Monday

Nahisi kanichoka!


Habari yako dada dinah!! pole kwa majukumu, dada mimi ni msichana wa miaka 27 nina mpenzi wangu ambaye tupo kwenye mahusiano kwa muda wa miaka sita sasa na tuna mtoto wa miaka mitatu.

Bado hatujaoana kwani  tunasoma na tulianza mahusiano wakati mimi nipo mwaka wa kwanza chuo na yeye mwaka wa pili.Tunasoma nje ya nchi ila mtoto yupo Tanzania analelewa na wazazi wangu.

Dada tangu tumeanza mahusiano mpenzi wangu alikuwa ananipenda saana na kunijali na nilivyojifungua pia aliendelea kunipenda.

Tulikuwa tukifanya kila kitu pamoja na tulishirikishana kila jambo,tulishea pass words za kila kitu,fecbuk,emails  nk!!

Mwaka jana akapeleka barua ya Posa kwetu! TatIzo langu ni kuwa mimi ni  mkorofi halafu nina wivu mnoo...yani kipindi chote hiko cha mahusiano yetu siku akichelewa kurudi tuu(maana tuna appartment huwa tunakaa pamoja kwa baadhi ya siku kwasababu tunaishi mikoa tofauti) hata simuulizi namvamia na maneno na some times nafanya fujo kabisa!

Nikiona kawasiliana na mwanamke zaidi ya mara mbili nafanya fujo! Yaan kanivumilia mnoo!ila nampenda na baada ya kufanya hivyo huwa najirudi nayeye ananieleza ukweli basi najiona mjinga then tunaendelea na maisha.

Ila tabia yangu siachi akifanya kingine naarudia!! yaani huwa nafanya fujo,nampiga na glass, navunja simu zake n.k ila ananibembeleza tunakaa sawa.
   

Sasa this time naona amechoka wa na visa vyangu maana december niligundua ananichit, ikaniuma sana na nikampigia huyo msichana akaniambia kweli yupo na mahusiano na mpenzi wangu na wana kama mwezi mmoja!(na huyo msichana ni malaya sana na yasemekana ameathirika sema mpenzi wangu hajui hizo story maana mpenzi wangu sio mtu wa kujichanganya na watu hivyo habari nyingi za mtaani mpaka mi nimpe). 

Then nikarudi kwa mpenzi nikafanya fujo kama kawaida but akanituliza na kuniomba msamaha, akasema ananipenda na hana fyucha na huyo dada sema alifanya hivyo maana nimezidi visa na ujeuri na imefika kipindi simpi mapenzi.

Akachukua simu akamcall yule dada kumwambia its over na akamtext whatsup kumueleza kuwa ana mpenzi wake anaomba waachane!

Alifanya yote  hayo mbele yangu na akambock koote! ila pamoja na yote hayo mimi nikawa nasindwa kumuamini kama kamuacha japo nikishika simu zake sioni kitu.

Alijitahidi kunionyesha ameacha but mimi wapi, nilimwambia nilimsamehe but moyoni nilikuwa naumia. Ikawa nikipiga simu asipo pokea on time naanza ugomvi, nikienda apartment akachelewa kurudi nafanya fujo tena za ajabu!

Akaniambia sasa hivi tusikutane nikae kwangu mpaka hasira ziishe ila bado nikawa nampigia kelele hunipendi ndomana waniambia nikae kwangu.

Nikakaa kwangu kama wiki huku twawasiliana na kugombana! juzi kanambia niende kule tumefurahi but usiku alilala nikashika simu yake ili nione kama anaendelea na yule dada. Sikukuta vya yule dada bali nilukuta meseji ya mwanamke mwingine akimlalamikia mpenzi wangu kuwa ahamini kama anampenda maana hakuna kitu chochote wanachofanya pamoja!(mesej ni ya tar 19 januar na yule dada wa kwanza tulisolve 23 dec) nikapiga ile namba kwa simu ya mpenzi wangu, akapokea huyo dada mwingine.

Yaani nilichanganyikiwa!! nikamwambia mpenzi wangu akasema hakuna chochote bali panic zangu tuu, nikaanza kumfokea akaniambia this time ananipiga maana nimezidi ujinga!!

Tukapigana hadi basi, mpenzi wangu akaondoka akaniacha appartment na hatukutafutana but usiku nilimcall akasema hawezi rudi mpaka mimi niondoke maana yeye ana mitihani(anafanya medicine huku ni miaka 7) amechoka fujo zangu anataka asome maana mimi sijielewi!!

Na kuhusu matatizo yetu akipata muda huko mbele atakuja mkoani kwangu tuongee kwa sasa anaomba asome!!
 

Kwahiyo dada nahisi mpenzi kanichoka na mimi nampenda saaana na yeye ananipenda ila ndio tumefikia hapo, je nifanyeje?

Amenichit kwa wanawake wawili ndani ya muda mfupi!!na huko nyuma hakuwa hivyo kabisaa!!

Tafadhali nishauri cha kufanya!! tulipanga ndoa tufunge mwaka huu, maana mimi ndo namaliza masters yangu mwezi wa pili.
Ahsante sana, nasubiri ushauri wako wako maana nahisi kuchanganyikiwa.

***************

Dinah anasema: Habari ni njema mrembo, shukurani kwa ushirikiano




Tabia yako ni mbaya na ulipaswa kuachana au kujirwkebisha kitambo. Unaweza kuwa na wivu sawa kwani ni suna  lakini kuwa agressive na violent  sio vema.




Pamoja na tabia yako mbaya bado sio sababu ya mpenzi wako kutereza nje ya uhusiano wenu mara zote hizo.





Mpenzi wako anatumia ''kasoro yako '' kitabia ku justify Umalaya wake na kwasababu anajua kuwa unajua kuwa Unatatizo hilo basi inakufanya rahisi kwake  kufanya makosa na kukusukumia wewe kuwa ndio umesababisha awe hivyo.




Mtu chake,  hata mimi huoji mume wangu kwanini anaongea na baadhi ya wanawake au wanaume.(si wameoa au wapenzi ambayo ni wanawake eti hihihi) Bibi alinambiaaaa usiamini mwezi wako kwa asilimia zote Mia, achia nafasi ya Wivu kwani bila wivu hakuna mapenzi.




Moving on.........Acha kuomba msamaha na kujiona mkosaji, mchumba wako ndio mkosaji mkuu na ameonyesha kiburi na kutojali kwa kusema atakuja huko kwako kuzungumzia issue iliyojitokeza.....basala ya ku sort out kabla ukweli haujapindishwa na kupoteza makali ya issue husika.




Angekuwa anajali na kujutia makosa yake ya kuku cheat na kukupiga( hakupaswa kukupiga au kupigana na wewe bali kukuzuia usiwe too agressive na kupiga).




Huyu mpezi wako huenda amekuzoea, anapenda the idea of ''nina uhusisno mzuri na mama mtoto wangu'' lakini hana mapenzi kwako na ikiwa yapo mapenzi basi  haoni thamani yako kwake na inamuhuwia vigumu kukuheshimu.





Pia uhusiano wenu unamapungufu ya mawasiliano, hamzungumzii uhusiano wenu ikiwa ni pamoja na mawazo ya kila siku mpaka mmoja afanye kosa ndio mmoja wenu a nazungumzia kuhusu kinachomkwaza.



Uhusiano ni kama kazi ofisini, kuna issue basi unaitwa na kuambiwa umekosea wapi na ujorekebishe vipi......boss akikaa kimya mpaka mteja aje kulalamika ni wazima unaweza kupoteza kazi.....sijui naeleweka?



Ushauri wangu kwako ni kuachana nae kwa muda alioomba kujiandaa na mitihani na akimaliza angalia kama atakuja kama alivyoahidi.




Tumia muda huu kujifunza namna ya kuzuia unapohisi hasira. Unaweza ku soma dua/sala kila unapojisikia ku exprode  pia omba msaada professionally kuhusu tatizo lako. Inategemea upo nchi gani ila natambua Ulaya inapatikana widely.




Oh nenda kaangalie afya ili kujua kama hujakopeswa HIV......hili lilikuwa la kwanza sema nimeputiwa.

Wengine wataongezea, kila la kheri.

Tuesday

Mume wa Ndoa, kaikataa Mimba!

"Ni mume wangu wa Ndoa na tumezaa mtoto mmoja mwenye mwaka, nimeshika Ujauzito tena wenye mwezi na nusu lakini Mume wangu kaukataa kwasababu nimechelewa kumuambia.







***********





Dinah anasema: Hello there! Hawezi kukurupuka tu na kuikataa Mimba wakati wewe ni Mkewe na mnafanya Ngono bila Kinga (obviously).













Mumeo nae wa wapi?!! Chini ya Miezi mitatu ni mapema sana kwa baadhi ya wanawake kujua kama wameshika Mimba unless ajipime au akapimwe, Tena baada ya kuzaa ndio kabisaa, maana mabadiliko ya mwili bado hayaja-settle hasa kama ulikuwa unanyonyesha.













Inawezekana kutakuwa na sababu ya kumfanya aikatae Mimba, huenda anatafuta namna ya kukuacha/achana nawe......kabla hatujamjaji hebu nisaidie....Je maisha yenu ya kimapenzi yakoje au yalikuaje kabla hujashtukia una Ujauzito?











Ulipopata ujauzito wa kwanza hali ilikuaje kabla ya tukio? Mlikubaliana mzae au ilikuwa "bahati mbaya" ?











Uchumi wenu ukoje? Je mnaweza kumudu mtoto wa pili? Mlikuwa mnatumia dawa za kuzuia Mimba?









Au labda kuna vijitabia ulivianzisha vinavyomfanya ahisi kuwa Mimba sio yake? Asije kuwa alikutegea kwa kutokukojoa ndani lakini akajifanya kakojoa na wewe bila kujua ukadhani umebeba manii yake.











Bila maelezo kamilifu kwakweli siwezi kusaidia kimawazo. Nahitaji maelezo yakinifu na yaliyojitoshereza.

Mapendo tele kwako...

Monday

Kupenda Attention kwenye Uhusiano.

"Mimi ni mdada wa miaka 30, sijaolewa na wala sina mtoto ila nina mpenzi ambae ndio kwanza tumeanza mahusiano, tuna miezi miwili tu.

Tatizo langu kubwa ni kwamba huyu mwenzangu ni mvivu kuwasiliana yaani kutuma msgs ni mpaka awe ametoka kazini au Mara chache akiwa kazini atatuma msg labda moja au anakaa kimya kabisa.

Pia nikimtumia ananijibu kwa ufupi tu and mara nyingine hajibu labda mpaka usiku kabisa ndio atapiga simu. Sasa Mimi ni mtu ambae napenda "attention" na isitoshe nafanya kazi Mkoani kwahiyo naona kuna ugumu kidogo hapo kwangu.


Kiukweli nampenda na yeye pia anaonesha kunipenda, sasa je nafanyaje juu ya hili suala?


Ina ishu ya Pili je ni mapema sana kuanza kuongelea mambo ya maendeleo Kati yetu? Yeye ni mkimya kidogo kuliko Mimi Kwahiyo pia ni Mzito kidogo kusema kama labda amekwazika kitu Ofisini.

Atasema amekwazika ila hatasema wazi ni nini kimemkwaza labda mpaka niulize sana, hapa pia nahitaji msaada wa namna ya kukabiliana na hii hali da Dinah?

Natanguliza shukrani zangu kwako na kwa wadau wengine.


**********

Dinah anasema: Shukurani kwa ushirikiano.


Unamiaka 30 hivyo nachukulia kuwa mwenzio ni wa umri huo au Mkubwa zaidi. Watu tulio 30+ huwa hatufanyi mambo kama teen au early 20, moja ya mambo yaho ni kupiga siku kila baada ya nusu saa na texts msg kila baada ya dakika 5.


Kwenye umri huo(nilioutaja) tunakuwa na mambo mengine muhimu yanayohitaji muda kuliko kutuma msg au kupiga simu mara kadhaa kwa siku.


Tangu uhusiano wenu bado ni mpya huenda hataki kuonekana "needy" kwako na ikawa sababu ya wewe kumkimbia(baadhi ya wanawake hukimbia needy men kwani wanakua kama Mama na sio Wapenzi kwa wanaume hao).


Sidhani kuwa ni uvivu, inawezekana kabisa ni kutingwa na Kazi....angalau anakukumbuka kabla siku haijaisha au baada ya Kazi hiyo inaonyesha anakujali.

Sote tunapenda "attention" na isipokuwepo au usipopewa na Mpenzi wako hakika utahisi upo "single" kwenye uhusiano na mpweke if that make sense! Mpenzi asipokupa hitaji hilo ni wazi anakudharau au hau-exist....upo tu kama Meza au Kiti (unatumika ukihitajika ila sio muhimu).


Jaribu kuzungumza na mwenzio na kumwambia umuhimu wa ninyi kuwasiliana kutokana na umbali ulipo kati yenu. Hisia za mapenzi pekee hazitoshi kuwafanya muwe karibu wakati kuna umbali kati yenu, mawasiliano ndio yatakayowasogeza na kuwapa ukaribu mnaouhitaji ili kuwa na uhusiano wenye Afya.


Onyesha kuwa simu yake kwako ni muhimu sana kwani inakupa Amani moyoni na kukuondolea hofu ya kama yupo salama au la!

Kubalianeni muda wa kuwasiliana, mf: asubuhi kabla na mara mkifika Kazini....wakati mnatoka na mkifika Nyumbani na kabla hamjalala. (This worked for Us kitamboo kati ya London na Scotland)....so ijaribuni.


Issue ya pili; Ndio ni mapema sana kuanza kuzungumzia masuala ya maendeleo kati yetu, lakini unaweza kuzungumzia masuala ya Kimaendeleo kwa ujumla....hii itamfanya ajue ni mwanamke wa namna gani linapokuja suala la Maendeleo.


Uhusiano ukikomaa ingia full-force na kumtuka kutumia "yetu" (badala ya yangu), "sisi"(badala ya mimi) kwenye mazungumzo yenu ya kimaisha na kimaendeleao.


Nadhani most wanaume huwa sio muongeaji kuhusu changamoto za kazini, hu-prefer kuumia kimya kimya kisha kudharau na kusonga mbele. Wanaume hubadilika wakishafunga ndoa au kuwa kwenye uhusiano na mwanamke kwa muda mrefu na kumuamini.

Kutokana na "umri" wa Uhusiano wenu sio rahisi kwa jamaa kujiachia kwako kwa kila jambo, hapa nadhani kuwa mvumilivu na akiwa comfortable ku-share mambo yake ya kazini na wewe atafanya hivyo.


Pamoja na kusemaa hivyo sio mbaya kuonyesha nia ya kuwepo kwa ajili yake. Always offer kuwa akama anataka kuzungumzia lolote asisite kwani upo pale kwa ajili ya kumpenda na kumsikiliza na kumshauri kama atahitaji.

Kila la kheri!

Mapendo tele kwako...

Friday

Mpenzi Busy na Kazi/Familia yake

Shikamoo dada Dinah & hongera kwa kazi nzuri unayofanya. Mimi nipo kwenye uhusiano kwa miaka miwili sasa.


Nampenda sana mpenzi wangu naye ananipenda. Napenda sana mpenzi wangu awe ananishirikisha kwenye mambo yake lakini huwa haniambii chochote kuhusu plan zake.

Kingine ni kuwa hatuna muda wa kuonana inaweza pita hata miezi mitatu yupo busy na kazi & I understand that, Weekends anakuwa na familia yake so kwa mimi hana muda.

Tunawasiliana kwa simu but yeye ni mvivu mpaka sometimes huwa naamua kukaa kimya. Atanitafuta na kuniuliza kwanini nipo kimya?

Napenda kuwa karibu naye na awe ananishirikisha mambo yake nifanyaje?
God bless you!!


******

Dinah anasema: Marhabaa mrembo, ahsante kwa ushirikiano.


Kwani mna muda gani tangu mmekuwa pamoja? Inashangaza kuwa mtu unaemuita Mpenzi hana muda na wewe isipokuwa Kazi na Familia yake.

Mtu anaekupenda siku zote atatafuta namna yeyote tu ya kuwa na wewe ana kwa ana, haijalishi yupo busy kiasi gani na Kazi au Familia yake.


Nahisi kama vile wewe sio muhimu kwake au kwenye maisha yake kama unavyodhania.


Inawezekana ni mapema sana kuanza kukushirikisha kwenye masuala yake ya kimaendeleo au pia inawezekana kwenye mipango yake ya kimaisha huko mbele wewe haupo....yupo nawewe ili kupoteza muda (sio serious kwenye Uhusiano).

Lakini!!! Kama anapata muda wa kuwa na Familia yake(hope ni ndugu na Wazazi wake na sio mke na watoto) ni wazi anaweza kuugawa muda wake huko kati yako na Familia yake....Mf: J'mosi anakuwa na wewe na J'pili anakuwa na Familia.

Weekend ina Masaa 48....kati ya hayo masaa ni kweli hawezi kutenga masaa 10 ya kuwa na wewe?!! Unless otherwise mnaishi mikoa mbali-mbali.

Kukutafuta kwa simu baada ya kumchunia sio kithibitisho cha Upendo au mapenzi.

Huyu mwanaume sio Mvivu bali hajali hisia zako kwake au haoni umuhimu wa kutumia muda wake na wewe bali watu wengine (kazini) na familia yake.

Tafuta nafasi ya kuzungumza nae ana kwa ana(sio simu wala texts) mueleze jinsi unavyojisikia kutokana na ukosefu wa mawasiliano(ya ana kwa ana).

Mwambie, Mapenzi pekee hayatoshi kuimarisha Uhusiano wetu, isipokuwa mawasiliano ya mara kwa mara na kutumia muda kuwa pamoja na kuzungumzia masuala ya kimaisha.


Ongezea, sio tu kwamba huwa nakosa amani kwa kutokuonana kwa muda mrefu, pia huwa na wasiwasi kama kweli unanipenda kama ninavyokupenda.

Endelea, mapenzi yangu kwako huongezeka kila tunapokuwa pamoja hata kama ni kwa Sekunde 60(Saa moja).

Malizia...naomba tuboreshe mawasiliano ya simu na ya kuonana ana kwa ana ili kuimarisha uhusiano wetu.

Majibu yake, kujitetea kwake au maelezo yake yatakufanya ujue umesimama wapi....

Kila la kheri.

Mapendo tele kwako...

Sunday

Mume wangu anichukia, anikana nifanyeje?

"Habari za kazi dada. Nimevutiwa sana na Blog yako. Mimi ni Mama wa miaka30 nimeolewa miaka miwili iliyopita na tumejaaliwa Mtoto mmoja. Mume wangu ni mtumishi mkubwa Serikalini.

Tatizo nililonalo dada na wadau wote ni kwamba Mume wangu nimetoka nae toka shule, kwenye mapenzi yetu hakuwahi kuninunulia hata chips!

Sikujali kabisa kwani nilielewa ni Dent baada ya muda nilishika mimba na nilipomueleza hakujibu kitu na akanitoroka kitu kilichopelekea kukosa kote Shule na Boyfrend.

Baadaye, zaidi ya miaka mitatu akantafuta na kuniomba msamaha kuwa ni kwasababu ya mazingira alokuwanayo akaogopa nakunikimbia. Nilimsamehe kwavile nilimpenda toka moyoni.


Kwajuhudi zangu binafsi nilikazana sana na shule hadi aliponitafuta nilikuwa Form6 na yeye akiwa chuo mwaka wa tatu lakini nilikuja kuhisi ubinafsi wake hapo kwani sikuwahi kupewa japo Kadi ingawa Chuo huwa tunapewa boom.

Nilifanikiwa kupata nafasi UDSMd nikamaliza vizuri. Mpenzi wangu huyo aliniomba kwa machozi anioe, nilimzungusha kwa miaka kadhaa then nikakubali.

Toka tumeoana ni vituko ndani ya nyumba, mara anisimange, mara nimfumanie na wanawake wakifanya starehe na kunikataa kuwa mie sio mkewe. Mara anifukuze kwa kudai namng'ang'ania anasema alikosea kunioa ili mradi tu ni manyanyaso.

Hanihudumii kwa chochote kile yaani sigusi gari lake, biashara zake wala hela zake. Hakai na document yoyote ndani anampa mama yake nazingine anaficha ofisini.


Amejenga nyumba kadhaa kwa siri, amenunua viwanja vingi tu hapa dar kwa siri, account zake ni za siri, miradi yake ananificha nakuja kuambiwa na mahawara zake wakijisifia kwangu.

Kwa kweli inaniumiza kupita kiasi hasa ukizingatia napenda kumtumikia MUNGU wangu lakini yeye hana hofu ya MUNGU. Anawaza ubinafsi, chuki, uchoyo na anataka nimpe mshahara  wangu utumike nyumbani wakati yeye hajui wala kuhusika na mahitaji yangu.

Chaajabu nakuta anawatumia pesa wanawake wengine, mwingine anamwomba ampe gari, anawanunulia gold wakati mimi niliyemvumilia hata mia yake siioni!!

Hivi juzi kanunua Simu ya Milioni 1.5 wakati mie kisimu nachotumia Mungu anajua. Nimemuomba nikasome kanifokea kama mtoto!


Ndugu zangu anawachukia kuliko kawaida ila wake ndio anataka waje tukae nao. Jamani wapendwa nisaidieni, kama vikao tumeshakaa x3 anaomba msamaha na kuahidi kutorudia lakini wazazi na Wachungaji wakiondoka nakiona cha moto.

Ndoa nilofunga ni ya kikristo nami ni mdada mzuri sio najisifia bure hapana, msomi na mcha MUNGU siwezi kumsaliti ingawa natongozwa sana.

Mtoto wangu ndio kwanza ana mwaka lakini nimechoka. Nisaidieni ushauri jamani wapendwa".

**************

Dinah anasema: Habari ni njema sana, Heri ya Mwaka mpya na ahsante kwa ushirikiano.

Natambua kuwa baadhi ya Watumishi wa Serikalini Ndoa kwao ni "status" kwamba hulazimika kuoa kwa ajili ya nafasi zao za kazi (waijua ile kama huna Mke huwezi kuwa Rais sort of thing), sasa baadhi hufunga ndoa na yeyote anaepatikana kwa wakati huo ambae ana ka-historia nae.

Wengi huepuka kuibua mtu mpya na kufunga nae ndoa haraka, hivyo huamua kurudi nyuma na kuangalia nani "anafaa" na sio anampenda.


Sasa kutokana na maelezo yako nahisi kuwa wewe ni "victim" wa "ndoa kwa status" kwake na sio Mapenzi.

Huyo Baba hakuwa na mapenzi kwako na kithibitisho ni pale alipokukimbia baada ya kumuambia kuwa umeshika Mimba pia kitendo cha kutoonyesha hisia zake za mapenzi kwako kwa-mf. kukununulia zawadi (siamini katika kumtegemea mwanaume lakini naamini kuwa mwanamke anatunzwa/tunukiwa Zawadi kama sehemu ya mapenzi).


Ikiwa mumeo anakukataa/kana mbele za wanawake wengine kuwa wewe sio mkewe ni wazi kuwa wewe sio Mkewe. Kumiliki Cheti cha Ndoa kinachothibitisha Muungano wenu sio Tija ikiwa haumo Moyoni mwake na hashirikiani na wewe kwenye masuala ya kimaisha na kifamilia..

Sina hakika kwanini bado unaendelea kuwemo kwenye Muungano huo, natumaini kuwa Ukristo wako na Kumuamini Mungu kwako sio Kigezo cha kuvumilia visivyovumilika.


Angalia utaratibu wa kumtaliki kupitia Mahakama (Kisheria). Nenda kawaone Wanawake Wanasheria kwa ushauri zaidi wa wapi pa kuanzia na kwa ajili ya kupata "mafao" yaliyochumwa mkiwa kwenye Ndoa na matunzo ya Mtoto wenu.

Hata kama hakushirikishi kwenye Mipango ya maendeleo na Documents anaficha kwa mama'ke bado Kisheria unahaki ya kupata Mgao kwani yote hayo yamepatikana ukiwa kwenye ndoa.

Kama sheria haijabadilishwa, nadhani kuishi na mtu kama mume au Mke kwa miaka 2 Kisheria inachukuliwa kama ndoa hata kama huna Cheti(common law).


Nipo mbali na Tz, hivyo sio rahisi kwangu kukuelekeza kwenye Vikundi vingine vinavyosaidia Wanawake Kisheria.


Natumai wachangiaji wengine wanaweza kusaidia kwenye hilo na pia kukupa ushauri tofauti na wangu ili upate kufungua mawazo na kufanya uamuzi wa Busara.


Kuwa Imara, seek furaha maishani mwako, usikubali kuwa Mtumwa wa "ndoa" ambayo haina faida kwako.


Kila lililo jema.

Mapendo tele kwako...

Pages