Sunday

Nifanye nini kupata mtoto wa Kiume-Msaada

"Mimi na mume wangu tumejaaliwa mtoto wa kike miaka miwili na miezi saba sasa. Tunaomba mungu sana hapo baadae tupate mtoto wa kiume hebu nipe darasa najua unaelewa haya mambo kuwa pamoja na kusali upate wa kiume je Kitaalam unataimu vipi ili iwe kweli wa kiume dear?Pia kama nataka twins pia nafanyaje?

Nitashukuru sana ukinipa data kwani ndio nataka kujiandaa kumtafutia Bridgitte mdogo wake baada ya miaka miwili. Naomba nisikuchoshe nikutakie siku njema na baraka msalimie baby wako Conso a.k.a mama Bridgitte"

Dinah anasema: Dada Conso na Shamimu asanteni kwa ushirikiano wenu, hakika suala hili ni common sana miongozi mwa wazazi wengi wanaopenda kuwa na pea za watoto weye jinsia tofauti.

Natambua kuwa mtoto yeyote akizaliwa upendo, hali ya kujali na furaha ni ileile bila kujali jinsia yake, lakini kama ingewezekana basi wengi tungependa kuwa na mchanganyiko wa jinsia...namna gani basi utafanikisha hilo ndio mbinde!

Kupata mtoto wa kiume inategemea zaidi familia zenu ninyi wawili, kwa maana kuwa kwenu kuna wanaume na wanawake kiasi gani hali kadhalika upande wa familia ya mume wako, ikiwa wanawake ni wengi zaidi kwenu na kwa mumeo pia wadada wengi basi utazaa watoto wakike tu au wengi (inategemea unataka kuzaa wangapi).

Lakini kama kwao mumeo wanawake wengi na kwenu wanaume wengi basi mtoto wa kiume kupatikana ni rahisi zaidi, ila ikiwa kwa mumeo kuna wanaume wengi na kwenu wanawake wengi bado uwezekano wa wewe kuzaa wa kike tu au wengi ni mkubwa.

Hivyo basi, ili kupata mtoto wa kiume inategemea zaidi na upande wako wewe mwanamke, nikiwa na maana kwenu kuna wanaume wangapi kwa maana ya wajomba, kaka zako, baba wakubwa na wadogo n.k. (ila binamu hawahesabiki).

Nini cha kufanya kupata mtoto wa kiume.
Kuna njia kuu mbili nizijuazo mimi ambazo zinaweza kusababisha wanandoa kupata mtoto wa kiume na njia hizo ni zile za Kisasa/Kitaalamu na asilia....nitafafanua kidogo asilia ambayo ndio naijua zaidi na ile ya kitaalamu ni straight foward.....lakini kabla napenda ufahamu yafuatayo;-

(1)-Mbegu zinazosababisha mtoto wa kiume hutoka haraka na kwa speed kubwa sana ili kuungana na Yai vilevile hufa haraka (hufa ndani ya masaa 3 ya mwanzo).

(2)-Mbegu zisababishazo mtoto wa kike hujivuuuta sana (maringo ya wanawake yanaanza b4 hata hatujawa viumbe kha! hihihihi) na hubaki hai kwa zaidi ya masaa 72 (zaidi ya siku tatu).

(3)-Bao zito na lenye afya ndio muhimu kusababisha mtoto wa kiume (mlishe mumeo lishe bora).

Hivyo basi ili kufanikisha hili unapaswa kutegea siku ambazo wewe unajua yai lako limepevuka na linasubiri kurutubishwa na mbegu ya kiume. Ukingonoka kwenye siku hatari kuliko zote ni wazi kuwa zile mbegu za jinsia ya kiume zitakuwa za kwanza kurutubisha yai na kufanya mimba ambayo itakuwa ya mtoto wa kiume. Hii ni njia asilia.

Njia ya kisasa ni ile ya kitaalam kuchukua yai lako na kuchagua mbegu za kiume tu kutoka kwa mumeo nakurutubia manualy (nje ya mwili wako) kisha wanakupandikiza, yaani wanakuwekea mimba (yai na mbegu walizounganisha) kwenye Womb (mji wa mimba) na hapo kunakuwa na uhakika wa kuzaa sio tu mtoto wa kiume bali wanaweza kuwa mapacha 2-3 wa kiume.....inaghalimu mamilioni ya shilingi though.

Kidokezo; imni ya kujaribu mpaka upate mtoto wa kike au kiume bila kuzingatia kwenu mkoje intrms of jinsia sio njema kwani mtajikuta mnazaa watoto ambao hamtaeza kuwamudu.

Natumaini maelezo yangu na ya wachangiaji wengine yatakuwa yamekusaidia kwa namna moja au nyingine, kwa niamba yao basi twawatakia kila lililo jema na Mungu afanikishe matakwa yenu kwa mapenzi yake.

Midaz!

No comments:

Pages