Tuesday

Ningependa kufunga Ndoa lakini anaharaka sana-Ushauri!

"Mambo vipi Dinah, Sorry nimejaribu kutafuta e-mail yako bila mafanikio lakini katika kuangalia huku na kule finaly nikaipata.

Mimi nina swali moja ambalo linanitatiza sana kuhusu mpenzi wangu ambae ninataka kumuoa lakini nasita kutokana na vitabia vyake. Hivi wewe binafsi unamchukuliaje mwanamke ambaye yuko very anxious for marriage kiasi kwamba akiona rafiki yake anaolewa basi ujue siku hiyo na wewe utakuwa na kesi.

Pia anakuwa na hasira zisizo na msingi. Yaani kila mara unapokuwa nae basi hakosi kukasirika(sio muda wote) but still anainsist marriage. Mimi natishika na matendo yake kiasi kwamba kila mara najiuliza...hivi nikioa si ndio itakuwa balaa kama kipindi hiki cha mapenzi bila ndoa hakuna kuelewana? bcoz naona hata adabu amepunguza but still anasema ananipenda sana.

In short she is soo aggressive and wants to control me such that anataka anachotaka yeye ndio kifanyike lakini mimi nikitaka jambo hakosi kuweka pingamizi. Nimemwambia nataka kumuoa mwakani (2009) lakini yeye hataki alikuwa anataka this year.

Zamani alikuwa mpole sana kwangu kiasi nikimwambia kitu ananisikiliza lakini siku hizi akinisikiliza basi ni kwa muda. Pia anatabia ya ku-revenge eg. Kama nilisave namba ya mwanamke kwenye simu yangu ambaye yeye hamjui basi ujue na yeye ipo siku atasave namba ya mwanaume na kumchokoza ili ampigie mida ya usiku mimi nikiwa nae, na nikiuliza basi najibiwa "IS MY FRIEND, I THOUGHT IT WILL BE OK WITH YOU BCOZ NA WEWE UNACHUKUA NAMBA ZA WANAWAKE"Naomba ushauri wako Dinah. David"

Jawabu:Asante David, mimi binafsi nitamchukulia mwanamke huyo hajiamini, hajakomaa/kua kiakili na anawivu wa kizembe.

Unajua, Mtu yeyote ambae hajiamini mara nyingi huvaa "wasifu" wa mtu mwingine pale anapoanza uhusiano mpya, kama ujuavyo siku hizi kabla hatujajikita kwenye uhusiano wa kimapenzi huwa tunaanza na kaurafiki fulani hivi kabla ya "date" ili kufahamiana vema sio?, sasa wakati unauliza maswali labda na kuelezea nini unapenda/taka kutoka kwa mwenza, huyo "date" anachukua yale unayopenda zaidi na kujitahidi kuwa hivyo hasa kama anahisi kakupenda au kunakitu anadhani atapata kutoka kwako.

Mfano unaposema "sipendi mwanamke/mwanume mlalamishi, mkaidi, mvivu n,k....napenda kuwa na mwanamke/mwanaume mwelevu, mpole, msafi nje na ndani, asie penda ulevi" n.k basi ujue huyo mwanamke/mwanaume atafanya vile upendavyo ili asikukose.

Mara nyingi hii sehemu ndogo ya jamii hufanikiwa kuwa na huo uhusiano lakini baada ya muda fulani mhusika (mwanamke/mwanaume) anachoka kule ku-"pretend/act" au kuvaa wasifu ambao sio yeye na badala yake anakuwa yeye kama yeye na hapo ndio utakapoanza kuona mabadiliko makubwa sana kama ulivyoshuhuida kwa mpenzi wako huyu.

Kuna uwezekano mkubwa kuwa mpenzi wako anataka kufunga ndoa kwa vile rafiki zake tayari wamefungandoa yaani anafuata mkumbo kwa kujiona kuwa anaachwa nyuma, mtu kama huyo hafai kwani baadae atakusumbua sana, pili huenda anahisi kapoteza sana muda kuwa na wewe na hivyo anahofia ukimuacha hatopata tena mtu wa kuji-"commite" kwake kama wewe (ndio maana nikasema hajiamini) hivyo anatumia nguvu (ukali, ujeuri, kisirani, visasi n.k.)

Mimi naamini kuwa swala la ndoa ni maamuzi ya watu wawili hasa ukizingatia maisha tunayoendsha hivi sasa, ofcoz kimila na kidesturi mwanaume ndio anachumbia lakini baada ya hapo ninyi wote wawili ndio mnapanga,shirikiana na kuelewana lini mfunge ndoa na hiyo inategemeana na aina ya maisha mnayoishi/endesha na aina ya ndoa (sherehe) mnayoitaka.

Kuna wale wanaopenda "simple" lakini bab-Kubwa (hapa unahitaji kipato cha maana na miezi kama mitatu mpaka sita hivi kujiandaa) alafu kuna wale wanapenda kubwa na bab-Kubwa(utahitaji zaidi ya miezi sita inategemeana na kipato), wengine hutaka ndogo na ya kawaida (hii inachukua siku saba tu kitu na box).

David ulivyotoa maelezo yako hakuna mahali umegusia wewe kumpenda yeye, sito kulaumu kama ile hali ya kumpenda inapungua kutokana na matendo yake ambayo ni ya aibu sana kama mwanamke (mambo ya usawa hayo), hata hivyo kitendo chako cha kutunza namba za wanawake wengine bila kumshirikisha yeye sio kitu kizuri (wewe hapo ulikosea pia).

Lakini kama unampenda na nia yako ni kufunga nae ndoa basi nakushauri mfanye maswasiliano....zungumzeni na mwambie wazi kuwa anahitaji kubadili mwenendo wake vinginevyo uhusiano wenu utakuwa hadithi, mwambie wazi tu kuwa unampenda lakini vitendo vyake vinakukatisha tamaa na unahofia kuwa ukifunga nae ndoa bado utakwenda kutafuta amani nje....Mikwara yenye ukweli ndani yake huwa inafanya kazi.

Kisha msikilizie, kama anakupenda kwa dhati ataomba radhi na kujitahidi kubadili tabia yake mbaya, maana ya kuomba radhi ni kubadilika, kama hubadili matendo basi hakuna sababu ya kuomba msamaha.

Kila la kheri!

No comments:

Pages