Wednesday

Vishawishi vinavyosababishwa na Teknolojia......

Hapo chini nimezungumzia Teknolojia inavyoweza kuchukua muda mwingi kuliko ule unaotumia kuwa na mpenzi wako, na nimetaja simu na Mtandao (internet )na vilevile swala la kutembelea Salon na Gym.

Sasa leo nazungumzia ni jinsi gani vitu hivi vinashawishi na hata kupelekea baadhi ya wapenzi wetu kutumia muda mwingi katika "kona" hizo kuliko ule wanatumia kuwa na sisi.

Simu za mkoni;
Ni wazi kuwa simu inarahisisha mawasiliano yakikazi, biashara na inatufanya tuwe karibu na wapedwa wetu kila siku bila kupoteza kiasi kikubwa cha pesa kwenda kumtembea ndugu jamaa na marafiki.

Lakini simu hizi pia zimekuwa ni kishawishi kikubwa kwetu kufanya mahusiano ya kimapenzi ya kihisia na mtu yeyote ambae anajua namba yako au wewe unajua namba yake.

Hii inaweza kutokea ikiwa mhusika mwenye jinsia tofauti na wewe anajisikia mpweke siku hiyo, amechukizwa na mpenzi wake, amesongwa na mambo mengi yanayomfanya ajisikie hana raha n.k. na hivyo akaamua kuwasiliana na wewe kwa kukutumia "text" na kila kitu kikaanzia hapo.

Vilele mpenzi wako au wewe unaweza ukapokea "text" yenye mrindimo wa kimapenzi kutoka kwa mfanya kazi mwenzio au mfanya biashara mwenzako au hata rafiki wa mpenzi wako kimakosa, lakini kwa bahati mbaya ukavutiwa nayo (ukidhani ni yako na mhusika kakuzimia) hivyo ukaijibu vema kabisa na mpekeaji akavutiwa na ulichojibu na hapo ndio unakuwa mwanzo wa.......

Hayo yote niliyoyasema na mengine unayoyajua kuhusiana na mawasiliano ya simu yakonoga huwa yanasababisha wenza wetu ku-set pin # ili usiweze kufungua simu yake(ikiwa una tabia hiyo), hata siku moja huwezi ukakuta simu yake imezagaa juu ya meza.........siku zote itabaki ndani ya bagi ambalo linafunguo, wakati wa kulala itawekwa uchagoni (chini yamto), akiwa anaongeza nguvu simuni basi hatocheza mbali na mahali hapo n.k.

Unaweza kuongezea kuhusu hili kwa faida ya watu wengine na hasa walengwa ambao ni wanawake.

Karibu sana.

No comments:

Pages