Tuesday

Sitaki kumpotezea muda na nimekuwa honest,lakini hanielewi-Ushauri

s"Dada Dinah, ni mara yangu ya kwanza kukuandikia lakini nimekuwa nafuatilia sasa blog yako hii na kwa kweli ni kitu ambacho tunakihitaji sana kwani inasaidia sana kufumbua matatizo mbalimbali ya kimapenzi.

Sasa mimi nina mpenzi wangu ambaye tumekuwa mbali kwa muda wa miaka mitano hivi, kutokana na mimi kuwa nje ya nchi. Katika kipindi chote hiki tumekuwa katika mawasiliano ya mara kwa mara ambayo kwa kweli yamesaidia kuweka live penzi letu.

Sasa kwa jinsi mambo yalivyo ukiwa nje ya nchi ni kwamba mambo yanaweza kuwa unpredictable sana, kwani kutokana na mambo yanavyokwenda sioni kama nitaweza kurudi nyumbani hivi karibuni, kwa kuzingatia hilo na pia kwa kuzingatia kwamba umri unakimbia sana mimi nina miaka 31 na mpenzi wangu ana miaka 30 nikaona kuwa itabidi kuchukua maamuzi mazito.

Kwahivyo nikamwambia mpenzi kuwa mimi naona kuwa ni vizuri kama kila mmoja wetu akaamua kumove on ikitokea kuwa atapata wa kumfaa ili isije ikafika kesho na kesho kutwa tukaza kupeana lawama kutokana na ukweli kuwa labda nikarudi nyumbani tukakuta kuwa hatuwezi kuishi pamoja sababu labda wote wawili tumebadilika sana kwani tumekuwa mbali mbali kwa muda wote huu kufikiria kuwa tungeishi pamoja.


Nilipomueleza hivyo mwenzangu aliumia sana na ikawa akinitupia lawama mimi kuwa eti labda nimepata mwingine na ndio maana naamua kumtosa, lakini kwa ukweli ni kuwa mimi nilikuwa naangalia picha nzima kwamba tusiwe tunapotezeana wakati kwani umri wetu ndio unakimbia.

Kwa jinsi mwenzangu alivyo react ni kwamba hakubaliani na hilo na kwakweli ameumia sana kitu kilichonifanya nijidoubt labda uaamuzi niliochukua si sahihi kwani imefikia mahali inaniumiza kichwa sana. Ukweli ni kuwa I do care for her lakini inabidi mara nyingine uangalie jinsi hali halisi inavyokwenda katika maisha.

Sijui wewe na wadau wengine mnaonaje kuhusu swala hili, naomba msaada na mawazo yenu wote. Ahsante sana na samahani kwa mail ndefu kama hii, tuendelee kuelimishana katika swala zima la mahusiano"

Dinah anasema:Asante kwa kuniandikia, nadhani kosa ulilofanya hapa ni kufanya uamuzi ulioegemea upande mmoja tu (upande wako peke yako) bila kumuhusisha yeye (mpenzi wako), umefanya uamuzi kisha ukampa matokea....yaani hamkuzungumza na wote wawili kukubaliana kumaliza uhusiano au kutafuta namna nyingine ili uhusiano wenu uendelee.

Mwanamke yeyote mwenye mwanaume Ulaya anatarajia Big, sasa unapomuibukia na kumaliza uhusiano ktk mtindo huu, kidogo inakuwa ngumu kuamini, kuelewa na kukubali.

Kumbuka mko kwenye uhusiano na kama walivyogusia baadhi ya wachangiaji, inawezekana katolea nje wanaume wengine wengi tu kwa ajili yako kwa vile aliamini kuwa siku moja mtakuja kuishi pamoja.

Mimi nakushauri, uzungumze nae na umpe picha kamili ya maisha ya huko uliko. Kwasababu, watu wengi hapa nyumbani hawajui ni kiasi gani maisha yanaweza kuwa magumu huko Ughaibuni (ugumu interms of kutoruhusiwa kutoka nje mpaka wakurudishie kitabu chako, unaweza ukasubiri milele*).

Ukiweka wazi ni nini hasa kinakuzuia wewe kusafiri au hata kurudi nyumbani kwa sasa na hujui lini utaweza kufanya hivyo, akikuelewa ndio uanze kuzungumzia suala la uhusiano wenu. Hakikisha unampa nafasi yeye kukuambia msimamo wake na nini hasa anataka out of uhusiano wenu....msikilize kwa makini. Kisha mpe maelezo kutokana na matarajio yake au atakayo out of uhusiano huo.

Weka kila kitu wazi, kama kuna uwezekano wa yeye kukufuata uko nini afanye na kama hakuna mwambie kwa uwazi kabisa kwanini haiwezekani, kwa sababu kibongobongo wapenzi hutegemea sana kupandishwa majuu lakini hawajui urahisi na ugumu wake.....sasa mpe hali halisi.

Hakuna uwezekano wa kukufuata na huna mpango wa kurudi Bongo sasa:
Mwambie hali halisi kuwa, umri aliofikia wanawake wengi hupenda kuanza kujiandaa na ndoa, kuanza familia n.k. na wewe ungependa kufanya hivyo lakini unasikitika kuwa hutoweza kutimizia hayo kutokana na umbali na mambo yanavyokuendea huko uliko. Muombe radhi kwa kumpotezea muda kwani mipango haikuwa kama ulivyotarajia.

Akikubaliana na wewe, ahidi kuendeleza urafiki na wasiliana nae kila upatapo muda. Akiendelea kutokukuelewa na kukutupia lawama then punguza mawasiliano kama sio kuyakata kabisa.

Kila la kheri!

No comments:

Pages