Monday

Mpenzi aninyanyasa kisa Umasikini, sasa ataka ndoa, je atabadilika?

"Habari dada Dinah, Mimi ni msomaji mkubwa wa Blog yako na ninapenda Posti kwani zimetusaidia wengi. Mimi ni mwanamke wa miaka 23 natokea Mkoani Tanga lakini kwa sasa naishai Zanzibar na mpenzi wangu alienichukua nyumbani.

Ninamshukuru Mungu kwani mpenzi wangu ananijali na kunitimizia mahitaji yangu ikiwemo na kuwasaidia wazee wangu nyumbani. Lakini huyu mpenzi anasema kwa kila mtu alie karibu nae kuwa kwetu ni masikini na sote tunamtegemea yeye. Hali hii huzidi hasa tukiwa na ugomvi.

Nimewahi kumwambia mara kadhaa kwamba sipendi tabia yake hiyo, lakini bado hana dalili yeyote ya kuachana na tabia hiyo. Ikitokea ananigombeza basi huwatusi mpaka wazee wangu jambo ambalo hunitia uchungu sana.

Zaidi ya yote anasema hafurahii sana ladha ya tendo la ndoa kwa hiyo anataka tufanye kinyume na maumbile, kitu ambacho mie siwezi kuthubutu kukifanya.

Kwa bahatimbaya au nzuri nimekutana na Kaka mmoja Mzanzibari ambae anadai kuwa ananipenda sana na yupo tayari kufunga ndoa nami nikamwambia kuwa ninampenda lakini kuna mtu ninaishi nae.

Kusema ukweli ninampenda huyu Mkaka niliekutana nae, aliomba akanitambulishe kwao lakini mimi nikamuomba akanitabulishe kama rafiki kwani sikutaka wajue kutambulishwa kama mpenzi wakati niko kwenye uhusiano na mtu mwingine japo sina amani.Familia yake walionyesha kunipenda.

Tatizo linalonisumbua ni kuwa huyu mpenzi ninaeishi nae ametangaza ndoa, lakini mie sitaki kuolewa nae kutokana na tabia zake za kinyanyasaji, sasa sijui nimueleze mama yangu ukweli wa mambo ili nipate mawazo yake au nikubali kuolewa nae kwa kuamini kuwa atabadilika!!

Au nitafute njia ya kuachana nae ili niwe na Kaka wa Kizanzibari alienitambulisha kwao kama rafiki lakini nia yake ni kufunga ndoa nami?

Naombeni ushauri
Asante"

Thursday

Baada ya miaka 2 nimegundua kuwa mimi ni The Other Woman~Nifanyaje?

"Hi Dada Dinah na wachangiaji wengine, asante na pole kwa kazi ya kutushauri maana wadada kilakukicha hatujambo kwa maswali. Mimi ni mwanaama wa miaka 27 mwenye mtoto wa mwaka mmoja. Nimekuwa na uhusiano na Kijana mmoja wa miaka 25 kwa muda wa miaka miwili, sikufichi ananipenda sana na kunijali.Kijana huyu anashughuli zake binafsi kwani amejiajiri.

Sasa kipindi chote hicho tumekuwa pamoja ni hivi karibuni tu ndio nimegundua kuwa kumbe mwenzangu alikuwa na msichana mwingine na wamejuana kwa muda wa miaka 5. Baada ya kugundua tulikorofishana na alikuja kuniomba msamaha na mimi bilakujijua nikakubali na kumsamehe na hii imetoeka mara chache mpaka nahisi kama vile Jamaa ana dawa ya kunifanya nisamehe haraka.

Mpenzi huyu amekwisha enda nyumbani kujitambulisha kwa mama, kiukweli jamaa ananifikisha na kunijali pamoja na mwanangu ingawa hatuishi pamoja. Lakini ninapofikiria kuwa nina mwenzagu huwa nakosa raha na wakati huohuo sielewi huyu jamaa ana nia gani na mimi.

Swali la Kwanza: Unadhani huyu jamaa anampango gani na mimi?

Swali la Pili: Je niendelee kuwa nae au niachane nae?

Kama ni kumuacha nimejaribu mara nyingi lakini kila akirudi nakuniomba msamaha najikuta nasamehe tu, pia anatabia ya kunitumia pesa nyingi kama hana akili nzuri ikiwa nitamchunia.

Naomba mnishauri wana Dinahicious,
Asante."

Sunday

Ushuhuda: Asanteni kwa Ushauri!

"Hi da Dinah na wanablog wanzangu, nimewahi kuja na swali “"Ex ananirudisha nyuma kihisia, nami nataka ndoa-Ushauri" Nashukuru kwa ushauri wenu kwa ujumla umenisaidia na namshukuru Mungu kwa kuwa mvumilivu na kuyafanyia kazi mawazo yenu.

Nimejitahidi sana hadi nimefikia hap, kwa ufupi nimefanya kama mlivyo nishauri kwani niliona anazidi kunifatilia nilichofanya nilinunua line mpya nikamtumia x-boyfriend wangu na kumwambia kwa upole kabisa kua hii line ndio yangu ya sasa. Ile ya zamani usiitumie nimempa Mother atumie hivo ukitaka kunipata tumia hii ya sasa.

Hivyo ametumia kuwasiliana kupitia hii ya sasa na kunitaka tuonane lakini kila siku nikawa namdanganya kuwa kuna kazi kidogo imenibana anisubiri baada ya wiki kama nne hivi nitakua free then tutaenjoy nae akakubali.

Baada ya kuona amekubali nikarudi kwenye line ile ya zamani na kuanza kuitumia hii mpya nikaitupa hivo akawa anashindwa kunitafuta kupitia ile ya zamani kwani nilishamwambia kua ipo na Mother.

Nafikiri amesubiri hadi mwisho amekata tamaa akaacha kunitafuta na kitu cha kushangaza zaidi njiani hatukutani kama zamani, kwa sasa naishi maisha safi raha mstarehe na mpenzi wangu hakuna anaenisumbua wala nini.
Nawashukuru sana".

Dinah anasema:Nafurahi kuwa umefanikiwa kufanya uamuzi na sasa unaendelea vema na mpenzi wako ambae unataka kufunga nae ndoa. Lakini mbinu uliyotumia sio nzuri na nitakuambia kwanini?

Umekosea sana kumpa matumaini ya kukutana na ku-enjoy nae wakati huna mpango huo. Mwanaume sio mtu wa kukata tamaa kirahisi hivyo hasa kama anakupenda, ikiwa atakukosa kwenye Line uliyotumia anaweza akajaribu kupiga au hata kutuma ujumbe kwenye namba yako ya zamani ambayo ndio unayotumia sasa.

Siku moja mpenzi wako ulie nae sasa anaweza kukutana na ujumbe kutoka kwa Ex wako huyo na hivyo kutaka kujua ukweli wa nini kinaendelea kati yako na huyo Ex. Sidhani kama ungependa hilo likutokee.

Pamoja na kuwa kwa sasa hamkutani mtaani haina maana jamaa amehama Mji au eneo hilo, ipo siku atarudi na mtakutana, je utamueleza nini kuhusianana ahadi uliompa?!!

Unachotakiwa kufanya ni kumwambia jamaa ukweli ulio wazi kuwa humtaki na sasa uko kwenye uhusiano mwingine na usingependa uhusiano wako huo uharibuke kwa sababu yake. Kama mtu mzima atakuelewa na kukubali kuwa hawezi kuwa na wewe kwa vile tayari una mtu mwingine.

Kila la kheri!

Thursday

Nataka kuolewa lakini nashindwa kupenda kila anaenitokea-Nifanye nini?

"Hello dada Dinah mimi ni binti in early twenties, ninatamani sana kuolewa na kupata japo mtoto mmoja soon. Bado niko shule lakini sielewi why I feel this way now! kwasababu nilikua against kuolewa kabla ya kumaliza masomo.

Niliwahi kuwa na Mpenzi ambae nilimpenda sana ila nilimuacha kwasababu nilidhani hakunipenda kwani we were breaking up and makingi up all the time, yaani maisha yalikuwa ndio hayo kwa muda wa miaka mitatu mpaka nilipoamua kuwa sasa I have had enough and called it off.

The guy bado ananitafuta kwa simu akitaka tuonane lakini mimi namchunia. Baada ya kuachana na huyo nikaanza kutoka na mwanaume mwingine ambae amenizidi umri kwani anamika 37 sasa. Tatizo ni kwamba jamaa anataka tufunge ndoa haraka iwezekanavyo.

Nyumbani hawamfahamu kwani bado sijamtambulisha, nilihakikisha anamjua rafiki yangu mmoja tu ambae nae alibahatika kwani aliomba lift. Baadhi ya ndugu zake wananifahamu na kufahamu uhusiano wetu kwani huwa ananikaribisha kwao na mwezi wa Pili kwama huu alitaka tuvalishane Pete.

Sina mpenzi mwingine na ninataka kuolewa lakini kusema ukweli simpendi huyu jamaa kihivyo, sura yake, na anavyoongea kwangu ni kero na pia he's terrible in bed. Nimekuwa nae kwasababu ya pesa, na kila ninapohitaji hunipatia pesa. Jamaa amejijenga vizuri kwani ana Kampuni yake na nyumba nzuri tu, pia huwa ananiachia niendeshe gari yake.

Nikaamua nimwambie kuwa siwezi kuolewa nae kwa sababu ni mkubwa kwangu na some other reasons which I cooked up but they sounded concrete. Yeye hataki tuachane kwani anadai kuwa ananipenda na anataka kuishi maisha yake yote na mimi pia anasema kuwa familia yake itamuona muhuni kama tutaachana.

Mie nimeshangaa jamaa bado anang'ang'ania kuwa na mimi wakati tangu tumekuwa pamoja sijawahi kumuonyesha mapenzi, yaani hata kumpa K ni ishu!! Mpaka anibembeleze kwa Wiki na wakati mwingine miezi. Mfano mwaka huu tumefanya ngono mara tatu tu.

I mistreated him kwa kumponda, kumnunia hata miezi miwili bila sababu ya msingi ili aniache lakini wapi! Kila kitu anachonipa na kuahidi ni perfect isipokuwa yeye. Nipo nae kwa vile hivi sasa sina kitu na sina mtu wa kuniangalia (money wise) kwani nina mzazi mmoja na kipato chake ni kidogo na sijawahi kumuomba mzazi huyo pesa kwa vile namuonea huruma.


Wakati niko kwenye Dilema hiyo, kuna kaka wengine wawili wanaonyesha interest kwangu. Wote wanasura nzuri na wanavutia na pia wana kazi nzuri ila mimi sina hisia za mapenzi, napenda sura zao na kazi zao. Mmoja ndio anaonekana mwema na anaweza kunioa ila naogopa kutoka nae kwani sina uhakika kamanitawapenda au itakuwa kama huyu Mjamaa, sitaki kuumia.

Dada Dinah naogopa nitakosa mwanaume wa kunioa kwani umri nao unakwenda lakini kila anaenitokea sivutiwi na sina hisia za kimapenzi, lakini rafiki zangu wakiwaona jamaa wanapagawa kweli.

Najua Email yangu ni ndefu sana, lakini am in desperate need for help na nilitaka nigusie yaliyopita na ninayokabiliana nayo hivi sasa ili nieleweke.

Nifanyeje?"

Monday

Nimekuwa na Mchumba kwa Mwaka, nampenda lakini sina uhakika-Ushauri


"Pole Dada Dinah kwa kazi ya kutushauri, mimi ni mwanamke mwenye miaka 26 nina Mchumba wangu mwenye umri wa miaka 36. Tumekuwa pamoja kwenye uhusiano wetu kwa mwaka mmoja.


Mchumba wangu huyu kwa mujibu wake ni kuwa anaishi kwenye nyumba yake, lakini toka tuanze kuwa pamoja kwenye uhusiano hajawahi kunipeleka kwake japokua ameniambia sehemu anayoishi. Kwa kawaida huwa tunaonana kila siku na pia mara nyingi tunaenda out kwa ajili ya diner n.k.


Naomba mnishauri, je anamapenzi ya kweli au ananidanganya tu, ningependa awe mume wangu Mungu akitujaalia. Asante"

Nashindwa kumuacha mume wa mtu-Nifanyeje?


"Natumaini wewe ni mzima na waafya. Mimi ni mwanamke wa miaka 24, naomba ushauri wako kama mdogo wako. Mimi nimetokea kumpenda mume wa mtu na nina amini ananipenda pia. Tumekuwa na mausiano kwa mwaka mmoja bila hata mke wake kujua na nina tamani sana kumjua mke wake.

Tatizo langu ni kuwa sijiamini kama huyu Mume wa mtu atakuja kuwa nami kama mpenzi wake wa kudumu, mimi binafsi nashindwa kumuacha kwasababu Jamaa mwenyewe ni innocent and very caring.
Naomba ushauri nifanye nini?."
Dinah anasema: Mie mzima wa afya namshukuru Mungu, Nashukuru sana kwa Mail yako na hongera kwa kuwa wazi pia kuwa na nia ya kuachana na huyo mume wa mtu lakini hujui uanzie wapi?
Ninaamini nia yako ni kuachana nae na labda ulipogundua kuwa ni mume wa mtu ulitaka kufanya hivyo lakini kutokana na hali ya kujali na upole anaokuonyesha unadhani kuwa ni mtu mwema na hivyo kuzidi kumdondokea kimapenzi. Ikiwa kama nia yako sio kuachana nae hakika usingekuja hapa kuomba ushauri na badala yake ungeendelea kivyako.
Uhusino wenu umekuwa kwa mwaka mmoja kwa vile mkewe hajui na wala hajahisi kuwa mumewe ana-cheat labda kwa vile anajali na amevaa ngozi ya kondoo hivyo mkewe anamuamini kupita kiasi na hivyo kutohisi kitu chochote kibaya.
Kama mkewe angejua au angehisi kuwa mumewe anagawa umasikini nje ya ndoa yao hakika angempa wakati mgumu sana na kupelekea Jamaa kuachana na wewe.
Sasa hebu tuambie kitu gani kinakufanya utamani sana kumuona mkewe? Ili umwambie kuwa mumewe ana-cheat (ni jambo jema japo ni ngumu kwa yeye kukuamini hasa kama mumewe atakataa na kudai kuwa wewe unamtaka) AU unataka kufanya ushindani ili kuzua ugomvi juu ya mumewe (sio vema kuumiza hisia za mwanamke mwenzio kiasi hicho).
Hisia za Mapenzi:
Kutokana na uzoefu hakika natambua kuwa ni ngumu sana kukabiliana na hii kitu kwani hupangi au kuchagua nani wa kumpenda, hisia za kimapenzi hujitokeza tu kwa mtu yeyote na wakati wowote, lakini kabla hisia hizo hazijaota mizizi (hazijakukaa sana) ni vema kuwa mdadisi kuhusu mtu uliempenda ili kujua ukweli kuhusiana na maisha yake ya sasa kimapenzi. Na mara tu baada ya kugundua kuwa amefunga ndoa ni vema kumkwepa.
Kutojiamini:
Ofcoz huwezi kuwa na hali ya kujiamini au kuwa na uhakika wa wewe kuwa mpenzi wake wa kudumu kwani huyo mwanaume sio wako na sio single ni mume wa mtu, siku yeyote ikiwa mkewe atagundua kuwa kajisahau na kuanza kurudisha yale yote ambayo labda mumewe anakosa na sasa kuja kupata kwako.
Vinginevyo, kama walivyogusia baadhi ya wachangiaji ni kuwa, ikiwa Imani zenu za Dini zinaruhusu na mkewe wa kwanza akaridhia then utakuwa mke wa pili.
Matokeo yake:
Wee bado ni binti mdogo wala huitaji kujiweka kwenye matatizo makubwa kama kuharibu ndoa ya mtu na vilevile kuishi na hatia ya kuharibu maisha ya watoto ambao ni matunda ya ndoa hiyo. Kumbuka watoto waliozaliwa kama matunda ya ndoa hiyo wataumia kama atakavyoumia mama yao.
Utakuwa umewanyang'anya baba yao, utakuwa umewaharibia maisha yao kwani hakuna mtoto anataka kumuona mama yake anaumia (unajua watoto tulivyo karibu na mama zetu). Huenda hujui yote haya kwa vile hukulelewa katika mazingira ya ndoa (kama mmoja wa wachangiaji alivyogusia), mazingira tuliokulia husaidia sana kwenye maamuzi yetu.
Nini cha kufanya:
Achana na huyu mume wa mtu kwania anakupotezea muda wako na kukuzibia bahati ya kukutana na wanaume, kwani kuna vijana wengi tu wenye umri mkubwa zaidi yako lakini hawajaoa na pia wapo vijana wenye umri wako (24-29) ambao wako huru.
Kila la kheri.

Mume kung'ang'ania picha za Ex wake ni kawaida?-Ushauri

"Habari Dada Dinah, Mimi ni mwanandoa ambaye nakaribia kumaliza mwaka sasa kwenye ndoa yangu. Tatizo langu ni kuwa mume wangu ana picha alizopiga na wapenzi wake wa zamani na hataki kabisa ziondolewe kwenye albam.

Ukigusia hilo suala ni ugomvi mkubwa, je Dada Dinah hiyo ni haki? au nichukue maamuzi gani? Nizitoe tu hapo na kuzichoma moto au nijifanye sijaziona na akiniuliza nimjibu kuwa sijui zilikokwenda na kumbe najua?

Maana yake kwa kweli zinanitia kichefuchefu. Tena kibaya zaidi ni za wasichana wa kizungu wawili tofauti, Je ndoa ndiyo zilivyo Dada Dinah au huyu mwenzangu ana lake jambo? Hao wasichana wako Ulaya yeye aliendaga kusoma huko siku za nyuma kama miaka mitatu ilopita na ndipo aliporudi akakutana na mimi tukaanza mahusiano na mpaka kufikia ndoa.
Naomba ushauri wenu jamani mnisaidie."

Dinah anasema: Ni njema tu Mdada, Unauhakika kuwa ni wapenzi wake au walikuwa marafiki tu wa Chuoni? Maana kuna Watanzania wengi wajinga wajinga wanadhani ni sifa kuwa waliwahi kutoka na Wakoloni (Wazungu) kimapenzi au kuthibitisha kuwa alisoma nje basi anatunza Picha za wanafunzi wenzake.


Ikiwa ni kweli ni wapenzi wake hakika anachokifanya sio haki, si hivyo tu mumeo hana heshima na wala hajali hisia zako kama mkewe. Katika hali halisi unapokuwa kwenye uhusiano wa kimapenzi wa kudumu na mtu hapaswi kuwa na Picha za wapenzi wake wa zamani let alone kuwa kwenye ndoa.

Picha za maisha ya shule/chuo yaliyohusisha wapenzi huwa tunaziacha nyumbani kwa wazazi, album za wanandoa huwa na picha zenu mlipokuwa wapenzi na zile za ndoa, za wazazi wenu ndugu, jamaa na marafiki sio exes.

Unapoingia kwenye ndoa unaacha kila kitu huko nje na kuanza maisha upya, ndio maana huitwa maisha mapya ya ndoa. Wote wawili mnaanza upya sio tu kama wapenzi/familia bali pia kama individuls.

Kama umejaribu kumuomba kwa ustaarabu aziharibu Picha hizo na yeye kuwa mkali na hata kuibua ugomvi basi kuna mawili ya kufanya;

(1)~Ziondoe na uzifiche mahali kisha tafuta njia ya kumfanya aongeze picha kwenye album ambayo ilikuwa na hizo Pics za Exes. Asipoziona ni wazi kuwa atakuuliza au kukushutumu kuwa umezitupa na kuibua ugomvi kama kawaida au anaweza kuuliza tu picha fulani ziko wapi? Mwambie ukweli kuwa Picha hizo zinakunyima raha, zinakufanya usijiamini n.k.

Kama ugomvi utakuwa mkubwa sana, basi mwambie "naona hili suala la picha za wapenzi wako wa zamani limekuwa ni tatizo kubwa kwenye ndoa yetu, hivyo naomba tuliwakilishe kwa wazazi wa pande zote mbili" katika hali halisi ni jambo dongo sana kulipeleka kwa wazazi wenu sio hivyo tu litamfanya asikie aibu na ku-give up....then acha siku mbili zipite alafu zipige kibiriti.

(2)~Tafuta picha za the hot guys kuliko yeye lakini wabongo na wewe ziweke kwenye album yenu. Au kama kuna picha ambazo ulipiga zamani ukiwa na wanaume ambao sio ndugu na yeye hawajui ziweke kwenye album hiyo....so he can learn the hard way.

Natumaini unafanyia kazi ushauri wa wachangiaji wengine.
Nakutakia kila la kheri

Tuesday

Mume aki-cheat na mwenye umbo tofauti na lako anaweza akawa bado anakupenda kama zamani?

"Dada Dinah mie naomba kuuliza,hivi kweli mumeo akitembea nje ya ndoa na mwanamke ambae hamfanani kabisa ikimaumbile anaweza akawa bado anakupenda?

Nimeuliza hivyo kwa kuwa mimi ni size 12 though kabla sijajifungua nilikuwa navaa chini saizi 14 juu saizi 12 kwa sasa nimepungua sana (na nimependa mwenyewe kupungua). Mwanamke ambae mume wangu alikuwa na affair nae for almost two months (kama ni mkweli) ni wale ambao ni ngumu hata kupata saizi dukani, yaani ni bonge la mtu lakini ni namba nane.

Inanifanya nisijue mume wangu anapenda miili gani? That is why I am not feeling like staying married to someone that am not sure anymore that he still loves me. Na wakati mwingine tukiwa kwenye gari wakipita wanawake wakubwa wenye namba nane huwa namcheki anavyowaangalia japo kwa wizi sana. Ingawa hata mimi huwa sometimes nawashangaa wanawake wenzangu. Sasa sijui nina wivu na sina Imani kwa sababu ameshani-cheat au ni normal"?

Naomba mnipe ukweli, je mume wako akitoka nje ya ndoa yenu na mwanamke ambae ni tofauti na wewe na baadae kukubali makosa na kurudi kwenye ndoa, je ataendelea kukupenda?

Asante".

Sunday

Mkwe anataka nimuache mwanae ni Hanithi, lakini tumesha-do mara kibao na yuko sawa-Nifanyeje?

"Habari Aunt? Mimi ni mwanamke wa miaka 24,nina boyfriend wangu ambae tumedumu kwa miaka mitatu na plan yetu ni kufunga ndoa. Alipanga kuleta Posa baada ya Mwezi wa Ramadhan lakini cha ajabu mama yake aliwafuata mama zangu wakubwa na kuwaambia kuwa huyo boyfriend wangu si mwanaume, kwamba ni hanithi.

Pia mama yake alinifuata mimi na kunambia kuwa mwanae hana uwezo wa kiume. Lakini mimi na boyfriend wangu tayari tumekutana kimwili mara kadhaa na mimi namuona yuko sawa ila huwa anapiz nje kwa kuwa tulipanga tusizae nje ya ndoa.

Siku nyingine Mama yake kanambia kama siamini basi nijarbu kumtega kwa kumwambia kuwa anipe mimba, nilipomwambia boyfriend wangu anipe mimba alinijibu kuwa yeye yuko tayari. To be honest nampenda kutoka moyoni na yeye ananipenda pia.

Hivi sasa niko njia panda kwani pande zote mbili wanataka niachane nae lakini mimi sijaona tatizo au mapungufu ya mpenzi wangu yako wapi. Kwangu mimi ngumu kuachana nae kwa kuwa tunapendana na tuna plans nyingi tulizopanga na ni za muda mrefu.

Naomba watanzania wenzangu mnisaidie kwa hilo niko njia panda.

Asante."

Dinah anasema:Habari ni njema tu lovey, asante sana kwa ushirikiano. Pole kwa misukosuko ya soon to be mother in law, hapo ni sawa na kujitukana na kujidhalilisha mbele ya wazazi wenzie. Yeye amejuaje kama mwanae hawezi au hana uwezo wa kuzaa? Hata kama huo ni ukweli yeye anahusika vipi na maisha yenu ya ndani ninyi wawili kama wapenzi?

Anyway, Kama walivyo akina mama wengi wenye watoto wa kiume hupenda sana kupata mjukuu pale wanapotaka wao, wengine hutumia neno "sitaki kufa kabla sijaona mjukuu) hivyo hufanya kila jambo ili mtoto wa kiume kuzaa iwe kabla au baada ya ndoa.

Utagundua kuwa, kuna baadhi ya kina mama wakishajua mtoto wao wa kiume anauhusiano utasikia anataka kijana huyo afunge ndoa (hata kama hayuko tayari) na ikitokea akafunga ndoa kutokana na matakwa ya mama, soon baada ya ndoa mama mkwe ataanza kudai mjukuu, akipata wa kike, atataka wa kiume n.k yaani ni kama vile wana-control maisha ya watoto wao wa kiume.

Huyu mama anaposema mwanae ni Hanithi anamaanisha mwanae ni Tasa (hana uwezo wa kuzaa), labda kwa vile kila msichana alietoka nae kabla yako hakushika mimba kwa vile Mwanae alikuwa mwangalifu au hakutaka kuzaa kabla ya ndoa.

Vilevile inawezekana Mama mkwe huyo anadhani wewe ni Tasa kwani umekuwa na mwanae kwa muda mrefu bila kushika mimba (si unajua wazazi wetu wao walitumia Majira na hivyo waume zao walikuwa wanamwaga ndani tu hakuna cha nje wala Condoms)huenda anajiuliza "kulikoni hawa watu hawapeani mimba miaka yote hii" hivyo anataka ushike mimba kabla mwanae hajakuoa.

Sasa huyu mama anachojaribu kukifanya hapa ni kutaka wewe uwe forced na wazazi wako kushika mimba kabla ya ndoa ili ukifunga ndoa baada ya muda mfupi wewe na mumeo mmpatie mjukuu. Kumbuka amekuambia kama "huamini mwambie akupe mimba".

Alafu kwanini wazazi wako wakatae kupokea posa wakati sio wao wanaokwenda kuolewa na huyo Kijana, kwa kawaida binti ndio huwa na uamuzi huo. Kwamba mtu akija kuchumbia kwenu wazazi wanasema watamjibu baada ya muda fulani, then unaitwa alafu unaambia kinachoendelea na wewe kukubali au kukataa (kizamani).

Kisasa wengi tunakuwa tunawajua wachumba (vishwa Pete) kabla ya posa hivyo hata posa ikipelekwa wewe unakuwa wa kwanza kujua na huenda ukawaambia wazazi kuwa wazee wa kadhaa wa kadhaa watakuja kuposa n.k. hivyo wazazi kukataa Posa kwa sababu ya majungu ya mzazi mwenzao sio haki.

Nini cha kufanya:
Hebu kaa chini na mama yako mazazi na uwaambie ukweli kuwa Mchumba wako anauwezo wa kufanya mapenzi kwani tayari mmekwisha fanya mara kadhaa ndani ya miaka 3.

Mwambie "tunapendana na niko tayari kufunga nae ndoa. Sielewi mama mkwe(sijui unamuitaje) anataka nini kutoka kwetu kwani hivi majuzi (itaje siku) alinifuata na kuniambia nimtege mchumba wangu ili anipe mimba, inamaana huyu mama anadhani ukoo wetu ni Tasa?!!"

"Mimi sitaki kushika mimba kabla ya ndoa na ndio maana nimekuwa mwangalifu na kujikinga kwa miaka yote mitatu" (hii trick ya kujifanya victim huku unatoa CHOZI siku zote hufanya miujiza).

Enedelea "Mama naomba mkubali posa ya mpenzi wangu kwani ni mwanaume pekee ninae mpenda na tumepanga kufanya mambo mengi kwa ajili ya maisha yetu na familia zetu, nisingependa kumpoteza mwanaume anaenijali, mwenye nia njema nami na mwenye upendo wa dhati".

Mama yako anakupenda, hakika atakuelewa na atafikisha ujumbe kwa Baba. Ikiwa bado wanashupalia uachane nae basi uamuzi ni wako, Funga ndoa na Mchumba wako bila ya kuwaharifu wazazi wenu na baada ya ndoa ndio wapewe taarifa.

Fanyia kazi maelezo ya wachangiaji wengine pia,
Kila la kheri!

Friday

Shukrani kwa Maoni, ushauri na Mawazo yenu, sasa nimejitambua!

"Nitakuwa mchoyo wa fadhila kama nisipo mshukuru muongozaji wa blog hiimy sister DINAH, shukrani zangu pia ziwaendee wale wote ambaowalisoma, au kuchangia katika ujumbe wangu ulio rushwa katika blog hii pendwa tarehe 18/08/2010 (Bofya hapa).

Kwa heshima na taadhima nawashukuru sana tena sana, sababu amini msiamini mmenionesha mwanga. Wapi nielekee. Nakubali kusema kuwa nilipoteza muelekeo ila kwa mchango na mawazo yenu na ushauri wenu kupitia hapa nimefanikiwa kufanyia kazi yote kutoka kwa kila mdau.

Kulinganana majibu hayo sasa nimejitambua, nasema hivyo kwasababu nilijaribu kumuomba tukae chini nijue kipi kinamsumbua akashindwa kutokea mahali ambapo tuliekubaliana zaidi ya mara mbili that means kweli hana mapenzi ya dhati kwangu.

Namshukuru Mungu ninaendelea vizuri na masomo yangu ya Ualimu, kwa wale ambao walishindwa kufahamu kama ninasoma ama la. Mimi ni mwanachuo wa Diploma ya Ualimu mwaka wa pili sasa.

Dada dinah pamoja na wale wenye mapenzi ya dhati na nia njema ktk blog hii Mungu awabariki sana."

Wednesday

Nimegundua mume wangu kampa mimba mwanamke wa nje-Ushauri

"Habari dada Dinah, mimi ni moja ya wadau wa blog yako. Nieolewa na ni mama wa mtoto mmoja ana miaka 3+ na ninakaribia kupata baby no.2 panapo majaaliwa mwishoni mwa mwaka huu.

Mwenzenu nina matatizo ambayo naomba wadau wanisaidie kunipa ushauri nini cha kufanya maana nimejaribu kufikiria sioni njia ya kutatua matatizo yangu. Mimi na Mume wangu tangu tumejuana tumekuwa tukiishi kwa amani na upendo, lakini cha kushangaza hivi karibuni nilimuona kabadilika sana kiasi kilichonifanya nianze kuchunguza kulikoni?

Mbona mambo hayaendi sawa kama zamani! baada ya kuanza uchunguzi niligundua mume wangu kuna watu anawasiliana nao sana bila kutaka mimi nifahamu wanawasiliana kwa ajili ya issue zipi. Hapo nilijawa na wasiwasi zaidi nikaamua kutega baadhi ya number kwenye simu ili msg zikitumwa asizione kwenye inbox ila ziingie kwenye folder tofauti.

Nilipokuja kufungua lile folder nilikuta msg nyingi za mdada mmoja ambaye ni mpenzi wake na alikuwa akilalamika kuwa hamtumii msg wala kumpigia simu nakuwa amepunguza kumjali na yeye ni mjamzito na ameamua kuitoa hiyo mimba kisa hamjali sababu hampigii simu.

Nilipoona hizo msg nilitamani kufa hapohapo! maana sikutegemea kama mume wangu angekuwa na mwanamke nje ya ndoa yetu ambayo bado changa. Nikaamua kumuuliza mume wangu akasema hana mwanamke nje na hategemei kuwa na mwanamke nje ya ndoa.

Nami kwa kuonyesha kuwa hamna msg niliyoona nilikaa kimya kwa muda wa wiki mbili bila kumuuliza kitu. Baadae nikakuta msg nyingine ya huyo mwanamke akimuuliza mume wangu anaamuaje kuhusu ujauzito alionao?

Nikaamua kuhamishia ile msg kwenye inbox na kumuomba mume wangu aisome ile msg na anieleze kuna kitu gani kinaendelea. Chakushangaza mume wangu akasema haijui hiyo msg, basi nikamwambia tupige hiyo simu tukiwa wote nae akakubali yule dada alipopokea akaanza na maneno yanaonyesha wao ni wapenzi wa siku nyingi.

Mumue wangu akajidai kumfokea yule dada lakini haikuleta maana yeyote, nikaamua kuchukua ile namba na nikaipigia mimi mwenyewe nikimuomba tukutane kwani nina shida nae, yule dada akakubali lakini hakutokea na simu yangu hapokei tena.

Huku mume wangu hajawahi kulala nje ya nyumba yetu hata siku moja na siku zote yeye huwahi kurudi kutoka kazini kabla yangu maana mimi huwa narudi kuanzia saa kumi na moja na kuendelea na yeye hurudi kuanzia saa nane mchana.

Hapo naomba dada Dinah na wachangiaji wengine mnisaidie kimawazo, nifanyeje maana nimepunguza sana upendo kwake kila nikimuona mume wangu namuona kama ni muuaji maana kama ameweza kufanya mapenzi nje ya ndoa tena bila ya kutumia kinga si anataka kuiteketeza familia yetu?!!

Asanteni"

Monday

Baada ya Ultrasound na kujua umri wa mimba Mpenzi kaikataa!

Habari Dinah,

Mimi ni mmoja wa waenzi wa Blog yako ila leo ndio mara ya ngu ya kwanza kukuandikia nikihitaji ushauri au msaada wa kimawazo. Nina umri wa miaka 25, na ninamshukuru Mungu kuwa nina Ujauzito ambao siku yeyote naweza kujifungua kwani tayari niko kwenye my due date.

Tatizo ni huyu baba mtoto ambae anaumri wa miaka 28. Nilipokuwa na mimba yangu changa about a month nilitokea kumchukia sana na nikawa na hasira za karibu karibu kitu kilichopelekea mimi na yeye tukatengana.

Nikaendelea kutunza mimba yangu hadi ilipofikia miezi minne then nikataka kujua mwenzangu anampango gani, hivyo nikamuuliza. Yeye akaniita tukayaongea na kukubaliana kwamba tutalea mwanetu nahivyo penzi likaanza upya.

Tukaenda kuangalia Ultrasound ikawa inasema Mimba ina miezi mitano na sio minne, tukarudia tena ikasema hivyo hivyo, yule mwanaume akaanza ku-doubt nakujiweka mbali kidogo na mimi. Kumbe sisi tulivyokuwa tunahesabu ni tofauti na wanavyohesabu wataalam.

Kumbe mimba inahesabiwa kuanzia siku ya mwisho ya Hedhi (last date of period) na sisi tulikuwa tunahesabu kuanzia siku ya kwanza ya kukutana kimwili (Date of Conception) so ikawa inatusumbua ila mimi nilikuwa na hakika kuwa yeye ni baba kwa sababu yeye ni mwanaume pekee niliyefanya nae mapenzi, sina mwanaume mwingine.

Cha kushangaza mwenzangu akaanza visa na pia nikagundua kuwa anatoka na mwanamke mwingine, nilipouliza kulikoni? akanijibu kuwa yuko serious na huyo mwenzangu, pia akadai kuwa hana uhakika kama mtoto ni wake. Kaendelea kusema kuwa hayupo tayari kuzaa kwani hajajipanga.

Niliumia sana, nikatafuta Daktari nakumuelezea na yeye akanielewesha namna ya kuhesabu tarehe kwa mara ngingine tena nikagundua kuwa mimi na baba mtoto tulikuwa tunakosea kuhesabu tarehe, basi nikamuandikia Email ndeefu baba mtoto wangu na kumueleza yote na pia kumuomba aende kwa Daktari yeyote ampe tarehe zetu za kukutana kimwili then tarehe yangu ya mwisho ya kupata hedhi ili apate ukweli. Naamini kuwa alifanya hivyo ila hakutaka kuniambia ili akwepe majukumu.

Baada ya muda nikawa namcheki ili aniambie amefikia wapi? akadai hawezi kuamua sasa mpaka mtoto azaliwe, cha kushangaza kazini kwao na kwa marafiki zake anatangaza kuwa mtoto ni wake. Nimehangaika mpaka sasa nakaribia kujifungua bila msaada wowote kutoka kwake, nilipokuwa najaribu kuomba msaada alikuwa akinijibu kijeuri au kukaa kimya.

Kanifanya niwe mpweke sana kwani kipindi cha mimba ni kigumu na kinachohitaji support ya hali ya juu. Nasikia kutoka kwa watu wengine kuwa anataka kuja kuomba amjue mtoto atakapo zaliwa, ila mimi nina hasira sana na sitaki hata kumuona.

Naomba ushauri wa kujenga na sio kubomoa wala sio matusi, huyu mtu ni wa kumsamehe kweli? na je tunahitaji mtu kama huyu kwenye maisha yetu (mimi na mtoto)?

Asanteni"

Sunday

Nina Ujauzito wa Miezi 2, je haya ni ya kawaida?

"Kwenu wadau wenzangu, Kwa mara nyingine tena naleta swali langu nahitaji michango yenu,
Mimi ni mwanamke nimeolewa na baada ya miezi 7 ijayo natarajia kuitwa mama. Tatizo lilonifanya nije kwenu kuomba ushauri ni kwamba tangu nimegundua kua ni mjamzito nimekua katika wakati mgumu sana mpaka inafikia kipindi nashindwa hata kufanya kazi.

Yaani napata kichefuchefu cha ajabu ila sitapiki, nakuchagua baadhi ya vyakula pia harufu harufu hizi za manukato au chakula mara nyingine zinanipa shida kweli lakini najipa moyo kwani najua haya ni mambo tu ambayo humtokea mama mjamzito pindi mimba inapokua changa.


Ila kubwa zaidi ni kwamba sijisikii kabisa kufanya tendo la ndoa na Mme wangu kitu ambacho naona kama vile nanyima haki yake, ila najitahidi sana kujiweka katika fikra za kimapenzi lakini nashindwa.


Namshukuru Mungu kuwa yeye Mume wangu ni muelewa, anaelewa nikimwambia ila sasa naona hali mbaya kwani ni wiki ya pili sasa sijisikii kabisa kufanya mapenzi. Nahitaji msaada wenu wa mawazo ndugu wadau, nahisi nitaipoteza ndoa yangu.

Ningependa kujua kua Je hali hii iliyonikumba baada ya kushika ujauzito ni kawaida kwa wanawake au ni tatizo lingine linanikumba?
Asanteni"

Tuesday

Mpenzi atishia kujiua Kisa sms ya Ex akiomba msamaha!-Ushauri

"Kwanza pole na hongera kwa kazi unayofanya ya kutoa ushauri kwa jamii. Mimi ni msichana mwenye miaka 23, nina mpenzi ambaye siku hizi ni kama kafichua makucha vile. Tumekuwa pamoja kwa muda wa mwaka mmoja.

Kilichonifanya niandike leo Dinah, ni huyu mpenzi wangu! mwanzo tulikuwa tunapendana sana na ahadi tele tele, yaani mikwaruzano haikuwepo na muda wote huo hatukuwahi kukosana. Basi siku moja tulikuwa tumekaa sehemu akaniomba nimuhamishie wimbo kutoka kwenye simu yangu kwenda kwenye simu yake.

Kwa utani tu nikamwambia nimeiacha simu nyumbani, jamaa akaja juu kwamba nimemdharau nikamuomba msamaha lakini wapi! akanipokonya simu huku akiuliza "unaficha nini?" Nikamwambia samahani lakini hakukubali na hivyo akachukua simu na akaenda nayo kwake.
Ile simu alikuwa kaninunulia yeye, kwenye simu hiyo kulikuwana sms za x- boyfriend akiniomba msamaha ili turudiane.

Mpenzi wangu akazidi kukasirika na kupandisha sana na akampigia huyo kaka nilieachana nae nakumpandishia aache kunifatilia. Kinachomuuma hasa ni bada ya kugundua kwenye zile sms kuwa Ex wangu anamzidi Elimu kwani kamaliza Chuo Kikuu na pia anamzidi kifedha. Lakini mimi sinampango nae huyo jamaa wala elimu yake wala fedha zake kwani niliisha achana nae na analijua hilo.


Sasa tatizo kubwa hapa ni kuwa mpenzi wangu huyu ananitishia kuwa atajiua na hatanii kweli, ni Mchaga alafu pia nimemzidi kielimu kwani hivi sasa niko Chuo Kikuu mwaka wa pili yeye aliishia Kidato cha 4 na kuanzisha Biashara zake zinazomuingizia hela.

Mimi kuwa Chuo Kikuu ndio limekuwa tusi tukiongea kidogo tyu utasikua "au kwa vile sijasoma najiua ili nikuache huru" Mpenzi wangu anamiaka 25 aliniambia hajawahi kuwa na mwanamke na mimi ni wake wa kwanza.

Dinah najieleza na kuomba kila kukicha na sasa ni miezi 3 imepita lakini msimamo wake ni ule ule wa kujiua, nikamwambia nirudishie simu lakini kila tukipanga kuonana anasema yuko busy. Nikimuomba ninunue simu nyingine hataki, ikabidi nijinunulie mwenyewe simu nyingine kama ile ile ili kuendeleza mawasiliano.

Sasa jamani huyu mwanaume niendelee nae? kama nikiendelea nae na nikajamkosea tena si atajiua!! na nisipoendelea nae na yeye akajiua mimi sinitakuwa matatizoni na Degree yangu ikaishie Segere?
Naomba ushauri kutoka kwa wachangiaji wote".

Nafikiria kuachana nae lakini nashindwa, nifanyeje?

"Heshima yako dada Dinah.
Napenda kutoa pongezi kwako na kwa wachangiaje wote ambao wapo bega kwa bega kutoa ushauri katika topic mbalimbali. Mimi ni mmoja wa wapenzi wa blog hii, nimekuwa nikifuatilia kwa karibu sana mada mbalimbali na kujifunza mambo mengi kwakweli.

Dada dinah kama unavyojua matatizo tumeumbiwa nayo binadamu hasa katika barangeni hili la mapenzi. Mimi ni kijana mwanaume, umri miaka 22. Kusema kweli mpaka sasa mwenzenu nipo njia panda kuhusu msichana ambaye ninampenda sana ila simuelewi hata kidogo kama kweli ananipenda ama la.

Ni miezi sita tangu ni mueleze hisia zangu juu yake bahati nzuri alinielewa na akanipa jibu zuri ambalo lilinifanya nisijute kumpenda. Tangu hapo nilikuwa nimechizika kwake nilipenda kila wakati eidha nimuone au nisikie sauti yake tu. Hapo ndipo nilipo fikia uamuzi wa kumnunulia simu ili mawasiliano kati yangu na yeye yawe rahisi.

Tangu hapo nikawa nampigia simu mara kwa mara wakati mwingine anapokea wakati mwingine hapokei, basi ninaamua kumtumia sms ambazo pia hakuona umuhimu wake, nasema hivi kwasababu ninapo muuliza kama amepata sms yangu hunijibu sms ipi? Ilikua inasemaje? Basi tu ilimradi.

Haya yote sikuyatilia umuhimu kwa kuwa nampenda ila wasiwasi wangu umeanza kuja hapa, tangu niwe na mahusiano nae sijawahi kukaa nae tukajadili kuhusu mapenzi yetu kwa kuwa huwa anakataa na kudai kuwa anashughuli nyingi.

Pili sijawahi hata kumkiss shavuni achilia mbali romance nimejaribu mara kadhaa kumuomba tutoke out japo twende hata beach lakini huwa ana kataa sababu ni hizo hizo. Nimemjali kwa mengi bado haoni umuhimu wangu kama mpenzi wake. Pia nikakubaliana na yote hayo hivyo mapenzi yakawa ni ya kwenye simu tu hakuna kuonana.


Kikubwa kinacho niumiza mimi mara kadhaa ninaweza kukutana nae katika mizunguko lakini cha ajabu huwa hana muda na mimi hata salamu mpaka nianze mimi. Nikikaa kimya hunipita kama hanioni. Dada dinah kiukweli nimekuwa sina raha muda mwingi nawaza kwanini ananifanyia hivi lakini nakosa jibu, hata yeye mwenyewe ninapo muuliza huwa hanijibu chochote.

Sasa sijui amedhamiria au ndio mapenzi yenyewe! naweza kusema alibadilika pale tu nilipo mnunulia simu na ilikuwa ni wiki moja tu baada ya kunikubalia ombi langu. Anayo nifanyia ni mengi mno ila sipendi kuwachosha wachangiaji kwa kusema yote.

Hivyo mwenzenu mpaka sasa nipo njia panda, neno nakupenda limebaki kuwakumbukumbu kwangu. Nimeshajaribu kufikiria kumuacha niwe alone lakini nashindwa, je nifanye nini mwenzenu.
Ahsanteni".

Sunday

Nimerudi, samahani kwa kukutenga!

Habari za leo mpenzi msomaji, mtembeleaji na mchangiaji wa D'hicious, nafurahi kusema kuwa nimerudi tena mahali hapa baada ya kupotea kwa muda wa wiki chache kutokana na mishughuliko ya kikazi (safari za hapa na pale) ambazo zilininyima muda wa ku-publish post mpya na kujibu maswali yaliyokuwa published.

Naomba radhi kwa usumbufu uliojitokeza kutokana na kutokupatikana kwangu. Namshukuru Mungu nimemaliza salama na sasa nimepata muda wa kuwa nawe tena.

Vilevile napenda kukufahamisha kuwa sito-publish maswali yote yanayozungumzia au kugusia ngono kwa undani kwa muda (Mwezi huu Mtukufu) ili kuepusha vishawishi na pengine kuharibu Funga za wenzetu Waislamu.

Asante sana kwa ushirikiano wako.

Mwenye upendo na kujali,
Dinah.

Tuesday

Mume wangu aninyanyasa nakudai "mimba ikitoka utapata nyingine"...

"Mimi ni mama wa kitanzania ninaeishi na familia yangu UK, nimeolewa miaka 12 iliyopita na ndoa yetu imejaaliwa watoto wa wiwili na mwingine wa tatu yuko njiani. Mimi nilikuja UK kwa ajili ya masomo na kumuacha mpenzi wangu ambae sasa ndio mume wangu nyumbani Bongo.

Wakati naondoka tulikubaliana kuwa nikikaa kwa muda nimfanyie mpango ili na yeye aje huku kusoma, lakini kutokana na ugumu wa maisha kwangu kama mwanafunzi niliekuwa chini ya wazazi sikuweza kufanikisha hilo na yeye hakuwa na pesa za kutoshana kumleta huku. Basi tukaamua kusitisha suala la kusoma na kwavile tulikuwa tunapendana tukaamua kuwa yeye aje huku kama mwenza wangu na hivyo mimi nitaendelea na shule wakati yeye akifanya kazi ili kumudu maisha yetu.

Baada ya mimi kumaliza na kufanikiwa kupata kazi kwenye Bank na tukafunga ndoa mwaka uliofuata, maisha yakawa mazuri, mapenzi motomoto kama mke na mume na baada ya mwaka mmoja tangu tufunge ndoa nikajifungua mtoto wetu wa kwanza.

Baada ya kumaliza likizo ya uzazi mume wangu akaamua kuacha kazi bila sababu ya msingi, mimi haikunisumbua kwa vile kazi yangu ilitosha kutufanya tuishi maisha ya kawaida. Mtoto wa pili akaja, nikaamua kukaa chini na mume wangu ili tujadili maisha yetu ya mbeleni kwani familia inakua, mume wangu akaahidi kurudi kazini. Lakini hakufanya hivyo na sasa mtoto wa tatu yuko njiani.

Mume wangu amekuwa mvivu, hajali, hana umpendo na asie na ubinaadamu kabisa, natoka nyumbani asubuhi na mapema kwenda kazini, narudi jioni nikiwa nimechoka si unajua tena ujauzioto! nikifika nyumbani kitu pekee nahitaji ni kupumzika, lakini wakati napumzika utasikia mume wangu anauliza "leo hatuli humu ndani?" wakati yeye anatazama TV. Kwavile nakuwa nimechoka na sitaki ukorofi mwanamke nainuka naenda jikoni na kuanza kuandaa chochote cha haraka haraka ili nipate muda wa kupumzika.

Siku moja nikaamua kuzungumza na mume wangu na kumwambia jinsi ninavyojisikia kuhusiana na suala zima la ujauzito, masaa mengi kazini na kumuomba tusaidiane shughuli za ndani ili kuepusha matatizo kwangu na kwa mtoto alie tumboni.

Sikuamini masikio yangu pale mume wangu aliposema kuwa " wewe ni mwanamke wa kiafrika ni lazima uhakikishe nyumba safi, chakula kinapikwa na kuangalia watoto. Kwani kuwa na mimba ni ugonjwa? wangapi wanakuwa na mimba zinatoka na wanapona alafu wanashika nyingine na wanazaa? ikitoka hiyo utapata nyingine".

Dinah ghafla nikajisikia sina nguvu, nikanyanyuka taratibu bila kusema kitu nikaenda zangu kupumzika. Tangu siku hiyo nikaamua kuwa kila Juma Pili nitakuwa napika chakula/kuandaa chakula kingi kwa ajili ya wiki nzima ili watoto wangu na baba yao wasishinde njaa.

Sasa ndugu zangu nauliza hivi, kama hali imefikia hivi na watoto wetu hawajafikia umri mkubwa kuishi na mzazi mmoja nitakuwa nakosea kama nikimvumilia mpaka watoto wakuekue kidogo ndio nitafute ustaarabu wangu au nitengane nae sasa ili nisimpatie matatizo mtoto alie tumboni?.

Mimi binafsi hisia za mapenzi kwa mume wangu hazipo tangu aliponiambia kuwa mimba sio ugonjwa na mameno mengine yote, yaani namuona kama mtu tu pale asie na umuhimu wowote kwangu. Sina uhakika kama hali hii nikutokana na ujauzito, hasira au mapenzi yameisha?

naombeni msaada wenu wa kimawazo.

Mdau wa UK"

Monday

Ni mdada mwenye Elimu zaidi ya Mchumba, je haiwezi kuwa tatizo tukifunga ndoa?

"Dinah mdogo wangu, hujambo?
Mimi ni mama wa miaka 41, niliolewa na kukaa na ndoa kama miaka 10 hivi na kupata mtoto mmoja. Mwamaume yule akaanza vituko na hata akanza kulala nje yando ayetu. Nilivyoona karaha zimezidi nilimueleza kua nitahama nyumbani kwake lakini hakuonyesha kujali na wala hakunibembeleza ili nisihame.

Siku ya siku nikatafuta nyumba, nilipofanikiwa nikamueleza kuwa nimepata nyumba na nategemea kuhama, lakini hakuniomba nibaki. Nikajua hakua ananihitaji tena basi nikahama. Baada ya mda mfupi nikatafuta shule nikaenda nje ya nchi kusoma.

Huku nyuma yeye akafunga ndoa na yule hawara yake (sisi ni Waislam). Nikadai Talaka akaitoa bila ubishi. Nikaendelea na masomo na Mungu akanisaidia nikamaliza salama na sasa nimepata PHD yangu tayari.

Hivi sasa kuna wanaume wawili mamekuja wanataka kunioa, mmoja kaishia form two na mwengine form four, shida yangu ni kua viwango vyao vya elimu ni vidogo mno na ndio kitu pekee kinanipa hofu kuingia kwenye hayo makubaliano ya ndoa na mmoja wao, ingawa nahisi bado nahitaji kuwa na mume.

Naomba mnishauri wanablog, Jee mwanaume ukimzidi elimu sana na hata kipato haiwezi kuwa tatizo ndani ya familia? ili kuwe na amani ndani ya ndoa ya hivyo mtu ufanye nini? Nahitaji kufanya maamuzi kati ya mmoja wao. Nahitaji sana kuolewa kama Mungu akinibariki. asanteni wote".

Thursday

Ex ananirudisha nyuma kihisia, nami nataka ndoa-Ushauri

"Dada Dinah na wasomaji wote, Mimi ni mwanamke mwenye umri wa miaka 22, nina mchumba wangu tunapendana sana na hivi karibuni tunatarajia kuoana.

Tatizo langu kubwa ni hivi, kabla ya huyu mchumba wangu nilikuwa na boyfriend ambaye nae mwanzo tulipendana sana ikaja kutokea hitilafu katika mapenzi yetu kwani alikuwa na mahusiano na mwanafunzi nje ya uhusiano wetu. Kabla ya kuchukua uamuzi nilijaribu kukaa nae nikamweleza ni jinsi gani naumia juu ya tabia yake aliyoianza.

Ilionyesha kuwa alinielewa na tukaendelea na mapenzi yetu kama kawaida, baada ya muda tena nikaja kuona sms ya yule yule mwanafunzi aliekuwa akitembea nae akimtaka aende kwake, kwakweli nilishindwa kuvumilia.

Nikaongea na Dada zake kwani yeye hana baba wala mama hao dada zake na kaka zake ndio walezi wake, japo kua mama yake mzazi amefariki hivi karibuni akiwa ananitambua kama mkwe wake mtarajiwa.

Dada zake walikaa Ex wangu na kuongea nae kwa kirefu zaidi, akawa kama ameelewa lakini baada ya mda mfupi mambo yakawa yale yale, basi dada zake wakaniambia kua wamejaribu kumuonya lakini hawaoni msimamo wake ni upi! Basi nikajitahidi kwenda nae hivyo hivyo, baadae nikachoka nikaamua kumwacha aendelee na mambo yake.

Sasa huyu Mchumba wangu ambaye nimeamini kuwa ananipenda labda aje abadilike hapo baadae nami nampenda pia lakini kila nikikutana nae njiani yule Ex ananiambia kua anaomba turudiane kwani amejifunza na amejua umuhimu wangu.

Anadai kila mwanamke atakae mpata anakuwa nae siku chache tu baada ya kugundua kua anamwanaume mwingine, na mimi nashindwa kumsahau kabisa na kila nimwonapo huyu Ex mwili wangu wote unasisimka.

Sijajua nifanye nini ili niweze kumsahau kabisa japokuwa alinitenda lakini nahisi kama kuna hisia zimebaki, naombeni ushauri wenu wadau japo kua najua wengine wataniponda hilo sinto jali zaidi nahitaji ushauri ili nijue njia ya kumsahau huyo Ex ili niweze kufunga ndoa kwa amani na Mchumba wangu wa sasa.

Asanteni
Mwanablog"

Dinah anasema: Hey asante sana kwa mail yako. Kutokana na maelezo yako inaelekea kuwa wewe umeingia kwenye uhusiano mpya muda mfupi tu baada ya kuachana na Ex wako hali inayosababishwa wewe kushindwa kuelewa hisia zako.

Ikiwa tayari umechumbiwa na mwanaume unaempenda na yeye anakupenda kwanini upoteze muda na huyo mwanaume ambae anakuja kwako kwa vile tu kila mwanamke anaekua nae anakuwa sijui na nini? Mwanaume anakuja kwako na kutaka mrudiane kwa vile anakupenda sio kwa vile wanawake wengine anaokua nao wanakuwa na tatizo fulani!!! hii ni sababu tosha ya wewe kuhama mtaa kabisa achilia mbali kubadili njia ili usikutane nae.

Nini cha kufanya ili umsahau Ex: Kama inawezekana basi hamisha makazi, ikiwa haiwezekani basi tafuta namna ya kumkwepa kama ulivyofanya mara tu baada ya kuachana. Hilo Mosi.

Pili, hakikisha unapotoka unakuwa na mchumba wako au mtu yeyote anaejua uchumba wenu kwa sababu za "kiusalama" kwamba jamaa likikuona na mtu mwingine halitopata nafasi ya kuongea nawe kuhusiana na hisia za kale.

Tatu, epuka kukaa mwenyewe kwani kunaweza kukufanya uanze kukumbuka yaliyopita, hakikisha akili yako inafanya kazi kila wakati kwa kufikiria mambo mengine muhimu kama vile kazi/masomo, maisha yako ya baadae na nini ungependa kufanya baada ya kuolewa, mipango ya ndoa yenu, aina gani ya gauni, rangi, ukumbi, wageni n.k.

Nne, jitahidi kuzungumza na mpenzi wako kwa njia ya simu kila siku kabla hujalala hii itasaidia kutokuwaza Ex, ukizungumza nampenzi wak kuhusu hisia zenu za kimapenzi na jinsi mnavyopendana ndio yatakayotawala akili yako mpaka utakapo pitiwa na usingizi.

Nakutakia kila la kheri kwenye kumsahau Ex na hatimae kufunga ndoa namchumba wako.

Wednesday

Mume kanitelekeza kisa Ndugu zake, Je nina ndoa au sina Ndoa?-Ushauri

"Pole na kazi Dada Dinah,
Mimi ni Mama wa watoto wawili, nilifunga ndoa 2004. Kwenye ndoa yetu ikatokea upande wa mume wangu hawajanikubali sana. Siku zilivyosonga mbele kukawa hakuna maelewano kabisa nyumbani kati yangu na mume wangu.

Mwaka 2008 December, Mume wangu akahama nyumbani na aliniachia mtoto ambae kwa wakati huo alikuwa bado ananyonya, nilijaribu sana kumbembeleza arudi nyumbani lakini sikufanikiwa, kwa sasa anaishi Arusha.

Mwaka 2009 July mtoto wetu mdogo aliumwa sana kiasi kwamba nilichanganyikiwa, nilimueleza baba yake ambae ni mume wangu alienikimbia lakini hakuja kabisa kumuona mtoto. Toka 2008 alivyoondoka mpaka leo amesha kuja kututembelea kama mara mbili tu kwa madai kuwa Dar na Arusha ni mbali sana, hivyo hawezi kuja mara kwa mara kwani huwa anachoka.

Mara chache anatuma zawadi kidogo za watoto. Na toka aondoke ameshatuma kama laki tatu hivi na watoto wote wanasoma sasa, hajui naishije na watoto wanakula nini, yaani kwa kifupi hana habari na watoto wake.

Sasa dada naomba ushauri wako, unaona hapo kuna ndoa tena?
Mimi ninafikiria nitafute makazi yangu nihamae na watoto wangu kwani ninapokaa ni kwake yaani ni nyumba yake.

Kama watoto wakimkumbuka sana baba yao huwa nawadanganya, ila huyu mkubwa (5yrs) naona ameanza kuelewa kwani akiniuliza huwa namwabia hali halisi namuona kama ananza kuelewa na anapata uchungu sana.

In short naona kuliko niendelee kuumia moyo wangu ni better ni give up, nianze maisha mapya, nifanye juu chini nisomeshe hawa watoto na nijihesabu kuwa ni single parent.
Unanishaurije?"

Dinah anasema:Pole sana kwa yote unayokabiliana nayo, inasikitisha kuwa mumeo amefuata matakwa ya wazazi wake na hivyo kukuoa na kisha kukuacha "solemba". Kwasababu tayari mmekwisha funga ndoa na bado of course mko kwenye ndoa kwa vile hakuna Talaka iliyotolewa na kwa mujibu wa Imani za Dini, wewe kama mkewe na mama wa watoto wake unahaki zote za kubaki kwenye nyumba hiyo. Hiyo nyumba ni yenu na sio yake.

Kutokana na maelezo yako nadhani kinachomshinda kuja kuwaona watoto mara kwa mara ni mwanamke/mke mwingine anaeishi nae huko, Arusha na Dar sio mbali kiasi kwamba mtu ukatembee mara moja kila baada ya miaka miwili! Lazima kuna kitu kinamzuia kuja huko mara kwa mara bila "sababu ya msingi" hasa kama mwanamke alienae hajui kama jamaa alioa/anawatoto.

Kibinaadamu Dada mpaka sasa huna ndoa, ni kama vile jamaa amekuweka spea tairi kwamba yakimshindwa huko Arusha basi wewe upo hapo kwa ajili yake (wapo wanaume wengi tu wa Kitanzania wanafanya hivi).



Huyo mwanaume kama anajali maisha mema ya watoto wake hakika hawezi kukufukuza kwenye nyumba hiyo, lakini kwa vile sio muaminifu (amekukimbia) hivyo kumuamini kwenye masuala mengine sio kitu rahisi. Inawezekana kabisa siku moja akaamua kuiuza nyumba yenu alafu wewe na watoto kuhamishwa bila kupenda.

Sasa ili kujiondolea hofu na kuwa na uhakika wa mahali pa kuishi na watoto wako ni vema ukawahi kumtaliki mumeo (mpe Talaka), kisheria ndani ya Tanzania una haki hiyo. Ni vema ukienda Ustawi wa Jamii lakini tatizo la hawa jamaa wanakalia kesi za watu kwa muda mrefu sana. Pia TAMWA inawanasheria wazuri ila wanazile za "njoo kesho" nyingi na hivyo kucheleweza mambo.

Mimi kama Dinah nakutokana na uzoefu wangu na "Mahakama" ningekushauri uende moja kwa moja Mahakama ya Wilaya ya hapo unapoishi na kuomba kumuona Hakimu anaeshughulikia masuala ya Familia na ndoa. Ukipata nafasi ya kumuona (inategemea how busy she/he is) then muelezee matatizo yako ya kindo tangu mwanzo, maisha yalivyo hivi sasa na nia yako ya kutaka kumtaliki mumeo.

Mumeo anaandikiwa barua ya kuitwa Mahakamani ili Hakimu aweze kusikiliza upande wa pili na kupata ushahidi au sababu zilizomfanya jamaa akukimbie, baada ya hapo unaweza ukapewa nafasi ya kueleza nia yako ya kumtaliki mumeo au Hakimu anaweza kuisema moja kwa moja (kwa vile tayari umekwisha mueleza nia yako).

Kesi itaendeshwa kwa muda wa kati ya wiki 2 mpaka mwezi mmoja, inategemea kama mumeo atakuja Mahakamani na kuwa mbishi kuchukua/kubali Talaka kwa sababu zake azijuazo yeye au atataka kurudiana na wewe n.k.

Kutokana na urefu/umri wa ndoa kisheria mali zinagawanywa kwa manufaa yenu wote wawili na watoto mliozaa, lakini wewe utapendelewa zaidi kwa vile umekuwa ukilea watoto peke yako kwa muda wa miaka miwili hivyo ni wazi nyumba itakuwa yako pamoja na mali nyingine zinazowahusu ninyi kama wanandoa tangu 2004-2010.

Vilevile mumeo atalazimika kisheria (Mahakama itaamua) kuwa anatoa kiasi fulani cha pesa kila mwezi kwa ajili ya matunzo na elimu ya watoto, hata kama wewe unuwezo huo bado kisheria atalazimika kuchagia unless otherwise wewe mwenyewe ukatae.


Ikitokea umefanikiwa kuachana na mumeo kisheria, hakikisha hujengi chuki na mpe nafasi ya kuwaona watoto wake au watoto kumuona baba yako kila anapopata nafasi ya kufanya hivyo. Hakikisha watoto wanakuwa na uhusiano mzuri na baba yako.

Kumbuka tofauti zenu na chuki ya wakwe zako haziwahusu watoto waliozaliwa. Ikitokea watoto wanataka kujua kwanini baba hakai hapo nyumbani unaweza kuwaambia tu kuwa anafanya kazi mbali na siku akipata likizo atakuja kuwaona. Kamwe usiwaambie watoto kuwa baba yenu hawaenzi ndio maana hayupo hapa.....hakikisha unajenga uhusiano mzuri kati ya baba na watoto hata kama baba huyo anakuja kuwaona mara moja kila baada ya mwaka.

Talaka sio suluhisho na siku zote wanaoteseka ni watoto, lakini kutokana na unayokabiliana nayo Talaka itasaidia wewe kuwa huru kiakili na kuendelea na maisha yako kama mwanamke na vilevile kuwa na mahali penye uhakika ili kukuza watoto wenu.

Hongera kwa kuonyesha msimamo wako kama mwanamke, hongera kwa kusimama imara kwa watoto wako kama mama.

Nakutakia kila la kheri katika maisha yako na watoto wako.

Friday

Wakwe hawataki niolewe na Kijana wao, nahisi nina ujauzito-Nifanyeje?

"Za kazi dada, pole kwa kazi ya kuelemisha jamii.
Mimi ni mwanamke mwenye miaka 23 sasa, lakini bado sijabatika kuolewa japokuwa nina boyfriend ambaye nampenda sana ila tatizo limejitokeza hivi juzi alipoenda kuwataarifu wazazi wake kuwa anataka tufunge ndoa.

Wazazi wake wamekataa na kumwambia mke wa kwanza wa mtoto wao ni lazima wamkabidhi wao kama wazazi, baada ya mpenzi wangu kunipa habari hizo sikujua nifanye nini wala niseme nini kwake.

Yeye anadai kwamba ananipenda hawezi kuniacha, lakini nimvumilie kwa muda na ndani ya miezi miwili ili atimize mashariti ya wazazi wake kwanza kwanza ndio ajue nini cha kufanya, leo hii (Email imenifikia Dinahicius wiki iliyopita) ndio kaenda kuoa nami najihisi mjamzito ila yeye bado sijamwambia,

Naomba ushauri please, nifanye nini?"

Dinah anasema: Namshukuru mungu kwa sasa niko salama baada ya kukamatwa na Hay Fever na ndio maana nilishindwa kujibu swali lako mapema, samahani kwa hilo.

Pole sana kwa Mkasa unaokabiliana nao. Kwa kweli nashindwa kuamini kama kuna Makabila ambayo bado yanasisitiza/lazimisha watoto wao kuolewa na watu walioawachagua wao kama wazazi. Hili la mke wa kwanza atafutwe na wazazi alafu baada ya hapo ndio kijana aoe anaemtaka yeye ndio nimeliesikia hapa! Inasikitisha sana.

Nadhani kuna mawili hapa Moja, ni kuwa wazazi wanamlazimisha kufunga ndoa na binti waliomtafutia wao (Inanikumbusha wimbo wa Binti Kimanzi) kama kijana anaeheshimu wazazi wake na kuwaridhisha kwa kila hali ni wazi itakuwa ngumu kwake kutaaa matakwa yao (inategemea na Mila, Utamaduni wao na Uoga wake yeye kama mwanaume).

Baadhi ya wanaume hufunga ndoa za kulazimishwa na kuishi na wake zao ambao hawana hisia nao kwa muda bila kushirikiana nao kimwili na kuwapa vituko mpaka wake hao kuomba Talaka na baada ya Talaka jamaa huenda kufunga ndoa na yule ampendae ambae ni chaguo lake ambae aliendelea na uhusiano nae wakati yuko kwenye ndoa batili.

Kama hii ndio nia ya mpenzi wako then hakuna haja ya kuwa na wasiwasi as long as unajua nini kinaendelea na siku zote anakuwa kwako.....hii haikufanyi wewe kuwa the other woman bali unamsaidia kuridhisha wazazi wake. Kumbuka mke "mtafutwa" ndio the other woman....ukimsadia kufanya vituko ni wazi mwanamke yule ataomba Talaka mapema.

Pili, inawezekana kabisa kuwa huyu jamaa anashindwa kukuambia ukweli tu kuwa hataki kufunga ndoa na wewe kwavile sio "wife type", anakupenda sawa lakini haoni kama unafaa kuwa mke wake. Kuna wanaume wengi sana hasa Afrika wanatekereza zoezi hili, utakuna Girlfriend wake mzuri kwa kila hali na wamekua pamoja kwa miaka mingi lakini anaishia kuoa "kitu cha ajabu" (mwanamke ambae wala hawaendani) na baada ya ndoa jamaa ataendelea na Girlfriend wa zamani au kuwa na Girlfriend mwingine ambae wanaendana nje ya ndoa yake.

Hii ni kwa vile baadhi ya wanaume wa Kiafrika wanaamini kuwa mke ana viwango vyake tofauti na mpenzi mzuri alienae mwenye kujipenda, kupenda maisha, kujali na kujituma/jitegemea kiuchumi. Nadhani umewahi kusikia wengi wakisema Uzuri wa mwanamke sio sura bali ni tabia.....imani hii ndio inapelekea wanaume kuoa bila mapenzi au attraction na hivyo ku-cheat on their wives kwa kutokana wanawake ambao wanawavutia na pengine kuwapenda nje ya ndoa zao. Inasikitisha lakini ni ukweli.

Sasa, kwavile unahisi kuwa unamimba nadhani ni vema kama utamjulisha jamaa kuwa umeshika mimba, kama kweli anakupenda na anania yakufunga ndoa na wewe baada ya "kuridhisha wazazi" na anajali maisha ya mtoto wake atakaezaliwa mwakani hatoendelea na ndoa au hata kama ataendelea nayo na kufanya kama "Binti Kimanzi" kwamba mume hatoi ngono, hali chakula chake, halali nyumbani n.k basi itakuwa vema.

Lakini kama mjamaa yuko serious na mke "mtafutwa" na anataka ku-share kitanda na kum-treat kama mke then sahau kama alikuwa mpenzi wako, hakikisha anajua umebeba mimba ya mtoto wenu ili asaidie kwa matunzo na malezi ya mtoto hapo baadae.

Mtoto atakapozaliwa (Mungu akijaalia mwakani) utakuwa na miaka 24, bado ni binti mdogo na una nafasi kubwa sana ya kuweka sawa maisha yako na kumlea mtoto wako kwa mapenzi yako yote. Mungu atakujaalia na utakutana na kijana mwenye kujali ambae atakuwa mume mwema hapo baadae.

Ni vema ukajifunza kudadisi asili, mila na desturi za mpenzi wako mpya ili kujua taratibu za kwako. Hupaswi kumuuliza yeye mwenyewe bali zungumza/uliza watu wenye asili kama yake ili usirudie makosa.

Usijipe hofu kipindi hiki ambacho unakuza kiumbe tumboni, jaribu kutuliza akili na kumfiria zaidi mtoto wako huyo atakae zaliwa. Ingekuwa nchi zilizoendelea hakika jamaa wa huduma ya Afya wangekupa Ushauri Nasaha na kukupa nafasi kama unataka kuendelea kutunza mimba au kuisitisha ikiwa changa (mimba ya mwezi mmoja ambayo ni kijibulungutu cha damu kinakumbwa wa mbengu ya Apple na Kisheria nchi za Magharibi unaruhusiwa kutoa) kwa njia za kisasa na salama zaidi.

Kwa bahati mbaya Tanzania hatuna utaratibu huo japo kuwa watu wanatoa mimba kienyeji na kwa njia za kizamani ambazo ni hatari kwa maisha yako, hivyo nisingekushauri ufanye hivyo japo baadhi ya wachangiaji wamegusia hilo.

Nakushauri utunze hiyo mimba kama kweli ipo na lea mtoto wako kwa kusaidiana na baba yake.

Kila la kheri!

Monday

Alinichumbia lakini akaoa mwingine, sasa ananisumbua, nimkomeshe vipi?

"Nawasalimu wote,
Mimi ni mdada mwenye umri wa miaka 33 hivi na nina mtoto mmoja wa miaka miwili na nusu. Nilitokea kupendana na kijana mmoja hivi wa kichaga ila kweli alichonitendea sitasahau. Ukweli mimi nilimpenda kutoka rohoni na sikuangalia ana nini ila nilisikiliza roho yangu na nikampenda, na kwa wakati ule niliamini pia na yeye alikuwa amenipenda kwa dhati.

Tulikaa muda wa kutosha na wote kwa pamoja tuliamua kuanza process za kuoana na kwa wakati huo nilikuwa na miaka 28, basi tulikubaliana kuona na mipango mbalimbali ilianza ikiwa ni pamoja na kunivalisha engagement ring.

Mimi nilishauriana na wazazi wangu na ikaamuliwa shughuli ya engagement ifanyike nyumbani kwetu, na ndivyo ilivyokuwa. Baada ya engagement nilisafiri kikazi nikaenda Nje na nilikaa huko kama wiki nne hivi, wakati wote huo nilikuwa nalazimika kumpigia mchumba wangu simu mara kwa mara kumjulisha hali.

Baadaye nilirudi Tz baada ya kazi iliyonipeleka huko kuisha. Kama mwezi hivi tangu nirudi nikagundua kuwa nilikuwa mjamzito, sikushtuka nilijua kisingeharibika kitu kwa sababu nilikuwa nimeshaweka mambo wazi.

Wakati huo nikaanza kupata tetesi kuwa huyo kaka ambae sasa ni mchumba wangu alikuwa ana uhusianao na mama mmoja aliyekuwa ameachika kwa mume wake akiwa na watoto watatu, hivyo huyo kaka alikuwa akiishi kwa huyo mwanamke, mimi sikuwahi hata kumshtukia kwa sababu pia mimi kazi zangu nyingi zilikuwa za kusafiri mara kwa mara.

Nilipofuatilia nilikuta ni kweli na ushahidi ni kuwa siku moja nilikamata wallet yake ikiwa na vyeti viwili vya angaza kimoja kikiwa na jina la huyo aliyekuwa mchumba wangu na kimoja kikiwa na jina la huyo mwanamke.

Kumbe walishakubaliana kuona, hata hivyo kulikuwa na picha ndogo ya huyo mwanamke kwenye wallet hiyo ya mchumba wangu. Nilipomuuliza alikana akasema sio wallet yake eti ni ya rafiki yake.

Niliendelea kukuza mimba yangu bila hata kupata msaada wowote kutoka kwake, na wakati huo ndio alikuwa akila maisha na huyo mwanamke aliyekuwa akiishi kwake na wakati huo huyo mwanamke alikuwa amemkabidhi Rav 4 ya Bluu, taratibu za kufunga ndoa na mimi zikawa zinapigwa chenga tu.

Kila nikimuuliza alikuwa hana jibu kamili, sasa na mimi nikaacha kumuuliza maana yake mtu mzima niliona kufunga ndoa sasa ni ndoto, siku moja kipindi cha Xmas huyo aliyekuwa mchumba wangu aliondoka na huyo mwanamke hadi nyumbani kwao Moshi kwenda kumtambulisha kwa wazazi wake hao hao waliomsindikiza kuja kwetu kunivalisha engagement ring ndio hao hao walimpokea huyo mwanamke na kukaa naye kwa muda wa wiki mbili.

Wakati akimpeleka huyo mwanamke kwao, nilikuwa nimebakiza wiki mbili tu kujifungua, Mungu akasaidia nikajifungu salama, na alikuja Hospitali, lakini hakutoa hata Shilingi moja na bili iliyokuwa inatakiwa ni 148,000.

Siku niliyokuwa natoka Hospitali alisingizia kuwa alikuwa anaenda Airport kumpokea rafiki yake lakini ukweli ni kwamba alikuwa ameenda kwa yule mwanamke. Hiyo haikuwa tatizo kwangu, kama niliendelea kujitunza mwenyewe kwa kipindi kile cha Ujauzito bila yeye kujishughulisha sitoshindwa sasa.

Huyo mwanaume alikuwa akija nyumbani kwangu na kutoa maneno ya kashfa na alikuwa akikuta mtoto amelala anamuamsha, haikuishia hapo, maternity ilipoisha, nilirudi kazini kwangu, na ndipo aliponifuata na kuniomba msamaha huku akalia.

Mimi nikamsamehe kwa sababu niliona labda hatarudia tena, basi nikampa sharti la kuhama ule mji tuliokuwa tukiishi mwanzo tukahamia mji mwingine na akafungua bisahara zake huko ambazo kweli ilibidi nimuongezee mtaji, niliamini angetulia.

Lakini kumbe haikuwa hivyo, baada ya kuona bisahara imekolea akaanza ufuska tena, na kwa kuwa mimi nilikuwa nafanya kazi field zaidi, basi kila nikisafiri alikuwa anaoa, wanawake wa kila aina, pete ya engenement aliyonivalisha akaichukua akamvalisha mwanamke mwingine tena, ikawa ni vurugu tu.

Nikirudi nyumbani nakuta Condom zimetumika zimetupwa chini ya uvungu, na siku moja nilikuta condom saba zilizotumika zimetupwa bafuni. Kweli ni story ndefu na siwezi kuandika yote. Niligundua huyu mwanaume alikuwa akipenda hela zangu sana kwani kila mshahara ukitoka anautaka wote hata senti habakizi, usipompa ndani hakukaliki.

Basi nilioona hali inakuwa mbaya nikaamua kuachana naye nikatafuta kazi sehemu nyingine nikapata, nashangaa alikuja katika huu mji ninaoishi akaulizia watu hadi akapajua ninaposihi sasa ameanza kunitishia, mara ataniua, mara atanifanya hiki na kile.

Shida yake anataka arudiane na mimi na baada ya mimi kuachana naye biashsra zake zimeyumba, manake hana msimamo ni kuhonga wanawake tu hana kai nyingine, na mpaka sasa mtoto ana miaka miwili na miezi 4 hajui anakula nini, anavaa nini wala anaishi vipi.

Sasa naomba mnishauri nimfanyeje manake nimeshatamani hata angetoweka duniani tu, maana hana anachofanya cha maana zaidi ya kunikosesha amani, mpaka sasa nimeamua kuishi na mwanangu tu. Naombeni msaada, ni nini naweza kufanya ili nimkomeshe.
Asante".

Thursday

Ex analazimisha nirudieane nae, nimekataa anatishia maisha yangu-Ushauri

"Habari dada Dinah! pole sana kwa kazi nzito uliyonayo ya kutusaidia kwa mawazo na kutuelimisha. Mimi ni kijana mwenye umri wa miaka 32 ni mwajiriwa wa Shirika moja hapa Dar.Nilipo kuwa Kidato cha 2, nilikuwa na mahusiano ya kimapenzi na dada mmoja, kwa ukweli nilimpenda sana.

Tulivyohitimu Kidato cha 4 kwa bahati mbaya mwenzangu hakuchaguliwa na mimi kuchaguliwa kwenda Kidato cha Tano, Wazazi wake waliamua arudie Kidato cha 3 Shule 1 ya Sekondari ambayo ilikuwa Wilayani na wakati huohuo mimi nilitakiwa kwenda kuendelea na masomo shule 1 huko Dar!

Kifupi ilikuwa siku ya majonzi kwetu kutengana kwani ndio ilikuwa mara yetu ya kwanza kuwa mbalimbali. Nashukuru Mungu nifanikiwa kumaliza Kidato cha 6 na mpenzi wangu alifanikiwa kumaliza Kidato cha 4! Mimi nilijiunga na Chuo Kikuu nae akaamua kwenda kujiunga na Chuo cha Ualimu.

Matatizo ya uhusiano wetu yalianza pale ambapo mwenzi wangu alimaliza na kupangiwa kituo cha kazi huko mkoa wa Tabora! kwani kwa kipindi chote ambacho tulikuwa mbalimbali tulizoea kupigiana simu angalau mara 3 kwa siku na hamna siku kupita hatujapigiana simu!

Baada ya yeye kupata hiyo ajira akawa hapigi simu hadi mimi nimpigie, nilikuwa naumia sana natabia ile mpya, siku 1 nikamwambia ukweli kwanini mimi ndio nimpigie simu na nisipopiga ndio siku hiyo hatuwasiliani? Akanijibu tena kwa ukali kuwa yeye kapelekwa huko(Tabora) kufanya kazi na wala sio kunipigia simu mimi.

Kwa kifupi yupo busy! Niliumia mno na jibu lile lakini kwa kuwa nilimpenda nilimuomba radhi kama swali lile limemuudhi, tukaongea mambo mengine tu. Baada ya miezi michache kupita, ghafla simu yake ikawa haipatikani.

Niliteseka sana ikabidi nimtafute dada yake ambaye yeye hakunificha aliniambia wazi kuwa mdogo wake(yaani mpenzi wangu) amefunga ndoa na anadai kaniacha mimi kwa kuwa sina future!

Nilihisi kuchananyikiwa nikawa kama siamini nachokisikia! Nilikubaliana na hali halisi japo iliniathiri kimasomo na ilinichukua zaidi ya miezi 6 kumsahau! Nashukuru nilimaliza Chuo na baada ya muda mfupi nilipata kazi nje ya nchi. Kitendo cha kuondoka Tz kilinisaidia kwa 90% kumsahau kabisa mwanamke yule na nimekaa huko miaka 4 nikachoka nikaamua kurudi Tz.

Niliporudi Tz nilianza kufanya kazi hapa nilipo(ilikuwa mwaka jana mwezi wa 8)!Mwezi February mwaka huu, asubuhi moja nikiwa kazini nilipokea simu kutoka kwa yule dada(Ex~girlfriend wangu) akadai kwa muda ule yuko Dar kaja kwangu kwani anamazumgumzo ya kina nami(kumbuka ni zaidi ya miaka 5 hatujaonana wala kuwasiliana).

Tukakubaliana, tukaongea mengi mojawapo ndio lililonileta kwenu ndugu zangu mnishauri, nalo ni:-Anadai kuwa kuolewa kule alilazimishwa na alikuwa hampendi yule mwanaume hata kidogo. Kwa kuwa alikuwa ananipenda mimi ndio maana ameamua kumwacha yule mumewe na kunifuata mimi!

Mimi nilimwambia ukweli kuwa; KWANZA ndoa ya Kikristo haina Talaka, PILI siwezi kuwa nae kutokana na ukatili alionifanyia! Wadau naomba ushauri wenu kwani sasa hivi imekuwa kero kwangu. Yaani mwanamke amekuwa akipiga simu na kutoa vitisho kuwa kama sitomkubalia basi atakunywa sumu nakuandika Waraka kuwa mimi ndio nimesababisha hivyo. Ili mimi nishikwe na Polisi na kutumikia kifungo kwa rest of my life.

Kwa ukweli mimi siwezi kurudiana nae hivyo naomba mnielekeze njia gani nizitumie ili niondokane na kero hizo! Kingine ni kuwa toka niachane na mwanamke huyu nimetokea kuwa chukia sana wanawake, sina hamu tena ya kuwa na mwanamke na ni mwaka 5 sasa sijawa na mahusiano ya kimapenzi na mwanamke!

Je hali hii ikiendelea ndio kusema sitooa tena na ukizingatia umri unaenda? Naombena msaada wenu ndugu zangu na akhsanten sana.
Collns H.M
Dar "

Dinah anasema:Kabla hatujapoteza muda, hebu chepuka kwenye kituo Cha polisi na ripoti vitisho kutoka kwa huyo Ex na waeleze sababu ya Mwanamke huyo kukupa vitisho hivyo, kisheria Polisi wanatakiwa kukulinda wewe kutokana na vitisho vya mwanamke huyo.

Kama anakufuata-fuata Ofisini au nyumbani kwako yeye atapewa barua kwa mujimu wa Mahakama kuwa haruhusiwi kukatiza karibu na wewe na akionekana eneo hilo (unapofanya kazi/ishi) polisi wanahaki ya kumuondoa kwa nguvu.


Sasa ikitokea kajiua atakuwa kajiua kwa matatizo yake mwenyewe na wewe utakuwa salama kwani Polisi watakuwa na maelezo yako yote. Hakikisha unapata copy (nakala) ya maelezo yako, jina na cheo cha Polisi aliechukua maelezo yako, muda (siku, tarehe na mwaka), na jina la kituo just incase polisi huyo atahamishwa au kupoteza ushahidi.

**********************************************************

Baada ya kutendwa na kuumizwa na mtu uliemuamini na kumpenda imekuwa ngumu kwako kuamini wanawake, sidhani kama unatuchukia wanawake wote bali hutuamini. Kuna hali fulani ya uoga wa mwanamke mwingine kurudia kilichofanywa na Binti uliempenda.

Kwa kawaida huwa nashauri mtu ajipe muda (kaa mbali na uhusiano wa kimapenzi) mpaka utakapo pona kabisa kihisia, kupona huko kunaweza kuchukua muda mrefu kuanzia miezi sita mpaka miaka saba. Urefu wa uponaji kihisia unategemea zaidi na muda wa uhusiano wenu.

Kama uhusiano...kwa Mfano: ulikuwa wa miaka miwili na zaidi kupona kwake huchukua muda mrefu pia. Kutokana na maelezo yako inaonyesha ulikuwa umepona lakini baada ya huyu mwanamama kuanza kukufuata fuata katonesha kidonda hivyo kukurudisha nyuma.

Hali hiyo ya "kuchukia" wanawake ikiendelea hakika hutoweza kuoa au tuseme kuishi na mwanamke unless other wise uamue kufunga ndoa na mwanamke ili kutimiza wajibu kitu ambacho ni hatari sana.

Ili kuepuka hilo wewe mwenyewe unatakiwa kuchukua hatua madhubuti za kukaa mbali na huyo binti "machafuzi" ili uweze kuendelea na maisha yako mapya, hilo moja.

Pili, unatakiwa kurudisha imani juu ya wanawake, kwani si wanawake wote tunatabia chafu. Kuthibitisha hilo angalia wanawake wote kwenye familia yako je wanatabia kama ya Ex wako? Hapana! sasa hiyo inamaana kuwa kosa la mwanamke mmoja halibebwi na wanawake wote Duniani. Kurudisha kwako imani juu ya wanawake ndio njia pekee ya wewe kuwa karibu na viumbe hao na hivyo kudondokea mmoja kimapenzi.

Ni matumaini yangu maelezo ya wachangiaji yamesaidia kwa kiasi kikubwa kufanya uamuzi wa busara ili uendelee kuishi kwa amani na hatimae kupenda tena.

Kila la kheri!

Wednesday

Niko nae kwa ajili ya mtoto wangu tu, sina hisia nae-Nitoke vipi?

"Hi dada dinah pole na kazi za kuisaidia jamii katika masuala muhimu ya maisha , mimi ni dada mwenye umri wa 25 nina mtoto mmoja wa miezi tisa sasa. Nimsomaji mzuri sana wa safu hii na nimefaidika sana katika suala zima la mapenzi.

Nilishawahi kuomba ushauri zaidi mara mbili na nilishauriwa vizuri nakutatua matatizo
yangu. Leo nimekuja tena kuomba ushauri katika haya yanayo nisumbua . Ninaishi na mchumba wangu ambaye ndio baba wa mtoto wangu huu ni mwaka wa pili sasa.

Nilikuwa nampenda sana ila sasa mapenzi yameisha kwani nina wasiwasi kuwa yeye hanipendi kutokana na vitendo vyake na pia hana samahani, hana pole, wala nakupenda tena wakati mwingine akikosa yeye atanigeuzia kibao mimi ndio niombe samahani.


Kwa mfano siku moja alilala nje ya nyumbani kwetu, aliporudi asubuhi sikumuuliza kitu nikakaa kimya, yeye alikwenda moja kwa moja kitandani kulala kwani ilikua 11 asubuhi na mimi kwakua usiku sikulala nikiwaza kapatwa na balaa gani nikarudi kulala, baada ya nusu saa hivi akaniambia oh kazini kulitokea wizi kwa hiyo haikuwezekana kuondoka.

Nikamuuliza mbona hujanitumia hata sms kua kuna tatizo limetokea unanipenda kweli?
akajibu "sikupendi! kwani nimekuletea mwanamke hapa ndani?akaniambia tena ndugu yako amewekwa ndani na kwakuwa ilikua Jumamosi hamna dhamana nika mwambia basi naenda kumuona huko nitaujua ukweli. Cha ajabu alikuja juu na kunikataza nisitoke nyumbani siku ile hata kwenda dukani hakutaka niende.

Dinah anasema: Kosa kubwa ulilofanya ni kukaa kimya, hii inaonyesha kuwa unamuogopa jamaa na yeye anajua kuwa unamuogopa na hivyo kuwa huru kufanya atakalo akiwa na uhakika hutosema kitu.

Tunapokuwa kwenye uhusiano na mnaishai pamoja technically mnakuwa mnaendesha maisha kama wanandoa hivyo kila mmoja wenu anakuwa na haki ya kuhoji mabadiliko yeyote yanayojitokeza Mf: uchelewaji, unajua muda wake ambao huwa narudi nyumbani sasa siku akichelewa kurudi katika hali halisi unapaswa kuhoji kwanini amechelewa au yuko wapi kwani muda umepita.

Aliporudi asubuhi yake, ulitakiwa kuhoji kilichomfanya alale nje na ungemwambia kabisa unataka maelezo ya kutosha na kuridhisha kwani kitendo chake kimekufanya ushindwe kulala kwa hofu, wasiwasi wa hali ya juu....sio kusema "kama kunatatizo ungeni sms".....alafu unaishia kuuliza "unanipenda kweli?".

Maelezo aliyokupa hakika hayaridhishi au niseme sio sababu ya kutosha ya kumfanya mwanaume mwenye familia na mwenye kujali kushindwa kuwasiliana na mpenzi wake na kumpa taarifa, kwa kifupi huyo mwanaume hana heshima juu yako na wala hajali hisia zako.

*********************************************************************

Siku nyingine tena nilituniwa sms na mwanamke akaniambia "hivi unajijua kua wewe ni bi mdogo tupo tulio anza?" nikamuuliza wewe nani? akajibu "siongei na mbwa naongea na mwenye kufuga mbwa", nikamwambia samahani maana inaonekana mimi ndio kikwazo cha wao kuwa pamoja akajibu "tuko pamoja wewe tu ndio ulikuwa hujui ila sasa umejua naona utapata presha".

Kwakuwa ile namba nilikua naijua toka mwanzo ni mdada ambaye tulikua tunakaa naye jirani ila alishahama nikaacha na naye, mume wangu aliporudi nilimuuliza na kumpa zile sms lakini cha ajabu aligeuka na kuniambia "hamuwezi kuniita mbwa kesho utaniambia vizuri la sivyo nitajiua au nitakuua nikafie jela" niliumia sana haijawahii kutokea.

Tangu siku ile sina tena wivu naye hata kidogo yaani hata akiamua kualala na mwanamke mbele ya macho yangu roho haini umi tena, niko hapa kwa sababu ya mwanangu kwani nampenda sana na sitaki ajeteswa na mama wa kambo.

Dinah anasema: Huna wivu kwa vile hakuna hisia za mapenzi juu ya mwanaume huyo, unajua wivu hujitokeza ikiwa kuna hisia kali za kimapenzi, sasa kama hakuna hisia za kimapenzi wivu utatoka wapi?

**************************************************************************
Imefikia mahali sasa kutoamini mwanaume hata siku moja, labda ashuke toka mbinguni lakini aliye zaliwa na mwanamke hapa Duniani sito thubutu kutoa moyo wangu tena. Huyu ndio aliye niingiza katika ulimwengu wa mapenzi nikamwamini sana lakini kwa sasa
nimemchukia zaidi ya upendo niliokua nao mwanzo.

Naomba mnisaidie ushauri je! niendelee kuishi na huyu mwanaume au ni toke nduki? Maana ninao uwezo mkubwa tu wa kumlea mwanangu bila baba yeke na kumove on with life all alone na sitopenda tena. Lakini nikiondoka mwanangu itakuaje maana sitaki kumuacha kwa kwa baba yake.

Dinah anasema: Huyu mwanaume aliekutambulisha kwenye Ulimwengu wa mapenzi ameumiza hisia zako vibaya mno na ndio maana umepoteza imani kwa wanaume kwa kunadhani kuwa wanaume wote wako hivyo, ukweli ni kuwa sio wote wanatabia za kishamba n akibinafsi. Wapo wanaume wametulia sana kiakili na wanajua kuthamini na kuheshimu wanawake.

Hamjafunga ndoa na huna hisia za kimapenzi juu ya huyu jamaa kutokanana vitendo vyake viovu hakika hakuna cha kupigania hapo ili ndoa isimame Imara! Nakubaliana na wewe kwenye kutoka nduki, tena wala usiangalie nyuma.

Kumbuka kuwa kuzaa sio uzee, wewe ni binti mdogo sana (nadhani unaona kina mama wa miaka 45-60 wanavyolazimisha ujana) sasa imagine wangekuwa na umri wako wa miaka 25? Tunza mtoto wako lakini kumbuka kuwa huyo ni baba wa mtoto wako na hivyo anatakiwa kuchangia matunzo ya mtoto wake na ana haki ya kumuona mtoto au mtoto kumuona baba yake. Hakikisha tofauti zenu zisisababishe mtoto kutomjua baba yake.

*****************************************************************************

Angalizo tu ni kwamba sina ndoa na huyu mtu, ilikua tufunge ndoa lakini mwezi ule ambao tulipaswa tufunge ndoa mama yake alifariki dunia na ndoa ikaahirisha na mpaka sasa hakuna kilichoendelea .

Nilimpenda sana na anauhakika siwezi muacha kwani nilimpa moyo wangu wote nilimfanyia kila kitu alichotaka, nilimtreat kama mtoto akiumwa naomba ruhusa kazini namhandle kama katoto kachanga na mlisha namuogesha namuimbia nyimbo hadi analala.

Inauma jamani ukimpenda mtu alafu akaku dissapoint kiasi hiki, yaani kweli sito penda tena! mwanzo na mwisho kupenda mtu anaye vaaa suruali. Naona niishie hapo maana machozi yanani tiririka kwa uchungu nilio nao kazi njema dada yangu.

Nitafurahi kama niyapata msaada wenu wa mawazo.


Dinah nasema: Pole dada mdogo kwa machungu unayokabiliana nayo, wala usilie kwani huyo mwanaume hastahili machozi kutoka kwa binti mrembo, mwenye kujali, ujuae kupenda na kijana kama wewe. Nimetoa maelezo yangu kutokana na maelezo yako hapo juu.

Ngoja nikupe kisa changu kilichotokea years ago ambacho natumaini kitakusaidia kuelewa situation yako. Mimi nilipokuwa nakua na hata kufikia umri wako nilikuwa mpinzani mkuu wa suala la ndoa, lakini hayo yote yalibadilika baada ya kushawishiwa na kimapenzi.

Wiki mbili kabla ya kufunga ndoa kuna kisa cha kifamilia kikajitokeza, nilikasirika sana na nikaomba ndoa ife, kwamba sikutaka kuolewa tena. Mdogo wangu wakati huo alokuwa na umri kama wako akaniambia " Da' Dinah mshukuru Mungu kuwa Mkasa huu umejitokeza kabla hamjafunga ndoa, huenda ni onyo juu ya huyo mchumba wako".

Nikaendelea kuishi na yule Mjamaa (mchumba) niliekataa kuolewa nae kutokana na issues za kifamilia....then from nowhere jamaa akaanza kuwa abusive(Emotinally as in masimango, lawama zisizokuwa na mwanzo n.k).....ikabidi nitoke nduki bila kuangalia nyuma...Lol! Nikaanza maisha yangu upya kama Mimi kwa kuhama mjini, kubadili kazi namtindo wa maisha yangu na baada ya mwaka na nusu hivi nikakutana na huyu ambae ndio Mume wangu wa sasa ambae ni mwema.

Ninachojaribu kusema hapa ni kuwa kuna mambo Mungu huruhusu yajitokeze ili kutufumbua macho, sasa mama yake alipofariki ndio pazia lilifunguliwa ili wewe uone ukweli wa tabia ya mchumba wako. Imagine mngefungandoa then alafu akaamua kuendelea na tabia zake chafu? Ingekuwa ngumu na ingekuuma zaidi ya inavyokuuma hivi sasa......Mshukuru Mungu amekuonyesha tabia halisi ya Mpenzi wako ambae soon atakuwa Ex.

Natambua kuwa bado unahasira sana, lakini ukijitoa kwenye maisha ya kunyanyasaji kutoka kwa baba mtoto wako utakuwa huru na utapenda tena.

Ni matumaini yangu kuwa maelezo ya wachangiaji wengine na nyongeza ya kisa changu halisi yatasaidia kwa kiasi kikubwa kufanya uamuzi wa busara na kuendelea na maisha yako.

Kila la kheri!

Friday

Tutadumu au ananipotezea muda tu-Ushauri!

"Habari dada Dinah! Pole na majukumu.
Hii ni mara yangu ya kwanza kuomba ushauri kwenye blog yako. Mimi ni mwanamke wa miaka 25, nina mtoto wa miaka 3.

Kwa sababu zisizozuilika nimeachana na baba wa mtoto karibu mwaka na nusu sasa. Baada ya hapo sikujihusisha na mwanaume yeyote yule hadi mwanzoni wa mwaka huu nilipotokea kupendana na kaka mmoja.


Penzi letu limekua kwa kasi sana lakini from the beggining nilishamwambia situation niliyokua nayo kabla sijakutana na yeye. Mwanzo ilimsumbua kwasababu hakutegemea,but after few days aliniita tukazungumza na tukakubaliana kuendeleza mapenzi yetu kwa kuwa my baby sio kipingamizi.


Mtoto wangu namhudumia mwenyewe kila kitu after all mimi nakaa kwa wazazi wangu ila yeye anakaa peke yake. Kinachonipa shida ni hiki MOJA -nakosa amani pale ninapoona anawachangamkia watoto wa majirani lakini wangu hamchangamkii kivile. Huwa ananiambia niende nae kwake kwavile weekends nashinda kwake kwakua wote hatuendi kazini.

Dinah anasema: Natambua kuwa ungependa mpenzi wako amchukulie mwanao kama mtoto wake lakini hiyo itakuwangumu kidogo hasa kama yeye mwenyewe hana mtoto, kwamba hana uzoefu wa kuwa baba.

Nadhani ni mapema sana kwa mpenzi wako kuanza kujenga mazoea na mtoto wako nahivyo kupelekea mtoto huko kumuita yeye baba, vilevile huenda anaogopa kuzoeana na mtoto huyo kwa vile hana uhakika na uhusiano wenu kwa maana kuwa ikitokea anamzoea mwanao kama mwanae na siku moja mkaachana ni wazi ataumia sana na pia mtoto ataumia kwa vile hawatopata nafasi ya kuonana tena.

Sidhani kama anachuki na mtoto wako ila inaweza kabisa inampunguzia ile hali ya kujiamini kutokana na ukweli kuwa kunamtu mwingine alifanya mapenzi na wewe na matunda ya mapenzi yenu ni huyo mtoto. ngumu sana kwa mtu yeyote kumchangamkia mtoto ambae sio wake.

Kumbuka kuwa mmekuwa pamoja miezi michache tu, na katika kipindi hicho kifupi sidhani kama ni haki kwakwe mpenzi wako au mwanao kuzoeana. Unatakiwa kuheshimu hisia zake na wewe kupunguza hali ya kujishitukia.

Yeye kuchangamkia watoto wengine zaidi kuliko mwanao haina maana kuwa hampenzi mtoto wako, kumbuka hao watoto wa jilani hawahusiani na wewe, hawakuzaliwa na wewe, hivyo anavyowachangamkia haina uhusiano wowote na mwanao, anawachangamakia na kuwapenda kama watoto.

Kama ambavyo sote tunapenda watoto wote bila kujali wazazi wao ni akina nani, lakini linapokuja suala la mtoto wa Ex wa mpenzi wako kidogo inakuwa tofauti, na ukikuta mtu anaonyesha kumpenda mtoto/watoto wako ndani ya kipindi kifupi tangu mkutane ujue kuna kitu nahitaji kutoka kwako na njia pekee ni kujipendekeza kwa watoto/mtoto wako.


MBILI -Siku zote za weekend ninapopika chakula nikiwa huko kwake, after eating he never says thank you au chakula kizuri/kibaya yaani ha-comment chochote. Sometimes nikitoka kazini nikimnunulia kitu cha kuvaa au hata take away sababu yeye hapiki na anarudi usiku he never says thank you.

Dinah anasema: Hii ni tabia ya mtu ambayo imejengeka kutokana na mazoea (inategemeana na mazingira aliyokulia) au kasumba iliyojengeka kutokana na mfumo dume, kwamba chochote kinachofanywa na mwanamke ni haki yake au ni wajibu wa mwanamke nahivyo hakuna sababu ya kushukuru.

Kuonyesha shukurani ni kitu muhimu sana kwenye uhusiano wa kimapenzi, na asante hiyo sio kwenye chakula, zawadi, ngono tu bali kwa kila jambo unalofanyiwa na mwenzio, hata ile hali ya yeye mpenzi kukujali unatakiwa kumshukuru, lakini kwa baadhi ya wanaume wetu wa Kitanzania inakuwa ngumu kwa vile hawajui.

Wakati wanakua baba zao (wazee wa Mfumo Dume) hawakuonyesha shukrani wala heshima kwa mama zao na hivyo wao kama watoto wa kiume wakadhani kuwa ni kawaida. Hivyo wajibu wako hapa ni kuweka wazi suala hili ili ajue kuwa unayomfanyia sio wajibu wako na wala sio haki yake bali ni mapenzi na hali ya kumjali, ni vema akaonyesha shukrani, akakuambia kama chakula kizuri au kibaya ili ujue wapi pa kuboresha au nini cha kuongeza, nini ununue na nini ukiepuke n.k.

TATU - Nikivaa nguo nzuri au nikipendeza hanisifii, yaani hana ile kusifia chochote changu.
Sasa napata mashaka why he is like this?au mimi ndio na-complicate mambo? kwangu mimi nahisi kuwa tabia yake sio normal.

Dinah anasema: Tabia yake ni ya kawaida sana kwa wanaume wengi tu hapa Duniani, kama nilivyosemahapo juu tabia hujengwa na mazoea sasa kama mazingira aliyokulia yalikuwa ya mfumo dume kwamba mwanamke haeshimiwi wala hathaminiwi inakuwa ngumu sana kwake kujua nini aseme kuhusu mwanamke, anachojua yeye ni kuwa mwanamke yuko pale kwa ajili yake, ampikie, amsafishie nyumba, amjali na kumridhisha kingono.

Zungumza nae na kuweka wazi hisia zako, alafu siku hadi siku anza kumsifia yeye na siku akivaa ovyo mwambie ukweli kuwa hajapendeza na bora abadilishe avae hivi au vile....hii itamsaidia kuelewa umuhimu wa kukusifia unapofanya jambo zuri au unapopendeza.

NNE, according to him anasema ananipenda, kuhusu future yetu pamoja hatujawahi zungumzia in deep but tuliongea one day. Kutokana na kuachana na baba wa mtoto wangu, naogopa sana kuwa na mwanaume lakini ndio hivyo mtu huwezi kuishi mwenyewe milele na ninampenda sana mpenzi wangu huyu wa sasa.

Lakini tatizo ndio hivyo simuelewi au niseme ni mimi ndio ninacomplicate things na kukosa amani.
Asante na naombeni ushauri nifanye nini, tatizo, ni langu au mwenzangu? Je kuna uhakika wa maisha ya mbele kama wapenzi?."

Dinah anasema: Asante sana kwa ushirikiano na uvumilivu wako, nimejaribu kutoa maelezo kwa kila swali hapo juu na hapa nitakupa maelezo kwa ujumla. Melezo yako kwenye kipendele cha nne yameonyesha kuwa wewe ni mdada mwenye uwezo mzuri wa kuchanganua mambo, umegundua kuwa tatizo ni wewe na sio huyo mpenzi wako japokuwa na yeye anavijitabia fulani ambavyo vinaongeza uzito kwenye tatizo ulilonalo wewe kama wewe.

Baada ya kuumizwa na hatimae kuachana na baba mtoto wako, umepoteza ile hali ya kujiamini na pia umekuwa ukifanya vitu kwa tahadhari kubwa (unajishitukia) kwa vile husingependa kilichotpokea kitokee. Hali hii inakufanya utamani au utake uhusiano ambao ni secure na commited au hata ndoa. Ni hali ya kawaida kwa mtu yeyote alietendwa na kuumia sana.....sasa hili ndio tatizo lako.

Uhakika wa maisha ya mbele hakuna mtu anaujua hata mtunzi wa kalenda hajui lakini siku zote sisi kama wanadamu huwa tunajitahidi kumuomba Mungu atupe uzima na aongeze baraka ili mahusiano yetu yasimame imara. Pamoja na kumtegemea Mungu pia sisi wenyewe kama pea (wapenzi) tunatakiwa kufanyia kazi ili mahusiano hayo yaendelee kuwa mazuri na yadumu kw amuda mrefu.

Kwa maana ninyingene najaribu kusema kuwa, kama unataka uhusiano wako uendelee na uwe na afya njema ni vema ukajitahidi kugundua tofauti za hisia za upendo kwa mwanao ambae ni sehemu ya mwili wako na mapenzi kwa mwanaume ambae sio sehemu ya mwili wako lakini anaumuhimu kwenye maisha yako.

Jifunze namna ya kuzungumza na mpenzi wako, namna ya kuwakilisha hoja zako, kujua mipaka kati ya mtoto wako na mpenzi wakoa ambae sio baba wa mtoto huyo (epuka kumzungumzia mtoto unapokuwa na mpenzi wako) ukiwa unamzungumzia mtoto kwa mpenzi wako itakuwa kama vile unamzungumzia Ex wako. Ni ngumu lakini jitahidi.

Umekuwa na mpenzi huyu mpya kwa takribani miezi mitano, mimi nakushauri upunguze speed kidogo ili u-enjoy maisha yako kama mama lakini pia ni binti mdogo wa miaka 25, kwani inaonyesha unaharaka sana hali inayoweza kuharibu uhusiano wenu usipokuwa mwangalifu kwani jamaa anaweza kuingia mitini kwa vile unampeleka-peleka, kumbuka wanaume wanapenda amani, hawapendi kulazimishwa wala kusukumwa-sukumwa.

Pamoja na kuwa umemhakikishia kuwa Ex hayupo tena kwenye maisha yako lakiniukweli utabai kuwa ni baba wa mtoto wako na mtakuwa na uhusiano fulani kwa ajili ya mtoto wenu kwani huwezi ukamkataza mtoto kuwasiliana na baba yake au baba yake kuwasiliana na mtoto wake.

Sasa wewe kuwa na mtoto ni headache kwake tayari kwani anaweza kuhofia mambo mengi kama vile....itakuwa vipi kama siku moja ikitokea jamaa anataka kurudiana na wewe kwa kisingizio cha mtoto wenu? huenda anafikiri kuwa itakuwa rahisi kurudiana kwa vile tayari mnamtoto......umewahi kufikiria hili, kujiweka kwenye nafasi yake ili ujue ni vipi anajisikia?!!

Mpaka sasa anajua kuwa wewe unamtoto na amekwisha muona au huwa anamuona mara kwa mara, wakati unajaribu kuhimarisha uhuaino wako vema kama utapunguza mawasiliano kati ya mtoto nampenzi wako, unapokwenda kwake kwa ajili ya weekend usiende na mtoto, nenda peke yako ili mtumie muda wenu kama wapenzi wakati mtoto atakuwa na bibi yake.

Acha kucheza kamchezo ka "a little family" kwa maana kuwa mnapokuwa pamoja ninyi watatu basi wewe unapata amani kuwa ninyi ni familia, ni mapema sana kwa hilo...mpe muda Mpenzi wako.

Ni rahisi kwa watu kusema ukipenda Boga penda na Ua lake, lakini wanasahau kuwa upendo kati ya mtoto amabe sio wako na mpenzi unatofautiana, Upendo unahitaji muda, upendo huwa haulazimishwi, upendo ni hisia na kama hisia hizo hazipo hakutakuwa na upendo....suala muhimu ni kwa yeye kumchukulia mtoto wako kama watoto wengine tu hapo jirani na kuheshimu nafasi ya mtoto kwako kama mama yake.

Natumaini umenielewa,kama kuna mahali nimekuchanganya tafadhali usisite kuniandikia nami nitafafanua. Jaribu kutembelea Makala za nyuma na baadhi ya maswali ili uweze kujifunza zaidi namna ya kuishi kwenye uhusiano na kuufanya uhusiano uwe na maendeleo na hatimae kuwa wa kudumu.

Kila la kheri!

Miaka 3....Happy B'day Dinahicous!


Dinahicious ni Blog ya kwanza inayozungumzia Ngono kwa undani na uwazi zaidi, imefanikiwa kwa kiasi kubwa, inajulikana zaidi kuliko miaka 3 iliyopita, inazungumziwa kwenye mitaa, sherehe na kwenye mikusanyiko mbalimbali.
Bila wewe Dinahicious isingefikia hapa, napenda utambue kuwa nathamini sana Ushirikiano wako kwa kutembelea, changia, kuuliza, kuizungumzia na kuiweka Blog hii kwenye Tovuti yako.
Katika kuadhimisha miaka 3, ningependa kukupa nafasi wewe mpenzi mtembeleaji, Msomaji na Mchangiaji (kwa kuuliza au kushauri) kutuambia umefaidika na nini hasa tangu tumeanza kukumbushana, fundishana, ambizana, shauriana, elekezana kuhusiana na masuala ya Kimapenzi, Ngono na Mahusiano?
Nakupenda sana!

Thursday

Uchoyo/ubahili wake unanipa hofu kama tutafunga ndoa-Ushauri

"Mambo Dinah mimi ni mwanamke mwenye umri wa miaka 27, ni mfuatiliaji mzuri wa Ushauri wako nina mpenzi yapata mwaka mmoja hivi sasa. Tumepanga tuje funga ndoa Mungu akijaalia.

Huyu mpenzi wangu sijui niseme ni mbahili, mchoyo au nimwitaje, maana kila wakati huwa analalamika hana hela hata tukitoka dinner anatanguliza kusema "yaani sasa hivi sina hela kabisa" hapo sijamuomba.

Kwa kawaida sina kawaida ya kumuomba hela yaani hata ninapokuwa nimepungukiwa au ninashida huwa namwambia anikopeshe halafu nitamrudishia baada ya muda Fulani lakini bado anasema hana hela.

Wote ni mfanyakazi na yeye anakipato kikubwa zaidi yangu. Naomba ushauri nifanye nini? nimsaidie vipi maana baadae asijekuwa mbahili hata kwa watoto wake."

Dinah anasema:Asante sana kwa ushirikiano na hongera kwa kuwa mmoja kati ya wanawake wachache wanaojitahidi kujitegemea kiuchumi. Ikiwa wewe una miaka 27, napata hisia kuwa mpenzi wako atakuwa kwenye miaka ya thelathini na kitu.


Kwa mwanaume yeyote kipindi hiki ndio pekee ambacho hudhani ni muhimu kujiweka sawa kimaisha kwa maana ya kufunga ndoa, kuwa na mahali pake pa kuishi, kuanzisha miradi ya kujiendeleza n.k. hilo moja.


Pili, inawezekana anamajukumu mengine kama ilivyo kwa sisi waafrika wote, kama wewe ni mkubwa kwenye familia yenu na umefanikiwa kupata kazi basi unachukua majukumu fulani kutoka kwa familia yako, inaweza kuwajengea wazazi, kusomesha wadogo zako n.k


Sababu ya tatu ninayoweza kuifikiria kwa haraka haraka ni Muda/wakati. Katika kipindi cha mwaka mmoja ni mapema sana kwake yeye mpenzi wako kuanza kukushirikisha kwenye kila jambo alifanyalo sio kwamba hakupendi bali hana uhakika kama yuko tayari kuweka wazi mambo yake binafsi labda kwa kuhofia kuwa utamkimbia kutokana na uwingi wa majukumu yake au utaendelea kuwa nae kwa kutegemea kupata kitu kwake na sio mapenzi ya dhati.

Pamoja na kugusia yote hayo hapo juu, inawezekana kabisa kuwa mpenzi wako ni mbahili, na hii inategemea na asili yake au jinsi alivyolelewa.


Nini cha kufanya: Kabla hatujampa hukumu ni vema tukajua ukweli wa mambo, je ni mbahili kweli? kuna jambo anafanya lakini anadhani ni mapema sana kukushirikisha? au kuna majukumu mengine ya kifamilia yanam-bana?


Ndani ya mwaka mmoja lazima utakuwa unajua kama jamaa anandugu ambao wanamtegemea ama la! Inawezekana kabisa ulidhani kuwa ni kitu ambacho hakikuhusu, lakini ni muhimu sana kujua watu wa karibu wa Mpenzi wako, sio lazima urafikiane nao au kuwafahamu kwa karibu bali kujua tu kuwa anawadogoz ake 3, anaishi na wazazi wake, kuna binamu n.k.


Ingekuwa mnaishi pamoja ingekuwa rahisi zaidi kwani mngegawana majukumu na kwa vile yeye anakipato kikubwa, angechukua jukumu la kulipia Nyumba na Bill ya umeme, wewe ukawa unashughulikia Bill ya maji, chakula na mahitaji mengine madogo madogo ya nyumbani na senti zinazobaki kwa pande zote mbili zinahifadhiwa kama akiba au inaenda kufanya jambo la maendeleo...kama mnajenga n.k.


Lakini kwa vile kila mtu anaishi kwake basi njia pekee ya kujua ukweli ni kutafuta muda mzuri wa kuzungumza nae kuhusiana na maisha yenu ya baadae kama wenza, tena ni rahisi zaidi kwa vile tayari mmepanga kufunga ndoa Mungu akijaalia. Wee anzisha maongezi haya kwa kuonyesha kuwa wewe ni "mama maendeleo" na hakikisha kila unalosema linauwingi kwa maana ya wewe na yeye.

Unaweza kuwakilisha hoja yako kwa utani Mf: mnatoka kwa ajili ya mlo wa jioni alafu yeye anasema sina hela.....cheka kisha muulize..."hivi kwanini wewe kila siku huna hela wakati wote tunafanya kazi? anaweza kukupa jibu la moja kwa moja kama kweli anamajukumu mengine au anaweza kusema "siku ikifika utajua kwanini huwa sina hela".....asipokupa jibu usijali kwani litabakia kichwani na atalifikiria jiono hiyo na usiku mzima na kukupa jibu atakapo kuwa tayari.

Au mpe kitu cheupe moja kwa moja....kwa upole na upendo lakini kwa kumaanisha, mwambie yote yalioujaza moyo wako, hali ya kujitegemea kiuchumi (kama ulivyosema hapa), mipango ya baadae, hofu yako juu ya maisha yenu na watoto hapo baadae n.k.

Maongezi hayo yatasaidia mpenzi wako kufunguka na kukuambia ukweli kama anasomesha ndugu zake, au anatunza hela kwa ajili ya kufunga ndoa, anajenga n.k. sasa ukipata ukweli kama ni mbahili au anamajukumu mengine tafadhali usisite kurudi tena hapa ili tujue namna gani tunaweza kusaidia kutokana na tatizo husika.

Kila la kheri!

Wednesday

Wifi na Shemeji walinishawishi nimuache mdogo wao, sasa najuta!-Ushauri

"Pole dada Dinah kwa kazi ngumu, mimi ni mwanablog wako wa muda mrefu. Nimesoma kisa cha dada Rhoda wa Mwanza aliye sex na shemeji yake na mimi imenitia moyo kusema ya kwangu ambayo na dhani ya kwake ni trailer sinema kamili iko kwangu.

Naomba nisitaje jina langu ila mimi ni mwanamke wa Kichaga nilikuwa na boyfriend wangu miaka ya nyuma ambaye wakati nakutana naye alikuwa anasoma Chuo kimoja hapa Dsm na mimi nilikuwa nasoma Chuo cha mambo ya Hoteli.

Tulikuwa tunapendana sana na kwa kweli yeye ndio alinitoa usichana wangu na kuniingiza katika ulimwengu wa mapenzi. Jamaa alikuwa ni mtu wa mazoezi so alikuwa fit everywhere kitandani. Mammbo yalienda vizuri mpaka kufikia maamuzi yakufungandoa atakapo maliza chuo na kupata kazi.

Kimsingi jamaa alikuwa ananitomba vizuri na alikuwa fit na mpaka niandikapo mail hii sijawahi kutombwa hivyo. Wakati jamaa anasoma alikuwa akiishi kwa kaka (baba zao ni mtu na mdogo wake)yake ambaye alikuwa ameoa na ni mfanyakazi Serikalini.

Lakini kwa bahati mbaya mke wa kaka yake alifariki wakati ambao mchumba wangu alikuwa amemaliza Chuo anatafuta kazi. Namwita mchumba kwa sababu process zote za kutambulishana tulikuwa tumekwisha zifanya.

Baada ya kaka mtu kufiwa na mke wake Wifi ambaye ni tumbo moja na kaka yake mchumba wangu akaanza kunishawishi nimwache mchumba wangu ambaye ni kama mdogo wake ili niolewe na kaka yake ambaye amefiwa na mke.

Kakamtu na dada yake (wifi na shemeji yangu) wakawa wanafanya kampeni kubwa ili mimi nimwache mchumba wangu ambaye ni mdogo wao kwa baba mdogo ili niolewe na kaka yake. Ikafikia mpaka kunidanganya kwamba mama yake mchumba wangu ambaye ni mama yao mdogo ni mchawi.

Nikaanza visa kwa mchumba wangu na baadae nikiamwacha ingawa alikuwa aninipenda sana na yeye alifikiria nimemwacha kwa sababu hana kazi kwani wakati huo alikuwa bado hajapata ajira. Nikaanza mapenzi ya siri na kaka yake bila yeye kujua na mchumba wangu huyo baada ya kunishawishi kwa muda mrefu turudiane akakata tamaa na kutafuta mchumba mwingine na alipopata kazi wakaoana.

Kwa bahati nzuri alihamishiwa Arusha kikazi ndipo mimi na kaka yake tukapata wasaa mzuri wa kuwa huru hapa Dsm na kuatangaza uchumba wetu. Kaka mtu alitumia nguvu nyingi sana kuhalalisha uchumba wetu ingawaje alipata vikwazo vingi sana kutoka kwa ndugu na jamaa waliokuwa wanafahamu kwamba mimi nilikuwa mchumba wa mdogo wake.

Kwa sababu ni mtu mzima (amenizidi miaka 12 kiumri) na ni mtu mwenye uwezo nyumba na magari hakupata vipingamizi vyovyote tukafanya bidii tukafunga ndoa.

Tatizo.
1.
Baada ya ndoa nimekuja kugundua mume wangu huyu hana nguvu za kiume na hii inatokana na uzito mwingi na kunywa pombe kupita kiasi. Mwanzoni wakati tunaoana nilidhania ni tatizo dogo kwa sababu tulikuwa hatuishi wote ila baada ya kunioa mwanume anakaa hata mwezi mboo haisimami.

Nimejaribu kuvumilia nimechoka, nimetamani kwenda nje ya ndoa lakini naogopa kwani mwanaume huyu anawivu na ananichunga sana. Nikikumbuka mchumba wangu wa mwanzo ambaye ni mdogo wake alivyokuwa aninitomba naatamani nimwache nimrudie ila jamaa hataki hata kuniona.

Nimejaribu kumtega hategeki na anaiambia hawezi kuingia kwenye shimo(kaburi) ambalo alishaingia akaokoka au ananiambia hawezi kuingia kwenye shimo moja na kaka yake. Mume wangu ananipa kila kitu nyumbani, chakula, magari, biashara ila mwanamke sitombwi nakaa hata miezi mitatu mume hajui kama nina kuma au sina.

Naombeni ushauri nifanyeje jamani kuachana tunashindwa kwa sababu ya nguvu tuliyo tumiaa kuahalalisha uchumba wetu na ndoa baada ya mimi kumwacha mchumba wangu ambaye alikuwa mdogo mtu.

Dinah anasema: Sahau Ex wako ambae ni mdogo Mume kwani umechelewa hivi sasa na yeye tayari anamke wake hivyo muache aishi kwa amani na hakikisha unadumisha heshima na thamani ya ndoa kw akutoingilia ndoa hiyo ili uwe mfano bora kwa vijana wengi ambao hawajafunga ndoa.

Huyu ni mume wako sasa, iwe uwezo wake wa kungonoka na mdogo au haupo kabisa haibadili ukweli kuwa ni mume wako ambae ulikula kiapo Mbele ya Mungu kuwa utakuwa muaminifu kwake, utaishi nae kwa uzima na maradhi.

Kutokana na maelezo yako ni wazi kuwa Pombe ni sababu kuu ya yeye kushindwa kukuridhisha kimapenzi, kwani pombe inapunguza nguvu za kiume kwa kasi ya ajabu hasa kwa wanaume wenye umri zaidi ya miaka 35.

Sasa wewe kama mke wake ni jukumu lako kuhakikisha jamaa aishi maisha yenye afya ili kuepuka matatizo mengine ya kiafya sio ngono pekee. Zungumza nae kuhusiana na tatizo lake la ulevi, nakuhakikishia akipunguza kunywa pombe uwezo wake wa kungonoka utakuwa mzuri tu.

Vilevile wewe unatakiwa kutuliza mawazo na akili yako juu ya huyo Mumeo na kuwa mbunifu zaidi na kumfundisha mbinu nyingine za kukuridhisha kingono na hivyo kuwa na uhusiano bora wa kingono ambao utawasogeza karibu zaidi na hivyo kuibua hisia za kimapenzi keati yenu...kumbuka ni Mumeo huyo.

2.Watoto aliozaa na mke wake wa kwanza ambaye ni marehemu wameisha kuwa wakubwa na hawanipendi na huwa wananiita Malaya kwa kuchanganya baba yao na baba yao mdogo hivyo ni ugomvi kila siku kwani walipokuwa wadogo walikuwa wanajua mimi ni mchumba wa uncle wao. Nikimwambia baba yao watoto hawaniheshimu anashindwa kuwakemea kwa sababu anawapenda sana.

Dinah anasema: Sio watoto tu wanaokuvunjia heshima nina hakika sehemu kubwa ya familia ya huyo Mumeo wanahisia mbaya sana juu ya uamuzi uliochukua. Huna haja ya kushitaki watoto kwa baba yao kwani wewe mwenyewe ulishindwa kujiheshimu siku ile ulipokubali kuwa mpenzi wa Shemeji yako.

Watoto hao sio tu anawapenda pia kuna huruma ndani yake, watoto kuendesha maisha bila mama yao hapa duniani ni ngumu tayari, sasa kwanini makosa yako mwenyewe yawaongozee ugumu wa maisha?

Jitahidi kuwa mvumilivu na siku ukiweza, jaribu kuweka wazi ni nini hasa kilitokea, waambie watoto hao ukweli kuwa wewe hukutaka kuolewa na baba yao bali baba yao na shangazi yao ndio waliokushawishi uachane na Baba yao mdogo kwa sababu ambazo mwenyewe na mumeo mnazijua. Hii itasaidia watoto hao kuelewa ukweli wa mambo na kupunguza attacks kwako, lakini haitorudisha heshima kwako.

3.Wifi yangu ambaye ndio alinishawishi niachane na mdogo wake niolewe na kaka yake amekuwa adui yangu mkubwa baada ya kuona maslahi aliyokuwa anayapata wakati anafanya kampeni niolewe na kaka yake hayapati tena baada ya mimi kuolewa ananiita mimi opportunist imefata mali za ndugu yake.

Dinah anasema: Mawifi wengi Duniani hivyo ndivyo walivyo, iwe wameshiriki kuharibu au kufanikisha siku zote mke wa kaka yao utakuwa adui tu. Achana nae na focus zaidi kwenye maisha yako na mumeo.

4.Shemeji yangu ambaye alikuwa mchumba wangu amezidi kuwa Handsome na mwili wake wa mazoezi namtamani mpaka namwota usiku anaitomba najaribu kumshawishi angalau anifanye chochote anachotaka mradi anitombe hata mara moja tu amegoma, amejaaliwa uume mkubwa, mgumu na mweusiiii ambapo mume wangu hata ikisimama hamfikii nusu kwani uume wake ni flabby and lazy.

Dinah anasema: Mamaa P hiyo ngono ya mara moja itabadilisha nini? Sana sana hizo dk 20 mpaka ufike kileleni zitamharibia jamaa ndoa yake ambayo sidhani kama angependa iharibike na ndio maana hashawishiki, kwa kifupi baada ya kutendwa na wewe sidhani kama atakuwa na nguvu za kumtenda mkewe na mtu aliemtenda....sijui unanielewa! Hivyo achakupoteza muda wako kumfirikia shemeji yako.

Of cause Ex wako utaendelea kumuona anavutia na anapendeza zaidi, ulimpenda na ulimuacha ukiwa bado unampenda. Mwenyewe umedai jamaa alikuwa fit sasa kama mkewe anamuangalia vizuri na kuhakikisha jamaa anaendelea kupendeza na kuvutia.....utalaumu kweli? Hilo ndio jukumu letu kuu kwenye ndoa....kuwatunza waume zetu kama wao wanavyotutuza sisi...hivyo na wewe fanya the same kwa mumeo. Kama ulikubali

Msinitukane jamani naombeni ushauri.

Ni mimi

P
Dsm. "

Dinah anasema: Asante sana kwa ushirikiano Dada P, nadhani wachangiaji wengi wamegusia points muhimu na hakika umezifanyia na somehow kusaidi kuanza kufanya uamuzi wa busara.

Hapo kuna mawili, Moja baki kwenye ndoa yako na jitahidi kumsaidia mumeo kuacha pombe ili uwezo wake wa kungonoka urudi na vilevile mfundishe/elekeze mbinu nyingine ili ajue namna ya kukurishidha kingono kwa kutumia njia nyingine ili kuongeza ukaribu wenu na kuibua hisia za kimapenzi.

Au, Mtaliki mumeo na kuendelea namaisha yako kama wewe, Mungu akijaali utakutana na mwanaume mwingine na ku-share maisha yenu. Lakini kamwe na ni marufuku kujipendekeza kwa Mume wa mtu, ulipewa nafasi ya kuwa nae lakini ukaichezea na kuipoteza, mwingine kaipata nafasi hiyo hivyo haiwezi kurudi tena kwako......waswahili walisema "Bahati haiji mara mbili".

Bibi yangu alisema " Jenga heshima kwa Ndugu na rafiki wa mumeo ili na wao wakuheshimu, kamwe usirafikiane nao kwa vile tu umeolewa na Ndugu yao"

......sentesi hii inamaanisha kuwa kinachoepusha hisia za kimapenzi kati yako na wanaume/wanawake wengine kwenye familia mbili tofauti ni HESHIMA.

Kila la kheri!

Pages