Monday

Kaniacha, lakini bado ananijali...je Kukeketwa inaweza kuwa kikwazo?-Ushauri

"Kwanza napenda kukupa pole na kazi ambayo unatuelimisha, nilikuwa sifahamu mambo mengi lakini kupitia kwenye blog yako nimejifunza vitu vingi sana.

Naitwa Jack ninaishi Tanga, nina umri wa miaka 25. Tatizo langu ni kwamba nimekeketwa tangu nikiwa mdogo sana hata kujitambua ilikuwa bado kwani nimekuja kutambua nikiwa mkubwa kuwa nimefanyiwa kitu hicho.

Nilipomuuliza Mama kwa nini umenifanyia hivi? akasema nilikuwa nasumbuliwa na ugonjwa wa lawalwa nikawa sina jinsi bali kukubali jibu la mama. Baada ya kukua ndio naona umuhimu wa kuwa kama wenzangu ambao hawajakeketwa.

Nilikuwa na boyfriend nikamueleza suala hili akakubaliana nami nikawa naenjoy pale napo fanya mapenzi aliweza kunifikisha kileleni kama kawaida tulidumu na Mchumba kwa miaka 3 na nusu lakini baada ya kwenda Dar es Salaam kwa masomo Mpenzi wangu huyo akanichiti na msichana mwingine na hivyo aliniacha mwaka huu mwanzoni.


Mimi bado nampenda sana ila yeye hakutaka kurudiana nami tena, japokuwa alikuwa amekwisha achana na yule dada aliyenichiti nae muda mrefu lakini hakutaka kuwa na mimi. Sijui kama ana msichana mwingine ama la. Mpenzi huyo ni mwanaume pekee ambaye nilimwambia kuwa nimekeketwa!

Hivi sasa nimepata boyfriend mwingine lakini bado hatujafanya mapenzi na ninaogopa kumwambia kama mie nimekeketwa sasa nitafanyaje ili ajue?

Mtu ambaye aliyekuwa ananifikisha kileleni ni mwanaume wangu huyo niliyekuwa nae miaka 3 iliyopita na ndie alikuwa ananipa raha kuliko niliyekuwa nae mwanzo kabla ya yeye. Sisikii kabisa hamu ya kufanya mapenzi kwa sasa nilikuwa nampenda sana mpenzi wangu wa zamani.

Nimejaribu kumuomba turudiane hataki, ila kama nina tatizo hunisaidia pia kama ninashida labda ya fedha huwa ananitumia, na nilipokuja kusoma alikuwa ananisomesha yeye mwenyewe, Da Dinah kila nikijaribu kuwa na boyfriend mwingine nashindwa nisaidie Dada yangu?
samahani kwa email ndefu utanisahihisha pale nilipo kosea?"

Dinah anasema:Asante sana kwa ushirikiano, ningependa akina dada wote waliokeketwa wasijisikie au kuchukulia kuwa wao ni waathirika(Victims) kwani inaweza kuchangia (Kisaikolojia) kwa kiasi kikubwa kutofurahia ngono.

Natambua tendo lenyewe ni la kikatili hasa ukizingatia kuwa binti unafanyiwa hivyo ukiwa ktk umri mdogo, lakini kwa vile limekwisha tokea hauna budi kukubali maumbile yako na kusonga mbele na maisha yako.

Mimi binafsi sidhani kama kukeketwa ni tatizo kwani mwanamke kuwa au kukosa kisimi hamfanyi mwanaume ashindwe kukupenda na hata kufurahia ngono, Kisimi ni kwa ajili yako wewe mwanamke na si mwanaume. Hata kama ni suala la kushukiwa chini bado kuna maeneo mengine anaweza kufanyia kazi na wewe ukafurahia kama ifuatavyo......

Kwa bahati nzuri wanawake tumeumbwa na maeneo mengi ya kusikilizia nakupata utamu, hii inategemea na utundu wako lakini mimi binafsi nimegundua maeneo sita tangu nimeanza kushiriki uhusiano wa kingono.

Maeneo 5 tayari nimekwisha changia hapa na Radioni ili wanawake wengine waweze kufurahia na wanaume kuyafahamu ili waweze kuyafanyia kazi vemana hilo eneo la sita nimegundua miezi michache iliyopita (nitachangia siku zijazo ili na wengine mkafurahie).

Uhusiano ule na wasasa: Kwavile uliamini tangu mwanzo kuwa kukeketwa ni jambo la ajabu (huenda ni kutokana na linavyolaaniwa kupitia vyombo vya Habari ) basi ilijengeka akilini mwako kuwa mwanaume atakae kuwa na wewe ukamwambia kuwa umekeketwa na akakukubali basi ndio atakuwa THE ONE.

Ulimuamini na kumpenda mpenzi wa zamani ambae inawezekana kabisa kuwa ndio alikuwa mwanaume wa kwanza kumpenda, kumuamini, kutoa "siri" yako na kufanya nae ngono, kutokana na kuhisi kukubalika kwa Jamaa huyo Kisaikolojia ukaamini kuwa hakutokuwa na mtu mwingine atakaekuparaha au hata kukupenda na kukubali japokuwa huna "Vikorombwezo" huko nyetini.

Sote tumepitia huko kwa mpenzi wa kwanza maishani, ni kweli kwa wanawake wengu huwa sio rahisi kumsahau yeye kama mtu, kusahau uhusiano ulivyokuwa na kutompenda mtu mwingine kama ulivyompenda yeye. Hakika unaweza penda mtu zaidi yake lakini mapenzi hayatokuwa enjoyable kama yale ya mtu wa kwanza), hii haina maana kuwa umg'ang'anie tu kwa vile ni 1st love hata kama yeye hataki.

Suala la yeye kukujali na kukusaidia haina maana kuwa anakutaka au anakupenda kimapenzi kama unavyompenda wewe, bali anakujali kama ex na angependa uendelee kuwa rafiki na njia peke ya kuendelez aurafiki huo ni kukusaidia na kuwa karibu kila unapomuhitaji labda kwa vile ni binti mwema, mzuri, unajiheshimu n.k.

Linapokuja suala la mpenzi uliyenae hivi sasa, huna haja ya kumwambia kuwa huna "vikorombwezo" kunako K na badala yake acha agundue mwenyewe na kama akiuliza mbona uko hivi hapo ndio utamwambia kuwa kwenu (kabila lako) huwa/walikuwa wanatahiri wanawake n.k

Huenda pia unahofia kuwa jamaa naweza asikufurahishe kingono ikiwa hutomwambia, unadhani kuwa ulipokuwa na yule wa kwanza alikuwa akikufikisha kwa vile alikuwa akijua....si ndivyo unavyodhania? Ukweli ni kuwa ulikuwa unasikia raha na utamu wa ngono kwa vile ulijiamini, ulikuwa unampenda na ulikuwa comfortable wakati wa tendo.

Mwanaume yeyote anaeujua mchezo (namna ya kufanya ngono ipasavyo) atakufikisha na kukupa raha isiyo kifani. Kitu muhimu ni wewe na yeye kujua kona nyingine za ume ambazo zinamsababishia mwanamke utamu (tafuta topic isemayo maeneo 5 ya kusikilizia utamu kwa mwanamke).

Kushindwa kupenda Bf mwingine: Ni kawaida kwa mtu yeyote anaetoka kwenye uhusiano wa kimapenzi wa muda mrefu kama wewe. Huwa ni ngumu sana kuanzisha uhusiano mwingine au niseme kupenda mtu mwingine. Baadhi hutumia muda huo kukusanya hisia zao na kuzi-review ili asirudie makosa pale atakapokuwa tayari kupenda tena.

Kwa kesi yako hakika itakuchukua muda mrefu kidogo mpaka utakapokubali kuwa umeachana na jamaa, hii ni kutokana na ukweli kuwa hujui kwanini hasa kakuacha na hivyo kila siku unapata matumaini ya Njemba hiyo kurudiana na wewe.

Kama unataka (sio lazima) kujisaidia ili kuondokana na hayo matumaini ambayo ni wazi yanakupotezea muda wa kuendelea mbele na maisha yako ya kimapenzi, ni vema kumuuliza mpenzi wako kwanini hasa ameamua kukuacha? Je ni kutokana na umbali kati yenu? Je ni aibu yake kuwa aliku-cheat? Je ameambukizwa HIV ndio maana hataki kuwa na wewe kwa vile anahofia kukuambukiza? n.k......kutakuwa na sababu moja inayomfanya ashindwe kurudiana na wewe.

Mimi kama Dinah nakushauri ujitahidi kumsahau kama mpenzi na jaribu kuji-keep busy na rafiki, ndugu na jamaa. Furahia maisha yako na kama huyo kijana uliyenae sasa unampenda basi focus kwenye penzi lenu na achana na ile njema ya zamani, kwani wakati wake umepita.

Ukiamua kupata ukweli:
Mara tu baada ya kujua ukweli kwanini alikutema, iwe ni Hasi au Chanya itakusaidia kusonga mbele na maisha yako. Kumbuka penzi ni hisia na hazilazimishwi bali hujitokeza zenyewe. Vilevile sio lazima hisia hizo zilingane bali kuzidiana na wakati mwingine kutokuwepo kabisa kutoka upande wa pili.

Kila la kheri!

No comments:

Pages