonifanya nijidoubt labda uaamuzi niliochukua si sahihi kwani imefikia mahali inaniumiza kichwa sana. Ukweli ni kuwa I do care for her lakini inabidi mara nyingine uangalie jinsi hali halisi inavyokwenda katika maisha.

Sijui wewe na wadau wengine mnaonaje kuhusu swala hili, naomba msaada na mawazo yenu wote. Ahsante sana na samahani kwa mail ndefu kama hii, tuendelee kuelimishana katika swala zima la mahusiano"

Dinah anasema:Asante kwa kuniandikia, nadhani kosa ulilofanya hapa ni kufanya uamuzi ulioegemea upande mmoja tu (upande wako peke yako) bila kumuhusisha yeye (mpenzi wako), umefanya uamuzi kisha ukampa matokea....yaani hamkuzungumza na wote wawili kukubaliana kumaliza uhusiano au kutafuta namna nyingine ili uhusiano wenu uendelee.

Mwanamke yeyote mwenye mwanaume Ulaya anatarajia Big, sasa unapomuibukia na kumaliza uhusiano ktk mtindo huu, kidogo inakuwa ngumu kuamini, kuelewa na kukubali.

Kumbuka mko kwenye uhusiano na kama walivyogusia baadhi ya wachangiaji, inawezekana katolea nje wanaume wengine wengi tu kwa ajili yako kwa vile aliamini kuwa siku moja mtakuja kuishi pamoja.

Mimi nakushauri, uzungumze nae na umpe picha kamili ya maisha ya huko uliko. Kwasababu, watu wengi hapa nyumbani hawajui ni kiasi gani maisha yanaweza kuwa magumu huko Ughaibuni (ugumu interms of kutoruhusiwa kutoka nje mpaka wakurudishie kitabu chako, unaweza ukasubiri milele*).

Ukiweka wazi ni nini hasa kinakuzuia wewe kusafiri au hata kurudi nyumbani kwa sasa na hujui lini utaweza kufanya hivyo, akikuelewa ndio uanze kuzungumzia suala la uhusiano wenu. Hakikisha unampa nafasi yeye kukuambia msimamo wake na nini hasa anataka out of uhusiano wenu....msikilize kwa makini. Kisha mpe maelezo kutokana na matarajio yake au atakayo out of uhusiano huo.

Weka kila kitu wazi, kama kuna uwezekano wa yeye kukufuata uko nini afanye na kama hakuna mwambie kwa uwazi kabisa kwanini haiwezekani, kwa sababu kibongobongo wapenzi hutegemea sana kupandishwa majuu lakini hawajui urahisi na ugumu wake.....sasa mpe hali halisi.

Hakuna uwezekano wa kukufuata na huna mpango wa kurudi Bongo sasa:
Mwambie hali halisi kuwa, umri aliofikia wanawake wengi hupenda kuanza kujiandaa na ndoa, kuanza familia n.k. na wewe ungependa kufanya hivyo lakini unasikitika kuwa hutoweza kutimizia hayo kutokana na umbali na mambo yanavyokuendea huko uliko. Muombe radhi kwa kumpotezea muda kwani mipango haikuwa kama ulivyotarajia.

Akikubaliana na wewe, ahidi kuendeleza urafiki na wasiliana nae kila upatapo muda. Akiendelea kutokukuelewa na kukutupia lawama then punguza mawasiliano kama sio kuyakata kabisa.

Kila la kheri!

Monday

Anataka nifanye Masters pia niwe msiri-Ushauri

"Mpendwa dada Dinah. Mimi ni mwanamke wa miaka 23 naishi jijini DSM. Nimekuwa nikifuatilia na kusoma mambo mbalimbali na ushauri wako na comments za washirika tofautitofauti. Nimeona bora nije na hii yangu ambayo kwa ukweli inanichanganya kichwa.

Ninae boyfriend kwa hapa nitamwita X mwenye miaka 26, nimekutana nae chuoni mwaka 2006 nikiwa naingia mwaka wa kwanza na hadi sasa tumeshadumu miaka 3. Tulikuwa darasa moja huko chuoni ila yeye kwa sasa anaendelea na Masters ambapo kwa mimi plan ni next year ndiyo niisome hiyo masters kwani sikupenda kuunganisha.

Mwanzo alipoanza kunidate alikuwa mtu mzuri sana, muda wote alikuwa karibu na mimi na tulipoanza mahusiano mambo yalibadilika kidogo japo aliniambia kuwa yeye ni busy person. Tulikuwa tunaonana kwake siku za weekend tu tena mchana. Siku za kawaida na hata kama ni darasan ni salaam tu basi then kila mtu na muda wake.

Nilipomuuliza alinijibu kuwa yeye ni mtu anaependa privancy hasa kwenye mambo yake ya binafsi kama mahusiano. Tuliendelea hivyo japokuwa alinitambulisha kwa baadhi ya marafiki zake wa chuoni na hata wa kazini kwake akiwemo Boss wake. Kitu ambacho kilinishangaza katika usiri wake ambao ulikuwa ni chuoni tu, kwani tukishatoka chuoni alijitahidi kuwa close na mimi.

Mara moja moja tulipokuwa darasani alikuwa anakuja kukaa na mimi na mda mwingine hapana, japokuwa darasa zima lilikuwa likikujua kuwa tunadate na walikuwa wanatushangaa tunavyoact kama hatujuani.


Hapo ndipo mambo mengine yakaanza, akaniambia anataka watu wachanganyikiwe kwamba wasiwe na uhakika kama tunadate kweli au la. Akawa akiulizwa "mkewako mzima?" anawajibu "sina mke mimi" na baada a hapo anawaacha kwenye mataa na kuondoka.


Kitu kingine ambacho kiliniuma sana ni kuwa hata kwenye party za chuo kama za darasa ambazo ni za usiku alikuwa haongozani na mimi, bali na marafiki zake 3 wa kiume na msichana mmoja. Ndani ya party anakaa na hao watu ila mda mwingi anatoka nje na kurudi


Wakati party inaendelea msg zake kwangu haziishi kutumwa kuwa nisijali nivumilie na niact kiutu uzima. Ukicheza mziki na mkaka anakuja kukutoa na kuniambia nijiandae tunarudi nyumbani. Kwa maana hiyo party ndio inaishia hapo.


Siku zilienda mara nyingine alikuwa na mikutano ya kikazi mpaka saa sita za usiku ndio anaweza kuniambia anatoka kikaoni, nilikuwa najiuliza ni kazi gani usiku? Nijuacho mimi ni kuwa anafanya kazi kwenye makampuni 2 ambayo kote kuwili alinipeleka.

Hatimae nikaja kusikia tetesi kwa watu wengi wa darasani kuwa X anafanya kazi ya upelelezi, tena na hivi alikuwa anasafiri sana kwenda nchi tofauti na hamna anayemuaga zaidi ya mimi tu basi mi ndio nikawa nasumbuliwa "vipi mumeo kaenda kufanya upelelezi?" na maswalimengine mengi.

Siku moja nikamuuliza, akaniambia "kazi zangu zote mbili unazijua haya ya upelelezi sijawahi kukuambia na wala siyajui ndio mana nikakwambia watu wambea sana wanaongea mno, wewe nisikilize mimi na si wao".

Kwa kweli haya yote yalinisumbua sana kichwa changu na mara kwa mara niliongea nae ila jibu lake ni kuwa eti nahitaji kumwelewa na tupeleke mahusiano kiutu uzima na si kitoto. Basi kwa vile nilimpenda nikaka kimya.

Ilimradi mapenzi niliyapata, nikiumwa yupo,nikiwa na shida ananisaidia, akiwa less busy naenda kwake na hata nikitaka kulala huko yeye sawa tu, pia yeye alikuwa anakuja kunitembelea nilikokuwa naishi na wakati mwingine analala. Marafiki zangu walimjua na aliwajua vizuri japo alikuwa ananiambia nisiongee nao kila kitu kuhusu mapenzi yetu kwani hataki umbea.


Siku moja nikamuuliza hivi una mpango gani na mimi wa mbeleni? akanijibu "nataka usome hadi masters mana kamwe sitaoa mwanamke asie na masters" na akaniambia kwa yeye ana plan ya kumaliza masters na kuendelea kusoma na ana mpango wa kuoa mwaka 2015 ila kwa sasa nijue tu kuwa sisi ni wapenzi mungu akipenda basi tutafika mbali.


Ila akaniambia ukitaka tuwe wapenzi zaidi inabidi ujifunze kuwa privancy person hiyo ndiyo sheria yangu,ukianza kuongeaongea sana mambo yetu na mengineyo tutaishia hapo.

Kwa saa tupo mbalimbali na huwa nafunga safari kumfuata chuoni na ninakaa nae siku tatu au mbili kisha narudi kazini. Mambo si rahisi kwa huu umbali ila najitahidi kumtembelea na hata mapenzi ya simu yanachukua nafasi kubwa zaidi kama nikiwa nimekosa kisingizio cha kuomba ruhusa kazini, maana kazi nazo si kila mara uombe ruhusa.

Basi mara nyingi mimi ndio nikawa nampigia simu kila siku jioni, inaweza kupita hata siku mbili kama sijapiga basi tena. Siku moja nikamwambia sipendi hiyo tabia kwa nini hapigi simu?akanijibu kuwa huwa anasahau kuweka credit basi nikamwambia "kama hunipendi uniambie kuliko kunipotezea muda".Tukaagana.

Kesho yake yeye akapiga simu ila sikuchangamka kama siku nyingine.Siku iliyofuata usiku akanitext "hujambo umeshindaje?usiku mwema", mimi nikamwendea hewani tukaongea vizuri tu mwisho nikamwambia "i love u",akanijibu "me too".


Nikamuliza "una uhakika?" akanijibu "sina budi ya kurudia kitu kwa miaka yote 3 tuliyokuwa pamoja hujakua tu?kua basi tuwe na mapenzi ya kiutu uzima" na akaniambia "kusema i love u kila siku haimaanishi ndo unapendwa naweza nikakuambia hivyo na bado nisimaanishi. Kwa kweli sikumwelewa, akaniambia mwisho tukagombana bure na yeye hataki hilo litokee bora tulale,basi tukaagana.

Huyu ndie mwanaume ambae ninae dada Dinah kwa miaka 3 sijapata jibu ni mwanaume wa aina gani huyu na kama kweli ananipenda na ana mpango na mimi. TAFADHALI NAOMBA UNISAIDIE KWA USHAURI NIFANYAJE.
Na washiriki wengine nahitaji maoni yenu tafadhali.

Ni mimi dada F"

Dinah anasema: Dada F, shukrani kwa ushirikiano na uvumilivu wako as nachukua muda mrefu kujibu kutokana na uwingi wa majukumu mengine ya kikazi na maisha. Nimefurahishwa na maelezo yako ya kina na kumfanya yeyote kuelewa picha nzima bila kuwa na maswali.....hongera kwa hilo.

Suala la Ushushushu sio muhimu sana as long as wewe unajua kazini kwake, na akitoweka siku zote huwa anakuambia kuwa anasafiri hivyo huitaji kujipa hofu na mimi binafsi sina uzoefu na masuala ya wapelelezi. Nitakupa maelezo kuhusiana na issue ya uhusiano wenu wa kimapenzi ambayo naamini yatafungua macho yako kwa kiasi fulani.

Mimi binafsi ninaamini kuwa sisi wanadamu lazima tupitie hatua sita za maisha ya kimapenzi na mahusinao. Ila tatizo la wengi huwa tunakurupuka na kutaka/kutegemea jambo fulani kabla ya wakati.

-Uzoefu/kutambua ujinsia wako kwanza (hapa unakuwa kwenye umri mdogo so jaribu kufurahia maisha na kupata uzoefu zaidi wa kimaisha na wakti huohuo unazingatia masomo/kazi, sio lazima ungonoke).

Pili:-Unapenda na ku-commit (hapa utakuwa mkubwa kiumri na umetulia kiakili).

Tatu:-Chumbia na Ndoa (kuwa na uhakika wa kuishi na huyo mmoja tu maisha yako yote).

Nne:-Familia(Uamuzi au kukubaliana kuzaa).

Tano:-Kufanya uhusiano wenu wa kimapenzi na ndoa kusimama Imara.

Mf-ninyi wawili bado wadogo, mnapendana sana tu (kutokana na maelezo yako bado mko hatua ya kwanza)...ila wewe unategea au unataka zaidi ya unachokipata kutoka kwenye uhusiano wenu, huenda ungependa siku moja ufunge ndoa na huyo mpenzi X hasa ukizingatia kuwa owte mnafanya kazi na mmeshakuwa pamoja kwa muda mrefu. Lakini yeye hayuko tayari kufanya hivyo kwani anachotaka yeye kwa sasa ni kurekebisha maisha yake na wakati huohuo kuongeza Elimu.

Kitu ambacho sisi wanawake huwa tunakikosea ni kuharakisha mambo, labda kutokana na " msukumo" kutoka kwa jamii inayotuzunguuka kuwa ukiwa kwenye uhusiano baada ya muda fulani basi lazima uolewe au hata kuzaa.

Lakini katika hali halisi tunatakiwa kujua nini hasa wapenzi wetu (wanaume) wanakitaka kutoka kwenye uhusiano husika na je ni hatua gani hivi sasa uhusiano wetu upo? kabla hatujaanza kurukia/harakisha hatua inayofuata kama sio kuziruka zote na kwenda hatua ya mwisho.

Sasa ninachokiona hapa ni wewe kutaka commitment na kuhakikishiwa nafasi yako, wakati yeye bado anajaribu ku-have fun. Kweli anakupenda lakini hiyo hamfanyi yeye kuwa na uhakika kwa 100% kuwa wewe ndio mke wake.......anahitaji muda.

Kwenye suala la wewe kuwa msiri, mimi sioni tatizo kwani naelewa kuwa kuna baadhi ya watu wanaaibu sana yanapokuja masuala yao ya kimapenzi.....yaani hawapendi kujionyesha wa watu wengine kuwa wao ni wapenzi. Sasa kwa vile mpenzi X ni mmoja kati ya hao watu ni vema wewe kuheshimu takwa lake hilo.

Nini cha kufanya: Jiulize nini hasa unataka out of the relationship with X, mawasiliano yenu yako bomba kama wapenzi, unapewa mapenzi yake yote, mnaonana kila mnapohitajiana, anakujali, kila mtu yuko huru kwenda kwa mwenzie, mnaoneana wivu (which ni dalili nzuri) X anaonyesha ameji-commit kwako.......nini kingine unataka?

Kama ni ndoa ndio utakayo ni wazi hutompata kwa sasa kwani yeye anadhania takuwa tayari akiwa na miaka 31 (2015) which wanaume wengi ndio hupenda kujipangia hivyo kuanzia 31-36 wawe wamefunga ndoa, huamini by that time wanakuwa somehow wamekamilisha "mipango" yao kimaisha.

Hivyo hapo kuna maamuzi 3 tofauti;
(1)-Endela na uhusiano huku ukimsubiri tumia muda huo kwenda kufanya hiyo Master yako au

(2)- Endela na uhusiano, furahia maisha yako na chukulia kila siku kama inavyokujia (mkifunga ndoa poa isipotokea ndoa poa).

(3)-Toka kwenye uhusiano ili kupata utakacho kwenye uhusiano mwingine (kama unaharaka sana na maisha ya wawili).

Nakutakia kila la kheri.

Thursday

Mume ni mwema lakini hataki kazi wala hatoi Unyumba-Ushauri!

"Habari mpenzi,
nimevutiwa sana na blog yako, kwa kweli ina story za kusikitisha na ukweli kuhusu maisha. Mimi ni mwanamke niliyeolewa naona nina matatizo ambayo nimekaa nayo kimya kwa muda mrefu bila kujua nimwombe nani msaada.

Nimejaribu kuongea na Mama yangu mzazi lakini nimepewa ushauri wa kuvumilia, nimejaribu kuongea na Mama mkwe wangu ushauri ni huo huo sasa sijui labda nipate ushauri toka kwa watu wengine sasa.

Story inaanza hivi; tumependana na mume wangu bila kuwa na kasoro, baada ya mwaka wa uchumba tukafunga ndoa Kanisani. Baadaya ya kuoana tu mungu akanijalia ujauzito nikazaa mtoto wa kike mwaka uliofuata, basi ilikuwa ni furaha tu.

Baada ya miaka miwili nikajaliwa mtoto wa pili wa kiume sasa, basi nayo ilikuwa heri. Sikuwahi kugombana na mume wangu wala kukosana kwa aina yoyote, maisha yalikuwa ni matamu haswa kwani ni msikivu kweli kweli. Chochote ukimwambia anafanya hata kupika hata kufua nguo zangu za ndani.....duuuh hadi wengine walikuwa wananiambia nimempa limbwata.


Basi baada ya kuzaa mtoto wa pili nikashangaa mwenzangu hana time na mimi si kwamba halali nyumbani laah anakula na tunalala wote, watoto anaangalia na matumizi yote anatoa lakini penzi kitandani hakuna, basi ikapita miezi kadhaa bahati mbaya kazi yake aliyokuwa anafanya ikaharibika.

Akawa hana kazi lakini hatukukata tamaa ya maisha tulianza kutafuta tukisaidiana maisha na tulikuwa na miradi yetu midogomidogo ilikuwa inatusaidia. Lakini bado pamoja na yeye kushinda nyumbani tu labda akihangaika kuomba kazi huku na huku mimi nikirudi kutoka kazi hana time ya kufanya mapenzi ila kuongea tunaongea vizuri na hatugombani hata siku moja.

Nikapata woga wa kumuuliza mwenzangu kama ana tatizo maana naona jogoo huwa anasimama kama kawa hasa wakati wa asubuhi lakini hajawahi kunitamkia ananitamani au kunitaka kuwa anataka tufanye mapenzi, mhhhh nikaja nikaona hii kweli kali.


Miezi sita ikapita hatujagusana ila tunakaa vizuri sana kula wote, kulala wote na kushare vitu vingine tu kama kutoka out n.k. Sasa limekuja suala la kazi, kila ninapomuombea kazi kwa watu na kuitwa kwa ajili ya mahojiano hapati. Juzijuzi nilimuombea kazi mahali nifanyapo kazi na akaitwa lakini akakataa kwenda akadai yeye hawezi kwenda kufanya kazi mahali ambapo mimi nafanya kazi.

Hapo mhh sikumuelewa nikajaribu kumueleza vizuri kuwa hatutakuwa ofisi moja ila jengo moja hakukubaliana na mimi . Sasa dada dinah, mtu kama huyo unamfanyaje?

Mwaka mzima umekaa ukishikilia familia na ukisali Mungu ampe kazi, ukimvumilia na kumpenda ingawa hakupi unyumba bila sababu maalum, sasa na kazi hataki kufanya anachagua badala ya kufanya yoyote for the sake of the kids, je nifanyeje? tafadhali naomba msaada hapo kama ni wewe ungefanyaje?-Magy"

Dinah anasema: Mpendwa Magy asante sana kwa ushirikiano na uvumilivu as nimechelewa kujibu, lakini natumaini maoni na ushauri wa wasomaji umesaidia wakati unasubiri kutoka kwangu.

Nitakupa maelezo na ushauri katika sehemu mbili, moja kuhusu kutokufanya Mapenzi na pili suala la yeye kugoma kufanya kazi sehemu moja na wewe.

Kwanini hafanyi mapenzi na wewe lakini anasimamisha!!
Kuna sababu nyingi ambazo zinaweza kumfanya mwanume apoteze hamu ya kufanya mapenzi, kumbuka hamu na nguvu ni vitu viwili tofauti tena kwa wanaume kusimamisha pia kuko kwa aina mbili kusimamisha kwa vile wako tayari kungonoka na kusimamisha kwa vile ni sehemu ya ujinsia wao kwa maana kuwa kuna aina mbili za mwanaume kusimamisha:- (1)-kutokana na mawazo ya kingono (2)-kutokana na kuwa stimulated kwa kushikwa au kuguswa na kitu kama vile shuka, chupi, mkono n.k


Mfano ni mwanaume kusimamisha asubuhi, ile haina maana kuwa anataka ngono japokuwa inaweza kufanyika ngono kama akikuona ukopembeni na ukamvutia then akapata mawazo ya kingono on top of msimao ambao ulisababishwa na mzunguuko wa damu wakati kalala......


Hivyo basi yeye kutokufanya ngono na wewe haina maana anamatatizo ya nguvu za kiume. Nadhani tatizo kubwa linaweza kuwa moja kati ya haya :-

Mosi, Hofu ya kuachishwa kazi (katika hali halisi unapewa taarifa mapema kuwa utapunguzwa/fukuzwa kazi), sasa ile hofu ilisababisha msongamano wa mawazo (stress) na hivyo kupoteza hamu ya kungonoka.

Pili, mabadiliko ya mwili wako baada ya kujifungua mtoto wa pili (Chunguza hapa), na jitahidi kurekebisha.....jipende na hakikisha unavutia zaidi, fanya mazoezi ya misuli kuanzia ya ulimi mpaka ya Uke.

Tatu, hapati attention ya kutosha kutoka kwako kama mpenzi labda kwa vile wewe huna muda as una-deal na watoto bila ushirikiano wake kutokana na stress.......(peleka watoto kwa bibi yako au kwa ndugu yeyote mnae muamini) mara moja kila baada ya wiki 2.

Nne, Yeye kuwa muanzilishi wa kutaka/kufanya ngono kitu ambacho huwa kina udhi/kera na kuchosha na hivyo mtu anaamua kutokufanya kabisa......(Kuanzia sasa usisubiri yeye aanze, anzisha wewe). Hii itamfanya ajiamini na kuhisi kuwa anavutia pia anafurahi kuona kuwa mkewe sio Gogo, pia mara moja kwa wiki mfanyie mumeo jambo litakalo mfurahisha, pagawisha na kumridhisha kingono).

Nini chakufanya kwa ujumla: Mumeo anahitaji ushirikiano mkubwa kutoka kwako, ushirikiano huo sio wa kumtafutia kazi au kumsukuma atafute kazi (kitu ambacho anakijua wazi yeye kama mwanaume) kwani kwa kufanya hivyo unamfanya apoteze ile hali ya kujiamini kama mwanaume na pia unasumbua Ego yake kwani yeye kama mwanaume kamili najaua kuwa ni wajibu wake kuwa provider kwa familia yake, sasa unapo-take over nakujaribu kumtafutia kazi inaweza kuchangia kumfanya azidi kuhisi kuwa yeye ni useless.

Natambua unafanya hivyo katika harakati za kumpa ushirikiano, kuonyesha uko pale kwa ajili yake na tayari kumsaidia mumeo kwa faida ya watoto wenu, yote haya wewe kama mwanamke ungefurahi kuyapokea kutoka kwa mumeo kama ungepoteza kazi......lakini sio mwanaume. Mwanaume anapewa ushirikiano kivingine.

Huyu mumeo anamengi sana akilini mwake hivyo hakuna nafasi kabisa ya kuweka mawazo ya kingono (kama unawajua wanaume vema utanielewa ninachokisema hapa). Sasa ili kumsaidia arudie hali yake ya kawaida unatakiwa kufanya kazi ya ziada......


Mf: kuongea nae vizuri, kumshauri/kumpa matumaini, kumshirikisha kwenye maamuzi (japokuwa hawezi kuchangia kwa sasa), kuonyesha unampenda na kuvutiwa nae zaidi sasa hana kazi kuliko alivyokuwa na kazi(anzisha ngono, cheza na mwili wake na kuwa mtendaji mkuu), kuonyesha kuwa unaweza kusimama wewe kama mama bila kuonyesha stress au kuzidia (anajua kuwa unazidiwa lakini sio lazima umuonyeshe au kulalamika kwani itamuangamiza kiakili), usionyeshe kukerwa na yeye kutokuwa na kazi, kumpa matumaini kuwa kazi ni kazi tu as long as senti zinaingia n.k.


Kwa kufanya hayo niliyogusia na mengine ambayo baadhi ya wachangiaji wameshauri hakika mumeo atakuwa comfortable na mawazo yanaweza kupungua na hivyo kuanza kupata nafasi ya kufikiria ngono akilini mwake na hata kuanza kuona kuwa unamvutia tena.


Kufanya nae kazi Jongo moja: Ukiachilia mbali matatizo mengine yanayoweza kujitokeza kwa kufanya kazi sehemu moja (unless otherwise Taaluma zenu zinafanana na mnawekeana mipaka vinginevyo sio nzuri/afya kwa uhusiano wenu wa kimapenzi.


Kama nilivyogusia hapo juu, kwa baadhi ya wanaume kusaidiwa na wake zao ktk mtindo wa ku-take over kama ulivyofanya wewe huwapotezea hali ya kujiamini na kuhisi kuwa "wameolewa" achilia mbali mwnaume huyo aende kufanya kazi Jengo moja na mkewe ambae ndio actually kamtafutia hiyo kazi na usikute kazi yenyewe ni ya kiwango kidogo kuliko mkewe........hapo haji mtu!

Uless kuna matatizo mengine kwenye ndoa yenu ambayo hukutaka kuyaweka hapa, lakini tatizo lako sio kubwa kiasi cha kutishia uhai wa ndoa yenu. Hakikisha unafanyia kazi ushuri uliopewa na nina kuhakikishia kila kitu kitakuwa safii na Unyumba utaupata lakini kwa sasa jitahidi ku-initiate ngono kila unapojisikiwa kutaka kufanya hivyo, usisubiri yeye akufuate au akuombe!....ni mumeo huyo hivyo unamfanya atake kufanya kwa kutumia uanamke wako au yeye anakufanya wewe utake kufanya kwa kutumia uanaume wake.

Kama ingekuwa mimi ningefanyaje: Mimi kama Dinah, kwanza kabisa ningekubali mabadiliko na kujaribu kubadili mtindo wa maisha yetu kama familia ili ku-save. Ningeonyesha mapenzi kwa mume wangu kuliko mwanzo, ningehakikisha namuondolea stress kwa kutumia mbinu mbali mabali za kumkanda na kuongea nae bila kulalamika wala kuonyesha kuwa nimezidiwa na majukumu.


Kila wakati ningemfanya aone kuwa niko nae sambamba ktk hardship na sio yake peke yake bali yetu sote. Ningempa support na kumshauri kuhusiana na kazi/biashara (sio lazima kuajiriwa) kwa kumpa mawasiliano au kumuonyesha sites/magazeti lakini sio kwa ku-take over na kuingilia Ego yake.


Ningemshawishi kwa maneno na vitendo kuwa kufanya mapenzi kunasaidia kuondoa au kupunguza stress, nikifanikiwa basi nitahakikisha namfanyia mambo hadimu ambayo najua yanaondoa stress hata kwa masaa mawili (which itamfanya anitake kingono mara kwa mara).

Kwa vile naelewa kuwa kipindi hiki cha hardship kinamfanya mume wangu kushindwa kutumia akili yake kufikiria/taka ngono na kusimamisha, basi ningetumia njia ya kumsisimua kwa kufanyia kazi mwili wake na kuhakikisha akili yake ime-relax kabla sijaanza zoezi zila la kumsisimua kingono.

Nakutakia kila lililojema!

Pages