Monday

Baada ya Ultrasound na kujua umri wa mimba Mpenzi kaikataa!

Habari Dinah,

Mimi ni mmoja wa waenzi wa Blog yako ila leo ndio mara ya ngu ya kwanza kukuandikia nikihitaji ushauri au msaada wa kimawazo. Nina umri wa miaka 25, na ninamshukuru Mungu kuwa nina Ujauzito ambao siku yeyote naweza kujifungua kwani tayari niko kwenye my due date.

Tatizo ni huyu baba mtoto ambae anaumri wa miaka 28. Nilipokuwa na mimba yangu changa about a month nilitokea kumchukia sana na nikawa na hasira za karibu karibu kitu kilichopelekea mimi na yeye tukatengana.

Nikaendelea kutunza mimba yangu hadi ilipofikia miezi minne then nikataka kujua mwenzangu anampango gani, hivyo nikamuuliza. Yeye akaniita tukayaongea na kukubaliana kwamba tutalea mwanetu nahivyo penzi likaanza upya.

Tukaenda kuangalia Ultrasound ikawa inasema Mimba ina miezi mitano na sio minne, tukarudia tena ikasema hivyo hivyo, yule mwanaume akaanza ku-doubt nakujiweka mbali kidogo na mimi. Kumbe sisi tulivyokuwa tunahesabu ni tofauti na wanavyohesabu wataalam.

Kumbe mimba inahesabiwa kuanzia siku ya mwisho ya Hedhi (last date of period) na sisi tulikuwa tunahesabu kuanzia siku ya kwanza ya kukutana kimwili (Date of Conception) so ikawa inatusumbua ila mimi nilikuwa na hakika kuwa yeye ni baba kwa sababu yeye ni mwanaume pekee niliyefanya nae mapenzi, sina mwanaume mwingine.

Cha kushangaza mwenzangu akaanza visa na pia nikagundua kuwa anatoka na mwanamke mwingine, nilipouliza kulikoni? akanijibu kuwa yuko serious na huyo mwenzangu, pia akadai kuwa hana uhakika kama mtoto ni wake. Kaendelea kusema kuwa hayupo tayari kuzaa kwani hajajipanga.

Niliumia sana, nikatafuta Daktari nakumuelezea na yeye akanielewesha namna ya kuhesabu tarehe kwa mara ngingine tena nikagundua kuwa mimi na baba mtoto tulikuwa tunakosea kuhesabu tarehe, basi nikamuandikia Email ndeefu baba mtoto wangu na kumueleza yote na pia kumuomba aende kwa Daktari yeyote ampe tarehe zetu za kukutana kimwili then tarehe yangu ya mwisho ya kupata hedhi ili apate ukweli. Naamini kuwa alifanya hivyo ila hakutaka kuniambia ili akwepe majukumu.

Baada ya muda nikawa namcheki ili aniambie amefikia wapi? akadai hawezi kuamua sasa mpaka mtoto azaliwe, cha kushangaza kazini kwao na kwa marafiki zake anatangaza kuwa mtoto ni wake. Nimehangaika mpaka sasa nakaribia kujifungua bila msaada wowote kutoka kwake, nilipokuwa najaribu kuomba msaada alikuwa akinijibu kijeuri au kukaa kimya.

Kanifanya niwe mpweke sana kwani kipindi cha mimba ni kigumu na kinachohitaji support ya hali ya juu. Nasikia kutoka kwa watu wengine kuwa anataka kuja kuomba amjue mtoto atakapo zaliwa, ila mimi nina hasira sana na sitaki hata kumuona.

Naomba ushauri wa kujenga na sio kubomoa wala sio matusi, huyu mtu ni wa kumsamehe kweli? na je tunahitaji mtu kama huyu kwenye maisha yetu (mimi na mtoto)?

Asanteni"

1 comment:

Unknown said...

Aisee.. story yako imeniumiza sana na imefanya nipate kitu new maana na mimi nilikua sijui jinsi ya kuhesabu ivo, ila cha msingi ni kumsamehe tu, huyu ni mume wako na atabaki kua mume wako atausipo taka kuishi nae, mimi ushauri wangu kaeni chini ongeeni pia msamehe maana nae binadamu anayo haki kusamehewa maana makosa yapo makubwa zaidi ya hayo watu wanafanya but most of people they forgive and start afresh. Msg: mpende baba wa mtoto wako

Pages