Monday

M3-Faida/Hasara na umuhimu wa ndoa!

M3 michango yako inanifurahisha sana kaka. Shukurani!

"NDOA ni muhimu na ina faida na hasara zake `Je ni vyema tukasubiri hadi tufunge ndoa ndipo tungonoane au ni vyema `tukapimana’ kwanza ili baadaye tukifunga ndoa tuwe tumejuana vyema? Na kama ni hivyo ina maana gani ya kufanya `fungate’.

Nini hasa FUNGATE, Ina umuhimu katika ndoa? Naomba utusaidie zaidi katika haya. N.B Hapa wengi tunashindana tunaposikia hoja ya kuwa `ndoa’ na ngono ni vitu viwili tofauti naya kuwa Ndoa ni mjumuiko wa vitu vingi ikiwemo ndoa.

Ni sawa kutegemeana na imani zetu, lakini zipo imani zingine `ngono’ hairuhusiwi mpaka ndoa, kwahiyo ngono ni kipengele muhimu kuliko mambo mengine. Hapa napo unasemaje?

Na kama ulivyosema ni vyema kuishi kimaadili na kiimani. Kimaadili na kiimani nijuavyo mimi, nikukwepa kabisa swala la ngono hadi ndoa itimie kama sikosei, sasa katika hoja tulizoshauriana hasa zile zinazowahusu `wapenzi’ kuwa mfanye hivi na vile.

Hawa je siwanafanya ngono nje ya ndoa, je kipindi hicho wakiwa wanafanya hivyo nje ya ndoa , kuna tofauti gani waliyoiona baada ya kuoana?

Hili lilikuwa swali la awali na nafikiri majibu tumeyapata. Basi katika mada zako zijazo pia utusaidie kutuelezea umuhimu wa `imani’ katika `ndoa’ au mapenzi kwa ujumla. "

Ahsante tena emu-three

No comments:

Pages