Sunday

Nilitalikiwa Kisa Usomi, sasa nimepata mpya lakini....Ushauri!

"Hi da Dinah!
Mimi ni msomaji na mfuatiliaji wa blong yako, shortly I like it and I you as well. Nina 30years nafanya kzi kama Mhasibu Ofisini kwa mkuu wa nchi hii! Dinah tatizo langu ni kutaka ushauri kuhusiana na mwanaume nilie nae, lakini kabla naomba nikupe hadithi ilivyokuwa.

Nilipokuwa na 25yrs niliolewa na mwanaume wa Kiislam kama mimi na nikaenda Chuo soon after ndoa! Baada ya kuanza chuo ikawa ni tatizo kwa wifi zangu na Baba mkwe that kwanini nisome kabla ya kuzaa alafu pia mume wangu ni Form 4? Kwa nini nimpite kielimu?

Tatizo likandelea na likawa kubwa, Baba mkwe alimwambia mwanae achague moja a Divorce au la yeye sio baba yake. Nilipokuwa mwaka wa pili mume wangu akanishauri niache chuo nami nikakubali lakini after 2 months mama yangu akaja juu kwanini niache chuo kisa shinikizo la baba mkwe?

Nikaenda kwa mshauri wa wanachuo Chuoni for ushauri, yeye ndio akanishangaa na kuiomba nirudi Chuoni ! In a dilema nikarudi chuo na within a week wifi yangu akaniletea Talaka Chuoni ! Nusu nijiue kwa kuchanganyikiwa ila kwa sababu ni Muislam tena safi sikufanya hivyo!

Niliumia kwasaabu yeye ndio alikuwa mwanaume wangu wa kwanza na sikuhitaji mtu mwingine tena maishani mwangu! Maisha yakapita na nikamaliza Chuo salama na kuanza kazi. Siku moja nikakutana na Ex baba mkwe akiwa na shida fulani, kwenye maongezi akaniambia "mwenzio anakuhitaji tena na bado hajaoa".

Mimi nikamsaidia shida yake bila kumjibu lolote, nilimsaidia kama binadamu lakini roho iliniuma sana kwa kusikia habari kuhusu Ex hubby wangu. Kwa bahati mbaya Baba mkwe alifariki Dunia mwaka 2009 na my Ex hubby akaja kutaka turudiane lakini mimi nikakataa.

Akaanzakunifanyia fujo wherever he sees me! One night nilikutana nae wakati narudi kutoka Kitchen party alinitolea Bastola , thanks God alikamatwa na kuswekwa rumande for a long time !Niliapa siitaji tena mwanaume, ila watu na wazazi hawakukubaliana na mimi , then nikaamua kuwa na mtu ingawa nilikuwa naogopa sana!


Sasa tatizo ni kitandani, yaani kuwa zaidi ya mara kumi nilizojaribu kuwa nae kitandani akitaka kugusa tu basii "kashacheka", akijitahidi na kusimamisha tena bado anaceka kabla hajagusa. Kaenda kwa daktari, kajaribu mazoezi , kasoma article zako nk ! imeshindikana !

NIFANYEJE? Je niachane nae na kusubiri mwingine au nivumilie?
jemmy, DSM "

No comments:

Pages