Tuesday

Nampenda ila ni Kicheche, nimtulizeje?

Habari Dada, 27 ni umri wangu, Mwaka 2010 nilianza mahusiano na binti mmoja akiwa Form 3 mwenye umri wa miaka 17. Nilimpenda sana tangu the first day namuona, kipindi hicho nilikuwa College. Kimaisha kwao hali si nzuri, kutokana na mapenzi yangu kwake niliweza kumsaidia Ada.

Kuna wakati hata kuiba chakula home kama Mchele, Unga na vitu vingine vingi ili asitaabike. Pia nilimsaidia kimasomo kama kufatilia shuleni kwao ambako nilijifanya ni Kaka'ke. Kutokana na shule kuwa mbali na anapoishi ilibidi ahame na kukaa kwa family friend wao.

Ukweli alikuwa hapendi Shule, kwani mara nyingi maudhurio yake hayakuridhisha. Alifika Form Four ila hakumaliza. Huyu mtu akahama pale alipokuwa akiishi akaenda kwa marafiki zake maeneo flani ya M'nyamala, sikupenda akae maana sifa za huko si nzuri.

Nilimsihi sana Arudi kwao hakutaka hata mzazi(single parent-mama)yake hamsikilizi mpaka leo. Kipindi hicho mimi nikamaliza Chuo. Nikaamua kufuatilia Skuli kwao nikaambiwa amefukuzwa, Baada ya hapo sikujua namna ya kumsaidia maana sikuwa na hela ya Shule ya Private, ninamuonea huruma sana.

Ananilaumu kuwa mimi ndio nimemfanya aache shule maana baada ya kuwa kafukuzwa alikuwa akija home analala hata siku tatu. Wakati huo mimi nilikuwa Jobless so nilichukulia advantage, baada ya muda nikamwambia baadae tuachane ili mimi nitafute kazi. Alilia sana ila baada ya wiki nikamuambia turudiane akakubali na baada ya wiki moja akanitosa na kunitukana matusi sijapata kuona. Nilichanganyikiwa na nililia kama mtoto mdogo hapo tukiwa na mwaka mmoja.

Kwa kweli alikuwa mtu wangu wa karibu sana. Nikapata kazi mkoani ambako nipo mpaka sasa. Nikamtext nikamwambia nimepata kazi mkoa flani nimefanikiwa interview. baada ya Wiki yaani mwezi tangu tuachane akanikpigia simu akidai kuwa mamake anaumwa ananiomba hela kwa huruma nikamtumia via mpesa.

Tukaanza tena mahusiano, ila alikuwa amebadilika sana. Siku nilimkuta na simu ambayo si yake akadai ni ya bf wake wa zamani. Niliongea na yule kijana na aliniambia huyo demu muhuni na anapenda sana kufanyiwa kinyume.

Sikujali nikaendelea nae, siku mmoja aliniomba nimuingilie kinyume na maumbile, hapo ndio nikajua jamaa alisema ukweli lakini sikukataa nilifanya.

Baada ya muda nilimuida aje huku Mkoani nilipopata Kazi ili apaone kwangu, Huku mkoani nilipopata kazi na alikaa miezi minne lakini tulikuwa tukigombana kila siku. Mara atoke mchana arudi saa tisa usiku, analewa, analeta Mashangingi nyumbani kwwangu. Nikamwambia arudi tu kwao ila nilimuonea huruma. Hiyo ilikuwa October mwaka jana, sikujua alipoenda. November nikamuona kwenye baa moja maarufu alikuwa amekaa na Mzee mmoja nikasalimiana nae akaondoka mida hiyo hiyo.

Nachukia mambo yake lakini sijui kanipa nini? Nampenda sana, nikaanza kumtafuta tena ila niliishia kutukanwa tu. December 31 mwaka jana akanipigia na kuanza kuomba turudiane, tukarudiana. Feb 2013 alienda mkoa flani jirani na napoishi na rafiki yake, alivyokuwa akirudi alipitia kwangu baada ya nimemdanganya nimenunulia vitu fulani vya ndani so akakasirika alivyoona sikuwa mkweli, hata hivyo tulitoka.

Siku mbili baada ya birthday yake tukavamiwa na vibaka ambao walitishia kumbaka mbele yangu. Waliiba pochi simu na kila kitu na walituumiza sana. So nikaona kama mkosi au labda ni jamaa alishawahi kuwa nao nilipoachana nae wametufanyia revenge.

Kaondoka Wiki iliyopita na sasa hanitaki tena. ILA NASHANGAA SIJUI KWA NINI MIMI HUUMIA SANA KULIKO YEYE. Alishawahi nishika na wanawake nje ila nahisi (sina uhakika lakini )yeye ni malaya zaidi coz kwao hawajali anaishi wapi. Nampenda nifanyeje?lengo atulie nimuoe ila elimu hana na hataki kusoma. Nifanyeje, nifanyeje?


Dinah anasema: Kaka mapenzi matamu lakini yanaumiza. Nashukuru kwa kuelezea Hadithi yote kwa kina lakini jibu lake ni fupi sana.
Huyo Binti ni bado ni Mtoto (hajakuwa kiakili), anatumia matatizo ya kifedha kwenye familia yake kama tiketi ya kutangatanga na Dunia. Inasikitisha lakini ndio amechangua mtindo huo wa Maisha.

Pia inaelekea anakutumia kiuchumi lakini hana mapenzi na wewe. Mambo ya kuachana na kurudiana kila baada ya Wiki mbili ni kupotezeana mida tu.

Futa mawasiliano yake na acha kumtafuta tena. Songa mbele, weka maisha yako sawa.
Muda ukifika utakutana na Binti mwenye tabia njema na atakae kupenda zaidi ya unavyompenda au kama unavyo Mpenda.

Hakikisha umeangalia afya yako(Kapime) ili uanze maisha mapya ukiwa unajua ulipo(Status) yako.
Wachangiaji wengine wataongezea....


Kila la kheri. Mapendo tele kwako!!

Monday

Simpendi Mume wangu baada ya kutambulisha Mtoto wa nje.

"Dada pamoja na wadau weninge ushauri wenu ni muhimu kwangu. Mimi nina miaka 22, nimeolewa miaka miwili sasa. Tatizo ni kuwa simpendi hata kidogo mume wangu.

Siku za mwanzo tulivyokutana hakuniambia kuwa ana mtoto. Baada ya wiki mbili akaniambia ana mtoto tangu hapo mapenzi yakapotea sikuwa na haja ya mwanaume wa namna hiyo kwani sipendi watoto wa nje hata kama nimemkuta.

Nimejitahidi labda nitampenda lakini mpaka leo wapi, sioni hata dalili sijui hata nifanyeje na nipo kwenye ndoa nitaachana nae vipi au nifanyeje? Asanteni jamani kiroho safi"


Dinah anasema: Pole kwa unayokabiliana nayo, mimi binafsi sipendi watoto wa nje ya ndoa au kabla ya ndoa ( wa ujana) lakini kutokana na maisha tunayoishi hivi sasa ni nadra sana kukutana na kijana wa miaka 25-32 ambae hana mtoto....wengi wanazaa iwe kwa uzembe na kutojali, kutegeshewa (PMU) au kusingiziwa.    

Sidhani kama humpendi mumeo, nadhani unahasira nae kwa vile unahisi amekudanganya, hilo moja.  Pili, ni hofu uliyonayo kuhusiana na hisia zake juu ya Mwanamke aliezaa nae na labda usumbufu utakao upata kutoka kwa mwanamke huyo hapo baadae.    

Baadhi ya watu wanaweza kudhani kuwa una roho mbaya lakini ni ukweli usioepukika kuwa kunapokuwa na Mwanamke mwenye mtoto lakini mpenzi wako hasemi mpaka baada ya kufunga ndoa....inakusanya maswali mengi yanayojenga hasira kuu.    

Kutokana na maelezo yako umegusia kuwa hupendi watoto wa nje, inawezekana kabisa umewahi kuliweka hilo wazi kwa Mume kabla ya ndoa hali iliyopelekea yeye kuogopa kukuambia kuwa anamtoto akihofia utamuacha.    

Maswali muhimu unayopaswa kumuuliza mumeo ambayo yanaweza kukusaidia kumsamehe, kujiwekea "sheria", kuanza upya na kusonga mbele na maisha yenu.    

1)-Hisia zake kwa Ex wake (mama wa mtoto) na je mtoto alizaliwa kwenye mazingira gani (ndoa, uhusiano kabla ya ndoa au usiku mmoja aka bahati mbaya).  

2)-Mtoto anaumri gani? anaishi wapi? na nani?  

3)-Je! kuna mawasiliano yeyote kati yao?     Jinsi atakavyokujibu ndivyo itakavyokusaidia kusonga mbele (unaweza kurudi kwangu kwa ushauri zaidi ukipata majibu ambayo ni tata kwako).  

Pia majibu ya mumeo kwa mswali hayo yatanisaidia mimi na Wachangiaji wengine(perhaps) kukuelekeza namna ya kuweka sheria ili mtoto aendelee kuwasilina na Baba yake (hana makosa) lakini  wakati huohuo Ex wa mumeo (mama mtoto) akae mbali na ndoa/familia yenu mtakayoianzisha.   

**Alafu mwenyewe mdogo masikini...anyway! Nakutakia kila la kheri,
Mapendo tele.....    

Saturday

Aisee! Nimerudi, Nilikuwa Busy making babies....

Haa! Asikuambie mtu....ukitaka kujua utamu wa ku-make babies panga. Yaani wewe na mwenza wako mnajua kabisa bao litakalopatikana  leo linaenda tengeneza Mtoto. Basi ile "thought" ya  "vimelea" vinaenda kuungana na Yai na kutengeneza Mwanadamu inakuongezea amani, utulivu, Mahaba na mapenzi.

Nadhani ni tofauti na ile ya kushitukizia, kwamba mnafanya tu kila siku bila Kinga....alafu hujui kama mimba imetunga au la!...well ningejaribu hiyo lakini nadhani tumemaliza KUZAA*.


Anyway, Asanteni wote kwa Ushirikiano, mmekuwa mkitembelea na kunitumia maswali, maoni na salamu bila kuchoka. Sikutegemea kuendelea kupata watembeleaji kati ya 2,000-7,000 kwa siku....ukizingatia Blog haikuwa "active". Hakika najua ikiwa "active" nitarudi kwenye 100,000+. Mungu awabariki sana kwa Upendo na Ushirikiano wenu kwangu.


Kuwa mama/mzazi ni jambo jema na baraka lakini pia ni kazi ngumu sana na inachukua muda wako mwingi (vingine vinakuwa havina maana isipokuwa mtoto/watoto). Natambua wengi mnalijua hilo lakini mimi ndio kwanza najifunza au niseme napata uzoefu mpya.


Pamoja na kuwa ni busy mam-astic(hehehehe) kwa wanangu, nitajitahidi sana sana kuwaletea mambo/uzoefu mpya wa kimapenzi, mahusiano na ngono(kama ilivyokuwa awali) sitotumbukizia masuala ya watoto.


Kuwa mzazi au kuwa na watoto ni Baraka ya Ndoa/Matunda ya uhusiano, haipaswi kutufanya tusahau kuwa sisi ni Wapenzi, hivyo basi nitaendelea kuwa nawe sambamba tukielimishana, kumbushana, ambizana na kuelekezana ili sote tufurahi katika Ulimwengu huu Mtamu.

Nasikitika tu kuwa sitoweza kujibu Maswali ya nyuma, nitajitahidi kujibu yaliyoingia kuanzia wiki iliyopita. Samahni kwa usumbufu.

Endelea  kuwa nami na asante kwa Ushirikiano.

Mapendo tele kwako...

Pages