Tuesday

Mwanamke ni "Victim" 2 & 3!


2-Tumuone mwanamke huyu ktk kuzuia mimba.

Mwanamke siku zote ndie anaeachiwa swala la kuzuia mimba, sote tunafahamu wazi kabisa kuwa matumizi ya madawa haya ya nabadili afya ya mwanamke, yanabadili utaratibu mzima wa kupata damu ya mwezi (hedhi) kwamba kuna baadhi ya wanawake huenda mara mbili hadi tatu kwa mwezi.


Wengine hawaedi kabisa (jiulize damu hiyo inakwenda wapi wakati ni lazima itoke ikiwa yai halijarutubishwa) hali hiyo husababisha mkanganyiko wa chembechembe asilia na hivyo kusababisha SARATANI ndani ya mwili au kutopata mtoto/watoto tena….kila ukipata mimba inachoropoka (inatoka sio kwa kudhamilia) n.k.


Linapokuja swala la kumalizia ndani mwanaume hujitoa kabisa na kusukuma jukumu lakuzuia mimba kwa mwanamke. Natambua kuwa hakuna madawa ya muda mfupi yakuzuia mimba kwa wanaume lakini kuna bidhaa ambayo ikitumiwa vilivyo mimba itazuilika, sasa kwanini bidhaa hii (Condom) isitumike kwa nyote wawili badala ya “kusakizia” mwanamke jukumu hilo as if yeye ndio mhusiaka mkuu wa kupata ujauzito?


Ile tabia au niseme kasumba ya “situmii condom kwa vile inapunguza ukaribu wangu na mke/mpenzi wangu” haina ukweli wowote, kuwa karibu na mpenzi/mkeo wako sio lazima umalizie ndani au ugusanishe ngozi yako ya uume na ngozi yake ya uke kwa ndani!



Kitendo cha wewe kufanya nae mambo mazuri na kwa ufundi yatakayowafikisha kwenye hatua hiyo tayari ni ukaribu, jinsi unavyo zungumza nae, jinsi uanvyomshika, unavyomheshimu, mthamini, unavyo onyesha mapenzi,msikiliza n.k. wakati mnafanya tendo hilo takatifu ndio mambo yatakayo kufanya uwe karibu nae a.k.a “Intimately” na sio kupiga bao ndani.


Mwanaume jaribu kuwa mbunifu na mtundu ktk anga nyingine ili kuwa “Intimate” na mkeo/mpenzi wako zaidi ya nyama 2 nyama ili kuepuka mimba na wakati huo huo kumsaidia huyu mama kulinda afya yake ili asiendelee kuwa “victim” ktk uhusiano wenu.



3-Tumuangalie mwanamke huyu ktk Ufungaji wa kizazi.

Baada yakujipatia watoto Fulani ambao mnadhani kuwa wanawatosha au ndio manaweza kuwamudu na hivyo kufanya uamuzi wa kufunga kizai 4 good ili muweze kufanya mapenzi bila kuhofia mimba/mtoto tena, kama kawaida Mwanamke husukumwa akafunge kizazi.


Mwanamke huyu sina uhakika kama ni kasumba, ujinga, kutokujua, kuwa tegemezi au? Habishi “in good way” wala haulizi/hoji kwanini yeye ndiye anaepaswa kufanya hivyo na sio mumewe/mpenzi wake au wote....waende mguu kwa mguu kwenda kufunga kizazi?.


Mara nyingi (nimeshuhudia kwa masikio yangu) mwanaume anakuja na sababu kama “watoto wakifa kwa ajili au magonjwa na nikataka kuzaa tena nitafanyaje?”…..Ukifa (mke) na nikaoa/kutana na mwanamke mwingine na akataka kuzaa na mimi nitamwambiaje?”…..ikitokea tumeachana (peana talaka) na nikaoa tena nakutaka kuzaa na huyo mwanamke nitafanyaje?”……

Sasa huoni kuwa sababu zako za “kibinafsi” zinamhusu pia mwanake huyo? Hayo yote yakitokea kwake yeye atafanyaje?

Nitashukuru kama nitapata maoni, mawazo, maelezo tofauti kuhusu hili au ukiweza ushauri zaidi kutokana na uzoefu wako……sote tunajifunza na nivema tukiweka mambo wazi ili tujifunze kwa kina zaidi.

Asante sana kwa ushirikiano.

No comments:

Pages