Friday

Kwanini W'wake pesa mbele mapenzi nyuma?

Imefikia wakati sasa nimekata tamaa, Dinah na wadau wengine mnajua kuwa ndani ya miaka saba kila mwanamke niliempenda na kuanzisha nae uhusiano anaonyesha kuipa pesa kipaumbele kuliko hisia za kimapenzi.

Awali nilidhani ni ugumu wa maisha kwa baadhi yao lakini nikaja kugundua hata wale mabanti waliotoka kwenye Familia zinazojiweza bado wanakuwa na hii kasoro ya kuthamini pesa zaidi kwenye uhusiano kuliko mapenzi yenu.

Je ni kasumba kuwa ukiwa na mwanaume ni lazima pia uwe mchimbaji wa dhahabu au ni nini hasa?

Imefikia wakati sasa naogopa kuanzisha uhusiano kwa vile nahisi hakuna atakae nipenda na kunipa penzi la kweli kama nifanyavyo mimi bali atakuwa na mimi ili kupata kile kidogo nilicho nilichonacho.

Jawabu: Shukurani kwa kuleta mchango wako hapa ulio katika mfumo wa swali. Hili suala nimekuwa nilisikia sana tangu nakua mpaka leo nimekomaa. Tena ni juzi tu nimetoka kuongea na Rafiki mmja akawa anasikitika kuhusu hili, hali inayofanya nitambue kuwa limekuwa tatizo kubwa kwenye jamii.


Inawezekana kabisa ikawa ni sehemu ya Asili ya mwanaadamu kuwa Mwanaume mtafutaji/mwindaji na Mwanamke mzazi na mlezi, lakini kutokana na maendeleo tuliyonayo hali imebadilika na sasa tunashrikiana na kusaidiana ktk kila jambo.

Kasumba ambayo imejengeka/zoeleka kuokana na mfumo dume inaweza kuchangia tabia hii kwa baadhi ya wanawake, vilevile kuna uwezekano kuwa ni mazoea yaliyobadilika na kuwa tabia na sasa imekuwa kama sehemu ya "Utamaduni" au niseme maisha ya baadhi ya wanawake kwa kisingizio cha "ugumu wa maisha".


Pia baadhi ya wanaume wanachangia hii tabia kuota mizizi na kuwa kasumba na hatimae "Utamaduni" (kama nilivyosema hapo juu) wa wanawake wengi kutokana na kitendo cha kutumia pesa kama "fimbo" au nyenzo ya kupata mwanamke.

Wapo baadhi ya wanaume ambao hujiona "Baba" kwa wapenzi wako (hasa kama ni wakubwa kiumri), kila ukikutana nae lazima akuachie "kitu kidogo" akisema nauli au kanunune soda.

Hii tabia wanayo akina baba wazazi (well baba'ngu miaka ile) mkipanga mihadi na kukutana lazima atakushikisha senti kabla hamjaachan akisema nunua kitu utakacho huko njiani.

Sasa Binti aliyezoea shikishwa Laki moja ya "nauli" na Mpenzi ajionae "baba" mara uhusiano huo ukiisha itakuwa ngumu sana kwake kuvumilia uhushiano mwingine bila kupewa pesa ya "nauli" kwa hiyari, na matokeo yake ama atahisi hapendwi (Kisaikolojia atakuwa akidhani kupendwa na mwanume ni kupewa pesa) au ataanza kukuomba kila mkikutana.


Kinachosikitisha zaidi kwenye hili suala ni kuwa Wanaume wengi wanapenda kujionyesha na "kujisigizia" mali ambazo hawana ilihali "kum-wow" mwanamke ili kushawishika kirahisi na akifanikiwa kumpata mwanamke husika Bwana atajitahidi kwa hali na mali ili aweze kuendeleza aina ya maisha fulani ambayo ameyaanzisha sambamba na uhusiano wake.

Hapo ni wazi kuwa uhusiano utaegemea kwenye ulichotumia kumshawishi (pesa/mali) na sio penzi kwani kilichomvuta kwako ni "misifa" na sio penzi au mvuto wao kwake japo kuwa wewe ulimpenda kimapenzi.


Kitu kingine ningependa kuongezea kwenye kujibu swali lako ni kuwa wanawake wengi wanapenda kusingizia ugumu wa maisha kama fimbo ya kupata senti kutoka kwa wanaume, na wanasahau kuwa ugumu wa maisha ni kwa kila mtu na sio Jinsia moja tu.


Mwanaume pia anakabiliwa na ugumu huohuo wa maisha lakini inakuwaje yeye anapata hata hicho kidogo chakukugawia wewe wanamke na wewe usipate ili mchange na kuwa na mahela ya kutosha kuendesha maisha kwa pamoja kama wapenzi?

Natambua pesa ni muhimu sana ktk maisha yetu ya kila siku na ni vema kuwa kwenye husiano ambao unajua kabisa utakuwa umelindwa kiuchumi, kihisia, kimwili n.k. incase of anything kama Mimba, kuugua namenginemengi ya kibinaadamu.

Pamoja na kusema hivyo ukubali ukweli kuwa unapoingia kwenye uhusiano unaingia kwa vile unampenda huyo mtu na unataka uchangie maisha yako na yake kwa ukaribu zaidi, mshirikiane kwa kila jambo.

Kidokezo

Penzi ni hisia na sio pesa au chochote kinachohusisha pesa. Kwa kumalizia tu napenda kusema kuwa ni vema unapomtokea mtu umtokee kwa kumueleza hisia zako za kimapenzi juu yake.

Ule mchezo/tabia ya kutongoza mabinti kwa kuwaahidi maisha mazuri, kuwapeleka popote watakako, kuwanunulia watakacho muiache. Wakati umefika kwa wanaume kuwa wazi na kuachakutumia pesa/uwezo wenu wa kimaisha ili kumshawishi mwanamke.

Just be yourself au a bit humble kama mambo yako safi na utakumbana na penzi la kweli lisilojali ulichonacho bali hisia zako tu.

****Samahani kwa kiswahili changu cha ovyo....Asante.

No comments:

Pages