Monday

Binti kaniacha...je nichukue gari langu n.k?-Ushauri

"Habrai yako Dinah,
Hebu tusaidiane hapa, nilikuwa na mpenzi wangu kwa miaka 4 hivi, na nia yetu ilikuwa tufunge ndoa mwaka huu. Baadaye binti alihama mji na kuishi mji mwingine kikazi, hivyo nikawa namtembelea mara mbili kwa mwezi, na nikafanya hivyo kwa takriban miaka miwili.

Kidogokidogo nikaanza kuona tofauti za mawasiliano na sikusita kumwambia, japo sikuona mabadiliko tofauti na hali kuzidi kuwa mbaya, nami nikaendelea kumueleza na kujaribu kuongeza mapenzi kwake ili nisimpoteze.

Baada ya kuona haitoshi nikaamua kumshawishi tufunge ndoa ili awe wangu kabisa na ikiwezekana nimrudishe mji ninaoishi mimi. Kwa kuwa dini zetu ni tofauti tukakubaliana kila mmoja akaongee na familia yake ili tuoane kila mtu na dini yake.

Mimi nikafanikiwa ila yeye akasema kwao hawataki kusikia eti mototo wao anaolewa na Muislam. Basi nikamshauri tuendelee tu kuwa wapenzi kwa muda zaidi kama hawataki tuoane kwa sasa.

Yeye akasema hana jibu maana anahisi anachanganyikiwa tu. Kuanzia hapo hali ikazidi kuwa mbaya mawasiliano ni tabu, sms nikituma asubuhi atajibu jioni, simu mpaka nipige mara 10 ndio ipokelewe nk. Hata nikisafiri kumfuata huko aliko ngono sipewi kwa kisingizio kuwa matatizo tuliyonayo yanamkosesha hamu ya ngono.

Hivyo nikakaa zaidi ya miezi 8 bila ngono japo tunaonana na kulala pamoja mara mbili kwa kila mwezi.Ghafla siku moja baada ya kutopokea simu zangu nyingi sana ndio akanambia alikuwa ananifanyia hivyo visa makusudi ili nimchukie alafu nimuache, maana anaona uhusiano wetu hauto work out as wazazi wake hawanitaki.

Katika kipindi chote hiki cha mapenzi kulikuwa na kusaidiana kwa hapa na pale na niliwahi kumuachia gari atumie. Jee ni haki niendelee kumuachia gari yangu atumie hata baada ya kuniacha?

Jee jamii itaniona nina roho mbaya, na nitajisikiaje siku nikikuta mwanaume mwingine anaye mtomba anatumia jasho langu? Nisaidieni mawazo yenu, kumbukeni kuna vingi nilivyomfanyia kama furnitures, Ada ya Pango etc.

Kindiki"

Dinah anasema:Kindiki asante sana kwa ushirikiano, Hakika kuna wanaume wenye mapenzi ya kweli na wavumilivu sana hapa Duniani. Nimesoma comments na nikagundua kina kaka wamekupa ushauri mzuri ambao natumanini umesaidia wewe kufanya uamuzi mzuri.

Hili liwe fundisho kwa kaka zangu, acheni tabia ya kuwafanyia kila kitu wanawake. Kwani nyie ni baba zao? Kama ni mapenzi mnapendana wote wawili, kama ni ngono mnaifanya wote wawili na kama ni utamu wote mnaupata, sasa inakuaje wewe umfanyie kila kitu yeye na yeye hakufanyii lolote zaidi ya kukuchanganya na Midume mingine?

Sisemi kuwa usimsaide au kumnunulia zawadi mpenzi wako au usimjali kiuchumi kama anahitaji msaada huo, la hasha! Linapokuja suala la kufanyiana mambo makubwa kama kununua Kiwanja, nyumba, gari n.k mnatakiwa kufanya hayo mkiwa na uhakika na uhusiano wenu, kwamba ni wa kudumu/wachumba mnaelekea kufunga ndoa hivyo sio tu unamsaidia yeye bali wewe pia kwani mtakuwa mnaishi pamoja au kwenda kuishi pamoja.

Mf. kwa kulipa pango la nyumba na kununua vitu muhimu kama fenicha, gari n.k itakuwa kwa ajili yenu wote wawili na sio yeye peke yake....sijui mnanielewa? Kuna wanawake ukiwa nao basi utasomesha wadogo zake wote na kujengea wazazi wake nyumba na ukikamilisha yote hayo anakutema vilevile. Wapo wanawake siku hizi wanachukulia wanaume kama ajira, yaani akiwa kwenye uhusiano ndio kapata ajira.

Mimi binafsi nakushauri uchukue Gari lako na uliuze ili kuondoa mikosi na kumbukumbu za huyo mdada. Vingine ambavyo havishikiki achana navyo. Next time unajiingiza kwenye uhusiano hakuna kununulia mtu gari, mtafutie Dereva.

Mungu atajaalia mwaka huu mpya utaanza maishamapya na mpenzi mpya atakae kupenda kwa dhati, kukuthamini na kukuheshimu. Hakikisha hurudii makosa.

Kila la kheri!

No comments:

Pages