Tuesday

Nahisia zaidi ya za Kirafiki, nimwambie?-Ushauri

"Hi Dinah,
Nilikuwa natembela blogs nikaona ya kwako, imenivutia na nikaona hapa naweza pata ushauri.

Mimi ni mdada wa miaka 34, nina binti wa miaka 8. kwa hivi sasa mie nipo single sina mume. Ninachoomba ushauri ni hiki.

Nilikutana na mkaka mmoja baada ya yeye kupewa contacts zangu na rafiki yangu ambae alikuwa amenitumia zawadi kutoka nyumbani. Baada ya hapo tulipanga kukutana na tukakutana, ikatokea kwamba tumelewana na tukawa marafiki sana.

Kila siku lazima tuongee katika simu na pia sms, muda ulivyoenda ikawa kama vile lazima tuwasiliane kila siku isipokuwa hivyo huwa najihisi kuna jambo limepungua. Nae baadae akakiri kwamba inakuwa hivo kwake.

Ikafika likizo ya Christimas akanialika kwa wazazi wake mimi pamoja na mwanagu, tukaenda tukafurahi na kurudi. SASA tangu kipindi hicho nimekuwa napata hisia tofauti kimapenzi na za kirafiki kwake.

Yeye ananiambia ananimiss anatamani kuniona lakini hasemi kama hisia zake zimekuwa zaidi ya Urafiki. Nitakutanae week mbili zijazo anakuja kwangu je nimwambie how I feel? lakini pia sitaki kupoteza rafiki....

Nifanyeje? nisaidie jamani i dont want to loose a friend and I also want to know what we feel for each other.

Thanks
Jenifer"

Dinah anasema:Shukrani kwa kustop mahali hapa na kuniandika maelezo haya. Huyo mwanaume anajua kabisa kuwa unampenda au unamtaka zaidi ya urafiki lakini hana uhakika kama utamkubali awe kama "mpenzi" kutokana na urafiki wenu.


Wengi huamini kuwa hakuna urafiki wa watu wa jinsia mbili tofauti ukaishia urafiki tu unless wewe na yeye muwekeane mipaka na kuidumisha vinginevyo ile kitu inaitwa "chemistry" inaweza ikabadili urafiki na mkawa wapenzi.


Naelewa hofu yako ya kupoteza urafiki na huyo Kijana iwapo utaweka wazi hisia zako lakini ukweli ni kuwa wanaume huwa hawana hizo hisia za "akinikataa nitamuangalia vipi usoni kama rafiki", hivyo mwanaume ambae ni rafiki yako akikutaka huwa anafocus kwenye hisia na anajua kabisa ukimtosa ataendeleza urafiki japokuwa wewe kama mwanamke utashindwa kutokana na aibu au kujisikia vibaya kwavile umemtolea nje ,pengine unaweza kudhani kuwa amekushushia heshima hasa kama huna hisia nae.


Lakini kwa case yako, wewe mwanamke ndio mwenye hisia kali za kimapenzi juu yake hivyo basi hakuna ubaya kama utaziweka wazi hisia zako hizo na yeye akajua wazi kuwa umemzimia, sio lazima sana umwmabie kwa maneno unaweza kutumia uanamke wako na ukafanya kwa
vitendo zaidi, wanaume ni waelevu sana na hunyaka chapchap ile "lugha ya machoni".

Nafurahi kusema kuwa hakuna mapenzi matamu kama yale yalioanza na kuegemea kwenye urafiki, mara nyingi mapenzi ya namna hii huwa hayana kukinahi wala kupauka kwa vile wote wawili mnafahamiana vema kama marafiki hivyo mnakuwa tayari mmeweka msingi mzuri kabisa wa maisha yenu ya baadae kama wapenzi.

Ni matumaini yangu utayafanyia kazi yale yote yaliyoelezwa na wachangiaji, mimi kama Dinah nasema dada, go for it....muonyeshe tu kuwa safari zako zooote hapo umefika na mabegi umeshusha....

Kila lililo jema.

No comments:

Pages