Saturday

Nitumie nini kuondoa michirizi ya Uzazi?

"Dinah dada nakukubali! Mimi nina shida naomba ushauri ikibidi kutatua tatizo langu. Mimi nina tatizo la michirizi iliyotokana na uzazi nina kitoto kimoja ila mwili wangu matakoni na hipsi kama kenge.

Sasa nilikuwa nauliza je hii michirizi itatoka? na ninunue kitu gani itoke maana nimeshakwenda maduka mbali mbali (jina kapuni) hamna kitu.Naomba ushauri wako/wenu nifanyeje ndoa yangu ipo mashakani? Nisaidie naomba saaaaana?"

Jawabu: Asante sana kwa kunikubali na pia kwa kuchangia swali lako mahali hapa. Nasikitika kusema kuwa michirizi (stretch marks) haitoki bali inapungua tu kwa kutumia bidhaa zilizotengenezwa maalumu kabisa kwa ajili hiyo.

Pamoja na kusema hivyo inasemekana kuwa kuna dawa za kuzuia na kuondioa kabisa alama hizo juu ya ngozi ambazo baadhi ya wanaume huziita "mistari ya utamu" lakini dawa hizo hazijathibitishwa kisayansi kitu kitakachonifanya niseme kuwa hakuna dawa ya uhakika ya kuzuia na kuondoa kabisha michirizi.

Michirizi hiyo hujitokeza kwa mwanamke yeyote (wengi wetu tunayo) sehemu mbali mbali za miili yetu kama vile kwenye matiti, matakoni, sehemu ya kwapa/chini ya mkono, mapajani, sehemu ya nyumba ya miguu na kinachosababisha hili kutokea na kutanuka kwa ngozi yako sehemu husika (mahali ilipo).

Michirizi hii pia huwapata zaidi mama wajawazito au wazazi na hilo hutokana na kutanuka kwa ngozi yako sehemu hiyo ya tumbo na meneo ya karibu kama vile kiunoni, n.k.

Natambua hofu ya ndoa yako kuwa hatarini kwa sababu ya mabadiliko ya mwili wako baada ya kujifungua kwa vile mistari hiyo (mabadiliko ya mwili wako) inaweza au inakusababishia ujisikie huvutii tena kama zamani au "ukajishitukia" kuwa mumeo havutiwi na wewe tena hali itakayokufanya umkimbie au uanze "vijitabia vya ajabu" kamavile kufanya mapenzi gizani, kwenda kubadilishai nguo mahali ambapo yeye hayupo, kulala na nguo zako, kufanya mapenzi ukiwa "full dressed" nakadhalika yaani kwa kifupi inakupunguzia ile hali ya kujiamini ukiwa mtupu(uchi) mbele ya mpenzi wako.

Mimi nauhakika kabisa kuwa mumeo hatosumbuliwa au kuwa "put off" na hizo alama ikiwa wewe bado ni yuleyule na unafanya mambo yako fulani kama awalia au ukaongeza ujuzi kidogo ili kufurahia zaidi.

Unachotakiwa kufanya ni kujirudishia tena ile hali ya kujiamini kwa kufanya mazoezi ili ku-shape up, kula na kunywa vizuri ili ngozi inawiri, badili mtindo wa mavazi......kwamba, kama ulikuwa mtu wa khanga mbili sasa pia moja, kama ulikuwa mtu wa khanga moja sasa piga gauni bila khanga au sketi na blauzi nakama ulikuwa mtu wa magauni basi sasa wewe anza kupiga suruali na kaptura, hali kadhalika unaweza kupia mini.


Yaani badili muonekano wako kwa ujumla na usijisahau ukawa mama nanihii, bali kuwa wewe na wakati huohuo mama wa mtoto wako sio MAMA FULANI( hili linaathiri wanawake kisaikolojia na kimwili pia).

Ikiwa unashindwa kuwa huru mbele ya mume wako hata baada ya kufanya nilivyokuambia basi ni wakati wa kuifanyia kazi Nguzo ya tano ya uhusiano bora ambayo ni mawasiliano, weka wazi hofu yako. Muulize mabadiliko gani anayaona juu ya ngozi yako tangu umejifungua? Akisema machirizi muulize je michirizi yako inamkera?

Asipo gusia michirizi kama sehemu ya mabadiliko juu ya ngozi yako basi ujue jamaa hana habari na anakupenda pia anafurahia kama ilivyokuwa awali.

Kila la kheri mdada!

No comments:

Pages