Thursday

Kwanini "romance" hufa baada ya kipindi fulani ktk ndoa?


Samahani mi nataka nitoke nje ya mada,naomba ruksa yako dinah na wadau kwa jumla. Mimi leo na kitu kimoja nataka nimuulize dada yetu,kama vp na washika dau karibuni,kwa lengo la mahala hapa ni kuelimishana na kuwekana sawa kuhusu maisha yetu ya kila siku.

Issu dada iko hivi,mwanamume anapompenda na kumtaka mwanamke huenda kwa nguvu zote na baada ya makubaliano mahusiano hukua na mapenzi hushika hatamu, zawadi kibao,out usiseme kila siku,ahadi za kila aina ili mradi tu kuonyesha ni jinsi gani mwanamme amempenda huyo mwanamke.

Mwisho wa siku wanavalishana pete za uchumba na hayawi hayawi mwisho yanakua wanaoana. Kama mungu anapenda huwa na familia kwa maana ya kuzaa watoto, hudumu ktk mapenzi kama yale ya mwanzo kwa muda na baadae taratibu huanza kuporomoka.

Suala la mume kutoka na mkewe kwa ajili ya matembezi na burudani huwa halipo tena,badala yake ni kuona mume anakwenda na wanawake wengine kwenye kumbi za starehe.

Hapo mimi ndipo nakuwa sipati jibu,najiuliza kwani yale mapenzi ya awali yamekwenda wapi?na ni nini kinasababisha na kupelekea hali hii kutokea? Usinitupe kapuni dinah naomba mtizamo wako(wenu )wadau.

Jawabu: Nashukuru kwa ushirikiano wako. Hili swala la kifo cha "romance" baada ya muda fulani wa uhusiano hasa baada ya watoto kuzaliwa husababishwa na mambo mbali mbali ambayo nitajitahidi kuyaelezea kwa kifupi na kukusaidia ama kuepuka au kuyaangalia kwa karibu ili "romance" indelee kuwepo siku hadi siku mpaka mwisho wenu.
Kujisahau kwa wapenzi mara tu baada ya kufahamu kuwa wamefunga ndoa na hakuna sababu ya kujaribu au kujitahidi kum-wow ili akuone kuwa wewe ni mpenzi bora kuliko wengine aliowahikuwa nao (hapa ukishangaa unamkosa mpenzi na ndio maana unajituma) hilo moja.
Pili, ni ile hali au kasumba ya mwanamke kujitoa/badili kutoka mpenzi na kuwa mama/mke mara tu baada ya kujifungua watoto fulani. Hii inatokana na shindikizo kubwa kutoka kwa jamii inayotuzunguka(yaani ukizaa mtoto wewe ni mtu tofauti, yaani hujichanganyi na kuongea na watu ambao hawajazaa hata kama ni umri mmoja), kitu kinachomfanya mwanamke ahisikuwa amekuwa mama na hivyo hapaswi kuwa kama alivyokuwa kabla hajazaa.
Tatu ni mwanamke kwa namna moja au nyingine ajione mpweke kutokana na kutopata usaidizi/ushirikiano kutoka kwa mume wake hivyo "comfort" aipatayo ni ile ya mtoto/watoto wake.
Mama hukaza zaidi ile-bond kati yake na mtoto hali inayomfanya awe karibu zaidi na mtoto/watoto na kumsahau mume/mpenzi (atamuona kuwa ni baba watoto na sio Mpenzi kama ambavyo yeye mume anamuona). Hili likitokea mume ataisi kuwa hapendwi/hajaliwi tena na hivyokwenda tafuta penzi nje.
Nne ni kupoteza ile hali ya kujiamini na hivyo anaamua kutojijali na kujipenda na hivyo anakuwa havutii tena kama mwanamke na anabaki kuwa hana habari na muonekano wake, kitu kitakachomfanya mpenzi/mume kuona mkewe havutii (kuona aibu kutoka nae) hapa kama ni mtu wa mikutano-mikutano, kuoka kwa kinywaji nakadhalika hakika ataibua kimwana mwingine anaevutia kwa "kampani" mkutanoni.
Yote kwa yote, ni vema jamii (hasa wanaume)watambue kuwa mwanamke anapokuwa mjamzito na kujifungua huwa anakabiliana na mabadiliko makubwa sana kiakili, kimwili na kiroho.
Mwanamke huitaji ushirikiano wa hali ya juu kutoka kwa mume wake, anahitaji kusaidiwa, anahitaji kukubushwa, anahitaji kupewa matumaini n.k ili arudi kama alivyokuwa awali.
Wanawake unafofautiana na kila uzazi unatofautina hivyo kila mtu na kila uzazi huwa na mabadiliko yake kivyake hivyo yanapaswa kushughulikiwa kitofauti ili mwanamke kurudia hali yake ya awali na hivyo kubaki mpenzi na sio mama Ashura!
Asante.

Saturday

Tangu nimeachana na wangu, sitaki Demu-Ushauri!

"Eti dinah wewe ni profesheno kwenye mambo ya LOVE???mi namatatizo kichizi ya kisaikolojia ,Tangu niachane na chick wangu feb 2007 mpaka leo sitaki demu na wala sijisikii kabisa kuwa na uhusiano vipi ninamatatizo gani???

Aalafu kwa nini simpati demu mwenye sifa ninazotaka?? best wishes"

Jawabu:Shukurani kwa kukubali ku-share tatizo lako hapa kwa faida ya watu wengine wenye tatizo kama lako au ambao watakumbana nalo hapo baadae.

Sidhani kama unatatizo, hiyo ni hali ya kwaida inatupata watu wote tunapoachana na wapenzi wetu ambao tulikuwa tukiwapenda sana au tumekuwa nao kwa muda mrefu. Inakuchukua muda mrefu kabla hujaondokana na hilo yaani kwa kifupi ni kuwa alikuumiza sana au uliumia sana kumaliza/ua uhusiano hali inayokufanya upoteze imani na wanawake kwa ujumla ukihofia wao kuwa kama yeye at the end. Japo kuwa sio kweli kwani wanawake tunatofautiana. Hivyo all u need is time to heal jeraha lako.


Sio rahisi kupata mwanamke mwenye sifa zote uzitakazo kwani huyo atakuwa "perfect" na "there is no such thing" hapa duniani, kwani hata Malaika hawako hivyo. Ukiwa tayari kupenda tena au kuwa kwenye uhusiano basi fuata moyo wako lakini suisahau akili yako.

Jiwekee sifa utakazo kwa mwanamke lakini ikiwa utamdondokea mmoja ambae ana-tick box 5 muhimu out of 10 mchukue nyingine utarekebisha ukiwa ndani ya uhisiano. Kitu muhimu cha kuzingatia sio sifa alizonazo bali hisia zako za kimapenzi juu yake na je utakuwa mtu mwenye furaha ukiwa nae karibu?

Sasa take your time to get over kilichotokea alafu ukiwa sawa/tayari mambo yatakuwa bomba kuliko ilivyo kuwa na EX, kumbuka kwenda taratibu, kuwa wazi na boresha mawasiliano ili ikusaidie kumfahamu mwenzio zaidi.

I hope nimekujibu vema na umenielewa.

Nitumie nini kuondoa michirizi ya Uzazi?

"Dinah dada nakukubali! Mimi nina shida naomba ushauri ikibidi kutatua tatizo langu. Mimi nina tatizo la michirizi iliyotokana na uzazi nina kitoto kimoja ila mwili wangu matakoni na hipsi kama kenge.

Sasa nilikuwa nauliza je hii michirizi itatoka? na ninunue kitu gani itoke maana nimeshakwenda maduka mbali mbali (jina kapuni) hamna kitu.Naomba ushauri wako/wenu nifanyeje ndoa yangu ipo mashakani? Nisaidie naomba saaaaana?"

Jawabu: Asante sana kwa kunikubali na pia kwa kuchangia swali lako mahali hapa. Nasikitika kusema kuwa michirizi (stretch marks) haitoki bali inapungua tu kwa kutumia bidhaa zilizotengenezwa maalumu kabisa kwa ajili hiyo.

Pamoja na kusema hivyo inasemekana kuwa kuna dawa za kuzuia na kuondioa kabisa alama hizo juu ya ngozi ambazo baadhi ya wanaume huziita "mistari ya utamu" lakini dawa hizo hazijathibitishwa kisayansi kitu kitakachonifanya niseme kuwa hakuna dawa ya uhakika ya kuzuia na kuondoa kabisha michirizi.

Michirizi hiyo hujitokeza kwa mwanamke yeyote (wengi wetu tunayo) sehemu mbali mbali za miili yetu kama vile kwenye matiti, matakoni, sehemu ya kwapa/chini ya mkono, mapajani, sehemu ya nyumba ya miguu na kinachosababisha hili kutokea na kutanuka kwa ngozi yako sehemu husika (mahali ilipo).

Michirizi hii pia huwapata zaidi mama wajawazito au wazazi na hilo hutokana na kutanuka kwa ngozi yako sehemu hiyo ya tumbo na meneo ya karibu kama vile kiunoni, n.k.

Natambua hofu ya ndoa yako kuwa hatarini kwa sababu ya mabadiliko ya mwili wako baada ya kujifungua kwa vile mistari hiyo (mabadiliko ya mwili wako) inaweza au inakusababishia ujisikie huvutii tena kama zamani au "ukajishitukia" kuwa mumeo havutiwi na wewe tena hali itakayokufanya umkimbie au uanze "vijitabia vya ajabu" kamavile kufanya mapenzi gizani, kwenda kubadilishai nguo mahali ambapo yeye hayupo, kulala na nguo zako, kufanya mapenzi ukiwa "full dressed" nakadhalika yaani kwa kifupi inakupunguzia ile hali ya kujiamini ukiwa mtupu(uchi) mbele ya mpenzi wako.

Mimi nauhakika kabisa kuwa mumeo hatosumbuliwa au kuwa "put off" na hizo alama ikiwa wewe bado ni yuleyule na unafanya mambo yako fulani kama awalia au ukaongeza ujuzi kidogo ili kufurahia zaidi.

Unachotakiwa kufanya ni kujirudishia tena ile hali ya kujiamini kwa kufanya mazoezi ili ku-shape up, kula na kunywa vizuri ili ngozi inawiri, badili mtindo wa mavazi......kwamba, kama ulikuwa mtu wa khanga mbili sasa pia moja, kama ulikuwa mtu wa khanga moja sasa piga gauni bila khanga au sketi na blauzi nakama ulikuwa mtu wa magauni basi sasa wewe anza kupiga suruali na kaptura, hali kadhalika unaweza kupia mini.


Yaani badili muonekano wako kwa ujumla na usijisahau ukawa mama nanihii, bali kuwa wewe na wakati huohuo mama wa mtoto wako sio MAMA FULANI( hili linaathiri wanawake kisaikolojia na kimwili pia).

Ikiwa unashindwa kuwa huru mbele ya mume wako hata baada ya kufanya nilivyokuambia basi ni wakati wa kuifanyia kazi Nguzo ya tano ya uhusiano bora ambayo ni mawasiliano, weka wazi hofu yako. Muulize mabadiliko gani anayaona juu ya ngozi yako tangu umejifungua? Akisema machirizi muulize je michirizi yako inamkera?

Asipo gusia michirizi kama sehemu ya mabadiliko juu ya ngozi yako basi ujue jamaa hana habari na anakupenda pia anafurahia kama ilivyokuwa awali.

Kila la kheri mdada!

Wednesday

Ushuhuda wa Mama Rahma! Unakmkumbuka?

"Its me mama Rahma,napenda kumshukuru Mungu kwa afya njema,nilijaribu kwenda kwa Daktari mwingine maana Daktari wangu niliona hayuko intrested kunisaidia nimeamua kutoa Kitanzi sasa nina afya njema najiamini na najitahidi kufanya mazoezi ya misuli ya uke na natarajia kutumia Vinega.

Ushauri wangu kwa wengine ni kuwa waangalifu tunapofanya kitu ambacho Mungu hapendi that's why mtu unapata matatizoada Dinah, sikufichi mapenzi ya mume wangu yalipungua but now he loves me.

Kumbe ile birth control ilinifanya ngozi ya uke iwe laini kiasi kwamba ilipoteza ladha(hali yake ya kawaida) lakini sasa nafurahia tendo kama mwanzo, ty Dada dinah"

Dinah-Mungu ashukuriwe kwa yote, Hongera sana kwa kurudia hali yako ya awali na kufurahia uumbaji wake Mungu. Pia nashukuru kwa kurudi tena nakushuhuida mafanikio yako, karibu tena siku nyingine.

Tuesday

Ningependa kufunga Ndoa lakini anaharaka sana-Ushauri!

"Mambo vipi Dinah, Sorry nimejaribu kutafuta e-mail yako bila mafanikio lakini katika kuangalia huku na kule finaly nikaipata.

Mimi nina swali moja ambalo linanitatiza sana kuhusu mpenzi wangu ambae ninataka kumuoa lakini nasita kutokana na vitabia vyake. Hivi wewe binafsi unamchukuliaje mwanamke ambaye yuko very anxious for marriage kiasi kwamba akiona rafiki yake anaolewa basi ujue siku hiyo na wewe utakuwa na kesi.

Pia anakuwa na hasira zisizo na msingi. Yaani kila mara unapokuwa nae basi hakosi kukasirika(sio muda wote) but still anainsist marriage. Mimi natishika na matendo yake kiasi kwamba kila mara najiuliza...hivi nikioa si ndio itakuwa balaa kama kipindi hiki cha mapenzi bila ndoa hakuna kuelewana? bcoz naona hata adabu amepunguza but still anasema ananipenda sana.

In short she is soo aggressive and wants to control me such that anataka anachotaka yeye ndio kifanyike lakini mimi nikitaka jambo hakosi kuweka pingamizi. Nimemwambia nataka kumuoa mwakani (2009) lakini yeye hataki alikuwa anataka this year.

Zamani alikuwa mpole sana kwangu kiasi nikimwambia kitu ananisikiliza lakini siku hizi akinisikiliza basi ni kwa muda. Pia anatabia ya ku-revenge eg. Kama nilisave namba ya mwanamke kwenye simu yangu ambaye yeye hamjui basi ujue na yeye ipo siku atasave namba ya mwanaume na kumchokoza ili ampigie mida ya usiku mimi nikiwa nae, na nikiuliza basi najibiwa "IS MY FRIEND, I THOUGHT IT WILL BE OK WITH YOU BCOZ NA WEWE UNACHUKUA NAMBA ZA WANAWAKE"Naomba ushauri wako Dinah. David"

Jawabu:Asante David, mimi binafsi nitamchukulia mwanamke huyo hajiamini, hajakomaa/kua kiakili na anawivu wa kizembe.

Unajua, Mtu yeyote ambae hajiamini mara nyingi huvaa "wasifu" wa mtu mwingine pale anapoanza uhusiano mpya, kama ujuavyo siku hizi kabla hatujajikita kwenye uhusiano wa kimapenzi huwa tunaanza na kaurafiki fulani hivi kabla ya "date" ili kufahamiana vema sio?, sasa wakati unauliza maswali labda na kuelezea nini unapenda/taka kutoka kwa mwenza, huyo "date" anachukua yale unayopenda zaidi na kujitahidi kuwa hivyo hasa kama anahisi kakupenda au kunakitu anadhani atapata kutoka kwako.

Mfano unaposema "sipendi mwanamke/mwanume mlalamishi, mkaidi, mvivu n,k....napenda kuwa na mwanamke/mwanaume mwelevu, mpole, msafi nje na ndani, asie penda ulevi" n.k basi ujue huyo mwanamke/mwanaume atafanya vile upendavyo ili asikukose.

Mara nyingi hii sehemu ndogo ya jamii hufanikiwa kuwa na huo uhusiano lakini baada ya muda fulani mhusika (mwanamke/mwanaume) anachoka kule ku-"pretend/act" au kuvaa wasifu ambao sio yeye na badala yake anakuwa yeye kama yeye na hapo ndio utakapoanza kuona mabadiliko makubwa sana kama ulivyoshuhuida kwa mpenzi wako huyu.

Kuna uwezekano mkubwa kuwa mpenzi wako anataka kufunga ndoa kwa vile rafiki zake tayari wamefungandoa yaani anafuata mkumbo kwa kujiona kuwa anaachwa nyuma, mtu kama huyo hafai kwani baadae atakusumbua sana, pili huenda anahisi kapoteza sana muda kuwa na wewe na hivyo anahofia ukimuacha hatopata tena mtu wa kuji-"commite" kwake kama wewe (ndio maana nikasema hajiamini) hivyo anatumia nguvu (ukali, ujeuri, kisirani, visasi n.k.)

Mimi naamini kuwa swala la ndoa ni maamuzi ya watu wawili hasa ukizingatia maisha tunayoendsha hivi sasa, ofcoz kimila na kidesturi mwanaume ndio anachumbia lakini baada ya hapo ninyi wote wawili ndio mnapanga,shirikiana na kuelewana lini mfunge ndoa na hiyo inategemeana na aina ya maisha mnayoishi/endesha na aina ya ndoa (sherehe) mnayoitaka.

Kuna wale wanaopenda "simple" lakini bab-Kubwa (hapa unahitaji kipato cha maana na miezi kama mitatu mpaka sita hivi kujiandaa) alafu kuna wale wanapenda kubwa na bab-Kubwa(utahitaji zaidi ya miezi sita inategemeana na kipato), wengine hutaka ndogo na ya kawaida (hii inachukua siku saba tu kitu na box).

David ulivyotoa maelezo yako hakuna mahali umegusia wewe kumpenda yeye, sito kulaumu kama ile hali ya kumpenda inapungua kutokana na matendo yake ambayo ni ya aibu sana kama mwanamke (mambo ya usawa hayo), hata hivyo kitendo chako cha kutunza namba za wanawake wengine bila kumshirikisha yeye sio kitu kizuri (wewe hapo ulikosea pia).

Lakini kama unampenda na nia yako ni kufunga nae ndoa basi nakushauri mfanye maswasiliano....zungumzeni na mwambie wazi kuwa anahitaji kubadili mwenendo wake vinginevyo uhusiano wenu utakuwa hadithi, mwambie wazi tu kuwa unampenda lakini vitendo vyake vinakukatisha tamaa na unahofia kuwa ukifunga nae ndoa bado utakwenda kutafuta amani nje....Mikwara yenye ukweli ndani yake huwa inafanya kazi.

Kisha msikilizie, kama anakupenda kwa dhati ataomba radhi na kujitahidi kubadili tabia yake mbaya, maana ya kuomba radhi ni kubadilika, kama hubadili matendo basi hakuna sababu ya kuomba msamaha.

Kila la kheri!

Thursday

Kutoa mimba ni sahihi?-Ushauri!

Bonyeza hapa kuona Picha inaonyesha kiumbe (mtoto) kilichotolewa, kilikuwa na umri wa wiki nane tumboni ambazo ni sawa na miezi miwili.
"Natoka nje ya mada kidogo naomba mitizamo yenu Dinah na wadau wengine katika suala la abortion/utoaji mimba je ni sahihi kwa wapenzi kutoa mimba baada ya kuingia bila kutarajiwa?kama hawajajiandaa na pia kuwa tayari kwa mtoto kifedha na hata kindoa-TEITEI".

Mtazamio wangu:Teitei nashukuru sana, hili swala bado ni nyeti sana kulizungumzia japo kuwa linafanyika sana ktk jamii nyingi hapa Duniani ikiwa ni pamoja na hapa nyumbani Bongo, ni kama ilivyo kwenye kuzungumzia ngono kwa uwazi/adharani.

Maelezo nitakayoyatoa ni ya wazi pia ni hali halisi, lakini kusema nitakacho sema sio kwamba naunga mkono swala zima la utoaji mimba. Mimi binafsi naamini kuwa utumiaji wa madawa ya kuzia mimba hasa ile "Morning after" ni utoaji mimba, lakini hili watu hawalioni au kulizingatia mpaka mimba ijengeke ndio wanaona "big issue", lakini katika hali halisi kuzuia mimba (unaruhusu iingie lakini isijengeke) na kutoa mimba (unaruhusu iingie na ijengeke kisha unatoa) kwangu mimi ni mauaji ya viumbe visivyo na hatia.


Kwa mujibu wa Imani zetu za kidini utoaji mimba sio sahihi na huesabika kama mauaji ambayo ni dhambi, lakini wakati huohuo mama anaweza kulazimika kutoa mimba kutokana na matatizo mbali mbali moja likiwa ni matatizo ya kiafya ambapo Daktari hupendekeza hilo, hili hufanyika kwa kufuata hatua za kisheria na vilevile kuzingatia maamuzi ya mama na baba wa mtoto, kwamba wako radhi mtoto afe mama abaki au wote wawe hatarini kufa ikiwa mimba haitotolewa.


Swala lingine ambalo ni la pili linaweza kufanya/sababisha pea/wenza watake kutoa mimba ni kutokuwa tayari kwa hilo kama ulivyosema hapo juu, kwamba mimba imeingia kwa bahati mbaya bila ninyi wawili kupanga, kwamba hamko tayari kuwa baba/mama au mnajua wazi kuwa hamtomudu malezi ya mtoto atakae zaliwa.

Natambua unataka kuuliza "kama ulijua hukua tayari kwanini sasa ulingonoka?" hebu tuwe wazi na nafsi zetu, ni wangapi hufikiria mimba au kuzaa pale tunapokwenda kufanya mpenzi au pale tunapovutiwa na wapenzi wetu? Mimba ni matokeo ya kungonoana na ni wajibu wetu (wake kwa waume kuwa waangalifu) lakini wakati huohuo tutambue kuwa kuna bahati mbaya ambayo husababishwa na watu kutojua kikamilifu kile wanachokifanya (ngono) kutokana na swala zima la ngono kuwa siri miongoni mwetu.

Tatu ni mwanamke "kumimbwa" na mwanaume aliyem-baka, kutokana na tendo lenyewe ambalo ni la kikatili na limefanywa na mtu ambae humjui, humfanya mwanamke kuathilika kisaikolojia na kiakili nakutaka kutokuwa na kumbu-kumbu ya mkatili huyo na njia pekee ya kuondokana na hilo ni kutozaa mtoto wake (m-bakaji) ambae akizaliwa ofcoz itakuwa kumbukumbu mbaya na ya maumivu makuu.

Kwa nchi zilizoendelea kunavituo vyakuwalea/angalia wanawake waliobakwa namimba zao na mara tu watakapijifungua watotow aliozaliwa huchukuliwa na kutafutiwa familia amabzo zinahitaji watoto, na kipindi chote hicho mwanamke huyo huenda kozi kali ya ushauri nasaha mapaka atakapo jifungua.

Kutokana na mfumo wa maisha tunayoishi sasa swala zima la utoaji mimba (kwa nchi zilizoendelea) limeachwa kwa mwanamke husika, kuwa yeye ndiye mwenye uamuzi wa nini kifanyike juu ya mwili wake na kabla hilo halijafanyika ni lazima mama huyo apatiwe ukweli wa athali/madhara na hatari za kutoa mimba, anatakiwa kufanya hivyo wakati gani, aina gani ya utoaji wa mimba anaitaka kisha wanakupa muda ukafikirie kabla hujaendelea na utoaji mimba.

Ukirudi baada ya muda waliokupa na ukawa na msimamo uleule wa kuendelea na uamuzi wako basi unapewa ushauri nasaha na unaelezwa tena nini kitafanyika, athari na matuzo baada ya huduma kukalimika alafu ndio wanaendelea....kutokana na maelezo yangu utatambua kuwa wenzetu wamelikubali na kuliweka wazi ili kuepusha utoaji mimba ambao sio wa kitaalam.

Asante.

Tuesday

Nimefiwa na baba, Mpenzi kaniacha pia-Ushauri!

"Mimi ni kijana mwenye umri wa miaka thelathini na tano niimeachana na mpenzi wangu karibu miezi miwili sasa, kilichopelekea tuachane ni mimi kutokuwa karibu nae pia kutofanya nae mapenzi kwa vile sikuwa najisikia kufanya hivyo na nilikuwa naona kama Dunia imenilemea kutokana na kuondokewa na Baba yangu Mzazi. Tatizo nililonalo hivi sasa ni kwamba bado nampenda na ninataka turudiane nifanye nini?"

Jawabu: Pole sana kaka yangu ka hilo lililopelekea wewe kuniandikia mimi. Nimefurahishwa na uwazi wako ktk hili. Niliposoma maelezo yako nikahisi kwamba ulikuwa unasumbuliwa na mawazo mengi kutokana na kuondokewa na mmoja kati ya watu muhimu sana ktk maisha yako, hali hiyo ilipelekea wewe kuwa na aina yua "Depression".

Sasa kabla sijakushauri nini cha kufanya ningependa ufahamu kuwa hali hiyo sasa imekwisha yaani umebadilika au niseme umepona na umekuwa wewe kama hapo awali na ndio maana swala la kutaka kutafuta suluhisho au njia ya kurudioana na mpenzi wako limekujia na umetambua kuwa wewe ndio ulikuwa sababu ya yeye kuondoka!

Ni wazi kuwa mpenzi wako hakujua kuwa wewe ulikuwa unasumbuliwa na "Depression" na kwa mawazo ya mwanamke wa kawaida ndani ya Bongo alihisi labda humpendi tena na ndio maana akaamua kujitoa kitu ambacho ktk hali halisi hakupaswa kukifanya na badala yake alipaswa kuwa mvumilivu, kukupa ushirikiano kwenye "nyanja" nyingine na sio ile ya kimwili tu.

Unajua watu tunapokea na kuchukulia matatizo kitofauti sana, kuna wale ambao wakikumbwa na tatizo kama lako huwa haliwapigi/shitua kama ilivyokutokea wewe, na hiyo inategemea zaidi na ukaribu/uhusiano kati yako na mpendwa wako ambae ni Mzee (baba'ko).

Ushauri wangu kwa kuanzia ni kujenga hali ya kujiamini tena kwa kuanza kujichanganya na marafiki (outing), jiunge "gym" au anza kufanya mazoezi ya viungo mepesi (kukimbia, push-ups n.k), soma sana vitabu vya "challenges", angalia funny movies (usiguse zinazohusu mapenzi au huzuni) au jishughulishe na mambo ya shamba, bustani hata kama ni ya maua, usafi n.k (kuwa-busy) na kamwe usipende kukaa peke yako ama kumtembelea mama yako kila wakati (atakurudisha nyuma yaani utakuwa na uzuni zaidi).

Ikitokea uko peke yako basi jitahidi kusikiliza muziki uliochangamka Mf ule wa Mr blue na Chillah wa "Nipo, nilikuwepo na nitakuwepo" au Fiesta wa Ray C au hata ule wa Ngoma zetu sijui kaimba nani au za Mr Ebbo kwanizitakuchekesha kimtindo......those kind of songs na kwa sauti ya juu (usisumbue majirani lakini).

Wakati unaendelea na utaratibu huo anza kwa kuwasiliana na mpenzi wako mara moja/mbili kwa siku (ni salamu najisni gani unamkosa na kumpenda, tafadhali usithubutu ukagusia tatizo lako) Kisha mambo yakiwa "swafi"(baada ya wiki mbili mpaka tatu utakuwa umerudisha kujiamini kwako) na hapo ongeza "gia".

Pendekeza kuwa ungependa kuonana nae kwa ajili ya kinywaji mahala fulani (sio nyumbani kwako/kwake) ikiwa ni mpenzi wa maua basi si vibaya "kuibuka" na "bunch" la maua tafadhali yasiwe ya "plastic" (wanawake wengi tunapenda maua lakini si wote tunathamini maua), ili ushinde basi nunua hereni nzuri kwa ajili yake.

Natambua kuwa mkikutana utapenda kumwambia "nakupenda sana na ninataka turudiane na tupendane kama zamani" ni maneno mazuri lakini sio mwanzo mzuri, nakushauri uzungumzie mambo ya kawaida tu kama siasa, movie, muziki, jamii n.k, mtegee aanze yeye.

Mpenzi wako akijaribu kugusia mambo fulani mliyokuwa mnafanya pamoja kama wapenzi, hapo ujue umeshinda na ndio atakuwa amefungua mlango wa wewe kuomba msamaha na kumueleza ni nini haswa kilikuwa kinakufanya uwe mbali na yeye hasa pale kunako uhondo (kitandani)!

Nakutakia kila la kheri na mafanikio katika safari hiyo ya kurudiana na Mpenzi wako umpendae

Pages