Thursday

Nilipinduliwa nikaolewa tena ila mume2 simuelewi-Ushauri

"Dear Dinah
Mimi ni mdada wa miaka 28 niliolewa na mume wa kwanza na nilijaliwa kupata nae watoto
wawili.Mume alikua hodari sana kwa kila kitu katika mambo ya ndoa na tulipendana
sana hadi nilipopinduliwa na mwanamke mwenzangu bahati yake sasa ndio anakula raha
zote.

Nilivumilia saana baada ya kupinduliwa kwa vile mwanamme tulipendana saana
na hasa nilizingatia kuhusu watoto kwani alionyesha mapenzi saana pia kwa watoto wetu wa
kinyume na sasa nilivyoachika.

Kama unavyojua ndoa za waislam ni mwaname ndio
anapoama kumuacha mwanamke huwa na haki japo wewe bado unampenda akiamua
kukuacha huwa halazimishwi kuwa na wewe ila mwanamke ni hadi uwe na sababu
ya kimsingi kama vile ametaka tigo au analewa na hakutimizii mahitaji, lakini mambo mengine
huwa huwezi kuachika!

Dinah anasema: Hii wala sio haki, mwanamke unakandamizwa kwa kenda mbele kha! Eti mpaka uwe na sababu. Pole kwa kuachwa ukiwa bado unampenda mumeo wa kwanza.

Anyway hayo yamepita! Nilikaa nimeumia kwa muda wa miaka sita sikutamani tena
mwaname yoyote kwani pale nilipoishi sikupata mwaname aliemfikia ex wangu hata robo
yake kwa hiyo nikaendesha tu maisha yangu mwenyewe na watoto wangu.

Kama unavyojua jinsia hasa mwanamke ukishaolewa na kuonja utamu wa ngono,
nilifanikiwa kumpata mwaname mwingine nchi nyingine lakini alikua na asili ya nchi
yangu lakini tu alizaliwa kule. Sasa tulikubaliana kuowana na tukajaliwa kuishi
nchi ambayo niliishi mimi. Na huyu pia tulipendana sana ila kwa bahati mbaya
hakuweza kupata kazi kwani nchi hiyo ilikua na ubaguzi sana wa wageni!


Nilibahatika kushika mimba na nilitabiriwa kuwa nitazaa mtoto wa kiume
kitu ambacho kilinifanya niende ughaibuni mwa Ulaya kwani ningezaa mtoto
wa kiume nchini mwangu baada ya muda mtoto huyo angelazimika arudi
kwao kwani watoto hawafati mama! Tulikubaliana vizuri na mume wangu
na tulikua tunawasiliana kama kawaida na mapenzi yalikua mazuri tu.

Kitu cha kushangaza niliposettle huko ulaya ughaibuni mwenzangu
kanibadilikia kabisa! Namfahamisha njia za wenzie wanavyofanya
ili tuweze kuishi pamoja lakini haonyeshi interest kabisa kuja kuishi
na mimi na kisingizio eti wenzake wamemwambia maneno mengi kuhusu
mimi eti namsema na kusema namsimanga!

Na kibaya kabisa hata mtoto wake ambae toka azaliwe hajamuona, hamjali kabisa
na sasa ndio hana hata mawasiliano na nikimpigia simu anaongea
kama kalazimishwa! Nikimuandikia email hajibu!

Nimejitahidi kufuata mafunzo yangu niliyofundishwa, kwani na mie pia kabla ya hii blong
yako nilialikwa na hadi nilikua nyakanga nimejitahidi kumfanyiakila aina ya mapenzi ili kuboresha ndoa yetu, ikiweno kumsemesha maneno mazuri vitendo na hata kumvumilia na wakati mwingine hata kujifanya mtumwa kwake pia huchangia mafunzo yote
ninayoyapata kumtumia na yeye pia kama general kwani nahofia yeye ni negative thinking na hapendi kuambiwa.

Eti unamfundisha lakini mwaname habadilika kabisa! Najua ananipenda lakini anapenda kunitesa kwani nimeshadai talaka hadi nimechoka haniachi na huniignore tu pindi nikiomba talaka!

Kibaya zaidi pindi nikimwambia mapenzi au kufanya mambo mazuri huwa
haonyeshi kufurahia kabisa lakini nastahimili na kushindwa, nikilalamika
hapo ndio hujibu Bomu yaani utajuta kuzaliwa na pia mara nyingi hupenda
kujibu urgument than mapenzi.

Imefikia hata hapo nchini kwangu hataki niende na hunipa sababu zake ambazo haziniingii akilini na nikilazimisha kwenda basi atanikimbia akae mbali eti kikazi hadi siku zangu ziishe nisafiri
na nikimpigia simu au kumtext hapokei au harudishi text au kupiga simu.


Alitokea kwenda kwao hata bila ya kuniambia na mimi kwa mapenzi yangu
nilifurahi na kutaka kumfuata lakini alivyojua nataka kwenda kwanza alinambia hakai
sana amekwenda tu kibisahara kidogo, nilivyosema nitakwenda na tutarudi nchi yangu
pamoja alinikatia hata simu akawa hapokei na matokeao nikaambiwa eti
simu niliyokua nampigia imeibiwa nikaona sasa huko ndio kukataliwa.


Nikawa najaribu hadi nikafanikiwa kumpata nchini mwangu nikawa naongea
nae lakini hana mood na hata nikimwambia naumwa au mtoto anaumwa
haonyeshi kutujali kabisa!

Email anasoma lakini hajibu kwani nikimpigia
huzungumzia salam alizozipata lakini hajibu na kila mara mie tu ndio
nimpigie na mara nyingi nikimpigia anakua hana mood ya kuongea na mimi!


Nampenda saana lakini naumia nimejitahidi sasa mwaka wa tatu lakini mwaname
haonyeshi hata dalili ya kubadilika!na anadharau sijapata kuona au kusikia!
naomba ushauri ndugu yenu nifanyaje kwani sipendi kuachika
na hata nikiachika sitamani tena mwanamme kwani wanaume
unakaa nao vizuri baada ya muda wanabadilika kitu kinakufanya
unachukia maisha yako na maisha ya ndoa na mapenzi kwa ujumla!.


Nimekaa kusoma tu za wenzangu huona mengine yanazidiana na yangu
lakini mimi sina raha ya maisha na hata mtoto wangu, na kila kitu kwangu
naona hakina faida ila nasoma dini yangu lakini mara nyingi huwa katika majonzi
na kuona kama mimi sina bahati duniani na leo nimeona na mimi nipate
ushauri kutoka kwako Dinah na wengine.
Ni mimi Salha"

Dinah anasema:Salha mpendwa asante kwa kunivumilia (nimekuwa busy kimtindo).
Ni mwanamke mvumilivu sana na sina budi kukupa hongera kwa hilo. Inasikitisha huyu mume wako wa sasa anasikiliza zaidi marafiki badala ya kujali maisha yake yeye kama yeye na familia yake ambayo ni wewe na mtoto aliyezaliwa.

Kama ulivyosema ndoa ya mwanzo ilikuwa ya kiislamu, sina shaka hata hii ya sasa ni ya kiislamu. Kwa mujibu wa Imani hii ya Dini inasemekana* (usininukuhu) kuwa mwanamke ni mtu wa kukaa ndani tu na mwanaume ndio mtu wa kujishughulisha na kuhakikisha anamtimizia mkewe mahitaji yake yote.

Apart from Imani hiyo ya Dini, utafutaji, uwindaji na kumuangalia mwanamke na kumpa mahitaji yake yote au kujitahidi angalau kidogo sio lazima yawe yote, wanaume wanaamini kuwa ni jukumu lao na hii ni kutokana na EGO zao as men.

Kutokana na maelezo yako inaonyesha kuwa hajisikii vema au niseme hatuko comfortable wewe kumfanyia kila kitu na yeye anakaa tu akisubiri kupewa au kuambiwa nini cha kufanya (ulipokuwa unampa mbinu za kujiunga nawe huko Ulaya) na "mwanamke" si unajua wanaume wengine na dharau zao, wanadhani wanawake zetu ni ku gossip tu na hatuna uwezo wa kujituma na kufanya mambo makubwa kimaisha na kijamii.

Sasa tatizo la huyu mume wako wala sio kubwa sana japokuwa litachukua muda mrefu kidogo kwa yeye kubadilika, tatizo lake ni kutojiamini kama mwanaume na kujishitukia kuwa anapoteza uanamme wake kwa vile wewe ni mwanamke unaejituma na kumuangalia yeye na watoto wako.

Kuna uwezekano mkubwa akawa anadhani kuwa, mumeo wa zamani ambae ni baba wa watoto wawili wa mwanzo ndio anaerekebisha mambo hapo nyumbani na yeye kama mumeo wa sasa anahisi kuwa ni useless na njia pekee ya kuonyesha uanaume wake kwako ni kwa kuwa na kiburi, m-bishi au mkorofi ndani ya uhusiano wenu.

Mwenyewe umekili kuwa anakupenda na wewe unampenda hivyo basi sio mbaya kama mtajitahidi na kuifanya ndoa hiyo kuendelea na pia kuwa bora kwakurekebisha maeneo machache ambayo mimi nadhani ndio chanzo cha yeye ku-withdraw kama mpenzi.


Kitu muhimu hapa ni ninyi wawili kushirikiana na kuwa kitu kimoja kama mke na mume na wakati huohuo wapenzi, na ili kufanikisha hili mumeo anapaswa kuacha tabia ya kusikiliza zaidi watu wengine na kujitahidi kuwaridhisha ili asionekane "anatawaliwa na mkewe".

Wanaume wengine ni wajinga wajinga, wakiona mwanaume mwenzao kapata mwanamke muhangaikaji na anajituma huwa wanapatwa na wivu na kuanza kum-feed mamneno ya uongo ili tu asifanikiwe kimaisha. Nasema hivyo kwa vile umegusia suala ya rafiki zake kusema wewe unamnyanyasa yeye. Hawa marafiki lengo lao ni kuharibu ndoa yenu na kwa vile mumeoo ana-give in upuuzi wao wewe unataeseka ndani ya ndoa yako.

Nini cha kufanya: Kwa vile umefanya yote ( kwa mujibu wa maelezo yako) nakujitahidi kumuonyesha mapenzi nakuongea nae vizuri kwa mapenzi lakini yeye haonyeshi kubadilika. Kuna uwezekano namna unavyowakilisha hoja zako sivyo ambavyo inatakiwa kwa mwanaume wa namna hiyo (asie jiamini,mwenye kiburi na dharau).

Mwanaume kama huyu ukimuibukia na issue inayokutatiza ktk mtindo wa mawasiliano na kumuonyesha mapenzi mara zote anakuona kuwa unajipendekeza kwake na kuwa uko-needy (kumbuka ni ndoa yako ya pili hivyo anadhani kuwa hutokwenda popote na utaendelea kuwa nae milele na kuvumilia upuuzi wake).

Sasa kama inawezekana wee mfuate huko kwenye nchi yake (huko anako ishi), kisha fanya nae mazungumzo kuhusu issues zote zinazokutatiza na zimekuwa zikikunyima raha kwa muda wa miaka mitatu sasa. Wakati unawakilisha hoja zako hakikisha hubembelezi na wakati huohuo humfokei (usiwe na hasira) na badala yake kuwa firm.

PSSST**Kwa vile hamjaonana kwa muda mrefu anaweza kutanga Ngono, hakikisha ukimpa usimfanyie mautundu yako yote au hata kama unavipya na badala yake kuwa mvivu-mvivu hivi, sio sana ila hakikisha unajifikiria wewe zaidi na sio yeye linapokuja suala la kupata utamu/kilele.**

Sasa kuna sheria za kuwakilisha hoja au issues zinazokutatiza kwenye ndoa au uhusiano wa kimapenzi kwa mujibu wa aliyenifunza nayo ni (1)-Vizia siku ambayo mumeo hayuko moody na tengeneza mazingira mazuri (badilisha mpangilio wa vitundani, ongeza/punguza mapembo.

(2)-Anza kwa kuelezea hisia zako juu yake, umuhimu wenu kwa watoto na namna gani basi watoto wote wanavyo muhitaji kama baba (hii itamfanya asihisi kuwa anatengwa na watoto wa ex mumeo)

(3)-Kumbushia maisha yenu ya kimapenzi mlivyokuwa mkianzana na jinsi gani ulikuwa unafurahia na kiasii gani basi unakosa hayo yote. Mueleze namna gani unajisikia kila unapozungumza nae na hisia hizo zinavyozidi kila mnapokuwa pamoja.

Mwambie kuhusu hisia zako dhidi ya marafiki zake, sio kwamba unawachukia lakini unahisi kuwa wanachukua nafasi yako...kwamba mumeo anafanya maamuzi kwa kufuata marafiki zake na sio wewe mkewe.

(4)-Muulize ni kitu gani hasa kinamuudhi kuhusu wewe? na ni kitu gani hakipendi kuhusu uhusiano wenu pia angependa kubadilisha nini ikiwa atapewa nafansi ya kubadili kitu kuhusu uhusiano wenu na ndoa kwa ujumla......mara nyingi hii itamfaya na yeye akuulize maswali hayo hayo kitu ambacho ndio unakihitaji.

(5)-Kumbuka kumpa nafasi ya kujieleza ikiwa anataka kufanya hivyo, usilazimishe aseme kitu kama haonyeshio kufanya hivyo (hapa inamaa unayosema yanamuingia taratibu).

(6)-Fikiri huku unaasikiliza maelezo yake na wakati huo huo kuelewa. Kwamwe usiongee wakati yeye anajieleza na ikiwa yeye ataingilia wakati unajieleza kaa kimya na umsikilize lakini kumbuka kufikiri huku unaongea/sikiliza hii itasaidia kuepusha mabishao.

(7)-Kamwe usionyeshe Kiburi wala usimuonyeshe kuwa unamuhitaji sana hata kama ni kweli unamuhitaji, mdhihilishie kuwa wewe ni mwanamke unaejiamini na unaweza kuendesha maisha bila mwanaume lakini huwezi kuzuia moyo wako kupenda, na mtu pekee unampenda ni yeye mumeo. Hivyo humuhitaji (as in need) bali unataka awepo kwenye maisha yako na watoto wako.

(8)-Sasa mueleze yote yalioujaza moyo wako, kumbuka kutokulalamika, kubembeleza, kulaumu, wala ku-demand na kubwa kabisa hakuna kuonyesha mapenzi.....mpe straight face na tazama macho yake....this is your moment inaweza kubadilisha mwenendo mzika wa ndoa yako.

(9)-Mara tu baada ya maongezi kuisha usionyeshe ile "straight face" na badala yake kuwa more loving na ikitokea anataka mambo fulani huu ndio wakati wa kumuonyesha zile vitu adimu, ambavyo hawezi kuvipata ovyo-ovyo.

(10)-Badilisha mtindo wa maisha yako, you are only 28 hivyo bado mdogo na unaweza kuwa bonge la sista duu kwa maana ya mavazi na kujipenda (sio lazima uvae nguo za ajabu ajabu unawez akuvaa kufuatana na Imani yako ya Dini lakini ukavutia nakupendeza). Hakikisha unavutia kuliko ilivyo sasa.

Ibua interest mpya, mfano kufanya mazoezi ili kuweka mwili wako vema zaidi na utavutia zaidi ukiwa mtupu, valia nguzo za ndani zenye mvuto, ongeza ubunifu kwenye mapishi yako n.k

Endelea namtindo huu mpya wa kimaisha na baada ya wiki chache utaona mabadiliko......lakini kama haitatokea ndani ya wiki chache (nazungumiza kati ya wiki 2-miezi 3) basi itakuwa ni wakati muafaka kupata msaada kutoka kwa wale waliowafungisha ndoa.

Kila la kheri!

No comments:

Pages