Friday

Maambukizo ya HPV

Human Papilloma Virus (HPV) ni maambukizo yanayotokea sana wanawake na huambukizwa kwa kufanya ngono, unapata maambukizo haya hata ukitumia kinga (Condom). Baadhi ya maambukizo haya huweza kusababisha Saratani iitwayo "Cervical" au Saratani ya Kizazi ambayo inaweza kusababisha usiweze kushika mimba/zaa ktk maisha yako yote au maambukizo mengine huko ukeni ambayo sio yale ya Ngono tunayoyajua nakutajia kila siku.

Hakuna dalili zozote za Saratani hii ya kizazi lakini ukiwahi kujua kuwa unayo kwa kufanya kipimo kiitwacho "Smear" basi unakuwa umeokoa maisha yako kwani Saratani hii inaua wanawake sambamba na ile ya Matiti.

Mwanamke anaeanza ngono mapema (chini ya miaka 21) anakuwa kwenye hatari kubwa ya kupata Saratani hii na wale wanaoanza Ngono ndani ya miaka 20 huwa x2 kwenye hatari ya kupata Saratani hii.

Huu ndio ukweli wa Ijumaa ya leo kwa maelezo zaidi Muone Dk bingwa wa magonjwa ya kike, Madaktari hawa wanapatikana kila Hospitali kuwa Nchini.

Mwisho mzuri wa wiki.

No comments:

Pages