Tuesday

Simjui mwenye Mimba!

Dada Pole na Majukumu, 

Sorry kwa yaliyo nikuta kwani unaweza kuona kama sina heshima kama mtoto wa kike.

Ni hivi nilikua na mpenzi wangu kwa mwaka mzima ila akawa hana mpango wa kunioa nikaanza kufanya mpango nipate mtu ambaye anaweza kujenga familia na yeye.

Kilichofuata sikumwacha mpenzi wangu wa zamani nikawa nadate na wote, sasa nimepata UJAUZITO na sijajua ni wa nani kabisa nachanganyikiwa sana.

Kwani nilipata Hedhi tarehe 10.12.2013, ndiyo ilikua mwisho wa kwenda hedhi. Ila tarehe 21,12,2013 nililala na kitu kipya hadi Asubuhi.

Nikarejea 22 kwetu. Tarehere 24 mkesha wa Xmas nikakesha na wa zamani hadi Asubuhi, najua ni tabia mbaya ila ilibidi kwa sababu mpenzi wangu wa zamani aling'anga'nia nikesha nae.


Sasa January sikuona siku zangu nilipo pima ni mjamzito. Je hapo nani anaweza kuwa ndiye mwenye mtoto.

Nimewaza sana nimekosa jibu sasa nina ujauzito wa miezi miwili.

Naomba ushauri.

**********************

Dinah anasema: ahsante, ila ungekuwa karibu ningekuchapa viboko za miguuni akyanani vile. Khaa! Kuna wanawake wa Bongo mnaujasili wa ajabu na wa kijinga....unaMix wanaume na kwa USHENZI hutumii Kinga!!


Kama ni miezi miwili na ushehe yaani Wiki 9 na siku fulani ni ya huyo Mpya na kama ni miezi Miwili kamili au na siku kadhaa ni ya huyo wa zamani.

Hayo ni mahesabu ya haraka haraka ili kujua mahesabu halisi ni vema kama ungenipatia Mzunguuko wako wa Hedhi je ni wa kawaida, Mrefu, Mfupi au unabadilika kila mwezi.

Hii itasaidia kujua ni tarehe gani kati ya 21-22 au kabla na 24-25 ni lini ulikuwa umepevusha yai....

Mbegu za Mwanaume hukaa ndani kwa muda wa Masaa 72 mpaka Wiki moja, inategemea na ubora/afya za Manii husika.

Sasa kwa vile uliwachanganya itakuwa. Ngumu sana kujua unae share nae Mimba ni nani kwani hatujui "speed" na ubora wa Mbengu za wa kwanza au wa pili kufanya nae ngono.

Mbaya zaidi umewachanganya ndani ya siku chache kati yao.....kwanini usitumie CONDOM jamaniii (*hitting my table*).


Anyway, pole...piga mahesabu tena ili ujue ukaribu wa tarehe za kupevuka na tarehe za kushika Mimba halafu ukifikisha miezi 3 umjulishe unaedhani ndio Mwenyewe, hilo moja.


Pili waambie wote, atakae kubali ndio huyo kwa kipindi hiki cha ujauzito na atakaekataa ndio hivyo tena.


Mtoto akizaliwa fanya utaratibu wa DNA test najua Bongo kwenye Hospitali kubwa Binafsi wanatoa huduma hii.

Vipimo hivyo vitasaidia kujua ukweli halisi na kumpa haki Baba wa mtoto na mtoto husika ikiwa unaamua kuendelea na Ujauzito huo.


Tuone wengine watakushauri nini?

Mapendo tele kwako...

Saturday

A-demand tuachane mara kwa mara!

Habari dada....

Nipo kwenye mahusiano kwa muda wa miezi minne sasa, lakini kila tunapogombana mwenzangu ana'demand tuachane.







Nikijitahidi kuongea nae anasema anataka kua peke ake. Tatizo ananipenda na mie nampenda pia ....na leo hii ndio kanikazia kweli anataka tuachane.







Kinachosikitisha tuanaachana bado

tunapendana na hakuna sababu ya msingi ya sisi kuachana.... So hii

hali inamaanisha nini....???





********************



Dinah anasema: Habari ni njema, nashukuru. Kwani wewe na huyo Binti mnaumri gani?





Alafu huwa mnagombana kuhusu nini hasa? Maana jambo laweza kuwa dogo lakini kwa mwenzio ni kubwa.







Miezi minne ni michache sana ku-declare "Uhusiano" unless otherwise huwa mnaonana kila siku ya Mungu au mnaishi pamoja.







Tuseme mmekuwa mkitoka (date) kwa miezi minne, inawezekana anakupenda ile ya ku-like na sio ya ku-Love hivyo hayupo tayari kuwa serious yaani kuwa kwenye UHUSIANO na wewe.









Vilevile Miezi hiyo 4 ni michache sana kuwa mnagombana-gombana.







Huenda mwenzio anataka kufurahia uanamke wake kwanza baada ya kutoka kuwa Binti wa fulani, anataka kuwa mwanamke mwenye maamuzi yake na uhuru wa kufanya atakalo alafu baadae ndio a-settle na kuwa serious kwenye uhusiano, hilo Moja.









Pili, kama Binti ni wakubwa kiasi say 25-29 basi nitasema "anatikisa kiberiti" ili kuona reaction yako je? Utambembeleza? Utamhakikishia kuwa unampenda kiasi gani na kumahidi er... pengine Ndoa hapo baadae.









Tatu, pengine ni Homono tu, unajua baadhi ya wanawake huwa zinawasumbua sana hasa wakikaribia Hedhi huwa na hasira/mkali, anachukia kila kitu/mtu n.k.







Nne, inawezekana kabisa ni utoto tu unamsumbua....





Nyongeza: Issue ya kuaminiana kwenye kutoka/mahusiano imekuwa pana na tata siku hizi kutokana na mitandao ya Kijamii.





Tuone wengine watakuambia nini....

Mapendo tele kwako...

Wednesday

Wife kapoteza Mojo baada ya Uzazi!

Habari dada Dinah, mimi ni msomaji na mfuatiliaji wa siku nyingi wa
blog yako!

Hakika unatoa elima endelevu kwa watu mahsusi. Dada Dinah ni takriban miezi 8 tangu Mwenyezi Mungu atujalie na
kutupatia zawadi ya mtoto kidume (kiume) mwenye umri wa miezi nane (8)
sasa.

Kila nikijaribu kumchezeshea na kujaribu kuamsha hisia zake
yaani hakuna response yoyote na haoneshi dalili zozote za kuhitaji
kupeana tendo la Ndoa.

Yawezekana ndivyo ilivyo kwa mama mzazi anayenyonyesha na kwa kuwa ndio mara yangu ya kwanza naingia kwenye Ndoa pengine ni hali ya kawaida waweza kunisaidia katika hili.


Mke wangu hajisikii kufanya tendo la ndoa na zaidi hajapata siku zake
tangu alipojifungua hadi hii leo miezi nana na ushee....!

Alishapima mara kadha wa kadha kujua labda kuna mimba au la, kwa kweli hana mimba.

Tumejaribu kumwona Dokta naye hajatupa sababu zaidi ya kutuambia ni uwezekano wa mabadiliko ya diet na hali ya hewa. Pengine unaweza kunisaidia zaidi labda utueleze tatizo hili linatokana na nini?

Mtoto wetu ni wa kwanza na katika ujana wake hajawi kushika mimba. Mimi nilihisi labda kuna tatizo huko ujajani kama kuna chochote huko nyuma labda liliwahi kutokea! Kwa maelezo hakuna!

Tunaomba msaada wako.


***************


Dinah anasema: Huyo Dakari nae eti hali ya hewa na Diet wakati mtu katoka kujifungua.....afukuzwe kazi khaa!


Hiyo ni hali huwatokea wanawake wengi baada ya kujifungua inaweza kuondoka baada ya miezi mitatu mpaka Mwaka, inategemea na mwanamke husika maana wanawake tumetofautiana.

Kuna sababu nyingi ambazo zinaweza kumfanya mwanamke apoteze hamu ya kufanya mapenzi ila kuu ni UCHOVU siku zile za mwanzo (unaruhusiwa kufanya ngono baada ya Wiki sita a.k.a 40 tangu kujifungua kiasili).


Hebu pitia topic hii


http://dinahicious.blogspot.co.uk/2008/10/ngono-baada-ya-kujifunguazaa-kiasiliii.html?m=1


Ili niweze kuelewa tatizo liko wapi ni vema kama Mkeo akanieleza mwenyewe kama mwanamke ili niweze kumpa mbinu za kurudisha Mojo.


Maana kuna wakati mtu unahisi kama vile umepoteza "ze mojo" ya kunanihii kumbe ni Uchovu + Mapenzi kwa mtoto = Baba take back seat.


Kuhusu Hedhi ni kawaida kwa Mama anaenyonyesha kutopata Hedhi mpaka atakapo anza kumuachisha mtoto kunyonya.


Kila la kheri.

Mapendo tele kwako...

Tuesday

Mimi ni mwanamke wa age 28 nimekuwa kwenye mahusiano miaka sita sasa. Nilikutana na kaka mmoja nikiwa chuo miaka sita iliyopita tukawa wapenzi na  aliniahidi kuwa tutaoana bahati mbaya tukapeana mimba kabla nikajifungua mtoto wakike sasa hivi anamiaka 5.

Katika mahusiano kumekuwa na ups and downs nyingi katika miaka yote nilikuwa namsisitiza atoe Mahari lakini wapi but mwaka juzi ndio alienda kujitambulisha rasmi na Mahari akatoa akaahidi tutafunga ndoa baada ya miezi tisa toka alipotoa Mahari. 

Lakini sasa umepita mwaka na ushee hamna kitu, kila nikimwambia ananiambia gharama ngoja nijipange.


Nikimshauri tufanye simple basi hataki na Kanisani kwenyewe kituo cha polisi sasa namuuliza hiyo ndoa tutafungia wapi kama Kanisani hauendi?


Mimi naenda ila ni dhehebu tofauti. Kinachoniumiza ni hivi sasa nina Ujauzito wa pili lakini mwenzangu ndio kazidi kubadilika nimemshika na sms za mapenzi mara tatu.

Ukifungua whatssap yake ndio utalia ni wanashushana kwa sms na video clips lakini namuona mwenzangu haoneshi mshituko kuwa amekosea. 

Mara ya kwanza aliniomba msamaha sana ila wakarudiana tena nimekuta sms tena za mwanamke mwingine nikachukua simu nikampigia huyo mwanamke cha ajabu na kipigo nikapigwa.

Sasa hivi ananiambia wameshaachana lakini bado huyo mwanamke huyo anapiga simu kwake nimetafuta njia yoyote ile ya kuiblock hiyo namba ya mwanamke lakini mwenzangu haoneshi ushirikiano anachukulia simple tu.

Imefikia  hatua wakiwa wanawasiliana anajirekodi kabisa, nimeona juzi nimeumia sana ili hali sasa ivi nina Mimba ya miezi saba.


Kila nikimuuliza ananiambia nimeshaachana naye. Huu ni mwaka wa tatu toka tumepata ajira yeye na mimi wote tunafanya kazi ila mie nipo Wilayani yeye Mkoani hivyo tupo mbali kidogo ingawa najitahidi kila weekend naenda lakini bado akaniambia hayo yote yanasababishwa na me kuwa mbali hivyo niwe naye karibu muda wote.


Sasa hapa nilipo sielewi niache kazi nimfuate ndio itakuwa suluhu au basi tuaachane tu nianzishe maisha mapya?


Najitahidi sana kumfanyia mazuri kumpa suprise kama zawadi mbalimbali lakini ndio hivo .


Kwa upande wa mapenzi ananipa vizuri kabisa tena bila kinyongo na huwa ananisifia sana pia kwa upande wangu kwani yeye ndiye aliyeniingiza kwenye Ulimwengu huu kwani mwanzoni nilikuwa mgeni sana maumivu kila tendo.


Hiyo yote ilikuwa kwasababu ya ubikira lakini siku hizi ameappriciate nafurahia naye nayeye anafurahia but tatizo ni hilo hapo juu sijui nimemkosea wapi.

Naomba ushauri wako mapema sana kwani nipo kwenye lindi kubwa sana la mawazo.

Asante

*****************************

Dinah anasema: Pole sana kwa yote unayokabiliana nayo. Kwanza kabisa USITHUBUTU KUACHA KAZI KUMFUATA huyo mwanaume...kamwe kamwe I beg you!


Humuhitaji Mwanaume bali Unamtaka mwanaume maishani mwako ili kukuongezea au kukupa furaha, kukupa ushirikiano, kusaidiana, kushauriana na pengine kuanzisha familia na kuitunza.

Kutokana na maelezo yako inaonyesha kuwa wewe ni Mwanamke unaejiamini ila Miaka sita ya uhusiano wenu na yeye kuwa mwanaume wako wa kwanza ndio vinavyokufanya uendelee kuvumilia visivyovumilika.

Mwanaume hana Mapenzi ya kweli, hana Utu, hana Huruma wala Shukurani, iweje wewe ufanye yote hayo kwa ajili yake....mpaka kumsamehe alipokusaliti na kukupiga na bado anataka uache kazi kwa ajili yake!!


Hajasema wazi kuwa Uache kazi lakini aliposema uwe karibu nae inamaana hiyo, acha kazi unde huko aliko.


Kuachana/Talaka sio kitu ambacho huwa napenda kushauri, lakini kutokana na matendo ya huyu Bwana (Cheating haisaameheki kwangu) hakika nitakushauri uchukue hatua hiyo.

Hapo hajafunga ndoa na wewe hakuthamini wala kujali hisia zako, sasa "akimilikishwa" Kisheria si ndio utakoma kabisa!


Mmekutana wewe ukiwa na miaka 22, sina hakika na umri wake ila nahisi alikuwa Chini ya miaka 30....katika umri huu wanaume wengi huwa hawajatulia kichwani, hawako tayari kuoa japo wanadhani kuwa wapo tayari.


Huenda alidhani amekupenda lakini baadae(baada ya kukua, akagundua kuwa hakukupenda kivile bali alikutamani tu).


Wewe ulimpenda na huenda uliamini unapendwa au utapendwa zaidi kwa vile amekukuta Bikira (kiuweli hii haiongezi mapenzi zaidi ya kufurahisha Ego ya mwanaume).


Ikiwa mwanaume huyo ameshindwa kubadilika ndani ya Miaka mitatu tangu umsamehe ni wazi kuwa hatobadilika daima na utaishia maisha ya taabu kihisia.


Kabla ya uamuzi wowote Jiulize maswali haya:-

Nini muhimu katika Maisha yako? Kuolewa na huyo mwanaume na kuendelea kuishi maisha yaliyojawa na Hofu, huzuni, maumivu ya hisia na mawazo?


Au Kuishi kwa amani na furaha ukiwa peke yako na watoto wako?

Kumbuka happy mummy, happy kids. Lolote utakalo amua hakikisha watoto wanakuwa na uhusiano mzuri na Baba yao.


Tuone wengine watakushari nini....

Kila la kheri!

Mapendo tele kwako...

Monday

Je Mwanamke yupo kwa ajili ya kupendwa?

Nimepitia blog yako imenifundisha mengi keep it up! Unasaidia jamii kwa kweli ktk masuala ya ndoa.


Mi ninakijiswali kidogo je mwanamke anapenda au yeye yupo kwa ajili ya kupendwa tu?

*********************

Dinah anasema: Ndio mwanamke anapenda kama ambavyo mwanaume anapenda, tofauti ipo kwenye kutongoza....mwanamke hatongozi kama wanaume wanavyotongoza.

Mwanamke akikupenda anaweza kutumia njia tofauti "kukutongoza" badala ya kukuambia moja kwa moja.


Kumbuka Mwanamke anawindwa, Mwanaume anawinda, hivyo sio "natural" Mwanamke kumtokea Mwanaume na kumtongoza lakini mapenzi yakimzidi juu ya mwanaume hutumia njia nyingine kushawishi ili mwanaume husika amtongoze (aanzishe)....

Njia hizo ni:

-Kujichekesha kila akikuona.

- Kujipitisha mbele yako mara kwa mara.


-Kukuangalia kwa wizi/haiba.

-Kukusalimia.

-Kuwa mwema kwako.

-Kutokezea mahali unapopenda kuwepo mara kwa mara.

-Kuongeza maringo akikuona....N.k


2) -Je akipenda anachukua hatua gani?

*************************

Dinah anasema: Anachukua hatua hizo hapo juu....

3) -Kwanini Upendo wake hadi alazimishwe ndio apende, je hawezi penda mwenyewe?

**************

Dinah anasema: Upendo wa Mwanamke kwa mwanaume haulazimishwi, inategemea kama anakupenda kabla hujamtokea.....

Kumbuka upendo takes time na unahitaji kumjua mtu vema, angalau kwa mwezi hivi only kama mnakutana kila siku, vinginevyo kuanzia miezi sita.

Huwezi muona tu mtu ukasema unampenda bali unapendezwa nae au unavutiwa na ungependa kuwa nae ili mjuane vema.


Mwanamke ni tofauti na mwanaume, unapomtokea na kumtongoza mara nyingi atahitaji muda.


Ni mara chache sana mwanamke anakubali haraka haraka, hata kama alikuwa anakupenda kabla hujamtokea bado hatokubali hapo hapo.


Mwanaume kama Muwindaji inabidi uongeze bidii ya kumfuatilia na kumshawishi ili akubali kuwa kweli unania ya kutaka kuwa nae au kuanzisha uhusiano nae.

Jinsi unavyo ongeza bidii kumfuatilia (kwa maana ya kumsalimia, kuongea nae kuhusu hisia zako kwake, kupiga stori nakadhalika) ndivyo ambayo mwanamke huyo ataanza kuvutiwa nawe na hatimae kuanza kukupenda.


Kama hakupendi utaona dalili moja kwa moja kuwa haupo akilini mwake....kama haupo akilini (Kuvutiwa) basi ni ngumu kuingia Moyoni mwake (Kupenda).

Mwanamke hubembelezwa, mwanamke halazimishwi...

Kila la kheri!

Mapendo tele kwako...

Wednesday

Kuasili Mtoto/Watoto

Habari gani Dada Dinah!



Mimi ni Mwanaume mwenye umri wa miaka 40, nimekua kwenye maisha ya Ndoa na mke wangu kwa miaka 12 sasa lakini hatujabahatika kupata Mtoto. Tatizo kubwa lipo upande wa Mke wangu kwani anashika Mimba vizuri tu lakini baada ya Muda uharibika.



Tatizo hilo limeanza tangu mwaka wa pili wa ndoa yetu tulipoamua kuanzisha familia. Tumekwisha poteza mimba nyingi mpaka ikafikia mahali mimi nikagoma kuendelea kujaribu kutokana na huruma kwa Mke wangu. Lakini mke wangu alionyesha kutojali na anasisitiza tuendelee kujaribu na siku moja mimba itakuwa vizuri na tutapata watoto wetu.



Dada mie nimechoka kiakili, kihisia na umri wangu unakwenda, nikamshauri kuwa tujaribu Adoption. Mke wangu akakataa kata kata akisisitiza tuendelee kujaribu tutafanikiwa.



Sielewi kwanini mwenzangu anang'ang'ania tuendelee wakati yeye ndio anaetaabika Kimwili!! Naomba ushauri, nifanye nini ili nimshawishi Mke wangu akubali kuadopt?


Asante Dada.
******************************* 




Dinah anasema: Poleni sana kwa tatizo mnalokabiliana nalo, tatizo hili ni sensitive sana, huwa nakimbia kulizungumzia kwani nahofia kuumiza hisia za waathirika.  Mimba/Mtoto ni jambo la Neema kwa Wanandoa kwavile "tumeaminishwa" kuwa ndoa ni mwanzo mzuri wa kuanzisha familia Bora, hivyo tunapofunga ndoa mara zote kinachofuata ni Mtoto/Watoto (kwa baadhi).



Ukiachilia mbali hilo pia kuna Pressure kwenye jamii na familia kwa Mwanamke kuzaa, kwamba Wanawake wengi Tanzania "wamejiaminisha" kuwa kuzaa ndio "UANAMKE"...."huwezi kuwa mwanamke kamili kama hujazaa"...."Mwanamke ameumbwa kuzaa".



Sasa wanawake wengi hufanya kila njia ili kuthibitisha kuwa wao ni "kamili", wengine hupitiliza na kubeba Mimba za Uongo(kuigiza) ili tu ionekane na wao walishika mimba hivyo ni "kamili".



 Hivyo nahisi ameng'ang'ania kuendelea kujaribu kwa sababu hizo hapo juu. Katika hali halisi uanamke sio Mimba wala Kuzaa, na kuzaa sio Mafanikio ya mwanamke kimaisha.



Kuna mengi mwanamke anaweza kufanya kuthibitisha kuwa yeye ni kamili na kafanikiwa. Unaweza usizae kutokana na Matatizo lakini uka-Asili (Adopt) kichanga na kumkuza, kumtunza, kumpenda na kumtimizia mahitaji yake kama watoto wengine katika jamii.



Nadhani Mkeo anahitaji msaada Kisaikolojia, anahitaji uondoa dhana ya "mwanamke kaumbwa kuzaa" na kukubali kuwa kama wanandoa mnatatizo na tatizo lenu halitoi guarantee kuwa siku moja litatoweka na litawapa watoto.



Zungumza nae tena kwa Upendo na umuambie kuwa pamoja na kuasili Mtoto mtaendelea kujaribu tena mara Kichanga wenu (mtakae asili) akifikia umri fulani....labda mwaka na nusu au miaka miwili na mkifanikiwa mtakuwa na watoto wawili badala ya mmoja.
 



Mhakikishie kuwa tatizo lenu halipunguzi mapenzi yako kwake, unampenda na utaendelea kumpenda akiwa mama wa watoto wenu wote iwe ni wa damu au wa kuasiliwa. Ukiona analeta mizinguo na kutumbukizia "emotions", ongeza Mkwara lakini kwa upole na upendo.....



Chomekea Mkwara kwa kusema....usingependa kupoteza miaka 10 ya mapenzi na ndoa yenu na usingependa mpoteza bahati ya kulea na kupenda mtoto wa kuasili mkiwa kama mke na Mume.

Mpe muda, usirudie issue hii mpaka mwenyewe ailete tena Mezani, natumaini akiirudisha itakuwa CHANYA.


Nawatakia kila la kheri kwa yote mawili.
Mapendo tele kwako...

Pages