Tuesday

Hili ni Buti au Posa?-Ushauri

Dada Dinah naomba niwasilishe shida yangu kwa njia ya kunukuuu.

"Stella! Najua kuwa unanipenda sana. Lakini tangu nimekuwa na wewe roho yangu inaniuma sana kila ninapoenda kanisani kuwa nafanya mapenzi kabla ya ndoa. Kwasababu nampenda Mungu wangu na natamani kuishi kwa mapenzi ya sheria zake naomba tuache kutenda dhambi hii.

Nisamehe sana kwa uamuzi huu mgumu. Nakuombea nawe ufuate mapenzi yake. Usiku mwema na mungu akubariki."

Je hapo nifanyaje? maana mpaka sasa sijamjibu kitu chochote hivyo naomba unipe jibu la kumjibu. Na pia nimemuomba kuonana nae na amekubali, je nikimuona nimwambie maneno gani?asante sana wako Stella.

Jawabu: Asante Stella kwa mail na pole kwa mshituko. Mpenzi wako ni mmoja kati ya wanaume wachache sana wenyewe uwezo wa kuwa wazi. Huyu bwana kutokana na Imani yake ya Dini amegundua kua mlichokuwa mkikifanya ni makosa/linyume na Imani yake na hakuwa na amani kila mlipokuwa mkifanya, hivyo unapaswa kuheshimu hilo.

Hayo maelezo yake hakika yanachanganya kidogo na huenda kuna mawili matatu ambayo mpenzi wako anawakilisha kutokana na ujumbe huo, kama nilivyoweka kichwa cha habari hapo, inawezekana kabisa akawa anakutaka wewe uamini kule anako amini, yaani muwe na Imani moja ili mfunge ndoa na kufanya mapenzi ndani ya ndoa.

Mpenzi wako huyu (kutokana na upande mmoja wa maelezo yake)hajakuacha wewe kama mpenzi bali ameacha kufanya ngono na wewe kabla ya ndoa na kama alivyosema anakuombea ili ufuate mapenzi yake Mungu. Inaonyesha huyu bwana anakujali na hata ulipoomba kukutana nae alikubali moja kwa moja bila kukuzunguusha.

Lakini pia kwenye maelezo yake hayo kasema kuwa "najua unanipenda" hakuna mahali amesema kuhusu hisia zake juu yako,hiyo inaonyesha kuwa wewe ndio ulikuwa unampenda zaidi kuliko yeye alivyokuwa akikupenda, natambua ulipokuwa ukifanya nae ngono uliamini kuwa anakupenda lakini haikuwa hivyo.

Unajua mwanaume ni kiumbe wa ajabu sana linapokuja suala la ngono, huwa hajui kumtosa mwanamke japokuwa hafurahishwi na anachokifanya au anajua kabisa kuwa ni kosa lakini bado ataendelea kukifanya ili kukuridhisha na kutokuumiza hisia zako.....hata akiamua kukutosa bila kukungonoa hutotambua, atafanya hivyo bila wewe kujua kirahisi. (kuna mbinu zao za kufanya hivyo nitazielezea ktk siku zijazo).

Sasa kwa vile tayari mmepanga kukutana inabidi iwe hivyo, ila mimi ningekushauri kuepuka kuzungumzia kilichotokea kwani hakuna litakalobadilika hasa kama wewe wataka ngono tu ndani ya uhusiano mliokuwa nao, ni wazi kuwa haitopatikana.

Ikiwa uhusiano wenu ulikuwa zaidi ya ngono basi unaweza kumjibu kwa SMS/Barua pepe kwa kumwambia "Samahani sitoweza kukutana na wewe kama tulivyopanga. Naheshimu uamuzi wako wa busara, pamoja na kuwa nakupenda nilikuwa nakosa amani kabisa kila tulipokuwa tukifanya mapenzi lakini nilikuwa nafanya hivyo kwa ajili yako nikidhani ulikuwa unapenda.

Ni jambo jema mimi na wewe kuacha dhambi hii na kufanya tendo hili takatifu kisheria na kwa mapenzi yake Mungu". Hapo utamuacha njia panda kama alivyokuacha wewe......uchune!

Kama anakupenda na ilikuwa posa basi atakutafuta iwe kwa simu/sms au barua pepe na kujaribu kukushawishi ili ufuate imani yake na hatimae kufunga ndoa au kukuuliza maswali au kuomba m-baki marafiki n.k.

Akiuchuna ujue buti.....usipoteze muda bali endelea na maisha yako kwani penzi halilazimishwi.

Natambua buti linauma haijalishi kama umepigwa la kwenye meno au ummempiga mwenzio kwenye ugoko, yote yanauma the same lakini siku zinapita na unajikuta umesahau. Ni sehemu ya maisha na hatunabudi kukabiliana na kila linalotujia liwe zuri au baya.

Endelea kuwepo hapa na kila la kheri.

Sunday

Familia haimtaki, kasaliti penzi letu-Jawabu

Asante M3 kwa kuleta mkasa huu hapa ili watu wachangie na vilevile kujifunza. Naomba ufikishe pole zangu kwa mhusika.

Huu bwana alipatwa na mshituko siku ya tukio na bado yuko kwenye mshituko ambao unaweza kuendelea kuwepo kwa muda mrefu zaidi kama ataendelea kunywa pombe kuzima/funika maumivu badala ya kukabiliana nayo ili kumaliza maumivu ya hisia zake.

Wanadamu tunatofautiana sana linapokuja suala la maamuzi hasa baada ya kushuhudia mtu “kakunja” mkeo , huyu bwana alimuamini mke wake kwa asilimia zote hasa ukizingatia milima na mabonde waliyopitia mpaka kufunga ndoa.
Kinachonisikitisha ni kuwa mke wake hajaomba msamaha, huenda na yeye bado haamini kuwa amebambwa “live” au hapati nafasi ya kufanya hivyo kwa vile wakati wote jamaa kalewa(mpatie anuani yangu ya barua pepe nijaribu kumuweka sawa).


Akumbuke tu kuwa mtu anapoamua kusaliti penzi mara. zote huwa anasaliti penzi na mmoja kati ya watu ambao wako karibu sana na yeye iwe ni rafiki wa mke/mume, jirani, mfanyakazi mwenzie, msaidizi wa kazi nyumbani n.k (kama umepitia moja ya makala zangu kuhusu kuteleza utanielewa). Hivyo suala la kusikitika kwa kusema “rafiki yangu mpenzi aliyenipa mtaji” aliondoe tena huyo ndio mbaya zaidi!


Ninachokiona hapa kutokana na maelezo yake ni kwamba, wewe(mume) huenda ulikuwa ukifanya kazi sana ili uweze kumtimizia mke wako mahitaji yake ili asije akashawishika na watu wenye mapesa(ukizingatia kuwa ametoka kwenye familia fulani).

Inawezekana kabisa kuwa ulikuwa umejisahau na kuweka nguvu zako zote na muda wako wote kwenye kutafuta pesa ukidhani kuwa kukidhi mahitaji ya mkeo kwa kuwa na Senti ndio kuonyesha mapenzi kusahau kuwa wanawake wengine mapenzi ya mwili ni muhimu zaidi kuliko pesa......ikiwa alikupenda na umasikini wako ni wazi kuwa pesa isingekuwa kishawishi kwa mkeo huyo.


Kitu muhimu unachopaswa kukifanya hivi sasa ni kutengana na mkeo kwa muda (kukaa mbali nae), kisha acha kunywa pombe (ulevi)hatua hii ya mwanzo itakusaidia kukabiliana na maumivu yako na wakati huohuo kujua hisia zako zimesimama wapi katika hali halisi.


Hatua ya pili ni kuzungumzia tukio hilo kwa uwazi kwa watu wa karibu na wewe ambao unajua kwa uhakika kuwa watakusikiliza, kukuelewa na kukusaidia kwa kukupa matumaini na ushauri mzuri utakaokufanya ajue hisia zako zilipo juu ya mke wako na nini unadhani kinaweza kuwa kumesababisha mkewe kutoka nje ya ndoa yenu.


Epuka watu wanaotoa ushauri wa haraka kama vile kumuita mkeo majina machafu, kukuambia umuache na ushauri mwingine ambao wewe unajua hautokusaidia.


Hatua ya tatu ni kukutana na wataalamu waliobobea kwenye masuala ya Ndoa na mahusiano ya kimapenzi ana kwa ana ili uweze kupata msaada mzuri zaidi utakaokusaidia kufanya maamuzi ya busara.

Mtaalamu yeyote wa masuala haya kitu cha kwanza kukuuliza kitakuwa je unampenda mkeo? Pili utaulizwa...kitu gani unadhani /hisi kinaweza kuwa ni sababu ya mkeo kutoka nje ya ndoa?


Ikiwa utahisi kuwa bado anampenda mkeo na kupata jibu nini hasa kinaweza kuwa sababu ya mkeo kuchomoka nje basi mtaalamu huyo atapaswa kuandaa siku ili wewe na mkeo mkutane na mpewe darasa kama “pea” na hapo kila moja wenu ataulizwa maswali kadhaa ili kuwasaidia nyote wawili kutambua hisia zenu kimapenzi. Baada ya hapo mtapewa muda ili muweze kuzungumza, yaani kuwasiliana sio kuzozana na kubishana.

Inawezekana kabisa baada ya hapo ukawa hayuko tayari kurudisha uhusiano kwa wakati huo, hiyo ni ruksa kabisa kwani itakuchukua muda kusamehe na kusahau . Lakini kuzungumzia hisia zenu mbele ya mtu ambae anaelewa masuala haya itawasaidia sana.


Hatua ya nne ni wewe na mkeo kuwasiliana, kuzungumza kwa uwazi kabisa kwa kutumia maswali yangu yafuatayo:-

1)-Uhusiano wenu tangu mmefunga ndoa mpaka ulipomfumania ulikuwaje? Kuna kitu chochote kipepungua/badilika?

2)-Kitu gani kiliwafanya mpendane na muamue kufunga ndoa? Je bado hicho kitu mnacho?

3)-Mnataka nini kutoka kwenye uhusiano wenu na je wewe unataka nini kutoka kwa mpenzi wako?

4)-Unahisi nini kila unapomfikiria au kumuona mpenzi wako hivi sasa?

5)-Unamchango gani au unanafasi gani kwenye uhusiano wenu?

6)-Vitu gani huwa mnafanya pamoja kama wapenzi?

7)-Mara ngapi mnafanya mapenzi kwa wiki na je mnatosheka?

8)-Je unadhani mpenzi wako anahitaji ku-improve? Nini hasa kiwe “improved”?

9)-Ikiwa unapewa nasafi ya kumuwekea mwenza wako mipaka ni mipaka gani utamuwekea?

10)-Ni wazi kuwa hamuaminiani kwa asilimia zote kutokana na tukio, je unadhani utaweza kumuamini tena mwenza wako ?

Haya maswali huwa nayatumia ninapofanya 1-2-1 na pea yenye matatizo ili kurudisha uhusiano wao ulipokuwa na kuwapa mbinu nyingine(kutokana na majibu yao) ili kuboresha uhusiano wao na kuzuia makosa kutokea tena......D'hicious inaamini ktk kuboresha mahusiano na sio kuvunja.

Kila la kheri.

Friday

Napata na kukosa hedhi, nifanyeje "nimimbike"?-Ushauri.

"Hongera kwa kutupatia mavitu motomoto,me ni mdau wako mkubwa,da dinah naomba unisaidie kwa hili; nimeolewa miaka 5 iliyopita na sijapata mtoto mpaka sasa na tatizo langu kubwa ni hedhi yaani kupata kwangu hedhi si kila mwezi.

Naweza pata mwezi huu na unaofuata nisipate hata miezi 2 au 3. Nilikosa hedhi kwa muda wa miezi 5 nyuma na nimepata mwezi huu nimeanza period tarehe 13/8/2008 hadi tarehe 8/10/2008 ndio nimemaliza na hitaji nibebe mimba hasa kwa mwezi huu.

Nimkumbushe vizuri tarehe za upevushaji ili ni-do na niweze kupata ujauzito.Yaani nina hamu kweli na mtoto mwenzio!
Asante. Mdau!"

Jawabu: Asante, Sasa Mdau umenichanganya kidogo hapa, inamaana umekuwa hedhini kwa takribani mwezi na nusu? Alafu unapokaribia hedhi huwa unahisi dalili zozote kuwa sasa unakaribia au inaibuka tu bila taarifa?....nisaidie nili nikusaidie kiuhakika zaidi.

Kabla sijakujibu (nasubiri ufafanuzi wako) ni vema basi ukaelewa suala zima la mzunguuko wako wa hedhi kwani kwa baadhi ya wanawake huwa wanachanganya mzunguuko huu wakidhani kuwa kila mwezi lazima apate hedhi ktk tarehe zile zile lakini ukweli ni kuwa tarehe kuwa hazijirudii kila unapokuwa hedhini inaweza ikawa siku nne kabla ya tarehe ya mwezi uliopita au siku saba mbele ya tarehe uliyopata hedhi mwezi uliopita.(inategemea zaidi na urefu wa mzunguuko wako wa hedhi).


Mzunguuko wa kawaida unachukua siku 24 mpaka 35, kwa maana kuwa mzunguuko mrefu ni siku 35 na mfupi ni siku 24 japokuwa wengi wanakwenda mzunguuko wa siku 28 tu bila kubadilika.

Mzunguuko huu unaweza ukaanzia tarehe 10th na kuendelea kuzunguuka na siku moja utajikuta unapata hedhi yako tarehe 31st Sept ambayo ni sawa na mwenzi mpya (yaani October) si ndio alafu usipoata hedhi mwezi mwezi wa kumi labda tarehe 28th kwako wewe unaweza kudhani kuwa umepata hedhi mara mbili ktk mwezi mmoja.......lakini katika hali halisi ya mzunguuko wako ni kwamba umepata hedhi miezi miwili tofauti kwani kinachohesabiwa ni ile siku ya kwanza ya kuona damu ambayo ni 31st na sio tarehe 1st ya mwezi uliofuata......sijui umenielewa hapo?


Kwa baadhi ya wanawake hasa wale ambao wanatumia madawa ya kuzuia mimba kuruka hedhi inaweza ikawa kawaida, pia wale ambao ndio kwanza wamevunja ungo pia inaweza kuwa ni kawaida bila kusahau kwa wale wenye matatizo fulani ya kiafya (kama kisukari, matatizo ya figo,au wapenzi wa ku "Diet" inayokunyima virutubisho muhimu unaweza kuruka hedhi.


Kuruka hedhi inaweza isiwe tatizo unapotaka kushika mimba/kumibika kama utajua dalili za yai lako kupevuka (kuwa tayari kurutubishwa) ila utahitaji kujega tabia ya kuhesabu siku zako na vilevile kusoma na kutambua mabadikiko ya mwili wako hasa maeneo nyeti nikiwa na maana uke.

Kuruka hedhi sio tatizo kubwa sana kama wewe unaafya njema na mara kwa mara yai linashuka kwa maana unapata hedhi hivyo uwezekano wa kukamata/shika/mimbika upo, ila utakachopaswa kukifanya ni kuwa mwepesi kugundua mabadiliko ya mwili wako ili uweze kujua kama yai limepevuka na linahitaji kurutubishwa na hapo ndio ufanye mapenzi na mumeo....nitakueleza mabadiliko gani ya mwili wako uyafuatilie jinsi ninavyoendelea.....


Pamoja na kusema hivyo kuruka hedhi huko kunaweza kuwa tatizo ikiwa tu umri wako ni mkubwa, kwani jinsi unavyokua uwezo wako na upevukaji wa mayai yako hupungua, uwezo wako kunyevuka(nyegeka) wakati wa kufanya mapenzi ili kurahisisha "usafiri" wa mbegu za kiume kwenda kuungana na yai lako lililopevuka, vilevile kama huna matatizo ya mirija ya "felopian".

Unaweza kutumia njia asilia (nitakuelekeza ukinipa ufafanuzi) ili kushika mimba au unaweza kwenda kumuona Daktari kwa ushauri zaidi na matibabu, mara nyingi wanakufanyia uchunguzi alafu kama huna matatizo mengine basi wanakupatia vidonge ambavyo vitasaidia na kuongeza muda wa upevukaji wa mayai yako kila hedhi inapokaribia.Nikija nitakupa maelezo ya mabadiliko ya mwili wako ambayo yatakusaidia wewe kujua kama uko tayari kumimbwa.

.......mida mida basi.

Thursday

Sikujua kuwa mpenzi ni Kaka,Nifanyeje-Ushauri

" Habari dada dinah mimi ni msomaji wako wa kila siku naitaji sana ushauri wako ili ni niweze kufikia hapo ninapotaka na naitaji sana ushauri wa wasomaji wenzangu.

Mimi ni msichana 24, kutoka ndani ya Tanzania tatizo nililonalo ni kwamba mimi nilikutanana na kijana mmoja ktk chuo kimoja basi tukatokea kupendana sana lakini siku moja tulijikuta wote kwenye msiba wa Binamu wa mama yangu ambaye kwa upande mwingine ni mjomba wangu ambae ikatokea kuwa ni baba yake mdogo Mpenzi wangu.

Sikuamini da Dinah lakini swali linakuja bado tunapendana sana na Je undugu uluopo unaweza kuwa kikwazo mpaka sasa bado hatujaachana na nilimuuliza Bibi yangu akaniambia kuwa uwezo wa kuishi mume na mke upo ila mpaka mama yangu akubali naogopa kumwambia mama nifanyaje?

Nimekuja kugundua kuwa huyo mpenzi wangu ni mtoto wa marehemu Binamu yake mama yangu mzazi je dada dinah mama akikataa mi nitakuwa kwenye hali gani? nampenda sana na yeye ananipenda mno naombeni ushauri wenu jamani jamaa yupo tayari kunioa.

Wazazi wetu ni Binamu wa damu. Kibaya zaidi nampenda sana na yeye ananipenda na tumeshangonoana. Hatutaki mapenzi yetu yawe ya siri tena, je dada dinah kama mama yangu akikataa nitafanya nini? Nimuache au niusikilize moyo wangu au jamii itanichukulia mimi ni maLaya?

Najiuliza maswali mengi sana kiasi kwamba nilimuuliza mchungaji akaniambia kuwa hilo swala halina tatizo kwa kuwa sisi ni mabinamu wa pili. Najiuliza tayari sisi tushafanya ngono sioni sababu ya wawo kunizuia?

Dada dinah mi sielewi nini hatma ya penzi letu, siunajua moyo ukishapenda, Natamani kumueleza mama lakini naogopa akisema hapana! mi nitaumia zaidi, naitaji ushauri wako na
wasomaji wenzangu"

Jawabu: Shukurani kwa ushirikiano wako, pole sana kwa kuwa katika utata wa kimapenzi na undugu. Kwa Makabila mengi Tanzania kuolewa na huyo kijana sio tatizo kwani undugu wenu sio that "strong".

Kwetu (pande zote mbili) ni ruska kabisa kuolewa na binamu yako yaani mtoto wa Mjomba (upande wa kike) sio Binamu mtoto wa Shangazi (upande wa kiume), nafikiri hii ni kutokana na Imani kuwa mtoto akizaliwa anabeba damu ya baba yake zaidi kuliko ya mama yake.(Kisayansi sijui, kimila ndio hivyo tena).

Napenda nikufafanulie hapa kabla sijakuambia nini ufanye. Mama yako na Baba wa Mpenzi wako ni mtu na Binamu yake kwa maana kuwa mmoja wao ni mtoto wa Shangazi/Mjomba(kuna damu za pande mbili tofauti hapo) kwa vile mmoja wa wazazi wao alioa au kuolewa na mtu tofauti ambae sio ndugu.

Huyo binamu mwenye damu 2 tofauti amekwenda kuoa mtu mwenye damu tofauti na sio ndugu na kuzaa mtoto ambae atakuwa na damu 3 tofauti ambazo zinafanya undugu uwe wa mbali kimtindo.

Watoto hao ndio wewe na Mpenzi wako mna damu za watu 3 tofauti kwa maana kuwa mama wa baba yako(bibi anadamu 2 tofauti), baba wa baba yako(babu anadamu 2 tofauti) na baba yako anadamu 2 tofauti.

Hali kadhalika mama wa mama yake mpenzi wako(Bi'mkwe anadamu 2 tofauti), baba wa mama yake mpenzi wako (babu'kwe anadamu 2 tofauti) na mama yake mpenzi wako (mam'mkwe anadamu 2 tofauti)....hivyo Technically ninyi sio ndugu wa damu.

Hakuna haja ya wewe kumuambia mama moja kwa moja bali mtumie bibi (hawa watu wanambinu zao za kizamani za kufikisha ujumbe bila kusababisha mshituko), itachukua muda lakini hatimae mama atajua nini kinaendela kati yako wewe na huyo mpenzi wako hasa kama mnakenda kufunga ndoa.

Lakini kama unahisi kuwa mama atakuwa mgumu kuelewa na unauhakika kuwa mnapendana sana na mnania moja ya kuishi maisha yenu yote pamoja milele na milele basi ni vema kufunga ndoa kwanza kisha ndio kumwaambia nini kimefanyika, hapo hatokuwa na namna ya kuweka kigingi au kukataa kwa kisingizio cha undugu ambao upo kati ya wazazi wake na wazazi wa baba wa Mpenzi wako.

Kila la lililojema.

Monday

Familia haimtaki, Kasaliti penzi letu,nimfanye nini?

"Unajua mapenzi ya ndoa ni kitu tofauti na mapenzi kwenye uhusiano wa kawaida. Linapotokea jambo ndani ya ndoa mnaweza mkasameheana yakaisha, lakini lipo jambo likitokea inakuwa kama kisu kimekata nyama pande mbili, kuziunganisha inakuwa sio rahisi inahitajika nguvu ya ziada.

Sijui wenzangu mtasemaje mkisikia kisa hiki `live' ambacho mhusika ndiye aliyeniletea na hatua aliyoichukua sijui wewe au mimi ungeweza kufanya hivyo.


'Rafiki yangu, hapa nilipo nimechanganyikiwa sina mbele wala nyuma. Wewe ndiye wa kwanza kukuhadithia kisa hiki kilichonikuta. Uliniuliza kuhusu hali ya shemeji yako, ukasema mbona hana raha, na unaona kama ananyong'onyea. Ni kweli, hana raha, na mimi mwenyewe namuone huruma kwa namna fulani, lakini hata hivyo nahisi adhabu anayoipata sasa bado haimtoshi kwa kitendo alichonifanyia.


Shemaji yako tumeoana kwa shida, wazazi wetu hawakukubali ndoa yetu, kwasababu hasa za utofauti wahali za kiuchumi. Mimi ni malalahoi, mwenzangu ametoke upande wa geti kali, lakini tukawa tumependana kupita kiasi. Hii ni habari ndefu kidogo.



Mapenzi yetu yalifikia kuposana, lakini posa ikagonga mwamba, sio tu kwa upande wa kikeni hata kwetu wazazi wangu walikataa wakisema familia hiyo ina nyodo, wanaijua sana. Lakini sisi hatukujali na kwakuwa tulishapendana tukasema mbele kwa mbele.


Visa vingi vilitokea, mpaka nikawekwa ndani kwa visingizio vya ajabu, siunajua tena hawa wenzetu wenye hela, wanaweza wakakusingizia kitu, ukajikuta umefungwa. Nilifungwa miezi kadha nikatoka jela, nabado mapenzi yetu yalikuwa pale pale, mwenzangu akawa amenisubiri na hatimaye wazee walisalimu amri, tukafunga ndoa.


Maisha yetu yalianza kwa shida, kwani jela iliharibu ajira yangu, na kupata kazi ikawa shida ajabu. Nikawa nabangaiza hapa na pale, na mungu akajalia nikajenga kibanda ambacho tunaishi na make wangu had sasa.



Mara nikaona mabadiliko ya ajabu kutoka kwa mke wangu, ile adabu na upendo nikaona kama vinafifia siku baada ya siku, lakini sikujali, kwasababu ya shughuli zangu. Ila, nikahisi kuna kitu, mbona safari za matembezi zimekuwa nyingi kulikoni, mara naenda kumuona shangazi mara mjomba nk. Lakini hata hivyo sikujali sana.


`Mwezi uliopita, … ' alipofika hapa aligeuza kichwa upande mwingine, nakahisi kuna msiba au vipi. Lakini nikahisi ni kitu fulani cha ajabu ambacho kimemkumba rafiki yangu.
'Mwezi uliopita siku kama ya leo nilirejea nyumbani mapema, sio kawaida yangu, huwa nashinda kwenye biashara zangu hadi usiku, na kama nitaamua kurejea nyumbani huwa namuarifu mke wangu mapema ili kama katoka aniachie ufungua mahali fulani.



Siku hii mbaya nilirejea ghafla, kwani nilihitaji pesa nikagomboe mzigo wangu wa pesa nzuri tu. Nilifika nyumbani, na kwa vile ni kwangu nilipitiliza ndani hadi chumbani , la haula, sikuamini macho yangu. Najuta kwanini nilirejea, nikaiona hiyo hali. Ogopa likukute lililonikuta.


Rafiki yangu mpendwa, ambaye tumeshibana, ambaye ndiye aliyenidhamini kwenye kesi yangu na ambaye ndiye aliyenisaidia mtaji wa biashara alikuwa …..sikuamini, `live' anafanya ufusuka na mke wangu…



Nilishikwa na butwaa, nikawa kama mtu aliyemwagiwa maji, nguvu iliniisha, na …' alipofika hapo niliona machozi yakimtoka.

Sijui kanini nilishindwa kufanya lolote, niliwaangalia weee, na wenyewe wakawa wameduwaa, wakisubiri nifanye la kufanya, lakini cha ajabu, niligeuka nakurejea kwenye biashara zangu, hadi jioni. Jioni nilifanya kitu cha ajabu ambacho sijawahi kukifanya, nilikunya kupita kiasi. Niliporejea nililala kama gogo, naikawa ndio tabia yangu hadi leo.



Unajua mpaka leo sijampiga mke wangu na wala sijasema chochote na huyo rafiki yangu, ila ndio wananiogopa kama nyoka. Rafiki yangu ananikwepa na kila akiniona anashituka kama kaona kitu gani sijui, mpaka watu wameshaanza kuhisi kitu.


Mke wangu ameisha/konda kwa mawazo, sijamsema, sijamfanya lolote na ninajifanya kama vile hakuna kitu kilichotokea.


Sasa rafiki yangu, sio kwamba nimepanga iwe hivyo, sio kwamba sikutaka kuchukua hatua yoyote, lakini nichukue hatua gani? nimuache?au nimfanyeje? ukumbuke kwao ni kama walimtelekeza, baada ya kung'ang'ania kuolewa na mimi.

Nimeshindwa la kufanya na siku zinaenda, na hata hamu ya kufanya mapenzi naye sina kabisa…nina mwezi sijui ladha ya mapenzi. SIJUI NIFANYEJE…


Dada Dinah, hata mimi nilishikwa na kigugumizi na sikumshauri chochote kwani mke wangu alifika na mazungumzo yaliishia hapo. Nikaona niliwasilishe hili swala kwako ili kama unaushauri, au kama wanakijiwe chako wanaweza wakashauri, ili nikikutana naye niweze kumpa hayo maoni.


Hayo ni mapenzi ya kusalitiana, je msamaha unaweza ukasaidia? Kifanyike kitu gani ili hali irejee, je upendo utaendelea kuwepo
emu-three"

Friday

Heshima hana tena, nimekosea wapi?-Ushauri!

"Habari za kazi dada Dinah. Mie nina langu moja ambalo naomba ushauri wako au wa wengine pia . Ni katika kupanuana mawazo.

Ni hivii… Mie ni mdada wa umri 26, sijaolewa. Hapo kabla nilikuwa na mpenzi ambaye nilidumu naye kwa miaka 4, naweza nikasema kuwa mapenzi yetu yalikuwa motomoto kipindi kama cha miaka miwili ya mwanzo. Nilikuwa nampenda sana jamaa, pia na yeye alikuwa ananipenda sana tu.

Tatizo lilikuja kuanza baadae, kwamba niliona kama ameanza kunidharau na kuwa haniogopi/heshimu tena. Hata inapotokea ugomvi mdogo anakuwa mwepesi kutamka.. ah unaweza kwenda kutafuta bwana mwingine!


Nikawahi kumuuliza rafiki yangu mmoja, kwamba kwa nini huyu mtu yuko hivi? Akanijibu kuwa NI KWA SABABU ULISHAMWONYESHA KWAMBA UNAMPENDA SANA! Kwamba nilichotakiwa kufanya ningeweka mapenzi yangu rohoni na kauka nayo, lakini nisingemwonyesha jamaa kiasi gani ninampenda!


Hivi sasa nimesha achana na jamaa mwenyewe. Na nimepata mwingine kama mwezi hivi umepita. Hatujafanya chochote zaidi ya kukutana na kuongea, kupeana ofa tu. Ninamwona ni mstaarabu na ninahisi anaanza kuniingia moyoni. Sasa swali langu ni kwamba je ni vibaya kumwonyesha/kumwambia jamaa kama unampenda sana?


Binafsi nahisi kwamba nikimwonyesha ninampenda sana na ninaridhika kuwa naye na sitamwacha (namaanisha ki ukweli na not pretending) ndio atazidi kunipenda zaidi. Je ni sign ya kuonyesha udhaifu wangu wa mapenzi kwake?

Na kwamba itamfanya yeye a-take advantage? Je kutokumwenyesha ni kiasi umemfia ni njia sahihi ya kumfanya mwanaume awe anakuheshimu? (Hapa namaanisha kwamba atakuwa anakuona hubabaiki, na yeye sio mwisho wa reli).

Naomba mawazo yenu wapendwa ili nijue jinsi gani ya kumfanya mpenzi wangu aniheshimu na anithamini."

Jawabu: Shukrani na pole kwa kuwa na mwanaume ambae alijenga kiburi baada ya kujua kuwa unampenda. Kabla sijaendelea naomba nikukumbushe kuwa kuna tofauti ua Kuogopa na kuheshimu, mtu anaekuogopa ziku zote hawezi kukuheshimu ila ataonyesha anakuheshimu kwa vile anakuogopa (heshima za uongo) na yule anae kuheshimu hata siku moja hawezi kukuogopa.


Unakumbuka usemi wa "mapenzi ni kikohozi hayafichiki"? basi ndio ukweliw enyewe huo. Ukijaribu kuficha wewe ndiye utakae kuwa unaumia kwa kujifanya kuwa mtu mwingine na sio wewe. Mapenzi ni zawadi pekee ya thamani unayoweza kumpa mtu na wewe kuipata kutoka kwake sawa sawa au ziadi.

Suala muhimu kwenye uhusiano wowote wa kimapenzi ni kuweka hisia zako wazi kwa mwenzio na yeye afanye hivyo hali itakayowafanya muwe huru na karibu zaidi.

Ikiwa wewe unampenda na unadhani kuwa yeye ndio mwisho wa Reli yaani safari zako zote pale umefika na mabegi umeweka chini (nimekumbuka maneno ya Chid Benz hehehehe) hakuna haja ya kulificha hilo, mueleze ajue....sio useme yote kwa siku moja, hapana.

Kuna namna ya kumfikishia ujumbe mpenzi kama wewe umefika bei (unampenda sana au kupita kiasi) na wakati huohuo kuonyesha kuwa unajiamini kama mwanamke kwamba unampenda na unamtaka lakini humuhitaji kwa maana kuwa huwezi kufa au kulala njaa bila yeye lakini maisha yako yatakuwa bomba na yenye furaha mkiwa pamoja....sijui unanielewa?

Wanaume ni wawindaji hivyo kama mwanamke kamfia mwanaume hulion ahilo na hutambua kuwa unamtaka/penda japokuwa unapokuwa nae kwenye uhusiano anaweza kuhitaji kuhakikishiwa kuwa kweli unampenda kwa kumfanyia au kufanyiana mambo tofauti tofauti.

Huyo jamaa najua kabisa hisia zako hivyo wewe kama vipi ruhusu tu uhusiano uendelee na wewe nenda na flow bila ya kujiwekea "kigingi" au hofu za Ex.

NB: wanaume wengine hawajui kuonyesha mapenzi kwa maneno bali vitendo na wengine ni kinyume chake hivyo kuwa mvumilivu mpaka hapo mtakapo zoeana na kuwa "comfortable" kwenye uhusiano wenu ndio umuelekeze mwenzio........

Pages