Tuesday

Wakati mwingine simpendi!...ushauri!

"Mambo dada yangu naomba nitoke nje ya maada kidogo mimi mdogo wako nahis nina matatizo maana nina boyfriend wangu ambaye tunapendana sana ananipenda na mimi ninampenda ila sometimes inantokea mimi ule upendo unaisha kabisa.

Anakuwa hajanifanyia kitu ila nakuwaa simpendi kabisa yaan hata kuongea naye nakuwa sipendi, hata kumuona nakuwa sipendi sasa nimeanza kuogopa sana je hilo ndio chaguo langu au sio maana naogopa inaweza ikaniletea problems huko baadaye.naomba ushauri wenu jaman.asante".

Jawabu: Usiogope kuhusiana na chaguo kwani ktk maisha ya kimapenzi mnayoendesha sasa swala la chaguo halipo kwani tayariumechagua nandio maana uko nae.....swala hapa ni mapenzi yako juu yake na mapenzi yake juu yako.

Hilo ni tatizo ambao wanawake wengi wanalo huwa tunaambiwa ni "moody" (sina hakika kama ndio kisirani) na kwa baadhi huwa ni "extream moody" hali inayonifanya wakati mwingine niwaonee huruma wapenzi/waume wao.

Sidhani kama humpendi ila kutokana na uchache wa maneno ktk lugha yetu ya kiswahil inabidi utumie neno hilo "simpendi" lakini katika hali halisi kinachokutokea ni kutokufurahishwa nae au niseme kuna wakati unahisi "you dont like him" kwamba hutaki kuongea, akikuangalia basi ni kosa, akikusemesha basi kwako itakuwa kama anakuchokoza au anatafuta visa lakini "you love him" kwamba moyoni mwako unampenda kwa dhati kabisa.


Hii inaweza kusababishwa na mambo mengi kama vile usumbufu wa kiakili unaosababishwa na msongomano wa mambo yakikazi, kiuchum, kimaisha kwa ujumla lakini kuu kabisa ni mabadiliko ya homono zako kama mwanamke.


Ukijichunguza vema utagundua hali hiyo inakutokea mara nyingi unapokaribia siku zako za hedhi, ukiwa uko ndani ya hedhi au baada ya kumaliza hedhi, hakuna dawa bali ni yeye mpenzi wako kulitambua hilo ili aweze kuepuka vijimambo ambavyo vitakufanya uhisi humpendi I mean "dont like him" sio "dont love him".

Lakini kumbuka tu kuwa wewe ndio mwenye tatizo hilo hivyo ni wewe ndio unapaswa kujitahidi kukabiliana na hili na kuzuia kum-push away mpenzi wako tangu useme mnapendana kuwa mwangalifu kwani kupata mwenza unampenda na yeye anakupenda sio lelemama, trust me hutohitaji kupoteza hilo.

No comments:

Pages