Monday

Ni kweli Wanaume wanapenda "Saa sita" Kifuani?


Sina hakika ni kwanini wenzetu (wanaume) wanapenda Matiti wakati sisi (wanauwake) ndio tunaonyegeka ikiwa yatafanyiwa "kazi" vizuri na kwa utaalam. Ukiachilia mbali hilo, matiti hutufanya tuhisi kuwa ni "wanawake" pia ni Mwanzo mzuri wa maisha ya mtoto).

Nakumbuka mara ya kwanza kuvaa Sidiria ilikuwa 2003, sikuwa nahitaji lakini nilidhani kuwa kuvaa Sidilia ndio "uanamke", basi nikaenda kupima size ya Matiti ili kupata "Bra" itakayonitosha vema. Wahudumu wakanishangaa na kusema kuwa ninge-save pesa nyingi kwa kutovaa "Bra" kwani sihitaji, lakini kwa vile nilitaka kujihisi kuwa ni mwanamke nilisisitiza kupata "Bra" yangu ya kwanza....TMI i know, sorry hihihihi....


Katika hali halisi hakuna Mwanaume anaependa kukutana na mwanamke ambae matiti tayari yapo tumboni (inategemea na ukubwa), hiyo haimfanyi mwanaume huyo kuchukia matiti yaliyoanguka ila angependa yaanguke akiwa Mkewe na sababu  iwe ni kunyonyesha watoto wao.


Hebu badilishakibao wewe ndio uwe mwanaume etii....alafu unakutana na na titi zipo tumboni, hapo hajanyonyesha/Zaa, utakuwa hujui raha ya  matiti yaliyosimama na pengine siku moja ungependa kupata uzoefu huo....Hebu fikiri.


Kwa bahati mbaya wanawake wengi kwenye jamii rejea topic ya Jinsi ya kutunza, wengi hujiachia tu kipindi ambacho matiti hayo yanahitaji "support". Hakika Matiti kuanguka ni kutokana na kunyonyesha watoto wa Mumeo, lakini kumbuka kuwa sio Wanawake wote wenye matiti yaliyoanguka wamenyonyesha, Wamezaa, Wametoa mimba au wanawaume/wapenzi....kwamba matiti yao yalianguka kitambo kabla hawajanyonyesha kutokana na kutoyatunza vema.


Ikiwa mumeo alikukuta ukiwa na matiti Saa sita bila shaka ataendelea kuyapenda akijua kuwa wanae waliyatumia "early days of their lives", obviously atakuwa amekubali mabadiliko uyapatayo kutokana na Uzazi....lakini at least aliyakuta Wima na yeye ndio kachangia yatazame Chini (baada ya kunyonyesha watoto).


Ukweli wenye maumivu ni kuwa, Asilimia kubwa ya wanaume wangependa matiti ya wake zao au wapenzi wao yadondoke wakiwa nao na sio wayakute yakiwa hivyo (matiti yamedondoka). Hali inayofanya wengi wao kuzungumzia u-wima wa matiti na kucheka au kubatiza yale yaliyolala kuwa ni Malapa.


Mimi binafsi huwa sipendezwi na hilo na siku zote huwa nasema kabla hujamcheka mwanamke mwenye matiti yaliyolala hakikisha wanawake kwenye familia yako bado matiti yao yapo wima na muhimu kabisa ni je Matiti ya mama yako uliyonyonya bado yamesimama(saa sita)?


Ikiwa kwa bahati mbaya wewe ulichelewa ama ulikuwa hujui namna ya kutunza matiti wakati yananza kujitokeza hakikisha Wanao wa kike wanajua(wafundishe), pia hakikisha unayapa "support" yakutosha unapofanya Mazoezi, Unapo karibia hedhi, unapokuwa Hedhini, utakapo kuwa Mjamzito na wakati unanyonyesha.




Kizamani na Kisasa....Changanya ushinde!

Kwa kawaida Wanawake tunadondoka kimapenzi haraka zaidi kuliko wenzetu. Huenda Mwanaume akawa amevutiwa na Muonekano wako, Uzuri, Uwezo kiakili, Sauti, Utembeavyo n.k. Mkaanza au mkakubaliana kutoka kama wapenzi. Hiyo hamfanyi yeye kukupenda wewe!


Enzi za Bibi yangu ilikuwa ni kawaida kwa Binti kuolewa bila kumpenda Mwanaume, kwamba kila kitu kinatayarishwa na familia mbili na wewe kama Binti unaambiwa tu utaolewa na Bwana fulani Mtoto wa Familia/Ukoo fulani.

Kabla ya kuchumbiwa Binti unakuwa tayari umefundwa kuhusianana mambo mengi tu kuhusu Mapenzi, Ndoa, Uzazi na Mabadiliko yatakayoendelea kujitokeza kwenye maisha yenu kama Wazazi na Wapenzi.

Ikiwa kwa bahati nzuri unamfahamu “Mchumba” na pengine ulikuwa unapendezwa nae basi unahitaji kumfanya akupende(baada ya ndoa) na ikiwa bahati akakupenda ghafla basi unapaswa kumfanya akupende zaidi, yaani umkae moyoni na kichwani(akilini).

Kipindi hicho Wanaume wengi walikuwa wanafunga Ndoa ili kuendeleza Ukoo(kuzaa) na kujiwekea heshima kwenye Jamii sio kwa mapenzi kama ilivyo sasa kwa baadhi yetu. Wachache sana walifunga Ndoa kwa vile waliwapenda Wanawake waliochaguliwa.


Hii bado inaendelea hadi sasa kwa baadhi ya wanaume wa “kisasa” na Wasomi, kwamba “anatafuta” Mke ili amzalie watoto na kuwalea, ampikie na kufanya shughuli zote za ndani.

**Kutokana na “Maendeleo” au sijui ni mambo ya Usawa siku hizi nasikia kuna Wanawake wanafunga Ndoa kwa sababu nyingine na sio mapenzi (hii ni topic nyingine).....tumalizie hii kwanza.


Changamoto:
Kutoa changamoto ni tofauti kabisa na kutokuwa msikivu au kutokuwa na heshima kwake. Wanaume hawakuzaliwa wakiwa wanajua kila kitu na ndio maana tukaumbwa sisi kama wasaidizi wao, kwamba kuna wakati wanahitaji kuwekwa sawa kiakili, kiutendaji(kitandani included), Sio kila asemacho wewe ni "ndio Bwana" hata kwenye suala ambalo halihitaji "ndio".


Mapishi:
Ukiachilia mbali suala la Kuridhishana na kufurahisha Mwili, kujua kupika aina mbali mbali za vyakula ni muhimu pia. Unapofundwa unaambiwa “ kamwe usiruhusu Mpenzi wako kula chakula cha mwanamke mwingine hata kama dada ni dada yake.

Kwa kawaida Wanaume wengi husifia na kupenda mapishi ya mama zao, sasa hapa ndio muhimu kujenga uhusiano mzuri na Mama mkwe nakuhakikisha unajifunza ili ukampikie mwanae nyumbani kwako.


Usafi wa nguo:
Najua wanawake wengi wa “kisasa” wanapinga sana hili lakini sie tuliofundwa na wa kisasa tunachanganya yote ili “kushinda” hihihihi....Kamwe usivundike nguo mpaka anaishiwa ya kuvaa, ni vema kuhakikisha nguo ni safi na zimenyooshwa vyema.


Maendeleo:
Hata kama huna kipato sio mbaya kuchangia maendeleo kwa kutoa mawazo mazuri na endelevu, na hata kuchangia katika utafutaji wa “info” kuhusiana na mfano Ujenzi, upatikanaji wa Mbegu za mazao fulani au Bidhaa kwa ajili ya mradi fulani n.k.

Kujali:
Zamani hakukuwa na urahisi wa mawasiliano hivyo ilikuwa muhimu kumpokea mpenzi na kumpa pole, kumkumbatia anapofika nyumbani, unakaa nae na kuulizia hali yake na siku ilivyokwenda.

Siku hizi ni rahisi kimawasiliano hivyo basi sio mbaya kama utaulizia anavyoendelea huko aliko....ni mpenzi wako tayari hivyo huwezi kuonekana “needy” ikiwa uta-check anaendeleaje akiwa kwenye mishughuliko yake badala ya kusubiri yeye ndio akupigie au akutumie ujumbe.


Jipende Kimwili:
Enzi zile ilikuwa ni Usafi, valia Khanga Mbili na kujifukiza Udi....inategema na ufanyacho ili kujipenda kimwili(kuvaa vizuri, kunyoa vinyweleo, kufanya mazoezi, n.k) aili mradi tu kinakufanya ujisikie vizuri na kukuongezea hali ya kujiamini na kuwa tayari kwa lolote(namaanisha Tendo)....siol azimalitokee lakini pia sio mbaya kama ukiwa tayari wakati wote.


Tunza Haiba ya Uanamke wako:
Pamoja na usomi wako au kuishi kwako sana na Wazungu, usisahau kuwa wewe ni mwanamke wa Kiafrika kwenye maadili (inategemea na kabila) fulani ambayo hao wa “kisasa” hawana na hiyo inakufanya wewe uwe tofauti na wanawake wengine wengi Duniani.

Pamoja na kusema hivyo haina maana uvumilie unyanyaswaji kwa vile tu kikwenu kunyanyaswa ni sehemu ya Maadili, chukua maadili mazuri na yenye manufaa kwako na kwa mpenzi wako.


Jitegemee:
Hupaswi kusubiri yeye afanye manunuzi fulani bali wewe kama mwanamke mwenye kipato unapaswa kuangalia nini kinahitajika/kosekana ndani na kurekebisha mambo. Natambua baadhi ya wanawake wenye kipato lakini hutegemea wanaume wawafanyie kila kitu wakiamini kuwa kufanya hivyo kutamzuia mwanaume huyo kuhonga nje ya uhusiano wake.


Unapoonyesha kuwa unajitegemea unamjengea mpenzi wako imani kuwa hata mkiwa na watoto na yeyekupoteza kipato au hata kufa wewe kama mwanamke utaweza kutunza watotowenu bila tatizo lolote. Ikiwa huna kipato basi sio mbaya kama utakuwa unamkumbusha mpenzi pale panapokuwa na mapungufu ya vitu ndani ya nyumba yenu.

Kidokezo: Vitu vidogo kwenye ambavyo pengine wewe unadhani havina umuhimu ndio hivyo hivyo vinavyoweza kuharibu uhusiano wenu.


Mf: Nguo zote chafu hivyo inabidi avae nguo ambayo haipendi na hivyo kuwa “uncomfortable” huko kazini, ikiwa kachekwa ni wazi hatokuwa na furaha hata akirudi nyumbani na hali hiyo ikiendelea ni wazi kuwa uhusiano wenu utakuwa Mashakani.

Ahsante kwa ushirikiano.

Wednesday

Jinsi ya kuchagua jinsia ya mtoto

"Nina kukubali uwezo wako kiushauri na kiuzoefu,Umejaliwa!!..Mimi ni kijana wa kiume  mwenye umri wa miaka 27,nina mchumba wangu na tuko kwenye harakati za kufunga ndoa.





Tatizo langu ni hili: Napenda sana first born wangu awe wa kike;[tei tei.....],na ninasikia kuna namna fulani ya kuweza kupanga jinsia ya mtoto japo ni kwa majaliwa ya mungu.





NIFANYEJE???? Naomba unisaidie jamanii!! Wako B.Z"



*****************************



Dinah anasema: Ahsante, Nashukuru sana. Ni kweli kuna namna ya kuchagua Jinsia ya mtoto kabla Mimba haijatungwa lakini bado haijathibitishwa Kisayansi/Kitaalam.





Kupata mtoto wa Kike sio ngumu sana kama ilivyo kwa mtoto wa kiume + inategemea zaidi kwenye uwingi wa jinsia hiyo upande wako(familia ya mwanaume).





Mbegu zinazosababisha mtoto wa kike "hutembea" taratibu kuelekea kwenye Yai na huishi kwa masaa 72-Wiki....hivyo wewe na mkeo hamtahitaji kusubiri "tarehe" maalum.





Kama kwenu au kwa baba mdogo/ mkubwa kuna wanawake wengi basi unaweza ukafanikiwa kupata Binti bila taabu kabisa.



Ila epuka kufanya mapenzi tarehe ambazo mkeo ajae anakaribia kupevusha Yai....fanya mapenzi baada ya hedhi na wiki mbili baadae.





Mbegu zinazosababisha mtoto wa kiume zipo "faster" na hufa haraka, hivyo kama unataka mtoto wa kiume inabidi kutegea "tarehe" maalum ili Mbegu iliwahi yai likiwa njiani...





Japokuwa suala la mtoto wa kiume linategemea zaidi upande wa Mwanamke, ikiwa kwako kuna wanaume wengi au idadi sawa na wanawake, urahisi wa kupata mtoto wa kiume ni kubwa.





Sehemu ya maelezo yangu ni kutokana na uzoefu wangu binafsi, tulipotaka mtoto wa kwanza awe wa Kiume tulikuwa tunafanya kwa kufuata "tarehe" maalum + mikao maalum(hakuna kifo cha mende wala vijiko)!!





Mtoto wetu wa Pili ambae ni wa kike, hatukufuata "tarehe" maalum...



Kifamilia, idadi ya wanaume kwetu ni kubwa kuliko wanawake.



Wengine wataongezea...

Mapendo tele kwako...

Tuesday

Nampenda ila ni Kicheche, nimtulizeje?

Habari Dada, 27 ni umri wangu, Mwaka 2010 nilianza mahusiano na binti mmoja akiwa Form 3 mwenye umri wa miaka 17. Nilimpenda sana tangu the first day namuona, kipindi hicho nilikuwa College. Kimaisha kwao hali si nzuri, kutokana na mapenzi yangu kwake niliweza kumsaidia Ada.

Kuna wakati hata kuiba chakula home kama Mchele, Unga na vitu vingine vingi ili asitaabike. Pia nilimsaidia kimasomo kama kufatilia shuleni kwao ambako nilijifanya ni Kaka'ke. Kutokana na shule kuwa mbali na anapoishi ilibidi ahame na kukaa kwa family friend wao.

Ukweli alikuwa hapendi Shule, kwani mara nyingi maudhurio yake hayakuridhisha. Alifika Form Four ila hakumaliza. Huyu mtu akahama pale alipokuwa akiishi akaenda kwa marafiki zake maeneo flani ya M'nyamala, sikupenda akae maana sifa za huko si nzuri.

Nilimsihi sana Arudi kwao hakutaka hata mzazi(single parent-mama)yake hamsikilizi mpaka leo. Kipindi hicho mimi nikamaliza Chuo. Nikaamua kufuatilia Skuli kwao nikaambiwa amefukuzwa, Baada ya hapo sikujua namna ya kumsaidia maana sikuwa na hela ya Shule ya Private, ninamuonea huruma sana.

Ananilaumu kuwa mimi ndio nimemfanya aache shule maana baada ya kuwa kafukuzwa alikuwa akija home analala hata siku tatu. Wakati huo mimi nilikuwa Jobless so nilichukulia advantage, baada ya muda nikamwambia baadae tuachane ili mimi nitafute kazi. Alilia sana ila baada ya wiki nikamuambia turudiane akakubali na baada ya wiki moja akanitosa na kunitukana matusi sijapata kuona. Nilichanganyikiwa na nililia kama mtoto mdogo hapo tukiwa na mwaka mmoja.

Kwa kweli alikuwa mtu wangu wa karibu sana. Nikapata kazi mkoani ambako nipo mpaka sasa. Nikamtext nikamwambia nimepata kazi mkoa flani nimefanikiwa interview. baada ya Wiki yaani mwezi tangu tuachane akanikpigia simu akidai kuwa mamake anaumwa ananiomba hela kwa huruma nikamtumia via mpesa.

Tukaanza tena mahusiano, ila alikuwa amebadilika sana. Siku nilimkuta na simu ambayo si yake akadai ni ya bf wake wa zamani. Niliongea na yule kijana na aliniambia huyo demu muhuni na anapenda sana kufanyiwa kinyume.

Sikujali nikaendelea nae, siku mmoja aliniomba nimuingilie kinyume na maumbile, hapo ndio nikajua jamaa alisema ukweli lakini sikukataa nilifanya.

Baada ya muda nilimuida aje huku Mkoani nilipopata Kazi ili apaone kwangu, Huku mkoani nilipopata kazi na alikaa miezi minne lakini tulikuwa tukigombana kila siku. Mara atoke mchana arudi saa tisa usiku, analewa, analeta Mashangingi nyumbani kwwangu. Nikamwambia arudi tu kwao ila nilimuonea huruma. Hiyo ilikuwa October mwaka jana, sikujua alipoenda. November nikamuona kwenye baa moja maarufu alikuwa amekaa na Mzee mmoja nikasalimiana nae akaondoka mida hiyo hiyo.

Nachukia mambo yake lakini sijui kanipa nini? Nampenda sana, nikaanza kumtafuta tena ila niliishia kutukanwa tu. December 31 mwaka jana akanipigia na kuanza kuomba turudiane, tukarudiana. Feb 2013 alienda mkoa flani jirani na napoishi na rafiki yake, alivyokuwa akirudi alipitia kwangu baada ya nimemdanganya nimenunulia vitu fulani vya ndani so akakasirika alivyoona sikuwa mkweli, hata hivyo tulitoka.

Siku mbili baada ya birthday yake tukavamiwa na vibaka ambao walitishia kumbaka mbele yangu. Waliiba pochi simu na kila kitu na walituumiza sana. So nikaona kama mkosi au labda ni jamaa alishawahi kuwa nao nilipoachana nae wametufanyia revenge.

Kaondoka Wiki iliyopita na sasa hanitaki tena. ILA NASHANGAA SIJUI KWA NINI MIMI HUUMIA SANA KULIKO YEYE. Alishawahi nishika na wanawake nje ila nahisi (sina uhakika lakini )yeye ni malaya zaidi coz kwao hawajali anaishi wapi. Nampenda nifanyeje?lengo atulie nimuoe ila elimu hana na hataki kusoma. Nifanyeje, nifanyeje?


Dinah anasema: Kaka mapenzi matamu lakini yanaumiza. Nashukuru kwa kuelezea Hadithi yote kwa kina lakini jibu lake ni fupi sana.
Huyo Binti ni bado ni Mtoto (hajakuwa kiakili), anatumia matatizo ya kifedha kwenye familia yake kama tiketi ya kutangatanga na Dunia. Inasikitisha lakini ndio amechangua mtindo huo wa Maisha.

Pia inaelekea anakutumia kiuchumi lakini hana mapenzi na wewe. Mambo ya kuachana na kurudiana kila baada ya Wiki mbili ni kupotezeana mida tu.

Futa mawasiliano yake na acha kumtafuta tena. Songa mbele, weka maisha yako sawa.
Muda ukifika utakutana na Binti mwenye tabia njema na atakae kupenda zaidi ya unavyompenda au kama unavyo Mpenda.

Hakikisha umeangalia afya yako(Kapime) ili uanze maisha mapya ukiwa unajua ulipo(Status) yako.
Wachangiaji wengine wataongezea....


Kila la kheri. Mapendo tele kwako!!

Monday

Simpendi Mume wangu baada ya kutambulisha Mtoto wa nje.

"Dada pamoja na wadau weninge ushauri wenu ni muhimu kwangu. Mimi nina miaka 22, nimeolewa miaka miwili sasa. Tatizo ni kuwa simpendi hata kidogo mume wangu.

Siku za mwanzo tulivyokutana hakuniambia kuwa ana mtoto. Baada ya wiki mbili akaniambia ana mtoto tangu hapo mapenzi yakapotea sikuwa na haja ya mwanaume wa namna hiyo kwani sipendi watoto wa nje hata kama nimemkuta.

Nimejitahidi labda nitampenda lakini mpaka leo wapi, sioni hata dalili sijui hata nifanyeje na nipo kwenye ndoa nitaachana nae vipi au nifanyeje? Asanteni jamani kiroho safi"


Dinah anasema: Pole kwa unayokabiliana nayo, mimi binafsi sipendi watoto wa nje ya ndoa au kabla ya ndoa ( wa ujana) lakini kutokana na maisha tunayoishi hivi sasa ni nadra sana kukutana na kijana wa miaka 25-32 ambae hana mtoto....wengi wanazaa iwe kwa uzembe na kutojali, kutegeshewa (PMU) au kusingiziwa.    

Sidhani kama humpendi mumeo, nadhani unahasira nae kwa vile unahisi amekudanganya, hilo moja.  Pili, ni hofu uliyonayo kuhusiana na hisia zake juu ya Mwanamke aliezaa nae na labda usumbufu utakao upata kutoka kwa mwanamke huyo hapo baadae.    

Baadhi ya watu wanaweza kudhani kuwa una roho mbaya lakini ni ukweli usioepukika kuwa kunapokuwa na Mwanamke mwenye mtoto lakini mpenzi wako hasemi mpaka baada ya kufunga ndoa....inakusanya maswali mengi yanayojenga hasira kuu.    

Kutokana na maelezo yako umegusia kuwa hupendi watoto wa nje, inawezekana kabisa umewahi kuliweka hilo wazi kwa Mume kabla ya ndoa hali iliyopelekea yeye kuogopa kukuambia kuwa anamtoto akihofia utamuacha.    

Maswali muhimu unayopaswa kumuuliza mumeo ambayo yanaweza kukusaidia kumsamehe, kujiwekea "sheria", kuanza upya na kusonga mbele na maisha yenu.    

1)-Hisia zake kwa Ex wake (mama wa mtoto) na je mtoto alizaliwa kwenye mazingira gani (ndoa, uhusiano kabla ya ndoa au usiku mmoja aka bahati mbaya).  

2)-Mtoto anaumri gani? anaishi wapi? na nani?  

3)-Je! kuna mawasiliano yeyote kati yao?     Jinsi atakavyokujibu ndivyo itakavyokusaidia kusonga mbele (unaweza kurudi kwangu kwa ushauri zaidi ukipata majibu ambayo ni tata kwako).  

Pia majibu ya mumeo kwa mswali hayo yatanisaidia mimi na Wachangiaji wengine(perhaps) kukuelekeza namna ya kuweka sheria ili mtoto aendelee kuwasilina na Baba yake (hana makosa) lakini  wakati huohuo Ex wa mumeo (mama mtoto) akae mbali na ndoa/familia yenu mtakayoianzisha.   

**Alafu mwenyewe mdogo masikini...anyway! Nakutakia kila la kheri,
Mapendo tele.....    

Saturday

Aisee! Nimerudi, Nilikuwa Busy making babies....

Haa! Asikuambie mtu....ukitaka kujua utamu wa ku-make babies panga. Yaani wewe na mwenza wako mnajua kabisa bao litakalopatikana  leo linaenda tengeneza Mtoto. Basi ile "thought" ya  "vimelea" vinaenda kuungana na Yai na kutengeneza Mwanadamu inakuongezea amani, utulivu, Mahaba na mapenzi.

Nadhani ni tofauti na ile ya kushitukizia, kwamba mnafanya tu kila siku bila Kinga....alafu hujui kama mimba imetunga au la!...well ningejaribu hiyo lakini nadhani tumemaliza KUZAA*.


Anyway, Asanteni wote kwa Ushirikiano, mmekuwa mkitembelea na kunitumia maswali, maoni na salamu bila kuchoka. Sikutegemea kuendelea kupata watembeleaji kati ya 2,000-7,000 kwa siku....ukizingatia Blog haikuwa "active". Hakika najua ikiwa "active" nitarudi kwenye 100,000+. Mungu awabariki sana kwa Upendo na Ushirikiano wenu kwangu.


Kuwa mama/mzazi ni jambo jema na baraka lakini pia ni kazi ngumu sana na inachukua muda wako mwingi (vingine vinakuwa havina maana isipokuwa mtoto/watoto). Natambua wengi mnalijua hilo lakini mimi ndio kwanza najifunza au niseme napata uzoefu mpya.


Pamoja na kuwa ni busy mam-astic(hehehehe) kwa wanangu, nitajitahidi sana sana kuwaletea mambo/uzoefu mpya wa kimapenzi, mahusiano na ngono(kama ilivyokuwa awali) sitotumbukizia masuala ya watoto.


Kuwa mzazi au kuwa na watoto ni Baraka ya Ndoa/Matunda ya uhusiano, haipaswi kutufanya tusahau kuwa sisi ni Wapenzi, hivyo basi nitaendelea kuwa nawe sambamba tukielimishana, kumbushana, ambizana na kuelekezana ili sote tufurahi katika Ulimwengu huu Mtamu.

Nasikitika tu kuwa sitoweza kujibu Maswali ya nyuma, nitajitahidi kujibu yaliyoingia kuanzia wiki iliyopita. Samahni kwa usumbufu.

Endelea  kuwa nami na asante kwa Ushirikiano.

Mapendo tele kwako...

Pages