Monday

Wazazi na jamaa wanasema nitafute msomi kama mimi, does it matter?

"Pole na kazi dada Dinah, kwanza nitangulize shukrani zangu kwa watu wote wanao toa ushauri na kutuelimisha mambo mbali mbali katika hii blog. Mimi ni mwanamke mwenye umri miaka 25, nimekuwa na boyfriend wangu kwa muda wa miaka 6, nilianza mahusiano nae nikiwa namalizia kidato cha nne, ila kwa sasa nipo chuo nachukua masters degree.

Mimi na boyfriend wangu huyu tunapendana sana, na pia namsaidia mambo mengi sana ya kifedha na hata yakimaisha (nikimaanisha ushauri), kwani kwa bahati mbaya hakufanikiwa kwenda shule kutokana na matatizo ya kifamilia, elimu yake ni ya kidato cha nne.

Hiyo yote ni kutokana na Wazazi wake kutojishughulisha nae tokea zamani, hawakujali suala la elimu, kutokana na hili alipitia maisha magumu saana kiasi cha kumfanya aanze kufanya dili mbalimbali ili apate hela za kuendesha maisha, na pia aliweza hata kupanga chumba akawa anaishi mwenyewe na kununua assets mbalimbali za nyumba.

Kwa ujumla ni mtu ambae anajipenda na anapenda maisha mazuri tatizo ni uwezo tu na kazi ya maana ambayo itakidhi mahitaji yake yote. Pamoja na hili anasaidia hata ndugu zake pia. Hivi karibuni mambo hayamuendei vizuri kabisa japo hajakata tamaa.

Anajitahidi hivyo hivyo, kwa sababu hii mara nyingi ananiomba mimi nimsaidie kifedha kwa sababu nampenda inabidi nimsaidie nimpe hela za matumizi na muda mwingine hata za kulipia nyumba. Na fanya hivyo kwasababu nampenda, na yeye ananipenda, yupo tayari hata kesho kuishi na mimi.

Swali langu lina kuja hivi, mimi nimesoma nategemea kupata master degree yangu miezi kadhaa ijayo, kwa ujumla namshukuru Mwenyezi Mungu ninamahitaji yangu yote, ila tatizo huyu boyfriend wangu, hajasoma ila ni mtu ambaye anajitahidi hivyo hivyo sio mvivu anapenda maisha mazuri, ila watu wanasema hatutadumu kwa muda mrefu kutokana na tofauti zetu, je mnasemaje kwa hili?

Swali la pili ni hili, tumejuana kabla hata sijaanza chuo, kwa kipindi chote hicho tulikuwa pamoja mpaka sasa nategemea kumaliza masters tupo pamoja, na pia ndio boyfriend wangu wa kwanza sijawahi kuwa na mwingine, je mnanishauri vipi hapa?

Kwani baadhi ya watu wananiambia nitafute mtu aliesoma kama mimi kwani tutaelewana zaidi kimaisha. Kuhusu suala la wazazi, wazazi wake wananipenda saana, ila tatizo lina kuja upande wa wazazi wangu wanataka nitafute msomi mwenzangu, ila kwa mimi siko tayari kwani nampenda huyu nilionae.

Kwasasa haijalishi kwani nipo tayari kumsaidia kwa lolote ili tu awe na maisha mazuri. Je hii ni sahihi? Naombeni ushauri wenu, je kuna future hapa kweli au tunaforce mambo tu kwa muda kwani yatakuja nizidia huko baadae kama asipo pata kazi au biashara ya maana.

Naombeni ushauri wenu na mtazamo wenu.

Dada K".

Dinah anasema:Asante mdogo wangu, natumaini kuwa umefanyia au unaendelea kufanyiakazi maelezo mazuri kutoka kwa wachangiaji, yasome yote kisha uyachanganue alafu uchanganye ndio ufanye uamuzi.

No comments:

Pages