Thursday

Sijui nini cha kuongea nae, yaani nakuwa-blank-Ushauri.

"Da Dinah happy new year! Blog yako imenisaidia sana kwa mambo mengi ambayo nilikua siyajui na yale nilo kuwa nayajua nimeweza imarisha zaidi, shukrani sana na pia kwa wote wanao changia watoa msaada mkubwa pia.

Da Dinah mimi nipo nje ya nchi kwa ajili ya masomo boyfriend wangu wa miaka minne sasa yupo Bongo, tumesha kwaruzana sana kwa ajili ya mahusiano yetu lakini nampenda kweli huyu kaka. Hilo si swali langu lakini just to give you an insight.

Mwaka jana mwishoni nilikua Bongo kwa likizo fupi na nilimtambulisha kwa Mama yangu Mama akampenda na yeye alikwisha nitambulisha kwao muda kidogo japokuwa mama yangu alikuwa anamsikia lakini hatukuwahi kukaa sote.

Niliporudi masomoni tukawa tunaendelea kuwasiliana vizuri tu sema siku hizi anakuja mpaka mtandaoni tunaongea lakini ukweli sijui nini cha kuongea nae, does that make sense?? Yaani na baki kucheka na kukumbushia yalopita madogo madogo na yanayo endelea huku kiasi nitaongea nae kuhusu nini kingine jamani online?

I love the idea that we chat but I've never done that with him so am blank! niwe naongea nini online? msaada dada yangu mpendwa...asante. M"

Dinah anasema: M heri ya mwaka mpya nawe pia, naona sasa mwaka ndio unachanganya...nimekuwa napata shida sana kuandika 2010 na hivyo nikawa naishia kuandika 2001, ila sasa nimezoa...anyway!

Uhusiano wa mbali ni mgumu sana na wengi huishia njiani, lakini njia pekee ya kufanikiwa kwenye uhusiano wa kimapenzi na mtu aliye mbali ni mawasiliano. Kwa bahati nzuri vijana wa sasa tumekuwa na Teknolojia na hivyo kuturahisishia sana linapokuja suala la mawasiliano.

Natambua wakati mwingine inaweza kuwa ngumu sana ku-keep maongezi kwa vile yeye hajui nini kinaendelea huko uliko na wewe hujui nini kinaendelea huko aliko, sio hivyo tu pia sisi wanadamu tunatofautiana kuna baadhi yetu tunapenda kuzungumza na wengine sio wazungumzaji.

Kama wewe ni mzungumzahi basi mazungumzo huja yenyewe yaani jinsi unavyoongea ndivyo ambavyo "topics" zinazaliana basi mnajikuta mnapiga soga mpaka mmoja wenu anaamua kuaga(hela imeisha n.k).....na wengine ni wa kimya kwamba akikupa habari anazodhani kuwa ni muhimu basi maongezi yameisha, utabaki kuuliza maswali nkupewa majibu mafupi.

Unaweza ukawa unazungumzia tofauti ya tamaduni za huko na Nyumbani, ukazungumzia sinema, habari za kisiasa, maisha kwa ujumla, mipango ya maisha yenu ya baadae, ni namna gani unakabiliana na masomo, leo Chuoni kulitokea nini, amekula nini, nani alipika (kama bado anaishai kwa wazazi), n.k.

Ukiwa unapa stori za huko uliko ambazo zinavutia na kuozungumzia mipango ya maisha ya hata yale maisha mlioishi miaka minne iliyopita......yaani unachanganya maongezi. Ili kumfanya na yeye aongee basi wewe unamuulizia habari za hapo nyumbani na watu mnaofahamiana nao n.k.

Pia mnaweza kuzungumzia ngono na hata kuifanya ngono kwa kutumia simu. Hii itawasaidia sana kupata zile kuwa karibu zaidi kihisia na hivyo uhusiano wenu kutotetereka.

Natumaini maelezo ya wachangiaji na nyongeza yangu yatasaidia ideas za kuendeleza maongezi na mpenzi wako.

Kila la kheri.

No comments:

Pages