Saturday

Namuonea huruma Soon to be Ex Wife-Ushauri

"Heloo dada Dinah, pole sana kwa kazi. Nimeona nikutumie hii mail kwa ajili ya ushauri.
Tatizo langu ni kwamba dada, mimi ni mdada wa miaka 24 nimeajiriwa. Huwa napenda sana kutembelea blogs mbali mbali na kuchat katika pita pita hizo nikakutana na mtu (Mwanaume) tukawa tunawasiliana aliniambia kuwa ana mtoto ila mama wa mtoto wametengena na yuko nje ya Tanzania kaolewa na Mwanaume mwingine na wamezaa.

Tuliendelea kuwasiliana kwa simu na kuchat kupitia internet hadi ilipofika siku tukaonana. Baada ya kuonana siku ya kwanza tuliendelea kuwasiliana kwa simu na pia kupanga miadi ya kuonana tena na tena hadi siku aliponitamkia kuwa anapenda niwe mpenzi wake.

Kiukweli nami pia nilimpenda ila kwa wakati huo nilikuwa kwenye matatizo na mpenzi wangu wa awali so nikaona haina haja ya kuendelea kuteseka wakati tayari kuna mtu anaonesha kunipenda kwa dhati.Basi tukawa wapenzi.


Tatizo lilianza pindi mpenzi wangu wa awali alivyogundua kuwa nina ukaribu na huyo mjamaa ambae kumbe anamfahamu. Siku moja akanipigia na kuniambia kuwa yule mtu ameoa tena kwa ndoa ya Kanisani na wanaishi wote na mkewe, nikamwambia mbona mimi ameniambia tofauti.

Basi ikabidi nimbane kweli huyu jamaa mpya nae akaniambia kuwa ameoa ila yeye na mkewe wana matatizo ya muda mrefu sana ambayo sio rahisi kusameheka na isitoshe huwa hawalali pamoja! na anachosubiri yeye ni ruhusa ya kupeana Talaka kwani swala lao limeshafika mbali.


Kwakuwa alikuwa ananionyesha mapenzi ya dhati, nikawa niko tayari kuendelea naye hapo nakiri kweli nilikuwa mdhaifu kwani nilistahili kuachana naye baada ya kugundua ukweli lakini tatizo ni kwamba tulishakula kiapo kuwa hatutaachana kwa namna yoyote ile.

Hadi sasa tuna muda wa miaka miwili. Ushauri niutakao ni je, niendelee na huyu mtu au niachane naye??? kwanini nataka ushauri wa hivyo ni kwa sababu nafsi inamuonea huruma sana mkewe ingawa kiukweli anaonekana wazi kuna kitu kikubwa alimkosea mumewe kwani mara nyingi huwa anamuomba msamaha naona hayo kwenye simu yake na pia huwa anapiga na huyu kaka huwa anaweka loudspeaker nami nasikia.


Ameahidi pindi atakapotengana na mkewe yuko radhi kunioa, hilo pia nahofia kwa kuwa sijui namna ya kuieleza familia yangu kwani itabidi niweke wazi kuwa alikuwa mume wa mtu kabla hawajasikia kwa watu.

Kwetu mimi ni mtoto wa pekee wa kike. Samahani kwa mail ndefu, na sijui kama nitakuwa nimejielezea vizuri ukanielewa ila kama utakuwa na maswali ya kuniuliza ili uweze kunisaidia sawa unaweza kuniuliza nitakuwa tayari kujibu ili nisiendelee kuteseka.

Asante sana, kazi njema.
Lizzy"

Dinah anasema: Mdogo wangu Lizy, mtu akishindwa kuwa mkweli mwanzoni kabisa mwa uhusiano ni wazi kuwa daima hatokuwa mkweli kwako. Kutokana na maelezo yako huyu Jamaa alikuwa anam-cheat mkewe via internet (wako wengi sana hawa viumbe wake kwa waume wanao abuse maendeleo ya mawasiliano).

Ni wazi kabisa wakati unakutana na huyu jamaa kwenye mtandao ulikuwa kwenye wakati mgumu kimapenzi hivyo kuwa Vanulable hali iliyopelekea huyo mpenzi mume wa mtu kuchukua advantage na kukulubuni. Ili aku-win akaamua kukupa mapenzi ya dhati ambayo alijua kabisa unayahitaji kwa vile ulikuwa huyapati kutoka kwa Mpenzi wako wa awali.

Kama walivyosema baadhi ya wachangiaji na pengine wewe pia unajua hasa kama ni Mkristo, kwamba Ndoa ya kikristo daima huwa haivunjiki unless mmoja wa wanandoa hao afariki. Hata kama wametengana bado hawatoruhusiwa kufungandoa tena unless mmoja wako kafa......vinginevyo labda Serikali iingilie na Talaka itolewe kwa amri ya Mahakama lakini hata hivyo mpaka Hakimu anakubali kuamrisha Talaka inatakiwa kuwe na vithibitisho kuwa wanandoa hao wametengena kwa muda gani na lini hasa ilikuwa mara ya mwisho kufanya ngono.

Kama bado wanaishi pamoja lakini "hawalali kitanda kimoja" bado haitoshi kumshawishi mtu yeyote kuwa wawili hao hawana ndoa. Ndio maana siku zote wanandoa wakitengana hushauriwa kuishi mbali-mbali kwa muda fulani (nadhani miaka miwili or something) ili Talaka yao Kisheria baade ije kuwa Valid.


Kama Jamaa hampi mapenzi, attention wala affection kutokana na kutumia muda mwingi kwenye Internet na pengine nje ya nyumbani pale anapokuwa na wewe ni wazi kuwa huyu mwanamke anahai ya kudai au hata ku-demand vitu hivyo na kila akifanya hivyo mumewe anakuwa mkali na kuzusha mabaya juu ya mkewe kwa vile tayari amejenga mapenzi na wewe hali inayomfanya mwanamama huyo kuomba msamaha kwa mumewe.


Mimi na wewe hatujui undani wa maisha yao ya kindoa as hayatuhusu, lakini kama kweli huyu Jamaa angekuwa hana nia na mkewe na anataka kweli kumtaliki basi angekuwa muwazi tangu mwanzo kuwa anafamilia lakini uhusiano wao sio mzuri na sio kukudanganya kuwa Mkewe kaolewa nje ya nchi.....hilo Mosi. Pili, angekuwa anaisha pake yake mahali, Tatu angekuambia tangu awali kosa alilofanyiwa na mkewe ambali anashindwa kumsamehe.

Mmekuwa kwenye uhusiano kwa muda wa miaka miwili ikiwa na maana ulinza na huyu Baba ukiwa mtoto wa miaka 22. Ktk umri wa miaka 24, mimi binafsi nisingekushauri kujikita na kuendelea na uhusiano na mtu ambae tayari alioa/ameoa na watoto kwani haitokupa Amani kwenye maisha yako yote, hasa ukizingatia kuwa sasa umekwisha anza kuhisi guilt kila unaposikia sauti ya mke wa jamaa akiomba msamaha n.k.

Sio tu utakuwa unadhurumu ujana wako bali utakuwa umeumiza mwanamke mwenzio na watoto ambao walikuwa matunda ya ndoa yao. Si huyu jamaa wala yule wa zamani...wote hawakufai.

Nakushauri umalize uhusiano na huyo Mume wa mtu kisha anza maisha yako upya, kumbuka kuwa unahitaji mwanaume ili ku-share nae mapenzi na sio mwanamke mwingine wala watoto wao.

Kitu cha mwisho ningependa kukisema ni kuwa, huyo jamaa sio tu kuwa anaroho mbaya kiasi cha kushindwa kumsamehe mkewe kwa kosa analolijua yeye pia hana heshima kwa wanawake wote kwa ujumla kwa sababu zifuatazo:-

-Kukudanganya wewe mwanamke on your face.
-Kumuweka mkewe kwenye loudspeaker.
-Kukuonyesha sms za mkewe.

Ukiangalia points hizi kwa undani ni kuwa alikuwa anajionyesha kwako ni namna gani basi "anatakiwa na mkewe" hivyo ukileta ujinga wakati wowote atarudi kwa mkewe.

Kila la kheri ktk kufanyia kazi yote uliyoshauriwa na kwenye kufanya maamuzi ya busara.

No comments:

Pages