Thursday

Kwanini "romance" hufa baada ya kipindi fulani ktk ndoa?


Samahani mi nataka nitoke nje ya mada,naomba ruksa yako dinah na wadau kwa jumla. Mimi leo na kitu kimoja nataka nimuulize dada yetu,kama vp na washika dau karibuni,kwa lengo la mahala hapa ni kuelimishana na kuwekana sawa kuhusu maisha yetu ya kila siku.

Issu dada iko hivi,mwanamume anapompenda na kumtaka mwanamke huenda kwa nguvu zote na baada ya makubaliano mahusiano hukua na mapenzi hushika hatamu, zawadi kibao,out usiseme kila siku,ahadi za kila aina ili mradi tu kuonyesha ni jinsi gani mwanamme amempenda huyo mwanamke.

Mwisho wa siku wanavalishana pete za uchumba na hayawi hayawi mwisho yanakua wanaoana. Kama mungu anapenda huwa na familia kwa maana ya kuzaa watoto, hudumu ktk mapenzi kama yale ya mwanzo kwa muda na baadae taratibu huanza kuporomoka.

Suala la mume kutoka na mkewe kwa ajili ya matembezi na burudani huwa halipo tena,badala yake ni kuona mume anakwenda na wanawake wengine kwenye kumbi za starehe.

Hapo mimi ndipo nakuwa sipati jibu,najiuliza kwani yale mapenzi ya awali yamekwenda wapi?na ni nini kinasababisha na kupelekea hali hii kutokea? Usinitupe kapuni dinah naomba mtizamo wako(wenu )wadau.

Jawabu: Nashukuru kwa ushirikiano wako. Hili swala la kifo cha "romance" baada ya muda fulani wa uhusiano hasa baada ya watoto kuzaliwa husababishwa na mambo mbali mbali ambayo nitajitahidi kuyaelezea kwa kifupi na kukusaidia ama kuepuka au kuyaangalia kwa karibu ili "romance" indelee kuwepo siku hadi siku mpaka mwisho wenu.
Kujisahau kwa wapenzi mara tu baada ya kufahamu kuwa wamefunga ndoa na hakuna sababu ya kujaribu au kujitahidi kum-wow ili akuone kuwa wewe ni mpenzi bora kuliko wengine aliowahikuwa nao (hapa ukishangaa unamkosa mpenzi na ndio maana unajituma) hilo moja.
Pili, ni ile hali au kasumba ya mwanamke kujitoa/badili kutoka mpenzi na kuwa mama/mke mara tu baada ya kujifungua watoto fulani. Hii inatokana na shindikizo kubwa kutoka kwa jamii inayotuzunguka(yaani ukizaa mtoto wewe ni mtu tofauti, yaani hujichanganyi na kuongea na watu ambao hawajazaa hata kama ni umri mmoja), kitu kinachomfanya mwanamke ahisikuwa amekuwa mama na hivyo hapaswi kuwa kama alivyokuwa kabla hajazaa.
Tatu ni mwanamke kwa namna moja au nyingine ajione mpweke kutokana na kutopata usaidizi/ushirikiano kutoka kwa mume wake hivyo "comfort" aipatayo ni ile ya mtoto/watoto wake.
Mama hukaza zaidi ile-bond kati yake na mtoto hali inayomfanya awe karibu zaidi na mtoto/watoto na kumsahau mume/mpenzi (atamuona kuwa ni baba watoto na sio Mpenzi kama ambavyo yeye mume anamuona). Hili likitokea mume ataisi kuwa hapendwi/hajaliwi tena na hivyokwenda tafuta penzi nje.
Nne ni kupoteza ile hali ya kujiamini na hivyo anaamua kutojijali na kujipenda na hivyo anakuwa havutii tena kama mwanamke na anabaki kuwa hana habari na muonekano wake, kitu kitakachomfanya mpenzi/mume kuona mkewe havutii (kuona aibu kutoka nae) hapa kama ni mtu wa mikutano-mikutano, kuoka kwa kinywaji nakadhalika hakika ataibua kimwana mwingine anaevutia kwa "kampani" mkutanoni.
Yote kwa yote, ni vema jamii (hasa wanaume)watambue kuwa mwanamke anapokuwa mjamzito na kujifungua huwa anakabiliana na mabadiliko makubwa sana kiakili, kimwili na kiroho.
Mwanamke huitaji ushirikiano wa hali ya juu kutoka kwa mume wake, anahitaji kusaidiwa, anahitaji kukubushwa, anahitaji kupewa matumaini n.k ili arudi kama alivyokuwa awali.
Wanawake unafofautiana na kila uzazi unatofautina hivyo kila mtu na kila uzazi huwa na mabadiliko yake kivyake hivyo yanapaswa kushughulikiwa kitofauti ili mwanamke kurudia hali yake ya awali na hivyo kubaki mpenzi na sio mama Ashura!
Asante.

No comments:

Pages