Thursday

Sikujua kuwa mpenzi ni Kaka,Nifanyeje-Ushauri

" Habari dada dinah mimi ni msomaji wako wa kila siku naitaji sana ushauri wako ili ni niweze kufikia hapo ninapotaka na naitaji sana ushauri wa wasomaji wenzangu.

Mimi ni msichana 24, kutoka ndani ya Tanzania tatizo nililonalo ni kwamba mimi nilikutanana na kijana mmoja ktk chuo kimoja basi tukatokea kupendana sana lakini siku moja tulijikuta wote kwenye msiba wa Binamu wa mama yangu ambaye kwa upande mwingine ni mjomba wangu ambae ikatokea kuwa ni baba yake mdogo Mpenzi wangu.

Sikuamini da Dinah lakini swali linakuja bado tunapendana sana na Je undugu uluopo unaweza kuwa kikwazo mpaka sasa bado hatujaachana na nilimuuliza Bibi yangu akaniambia kuwa uwezo wa kuishi mume na mke upo ila mpaka mama yangu akubali naogopa kumwambia mama nifanyaje?

Nimekuja kugundua kuwa huyo mpenzi wangu ni mtoto wa marehemu Binamu yake mama yangu mzazi je dada dinah mama akikataa mi nitakuwa kwenye hali gani? nampenda sana na yeye ananipenda mno naombeni ushauri wenu jamani jamaa yupo tayari kunioa.

Wazazi wetu ni Binamu wa damu. Kibaya zaidi nampenda sana na yeye ananipenda na tumeshangonoana. Hatutaki mapenzi yetu yawe ya siri tena, je dada dinah kama mama yangu akikataa nitafanya nini? Nimuache au niusikilize moyo wangu au jamii itanichukulia mimi ni maLaya?

Najiuliza maswali mengi sana kiasi kwamba nilimuuliza mchungaji akaniambia kuwa hilo swala halina tatizo kwa kuwa sisi ni mabinamu wa pili. Najiuliza tayari sisi tushafanya ngono sioni sababu ya wawo kunizuia?

Dada dinah mi sielewi nini hatma ya penzi letu, siunajua moyo ukishapenda, Natamani kumueleza mama lakini naogopa akisema hapana! mi nitaumia zaidi, naitaji ushauri wako na
wasomaji wenzangu"

Jawabu: Shukurani kwa ushirikiano wako, pole sana kwa kuwa katika utata wa kimapenzi na undugu. Kwa Makabila mengi Tanzania kuolewa na huyo kijana sio tatizo kwani undugu wenu sio that "strong".

Kwetu (pande zote mbili) ni ruska kabisa kuolewa na binamu yako yaani mtoto wa Mjomba (upande wa kike) sio Binamu mtoto wa Shangazi (upande wa kiume), nafikiri hii ni kutokana na Imani kuwa mtoto akizaliwa anabeba damu ya baba yake zaidi kuliko ya mama yake.(Kisayansi sijui, kimila ndio hivyo tena).

Napenda nikufafanulie hapa kabla sijakuambia nini ufanye. Mama yako na Baba wa Mpenzi wako ni mtu na Binamu yake kwa maana kuwa mmoja wao ni mtoto wa Shangazi/Mjomba(kuna damu za pande mbili tofauti hapo) kwa vile mmoja wa wazazi wao alioa au kuolewa na mtu tofauti ambae sio ndugu.

Huyo binamu mwenye damu 2 tofauti amekwenda kuoa mtu mwenye damu tofauti na sio ndugu na kuzaa mtoto ambae atakuwa na damu 3 tofauti ambazo zinafanya undugu uwe wa mbali kimtindo.

Watoto hao ndio wewe na Mpenzi wako mna damu za watu 3 tofauti kwa maana kuwa mama wa baba yako(bibi anadamu 2 tofauti), baba wa baba yako(babu anadamu 2 tofauti) na baba yako anadamu 2 tofauti.

Hali kadhalika mama wa mama yake mpenzi wako(Bi'mkwe anadamu 2 tofauti), baba wa mama yake mpenzi wako (babu'kwe anadamu 2 tofauti) na mama yake mpenzi wako (mam'mkwe anadamu 2 tofauti)....hivyo Technically ninyi sio ndugu wa damu.

Hakuna haja ya wewe kumuambia mama moja kwa moja bali mtumie bibi (hawa watu wanambinu zao za kizamani za kufikisha ujumbe bila kusababisha mshituko), itachukua muda lakini hatimae mama atajua nini kinaendela kati yako wewe na huyo mpenzi wako hasa kama mnakenda kufunga ndoa.

Lakini kama unahisi kuwa mama atakuwa mgumu kuelewa na unauhakika kuwa mnapendana sana na mnania moja ya kuishi maisha yenu yote pamoja milele na milele basi ni vema kufunga ndoa kwanza kisha ndio kumwaambia nini kimefanyika, hapo hatokuwa na namna ya kuweka kigingi au kukataa kwa kisingizio cha undugu ambao upo kati ya wazazi wake na wazazi wa baba wa Mpenzi wako.

Kila la lililojema.

No comments:

Pages