Thursday

Baba kanilea na kunisomesha, Mama anasema si baba yangu!!

"Hi Dada dinah nina matatzo sana hivyo I need your advice. Mimi ni kijana wa miaka 21, it is a long story but I wil make it short and clear. Ni kwamba, mimi nimezaliwa Kenya when my dady met with Mum there but walikuwa ni wapenzi yaani hawakufunga ndoa.


Nilipofikisha miaka 2, baba alinichukua nikaenda kuishi Moshi na bibi, anadai kuwa matunzo kwa mama hayakuwa mazuri. Tangu alivyonichukua hadi nafikisha miaka 17 Mama hakuwahi kuja kuniona wala hakutaka kujua habari zangu japokuwa hakuwa mbali sana yaani ni kiasi cha kutumia Tsh elfu3 kama nauli.


Nilipofikisha hiyo miaka kumi na saba ndio akaja kuniona. Kipindi chote nilikuwa naishi na baba tu kwani alirudi nyumbani. Sasa baada ya Mama kuja anadai eti yule niliyekuwa naishi nae na kuamini kuwa ni Baba yangu was not my father na kwamba my father is from Uganda but huyu Baba ndio ninayemfahamu, ndiye aliyenilea na kunisomesha mapka nilipofikia na hajajua hilo, kwamba mimi sio mtoto wake. Je nifanye nini?"

Dinah anasema:Pole kwa mawazo yanayosonga akili yako hivi sasa kuhusiana na ukweli juu ya nani ni baba yako wa damu. Ukweli utabaki kuwa mama siku zote ndio anajua baba wa mtoto ni nani?

Nasikitika kusema kuwa kuna akina baba wengi tu walilea na wanaendelea kulea watoto ambao Kibailojia au kidamu sio wa kwao lakini kwa vile wanashiriki tendo la ndoa na wake/wanawake zao basi hujenga ukukaribu na mimba ile na mtoto anapozaliwa huona kabisa kuwa ni wa kwake na hivyo kujenda bond kama baba hali ambayo humathiri Kisaikolojia huyu baba na hatimae kuona mtoto huyo anafanana na watu wa karibu na familia yake kama sio yeye mwenyewe.

Pamoja na kusema hivyo, sina maana kuwa huyo si baba yako na wala siwezi kukubaliana wala kukataa kuwa yule Mganda pia ndio baba yako wa damu. Kama walivyogusia baadhi ya wachangiaji huenda hata huyo Mganda sio baba yako.

Kutokana na maelezo yako inaonyesha wazi kuwa hauko interested na mwanamke huyo japokuwa ndio aliyekuzaa hivyo huna budi kumpa heshima kama mzazi wako wa kike kwani hajui kuwa mama ni nini hasa kwani sio yeye aliyekulea bali bibi yako.

Sitokulaumu kwa kupoteza interest au hata mapenzi juu ya mzazi wako huyo wa kike kwani hakutaka kujihusisha na wewe, sasa kwa vile umekuwa mkubwa na yeye anazeeka ndio kashituka na kuona hakutakuwa na mtu wa kumsaidia hapo ndio akakumbuka ala kumbe nina mtoto Tz!

Inawezekana kabisa hakujua ni namna gani atakujia na hakutaka kuomba msamaha kutokana na kujiweka mbali na maisha yako wakati ulipokuwa ukimuhitaji zaidi (ulipokuwa mtoto) na njia pekee ya kujiweka karibu na wewe ili kupata atakacho ni kupandikiza uongo bila kujali (Again) kuwa akuwa atakupa msongamano wa mawazo (stress), kuumiza hisia zako (emotional) na Kisaikolojia.

Mimi nakushauri kama ifuatavyo,
Mosi, Kamwe tena mwiko kabisa kumueleza baba yako Mtanzania kuhusu hili suala, kwani litamuumiza sana na hata kusababisha matatizo makubwa (inategemea na atakavyolipokea) sio yeye tu bali Bibi yako, ndugu jamaa na marafiki.

Ikiwezekana kaa mbali na huyo mama kwa kumwambia kuwa huitaji kuwa nae karibu kwa na asikutembelee wala kuzoea kuja hapo nyumbani na badala yake mwambie wewe utakuwa ukimtembelea huko Kenya kila unapohitaji kufanya hivyo kwani tayari wewe ni mtu mzima.

Pili, Ukisha muweka mbali tafuta wasaa na uzungumze nae hata kama ni kwa simu na umwambie yalioujaza moyo wako ikiwa ni pamoja na msimamo wako juu ya baba aliyekulea (hata iweje ndio unamtambua kama baba yako n.k) na juu yake(utampa heshima kama mzazi wa kike na hadithi za masiha yake ya ujana azi-keep mwenyewe).

Tatu, Kama unataka/ukipenda kuwa na amani moyoni juu ya Mzazi wako wa Damu basi utalazimika kum-bana mzazi huyo akupe ukweli halisi kama kweli anauhakika kuwa Mganda ndio Baba wa damu au anadhania tu lakini inawezeakana hata yeye sio baba na ukweli ni kuwa hajui baba ni nani na akaamua kusingizia wanaume wote aliotembea nao.

Usimuonee aibu wala usihisi Guilt kutokana na katabia kake kachafu ka kulala na wanaume ovyo tena bila kinga, hakikisha unam-bana akupe ukweli wote mpaka kwanini hasa akamsingizia huyu baba wa Tz na kitu gani kilimfanya asijihusishe na wewe na sasa nini kimemfanya akukumbuke (yote yalioujaza moyo wako yatoe) kwani unahaki zote za kujua kwa uhakika kama huyo Mganda ni baba wa damu au unaenda kubahatisha tu!

Akihakiki na kukupa maelezo ya kutosheleza na wewe kuhisi the argue ya kutaka kujua ukweli basi omba mawasiliano ya huyo Mganda ili ufanye nae mawasiliano na ikiwezekana kufanya vipimo vya DNA ili upate amani moyoni na sio kwenda kuanza kujipendekeza kwa mtu au hata familia ambayo huijuia achilia mbali Tamaduni zao za Kiganda.


Akisita nakuja na hadithi nyingine ambazo zinaashiria kuwa hana uhakika na Mganda, kwamba inawezekana pia sio baba wa damu basi achana na the issue na endelea na maisha yako na baba wa Tz. Wewe hautokuwa wa kwanza kulelewa na mzazi ambae sio wa damu kwani kuna watoto wengi tu wanalelewa na wazazi ambao sio wa damu lakini wanapendwa, kujaaliwa, kupewa msingi na mwanzo mzuri tu wa kimaisha kama ulioupata wewe.

Kuna watoto wanaishi na wazazi wao wa damu lakini hawapati ulichokipata wewe, kwa uzoefu wako umeona kabisa kuwa mama hakukutaka ulipokuwa mdogo na alikupa matunzo mabaya kiasi kwamba baba Mtz akahofia kuwa ungeendelea kuishi na mama huyo huenda usingefikisha miaka 21, ungejifia ktk umri mdogo sana.

Kumbuka kwenye suala la DNA, hakikisha humpi jukumu lakufuatilia kwani anaweza kuwa ana-demand pesa kwa kisingizo cha kufuatilia, hakikisha unalifanya mwenyewe na kama hakuna sababu ya wewe kufanya vipimo hivyo kwa vile una amani moyoni kuwa Baba Mtz ndio baba yako hakikisha unamuweka mama huyo mbali kabisa na familia yako ya Tz ili kuepusha matatizo ambayo yatakuathiri wewe na Baba mTz.

Kama nilivyosema awali kuwa kuna asilimia kubwa sana ya kina baba hapa Duniani wamelea na kusomesha watoto ambao sio wao wa damu, lakini kwa vile hawataki masumbuko ya akili, Saikolojia, hisia na hata kuharibu ukaribu wao wa kifamilia wanaamua kudharau maelezo ya watu wengine pia vipimo ya DNA na kuendelea na maisha yako kama kawaida.

Najipa matumaini kuwa umefanyia kazi maelezo na ushaurio kutoka kwa wachangiaji na utafanya uamuzi wa busara ili kuishi kwa amani na furaha.
Kila la kheri!

No comments:

Pages