Tuesday

Hili ni Buti au Posa?-Ushauri

Dada Dinah naomba niwasilishe shida yangu kwa njia ya kunukuuu.

"Stella! Najua kuwa unanipenda sana. Lakini tangu nimekuwa na wewe roho yangu inaniuma sana kila ninapoenda kanisani kuwa nafanya mapenzi kabla ya ndoa. Kwasababu nampenda Mungu wangu na natamani kuishi kwa mapenzi ya sheria zake naomba tuache kutenda dhambi hii.

Nisamehe sana kwa uamuzi huu mgumu. Nakuombea nawe ufuate mapenzi yake. Usiku mwema na mungu akubariki."

Je hapo nifanyaje? maana mpaka sasa sijamjibu kitu chochote hivyo naomba unipe jibu la kumjibu. Na pia nimemuomba kuonana nae na amekubali, je nikimuona nimwambie maneno gani?asante sana wako Stella.

Jawabu: Asante Stella kwa mail na pole kwa mshituko. Mpenzi wako ni mmoja kati ya wanaume wachache sana wenyewe uwezo wa kuwa wazi. Huyu bwana kutokana na Imani yake ya Dini amegundua kua mlichokuwa mkikifanya ni makosa/linyume na Imani yake na hakuwa na amani kila mlipokuwa mkifanya, hivyo unapaswa kuheshimu hilo.

Hayo maelezo yake hakika yanachanganya kidogo na huenda kuna mawili matatu ambayo mpenzi wako anawakilisha kutokana na ujumbe huo, kama nilivyoweka kichwa cha habari hapo, inawezekana kabisa akawa anakutaka wewe uamini kule anako amini, yaani muwe na Imani moja ili mfunge ndoa na kufanya mapenzi ndani ya ndoa.

Mpenzi wako huyu (kutokana na upande mmoja wa maelezo yake)hajakuacha wewe kama mpenzi bali ameacha kufanya ngono na wewe kabla ya ndoa na kama alivyosema anakuombea ili ufuate mapenzi yake Mungu. Inaonyesha huyu bwana anakujali na hata ulipoomba kukutana nae alikubali moja kwa moja bila kukuzunguusha.

Lakini pia kwenye maelezo yake hayo kasema kuwa "najua unanipenda" hakuna mahali amesema kuhusu hisia zake juu yako,hiyo inaonyesha kuwa wewe ndio ulikuwa unampenda zaidi kuliko yeye alivyokuwa akikupenda, natambua ulipokuwa ukifanya nae ngono uliamini kuwa anakupenda lakini haikuwa hivyo.

Unajua mwanaume ni kiumbe wa ajabu sana linapokuja suala la ngono, huwa hajui kumtosa mwanamke japokuwa hafurahishwi na anachokifanya au anajua kabisa kuwa ni kosa lakini bado ataendelea kukifanya ili kukuridhisha na kutokuumiza hisia zako.....hata akiamua kukutosa bila kukungonoa hutotambua, atafanya hivyo bila wewe kujua kirahisi. (kuna mbinu zao za kufanya hivyo nitazielezea ktk siku zijazo).

Sasa kwa vile tayari mmepanga kukutana inabidi iwe hivyo, ila mimi ningekushauri kuepuka kuzungumzia kilichotokea kwani hakuna litakalobadilika hasa kama wewe wataka ngono tu ndani ya uhusiano mliokuwa nao, ni wazi kuwa haitopatikana.

Ikiwa uhusiano wenu ulikuwa zaidi ya ngono basi unaweza kumjibu kwa SMS/Barua pepe kwa kumwambia "Samahani sitoweza kukutana na wewe kama tulivyopanga. Naheshimu uamuzi wako wa busara, pamoja na kuwa nakupenda nilikuwa nakosa amani kabisa kila tulipokuwa tukifanya mapenzi lakini nilikuwa nafanya hivyo kwa ajili yako nikidhani ulikuwa unapenda.

Ni jambo jema mimi na wewe kuacha dhambi hii na kufanya tendo hili takatifu kisheria na kwa mapenzi yake Mungu". Hapo utamuacha njia panda kama alivyokuacha wewe......uchune!

Kama anakupenda na ilikuwa posa basi atakutafuta iwe kwa simu/sms au barua pepe na kujaribu kukushawishi ili ufuate imani yake na hatimae kufunga ndoa au kukuuliza maswali au kuomba m-baki marafiki n.k.

Akiuchuna ujue buti.....usipoteze muda bali endelea na maisha yako kwani penzi halilazimishwi.

Natambua buti linauma haijalishi kama umepigwa la kwenye meno au ummempiga mwenzio kwenye ugoko, yote yanauma the same lakini siku zinapita na unajikuta umesahau. Ni sehemu ya maisha na hatunabudi kukabiliana na kila linalotujia liwe zuri au baya.

Endelea kuwepo hapa na kila la kheri.

No comments:

Pages